Polisi apigwa risasi na kufa

ni kweli lakini furaha yangu iko pale pale, Awe amepaliwa na mfupa akafa awe amepigwa risasi kafa kwa uzinzi imradi polisi...kwangu mimi naona safi tu.
Si vizuri kufurahia kifo cha binadamu mwenzako, huenda hata hakuhusika na ile ishu ya Jan. 5.
 
wakuu....hii story ya kupigwa risasi polisi nilivyosikia ni kwamba kuna majambazi yamemliza mfanyabiashara kiasi cha pesa ambacho mpaka sasa hakijajulikana.....mfanyabiashara huyo alikuwa anaenda kuweka pesa hizo CRDB bank pale uhuru road, wachizi wakamtokea, walipokuwa wapo njiani kukimbia wakakutana na huyo polisi hana hili wala lile katoka duka la hardware kununua anachojua mwenyewe.....wanaume wakajua huyu ni nuksi wakamuwahi.....kwa hiyo polisi amekufa bila kujua kilichomuua ni nini.....huku nyuma majambazi hao wakimuacha yule baba mfanyabiashara akilia barabarani kama mtoto mdogo.....kweli pesa ni maua....hunyauka na kuchanua
Dah!! Pole sana kwa huyo mfanyabiashara, na mwenyezi Mungu ailaze roho ya askari mahali pema...amen!
 
Very sad! Haingii akilini ama kwa kutokujua baadhi yetu humu JF eti tunashangilia "askari kuuawa"! Ndugu zangu, tunachotakiwa kupinga daima ni damu ya mwanadamu kumwagwa bila sababu/hatia yoyote ile. Askari wa watu alikuwa katulia chini ya kivuli hana hili wala lile; yawezekana hata pengine alikuwa na matatizo yake binafsi mara ghafla wanatokea watu wasiojulikana na kumuua - wengine wetu humu tunashangilia - HUU NI WENDAWAZIMU! Jamani askari yule ni binadamu kama sisi, hakuwa katika mapambano yoyote yale na raia; just mpita njia.

Jamani hebu tuwe na ka-ubinadamu kidogo; kwa utaratibu huu bado hatujamjua adui yetu halisi ni nani na namna ya kupambana naye ni vipi vinginevyo tutaendelea kukorogana wenyewe kwa wenyewe na kati ya raia na askari bila sababu. Tukijue kwanza chanzo cha matatizo ya taifa letu halafu mapambano yaelekezwe huko. Ni juavyo mimi askari wanatumika tu na kazi yao ni kufuata amri tu.

Tuwe makini, tuepushe uhasama usio na msingi vinginevyo kuwafikia wa-tunisia na wamisri safari bado ndefu.
 
Mi sidhani kama hapa kuna haja ya baadhi yetu kulifurahia hili tukio wakati ukweli wake kwamba kwa nini limetokea hatujui
Kuna kipind askari mmoja kama kumbukumbu ziko sawa pale ubungo alipambana na majambazi ya benki wananchi walimshangilia sana sasa usije kuta huyu askari alikuwa ni wa namna ile ..........
 
What does this say about the majority of JF members who comment on stories without knowing the details??????
 
hii habari imekaaje? hata mtoa habari katokomea
Nipo mkuu ila naona watu washajulishwa kila kitu kuwa yule askari alikuwa na 50 zake hadi kifo kinamkuta mkuu. Nilichokiona ni kuwa watu wanachuki sana na Polisi kiasi cha kufikia kushabikia kifo kama vile wanamkomesha IGP Mwema.
Mungu ailaze roho ya marehemu. Amen.
 
This is developing story if it is true. Maoni mengi yaliyotolewa humu yameona the bitterness between people and our police forces. Lets take these comments seriously that Mwema needs to do something to clear a negative image created by his front liners on the public.
Ni kweli kabisa ikifikia polisi anakufa watu wanashangilia utafikiri si binadamu kuna sehemu kosa limefanyika na inabidi kurekebisha.
 
Nipo mkuu ila naona watu washajulishwa kila kitu kuwa yule askari alikuwa na 50 zake hadi kifo kinamkuta mkuu. Nilichokiona ni kuwa watu wanachuki sana na Polisi kiasi cha kufikia kushabikia kifo kama vile wanamkomesha IGP Mwema.
Mungu ailaze roho ya marehemu. Amen.

Sasa ndio tuseme habari nusu ukweli imekupa ulichokitaka (mission accomplished) unaendelea na uunganishaji wa mikwaju.
 
Aliyetufikisha hapa ni JK na RA wakisaidiwa na EL pamoja na Chenge kwa ridhaa ya Ben Mkapa.
 
Bora habari hii hatimea imeelekea kuwa hivyi ilivyo maanake vinginevyo watu wangeisaida polisi kwa maoni yao waliyo ya toa hapa.
 
Counting down 3-1=2 the equilibrium must be reached iwe kwa sababu yeyote ile.
 
Yote nayakubali JF lakini kuua hapana, pole kamanda. Wangeua Andengenye labda maana aliyeuawa huenda hajawahi kuua
 
subiri siku polisi watakapo mmiminia ndugu yako risasi,ndio utawajuwa polisi ni nani,ama subiri siku watakapo kubambikia kesi ndio utawaeleza wao ni kinanani,hayajakukuta wewe,tuulize tukueleze mkuuu,polisi waone tu mitaani usije ingia ktk anga zao pale kituoni ama mahali popote pale utaeleza kilichomnyoa kanga manyoya,

kweli Jerry wa Muro
 
Si vizuri kufurahia kifo cha binadamu mwenzako, huenda hata hakuhusika na ile ishu ya Jan. 5.

