Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Nimemsikiliza huyu Prof nguli wa sheria toka nchini Kenya akizungumzia juu ya uzalendo wa hayati JPM juu ya kuwa kiongozi aliyekuwa kada wa CCM. Na kwa mujibu wa Prof Lumumba anadai CCM ni chama kinamchomuenzi hayati Julius Nyerere ndio maana kinakuwa kinahakikisha kuwa rasilimali za taifa la Tanzania zinatumika kunyanyua na kuendeleza maisha ya Watanzania.
Hivyo Prof Lumumba anadai kuwa sababu hayati JPM alikuwa mwanaCCM ndio maana alimuenzi hayati Nyerere kwa kuhakikisha anatumia rasilimali za taifa letu kuinua maisha ya Watanzania.
Jambo ambalo nimegundua kuwa huyu Prof Lumumba ameongea kwa kuangalia sarafu upande mmoja, huku akiwa haijui vizuri Tanzania. Maana kama anaijua vizuri Tanzania asingeongea pumba kama hizi.
Kwa haya maisha duni wanaoishi Watanzania ndio aseme CCM kwa miaka hiyo yote tangu itawale imeinua maisha ya watanzania masikini? Hata hayati JPM alipokuwa madarakani mbona umasikini umekuwa mkubwa? Mama lishe na wenye maduka wamefunga, ajira zilisimama, wafanyakazi hawajaongezwa mishahara. Huku ndio kuinua maisha ya wananchi? Mbona 80% wanamaisha duni? Au Prof. Lumumba na usomi wake anaona kununua ndege na kujenga Ubungo interchange ndio kuinua maisha ya watu!