Pingamizi la CHADEMA juu ya Siyoi na uthibitisho kuwa Siyoi si Mtanzania

Uraia uko wa aina mbili:

1. Wa kuzaliwa: ambapo kama umezaliwa Tanzania, bila kujali uraia wa wazazi wako, unakuwa raia wa TZ hadi hapo utakapofikisha umri wa miaka 18 na kuamua kuukana uraia wa nchi uliyozaliwa.

2. Uraia wa kupewa kwa mujibu wa katiba ya nchi. Hapa kuna kigezo cha mtu kuwa ameishi Tz kwa miaka kadhaa na ameomba uraia na kutimiza masharti ya kikatiba na sheria.

Kwa Sioi kama hakuukana uraia wa nchi alikozaliwa (ndivyo ilivyothibitishwa na uhamiaji) ina maana bado ni raia wa nchi husika. Tukumbuke kuwa sheria za Tanzania haziruhusu uraia wa nchi mbili.

Ulichoandika hapo point namba 1 SIO SAHIHI. Soma tena sheria ya uraia.
 
Kwenye hili sakata kitu kikubwa kinacho ibua haya yote ni DUAL CITIZENSHIP yaani uraia wa nchi zaidi ya moja
Na hapa Sioi anatuhumiwa ana dal citizenship ya Tanzania na Kenya, ambapo kisheria mtu mwenye dual citizenship akifikisha umri wa miaka 18 anatakiwa kuukana uraia wa nchi nyingine ili abaki na wa Tanzania vinginevyo ata cease to be a citizen of Tz.

Je kwa mujibu wa sheria zetu za uraia dual citzenship inakuwaje

1. Mtu yeyote atakaye zaliwa Tanzania na mmoja wa wazazi wake akawa sio raia wa Tanzania

2, Mtu yeyote atakaye zaliwa nje ya Tanzania na mmoja wa wazazi wake akawa sio raia wa Tanzania

3, Mtu yeyote atakayezaliwa nje ya tanzania na wazazi wote wa tanzania lakini nchi hiyo ikamtambua mtoto kama raia wao kwa kuzaliwa nchini kwao bila kujali uraia wa wazazi(haita husu kama wazazi wanafanya kazi za kitaifa kama ubalozini nk)

4, upo na wakurithisha nimeusahau, nitauweka baadae, ambao hauhusu kabisa sakata hili

Ukiwa umezaliwa katika mazingira haya utalazimika kuukana uraia wa nchi nyingine ili ubaki na uraia wa Tanzania

Sioi angeweza kuangukia namba 2 iwapo kama mmoja wa mzazi wake ni Mkenya

Au angeweza kuangukia namba 3 iwapo kama Kenya ingekuwa kama USA, kwamba kitendo cha yeye kuzaliwa Kenya tu kinampa uraia wa Kenya bila kujali uraia wa wazazi.

Kwa mantiki hiyo Sioi hawezi kuukana uraia ambao hana, Kenya ni kama sisi Tanzania foreigner wakija kupata mtoto hapa Tz mtoto hapewe uraia kwakuwa wazazi wake wote wawili sio raia

I stand to be corrected
 
Chadema bana kama Barca
keep them on their heels, keep busy within their area closer to their own goal.
Wakati wao wakihangaika kutafsiri sheria sisi tunazidua kampeni, good tactics indeed.
 
Kwenye hili sakata kitu kikubwa kinacho ibua haya yote ni DUAL CITIZENSHIP yaani uraia wa nchi zaidi ya moja
Na hapa Sioi anatuhumiwa ana dal citizenship ya Tanzania na Kenya, ambapo kisheria mtu mwenye dual citizenship akifikisha umri wa miaka 18 anatakiwa kuukana uraia wa nchi nyingine ili abaki na wa Tanzania vinginevyo ata cease to be a citizen of Tz.

