Pingamizi la CHADEMA juu ya Siyoi na uthibitisho kuwa Siyoi si Mtanzania

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
CHADEMA imemwekea pingamizi mgombea wa ccm Siyoi kwa madai kuwa si raia wa Tanzania.CHADEMA imenasa barua ya siri yenye Kumb no.AR/C/32/VOL1/85 ya Feb 29/2/2012,kutoka kwa Afisa mfawidhi wa uhamiaji mkoa wa Arusha kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha,ikifafanua uraia wa Sioyi na katika ufafanuzi huo Ofisi ya uhamiaji inakiri kuwa kwa yeyote aliyezaliwa nje ya nchi,ukomo wa uraia wake ni pale anapofikisha miaka 18 na baada ya hapo anapaswa kuukana uraia wa nchi alipozaliwa na Sioi Sumari alizaliwa Kenya,na hakuwahi kuomba uraia wa Tanzania.

Image.jpg
Image (2).jpg
Barua ya siri kutoka uhamiaji kwenda kwa Rc.jpg
Barua ya Siri kutoka uhamiaji kwenda Rc.jpg
 
Nilitamani sana tukishinde CCM hiki kwa kura uwanjani sasa huyu paka mweusi kwa jina la Sioi naye katokea wapi mbona anatuharibia mechi hivi, aggghhh!!!!!!!!!

Mambo mengine bana, mpaka kero; ina maana hata huyu Meneja Kampeni wa kukodi, hili li-rugaruga kwa upande wa CCM Lowassa naye hakulifahamu hilo mpaka wanamvuna baba wa watu mahela meeengi kupitia kwa 'Askofu wa Tanzanite' wakati CCM Orijino ilishasema kuwa huyo mtu hapan???????

Mwigulu Nchemba naye bana, huu si utapeli kweli huu kwa Mhe Lowassa mchana kweupe hivi hivi mpaka CHADEMA bao la kisigino hivi??????

Big up sana Vicent Nyerere na Makamanda wote mliokua mnasaidiana huko ila mturudishie japo NUSU VIINGILIO maana wengine bado tulikua bado tuko kwenye foleni huku nje ya uwanja hivo mechi hatujaona kitu mara tunasikia eti ni KO zile za ki-Mike Tysoni tu daahh!!.
 
Sioi movie is yet another intriguing one and worth beholding. Inspite of its unending formidable social woes, this country has never run short of such gripping drama.
 
Hivi wewe ni Pro-Chadema au msemaji wa ofisi ya Uhamiaji Arusha? Wewe basi kifungu cha sheria kinacho thibitisha Sioyi sio raia wa Tanzania, weka na uthibitisho wa Siyoi ni raia wa Kenya..

Kweli huyu dogo kiboko kila mkipiga hesabu zenu kwenye box la kura atashinda kwa mbali sana, mmeamua kuja na mbinu za kitoto.

Kama Chadema mnakubalika Arumeru kwa nini mnaangaika hivyo mpaka mnatia huruma.
 
Mimi ni Crashwise...kawaulize Uhamiaji nimeupataje barua zao siyo mimi.....yaani CCM Arumeru mmechanganyikiwa na bado...
 
..kwa Complications kama hizi, CCM walikuwa wanamtumia Rostam kuzimaliza. hebu tusubiri tuone.
Nadhani pia ndio sababu Mkapa amesita kwenda kuzindua kampeni kwasa babu ya hili zengwe.
 
CHADEMA imemwekea pingamizi mgombea wa ccm Siyoi kwa madai kuwa si raia wa Tanzania.CHADEMA imenasa barua ya siri yenye Kumb no.AR/C/32/VOL1/85 ya Feb 29/2/2012,kutoka kwa Afisa mfawidhi wa uhamiaji mkoa wa Arusha kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha,ikifafanua uraia wa Sioyi na katika ufafanuzi huo Ofisi ya uhamiaji inakiri kuwa kwa yeyote aliyezaliwa nje ya nchi,ukomo wa uraia wake ni pale anapofikisha miaka 18 na baada ya hapo anapaswa kuukana uraia wa nchi alipozaliwa na Sioi Sumari alizaliwa Kenya,na hakuwahi kuomba uraia wa Tanzania.

View attachment 48967
View attachment 48968
View attachment 48969
View attachment 48970

Hakuna kitu hapo, zaidi yakupoteza muda wote. Yote haya kamati kuu ya CCM ilipelekewa na kuona hayana athari. Na mwenyekiti wa kamati kuu ni RAIS WA NCHI. Na hizi barua kabla ya kamati kuu kukaa zilipitiwa na usalama wa Taifa na Uhamiaji na ndipo wakamshauri Rais kuwa hoja hazina msingi. Hii ni wazi kabisa SIOI NI TISHIO ARUMERU, CDM WANA WEWESEKA KILA UPANDE

Ignorance of the law is no defence. Mtu umeshaichambua sheria na kufafanua aina zote za uraia kisha unakuja na general statement eti "...kwa kutokujua sheria huwa wale wanaotuthibitishia kuwa wao sio raia wa nchi hiyo ... maombi yao huwa yanafikiriwa". Huyo Afisa Uhamiaji asitake kuchakachua mambo suala hapo linabaki kuwa - submission of renunciation certificate. Its too late for Sioi.
 
Mmeshindwa kushindana kwa sera sasa mnaingia kwenye personal life?
Hii inanikumbusha ya 2010 ya Slaa kuiba mke wa mtu!!
 
Mimi ni Crashwise...kawaulize Uhamiaji nimeupataje barua zao siyo mimi.....yaani CCM Arumeru mmechanganyikiwa na bado...

Mimi ni Crashwise (Mtu mwenye fikra chache kuzidi hata punje ya mchanga) ...kawaulize (wakina nani ww? mie ntakuja muuliza mwenza wako) Uhamiaji nimeupataje (sio kiswahili sahihi, waonyesha ww si mtanzania) barua zao siyo mimi.....yaani CCM (Chama Dume) Arumeru mmechanganyikiwa (Sio ww ? kwa nn uweke mapingamizi) na bado (na kweli na bado lazima mwaka huu nikufanye mchicha)

Kama kawaida yako habari zako sio zakuaminika humu JF , JITOE !

Hivi wewe ni Pro-Chadema au msemaji wa ofisi ya Uhamiaji Arusha? Wewe basi kifungu cha sheria kinacho thibitisha Sioyi sio raia wa Tanzania, weka na uthibitisho wa Siyoi ni raia wa Kenya..

Hivyo viambatanisho havitoshi?
 
Na nyie Magwan.da kama kweli hoja ya uraia haina mashiko kwanini mnaikomalia. Hebu jikazeni huko na muache visingizio vya kikekike. Mmeona Sioyi ni kigingi ndiyo mnaanza kujiangusha ili mpewe penalty? Stop being ridiculous!
 
Hili ni rahisi sana kwa siyoi kulitupilia mbali - kuonesha kuwa hakuzaliwa Kenya na b. kama alizaliwa Kenya aliukana uraia wa Kenya alipofikisha miaka 18.
 
Back
Top Bottom