Ni mapema mno kuhisi sababu ya polisi kuuwawa...ila kama kuna watu wanafikiri ni siasa ....sio siasa....
Tulionya hapa toka mwanzo kuwa wakazi wa mikoa ya Arusha na Moshi...wana msemo "damu haiendi bure".....ukiwafanyia uonevu bila kuangalia kuwa ni siasa au dini....Hata ipite miaka ni lazima watalipiza tu......kuna haka kubwa kwa serikali na jeshi la polisi kwa ujumla kwenda kwa wafiwa na wazee wa jadi..wenye ushawishi..ili walipishwe faini ya mbuzi au ngombe..kufidia yale mauwaji...lakini iwapo watataka kufanya ubabe kama wa baadhi ya wabunge wanaoshabikia yale mauwaji...wajuwe tu kuwa watu wa kule sio wa DAR..kule watavizia tu..mmoja mmoja...hiyo ndio asili yao...kama wanabisha wakamuulize ....Aloyce Kimaro...alipewa shamba wakamuangalia tu...wamekuja kulichukua miaka 5 imepita...na anabahati walikuwa wanataka kichwa chake wakitundike kwenye lango la kuingilia kwenye shamba ....

Serikali kama ina pesa za kujenga barracks za kutosha Arusha inaweza kukaidi ushauri wa kuomba amani na kuomba msamaha kwa wazee..lakini kama inategemea askari polisi waishi mitaani wataendelea kuviziwa na bisibisi kila siku.......
Tena wananchi wa Arusha wamesikitishwa sana na kitendo cha Kikwete kuwatishia kuondoa maofisi ya kimataifa Arusha ...kwa ajili ya siasa......nchi hii bwana...wakati Nairobi ..watu walichinjana live..bado waakatetea ofisi za UN ..zikaendelea kuwa GILGIL....na kupiga ndogo ndogo na makao makuu ya africa mashariki yawe Nairobi......siisi siasa tu tunataka kusema tukose wote....huo ni uswahili na visasi...!!!
 
Msiongee tu hilo suala halijafafanuliwa kwamba kapigwa kwa kisasi au ni majambazi mie huwa siwezi kucomment kitu nisichokifahamu unaweza kuamka kesho ukakuta ni ishu tofauti embu subirini kamanda wa polisi au sehemu husika walielezee tukio hilo limetokeaje!!!

Sio vizuri kuanza tu kusifia wakati hujui cause ya tatizo ni nini si ajabu huyo askari hakuwa na kosa kabisa!yawezekana ameonewa! Tusubiri taarifa za magazetini na redioni ila mtoa taarifa tunakushukutu sana kwa informations!

Apigwe na majambazi au nani hilo si la kujadili. mimi nasema mmoja baada ya mwingine. Mpaka wakome waone kuwa kufanya kazi kuonea nao wataonewa. c polisi tu walijifunza kutumia bunduki bali sisi sote. Hata Rostam atapiwa na vichaa au majambaZI
 
Askari Polisi apigwa risasi na majambazi
WATU wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha ya moto, wamemjeruhi kwa kumpiga risasi kichwani na ubongo kutoka nje, askari Polisi, Konstebo Emmanuel Gama (30), baada ya majambazi hao kutilia shaka kuwa askari huyo na mwenzake walikuwa wanawafuatilia.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana saa 5 asubuhi katikati ya Jiji la Arusha eneo la Majengo, wakati askari akiwa na mwenzake aliyetambulika kwa jina moja la Konstebo Hassani,
wakitafuta vipuri vya magari kwenye moja ya maduka yaliopo eneo hilo la Majengo.

Majeruhi huyo ambaye baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru akiwa hajitambui, amehamishiwa Hospitali ya Serian, baada ya hali yake kuwa mbaya, kwani amepoteza fahamu.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kuwa majambazi hao walikuwa zaidi ya watatu na walikuwa wakitumia gari ndogo ambalo halikujulikana na walikuwa wakifuatana kwa nyuma na gari nyingine aina ya Pick Up, gari ambalo linadaiwa lilikuwa likiwafuatilia kwa kuwafukuzia.

Shuhuda huyo, Leonard Mushi maarufu kwa jina la Nyokaa ambaye ni fundi magari Majengo, alisema majambazi hao baada ya kufika eneo hilo, walishtuka kuona gari la Polisi lenye namba T806 ASD aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa ikitumiwa na askari hao ipo mbele yao.

Akizungumzia tukio hilo, askari aliyesalimika, Konstebo Hassan alisema walisimama ghafla kwa lengo la kutafuta vipuri vya magari ambapo yeye baada ya kuteremka kwenye gari, ghafla alimwona jambazi nyuma yake akikoki silaha huku akiwa amemwelekezea mwenzake.

Alisema aliamua kulala chini ndipo jambazi huyo alipofyatua risasi moja iliyompiga Gama kisogoni kwani ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa ni miongoni mwa askari waliofika katika Hospitali ya Mount Meru kumjulia hali majeruhi huyo; na pamoja na mambo mengine ameahidi kufanya uchunguzi na msako juu ya majambazi hao na kuhakikisha watatiwa mbaroni.

HabariLeo | Askari Polisi apigwa risasi na majambazi
 
Back
Top Bottom