Pingamizi la CHADEMA juu ya Siyoi na uthibitisho kuwa Siyoi si Mtanzania

Hakuna kitu hapo, zaidi yakupoteza muda wote. Yote haya kamati kuu ya CCM ilipelekewa na kuona hayana athari. Na mwenyekiti wa kamati kuu ni RAIS WA NCHI. Na hizi barua kabla ya kamati kuu kukaa zilipitiwa na usalama wa Taifa na Uhamiaji na ndipo wakamshauri Rais kuwa hoja hazina msingi. Hii ni wazi kabisa SIOI NI TISHIO ARUMERU, CDM WANA WEWESEKA KILA UPANDE

Kinacho fanywa na chadema kuhakikisha sheria zina fatwa lakini kama raisi wa nchi ali apa kuhakikishe katiba inafatwa ataamua kuwaamulishwa vibaraka wake wafanye watakavyo basi watanzania wanajua ukweli uko wapi na haitakuwa mara ya kwanza....
 
Kwa upande wangu bado sijaona mahali ambapo ofisi ya uhamiaji ikimtaja SIOI kuwa sio Raia wa Tanzania,nilicho kiona ni kwamba uhamiaji unasema "kama kweli SIOI kazaliwa kenya anatakiwa kuthibitisha kuwa yeye sio raia wa kenya" ambalo tayari ni swala dogo sana kwa chama kinacho hitaji kushika DOLA.

Lakini pia kuna sehemu uhamiaji unasema "kama alizaliwa huko wakati wazazi wake wakiwa ktk shughuli za kiubalozi,mtu huyo hata hesabika kuwa ana uraia wa nchi mbili" swali je SIOI alizaliwa kenya wakati wazazi wake wakiwa na shughuli za kiubalozi? kama YES basi pingamizi hilo litakwama

ngoja tusubiri
 
Sioi movie is yet another intriguing one and worth beholding. Inspite of its unending formidable social woes, this country has never run short of such gripping drama.

Kitu muhimu katika hili sheria ifuatwe ili kukidhi dhana ya utawala wa sheria. Kwa upande mwingine, natumaini nguvu ya Joshua Nassari na Sioi S. Summari itajulikana baada ya tarehe 01.04.2012
 
Mmeshindwa kushindana kwa sera sasa mnaingia kwenye personal life?
Hii inanikumbusha ya 2010 ya Slaa kuiba mke wa mtu!!

Mzee imekuwaje tena serikali ya CCM inatoa mapungufu ya mgombea wao halafu Rejao unaita "personal life" wakati mambo ya Slaa hajakuwa personal life?
 
Wewe basi kifungu cha sheria kinacho thibitisha Sioyi sio raia wa Tanzania, weka na uthibitisho wa Siyoi ni raia wa Kenya..

.

Mkuu unapaswa uelewe kuwa 'the burden of proof lies upon the shoulders of the suspect'. Pitia pitia kidogo sheria za nchi akili itaamka tu bila shaka!
 
Acha kupiga ngumi ukutani wewe mwana CCM Lowassa.

Ukisikia CCM Orijino ya yule baba nanahii wakishasema hapana basi mjue ndio hivo. Ubaya sasa ni kwamba mlileta ubishi naye Rais Kikwete kawaachieni puto liwalipukieni usoni kiulaiiiini kama hivi; ngoma ya akili sana hiyo usipime lakini!!

Unafikiri shujaa wako presha mpaka Ujerumani yeye hakuwekewa mambo yote hayo wazi mezani kwake, we vipi wewe?????

Acha kupigana vita na mjumbe mleta habari ya moto moto mkuu Crashwise, cha msingi wewe pigana na ile barua ya siri. Mbona tu wala hamjiulizi kwa nini uongozi mzima wa CCM orijino hawapo kwenye kampeni zenu wala Mzee Ben kutokutokea kwenye ufunguzi??

Yaani wewe ni mpaka ugusishwe Tomaso mkubwa!!!!!!!

Mimi ni Crashwise (Mtu mwenye fikra chache kuzidi hata punje ya mchanga) ...kawaulize (wakina nani ww? mie ntakuja muuliza mwenza wako) Uhamiaji nimeupataje (sio kiswahili sahihi, waonyesha ww si mtanzania) barua zao siyo mimi.....yaani CCM (Chama Dume) Arumeru mmechanganyikiwa (Sio ww ? kwa nn uweke mapingamizi) na bado (na kweli na bado lazima mwaka huu nikufanye mchicha)

Kama kawaida yako habari zako sio zakuaminika humu JF , JITOE !

 
Na nyie Magwan.da kama kweli hoja ya uraia haina mashiko kwanini mnaikomalia. Hebu jikazeni huko na muache visingizio vya kikekike. Mmeona Sioyi ni kigingi ndiyo mnaanza kujiangusha ili mpewe penalty? Stop being ridiculous!

Radhia Sweety,
Fikiria yaliyomkuta Siyoi ndio yangekuwa yamemkuta Kamanda Nassari unadhani Magamba nao wangemuacha hivi hivi? Hii ndio siasa bana. One mistake, one gool. Tayari Jimbo tumeshalichukua!
 
Mkuu wa mkoa anaitaka Uhamiaji impe taarifa za uraia wa mgombea wa CCM?

Nlifikiri Mkuu wa Mkoa anafanya kazi za serikali na si za kisiasa!

Anyway ngoja tukae kimya tuone.
 
