Polisi wa FFU auliwa na Wananchi wenye hasira (Tegeta)

Nilikuwa natokea boko kuelekea mjini, njiani mume wangu kanipigia simu niwe mwangalifu kwani alisikia tegeta kuna vurugu. Aisee, niligeuza gari nikatembea miguu kuja kwenye eneo la tukio, yaani ilikuwa kama vile Afghanistan.

Nililazimika kugeuza gari na kurudi nyumbani. Polisi walikuwa wakirusha risasi ambazo sijui zilikuwa za moto au za mipira ila pia niliona moshi mwingi unaofanana na ule wa mabomu ya machozi. Polisi aliyeuliwa alivamiwa na mawe.

Pia kuna baadhi yao kadhaa waliojeruhiwa na gari lao kupigwa sana mawe. Kusema kweli hali ilikuwa ni mbaya sana..........Inabidi mkuu wa kaya aingilie swala. Waliowawa nimewaona na macho yangu ila cha kushangaza kamanda wa polisi analificha hili pale alipoongea redioni.

asante kwa taarifa. hata kama ina upungufu kidogo si neno
 
channel 10 news (1900 hrs) wamereport no deaths,,,, ni kwamba wanaficha ama mleta mada kakosea kidogo jmn??
Sina lengo la kucrush mtu yeyote, nisieleweke vibaya, nipo na lengo la kutafuta ukweli tu,
 
yaani ama kweli pinda atajutia kauli yake ya liwalo na liwe maana naona wananchi wameamua kama noma na iwe noma dah
 
Inatisha!Tanzania sasa mambo si shwari halafu viongozi wetu wametulia tulii...
 
JAmani mbona mwaenda mbaali saaana ,mwafika Afghanistani ,yaani hayo bado hayajashinda hata yale ya Unguja ,na zaidi kule Pemba 2001 , Zenji ni kawaida na sasa imekuwa ni mazoea na karibu itakuwa kama mchezo,si unaona Palestina kule imekuwa kama mchezo kati ya raia na majeshi ya Israel ,, Yaani mpalestina anaweza kutafuta japo korokochi na kumchokoza jeshi wa Izrael ili wapate kutimuana na ni kawaida ,wapalestina wanajua kuwa probability ya kifoau kujeruhiwa ipo ,huwa wameshaondoa hofu ,ndio karibu wazenji watafikia stage hio.

Poleni sana ila mtazoea tu.
 
Poleni sana Wafiwa, MUNGU AWAPE TULIZO MOYONI MWENU.

Serikali kweli mnaua Raia kwa sababu ya Mwekezaji mmoja?, Hakuna sehemu nyingine ya kumpa?, au Mna Hisa pamoja?, Mnataka Tufanye nini?
 
good news.this is just a slice of what big is about to come.mapinduzi daima.
 
Rip wananchi waliofariki na hao maaskari wakafie mbali maana wanatumwa na kujitoa ufahamu!


Hahahahahahaha kaka umenivunja mbavu zangu mie lol.. Ila kweli kaka mipolisi ya bongo ibabore sana lol
 
polisi mmoja wa kikosi cha ffu ameuliwa wakati wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya leo na raia wenye hasira maeneo ya tegeta namanga. Pamoja na skari, kuna raia wawili pila waliouliwa na askari hao wa ffu huku wengine wengi wakiwa wameumizwa vibaya. Hii ilitokea kwenye purukushani iliyoanzhishwa na mmiliki wa kituo cha mafuta aliyeanza kuvunja makazi ya wananchi hao.

Yawezekana wengi wamepoteza maisha yao, ila kwa macho yangu nimemuona askari mmoja kauliwa na wananchi wawili ila walioumia ni wengi sana. Hali ilikuwa ni mbaya sijawahi kuona. Nimeona ile kwenye tv. Nilijua tu vitu kama vile vinatokea afghanistan, syria na iraq siyo tanzania. Mbaya zaidi rais mwenye kapita na kuacha mapambano yakiendelea

mapambano kati ya polisi na raia yameendelea kwa muda mrefu hata baada ya rais kupita, ambako pia gari la rais na msafara mzima lilirushiwa mawe.....inabidi polisi waseme ukweli kuhusiana na hili jambo.. Hali bado tete kwani wananchi wana hasira na serikali kuruhusu mwekezaji huyu kujichukulia sheria mikononi mwake ya kuwahamisha na kuvunja makazi yao

chanzo, nilikuwepo eneo la tukio

liwalo na liwe!
 
Ningekuwa eneo la tukio leo, ka beretta kangu lazma ningekatumia kumpopoa japo askari moja! Dah! Nimeukosa huo mpambano, next time ntajitahidi kuwepo! Hii serikali zaifu lazma tuifundishe adabu! Aluta continua!
 
channel 10 news (1900 hrs) wamereport no deaths,,,, ni kwamba wanaficha ama mleta mada kakosea kidogo jmn??
Sina lengo la kucrush mtu yeyote, nisieleweke vibaya, nipo na lengo la kutafuta ukweli tu,

Hii nchi kwa kuficha wanaongoza mkuu!
 
Back
Top Bottom