Mmeshindwa kushindana kwa sera sasa mnaingia kwenye personal life?
Hii inanikumbusha ya 2010 ya Slaa kuiba mke wa mtu!!

Au yule DC wa Igunga kudai amevuliwa 'hijab' ambayo ikawa ndo mtaji wa M.agamba kuombea kura na kushamirisha udini ktk kampeni zao
 
Hata kama Msimamizi wa Uchaguzi akikataa kumuengua Sioi, Wananchi wa Arumeru hawapo tayari kuongozwa na MKENYA!
 
Mkuu wa mkoa anaitaka Uhamiaji impe taarifa za uraia wa mgombea wa CCM?

Nlifikiri Mkuu wa Mkoa anafanya kazi za serikali na si za kisiasa!

Anyway ngoja tukae kimya tuone.

Tambua kuwa mkuu wa mkoa anafanya kazi ya kumwakilisha Mh Raisi na wakati huo ni mwanachama wa CCM,so kuomba taarifa kwa uhamiaji ni kutaka kujiridhisha kama mwakilishi wa Raisi ambao chama chao ndicho chenye dola ili wasije wakawekewa pingimazi kama walivyo fanya CDM.

Nadhani ume elewa sasa kuwa baada ya mkuu wa mkoa kupata taarifa hiyo,hawezi kuiweka ktk draw wala kuikalia ni lazima alipeleka taarifa kwa anaemwakilisha ambae pia ndie mwenyekiti wa chama husika.

so mpaka wamemruhusu kugombea kupitia kwa Mwenyekiti wa chama ni dhahili shahiri kuwa hakuna issue hapo,

Kwa ushauri tu CDM wasipoteze pesa kufungua kesi kwani mwisho wa siku jamaa atakuwa huru
 
sheria za nchi lazima ziheshimiwe na viongozi wameapa hilo, hivyo mtu akikosa vigezo lazima aenguliwe kwani tuna heshimu utawala wa sheria.

let him go hatuwezi kukubali tume ya uchaguzi kutengeneza ruling mbaya nchini kwa kuruhusu mgombea asiye na sifa kwa vigezo vya magamba.
 
Hii ni wazi kabisa SIOI NI TISHIO ARUMERU, CDM WANA WEWESEKA KILA UPANDE

Sioi si tichio kwa CDM ila tunataka tuweke sawa uwanja wa mpambano. Hatutaki tushindanishwe na Mkenya maana sisi mgombea wetu ni Mtanzania (Kamanda Nassari). Tunataka CCM walete Mtanzania.
 
Kwa upande wangu bado sijaona mahali ambapo ofisi ya uhamiaji ikimtaja SIOI kuwa sio Raia wa Tanzania,nilicho kiona ni kwamba uhamiaji unasema "kama kweli SIOI kazaliwa kenya anatakiwa kuthibitisha kuwa yeye sio raia wa kenya" ambalo tayari ni swala dogo sana kwa chama kinacho hitaji kushika DOLA.

Lakini pia kuna sehemu uhamiaji unasema "kama alizaliwa huko wakati wazazi wake wakiwa ktk shughuli za kiubalozi,mtu huyo hata hesabika kuwa ana uraia wa nchi mbili" swali je SIOI alizaliwa kenya wakati wazazi wake wakiwa na shughuli za kiubalozi? kama YES basi pingamizi hilo litakwama

ngoja tusubiri

Marehemu Jeremia Sumari[JERRY SOLOMON kwa wakati huo] baba yake Siyoi alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni iitwayo Shell Chemical Company of Eastern Africa nchini Kenya. Hakuwa ubalozini.
 
Mzee imekuwaje tena serikali ya CCM inatoa mapungufu ya mgombea wao halafu Rejao unaita "personal life" wakati mambo ya Slaa hajakuwa personal life?
CCM inazingatia utawala bora na washeria, walitaka kuconfirm uraia wa Sioi baada ya rumors kuwa yeye siyo raia wa Tanzania! but all the official organs responsible for dealing with citizenship issues in the country confirmed that Sumari is a citizen!
 
Hivi wewe ni Pro-Chadema au msemaji wa ofisi ya Uhamiaji Arusha? Wewe basi kifungu cha sheria kinacho thibitisha Sioyi sio raia wa Tanzania, weka na uthibitisho wa Siyoi ni raia wa Kenya..

Kweli huyu dogo kiboko kila mkipiga hesabu zenu kwenye box la kura atashinda kwa mbali sana, mmeamua kuja na mbinu za kitoto.

Kama Chadema mnakubalika Arumeru kwa nini mnaangaika hivyo mpaka mnatia huruma.

dah! Kumbe na wewe uko kundi la lowassa sio? Magamba wenyewe hawamtaki huyu dogo, sasa wewe kumpigia chepuo ndio unatuambia nini?
 
Sioi si tichio kwa CDM ila tunataka tuweke sawa uwanja wa mpambano. Hatutaki tushindanishwe na Mkenya maana sisi mgombea wetu ni Mtanzania (Kamanda Nassari). Tunataka CCM walete Mtanzania.
Malizia kabisa, Mtazania anayeishi Marekani!
 
Kamati kuu walipokutana kabla ya kuja na jina la Sioi hii ilikuwa ni agenda kuu
Waliidadafua kupitia kona zote na wakajiridhisha kabla ya kuja na jina
 
Back
Top Bottom