Je kwa mujibu wa sheria zetu za uraia dual citzenship inakuwaje

1. Mtu yeyote atakaye zaliwa Tanzania na mmoja wa wazazi wake akawa sio raia wa Tanzania

2, Mtu yeyote atakaye zaliwa nje ya Tanzania na mmoja wa wazazi wake akawa sio raia wa Tanzania

3, Mtu yeyote atakayezaliwa nje ya tanzania na wazazi wote wa tanzania lakini nchi hiyo ikamtambua mtoto kama raia wao kwa kuzaliwa nchini kwao bila kujali uraia wa wazazi(haita husu kama wazazi wanafanya kazi za kitaifa kama ubalozini nk)

4, upo na wakurithisha nimeusahau, nitauweka baadae, ambao hauhusu kabisa sakata hili

Ukiwa umezaliwa katika mazingira haya utalazimika kuukana uraia wa nchi nyingine ili ubaki na uraia wa Tanzania

Sioi angeweza kuangukia namba 2 iwapo kama mmoja wa mzazi wake ni Mkenya

Au angeweza kuangukia namba 3 iwapo kama Kenya ingekuwa kama USA, kwamba kitendo cha yeye kuzaliwa Kenya tu kinampa uraia wa Kenya bila kujali uraia wa wazazi.

Kwa mantiki hiyo Sioi hawezi kuukana uraia ambao hana, Kenya ni kama sisi Tanzania foreigner wakija kupata mtoto hapa Tz mtoto hapewe uraia kwakuwa wazazi wake wote wawili sio raia

I stand to be corrected
Nakubaliana na wewe. Nimeitazama kwa haraka sheria ya uraia ya Kenya, Cap 170. Nilitaka kujua kama sheria hiyo inampa uraia mtu tu kwasababu amezaliwa Kenya. Hapana. Ili uwe raia wa Kenya inabidi ujiandkishe. Utaruhusiwa kujiandikisha kuwa raia wa Kenya kama; moja: umeazliwa Kenya, na pili: mmoja wa wazazi wako ni raia wa Kenya.

Kama Sioyi hakuwahi kujiandikisha kuwa raia wa Kenya (nafikiri ndivyo hivyo) hawezi kuwa raia wa Kenya. Alipozaliwa tu alikuwa raia wa Tanzania kwa mujibu wa kufungu cha 6 cha sheria yeti ya Uraia. Upo uwezekano mkubwa pingamizi la Nassari likatupwa.

Nassari pia amekosea kidogo katika barua yake ya pingamizi. Ame-refer sheria ya uhamiaji ambayo ni tofauti na sheria ya uraia. Wapo majaji ambao wangelitupa pingamizi hili kwa msingi huo tu - ku-refer to a wrong provision of law.

I stand to be corrected as well.
 
Hili ni rahisi sana kwa siyoi kulitupilia mbali - kuonesha kuwa hakuzaliwa Kenya na b. kama alizaliwa Kenya aliukana uraia wa Kenya alipofikisha miaka 18.

Sijakuelewa mzee wa Detroit,,unamaanisha? hata hivo barua ya uhamiaji mwisho kabisa pale "Hata hivyo endapo alizaliwa nje ya nchi wakati wazazi wake wakiwa huko kwa shughuli za kibalozi mtu huyo hatahesabika kuwa na uraia wa nchi mbili,,Maana yake anakuwa na uraia wa nchi ipi?
 
Nakubaliana na wewe. Nimeitazama kwa haraka sheria ya uraia ya Kenya, Cap 170. Nilitaka kujua kama sheria hiyo inampa uraia mtu tu kwasababu amezaliwa Kenya. Hapana. Ili uwe raia wa Kenya inabidi ujiandkishe. Utaruhusiwa kujiandikisha kuwa raia wa Kenya kama; moja: umeazliwa Kenya, na pili: mmoja wa wazazi wako ni raia wa Kenya.

Kama Sioyi hakuwahi kujiandikisha kuwa raia wa Kenya (nafikiri ndivyo hivyo) hawezi kuwa raia wa Kenya. Alipozaliwa tu alikuwa raia wa Tanzania kwa mujibu wa kufungu cha 6 cha sheria yeti ya Uraia. Upo uwezekano mkubwa pingamizi la Nassari likatupwa.

Nassari pia amekosea kidogo katika barua yake ya pingamizi. Ame-refer sheria ya uhamiaji ambayo ni tofauti na sheria ya uraia. Wapo majaji ambao wangelitupa pingamizi hili kwa msingi huo tu - ku-refer to a wrong provision of law.

I stand to be corrected as well.
Upo sahihi kabisa mkuu...
In simple logic, mfano tukisema sio raia wa Tanzania atakuwa raia wa wapi? wakati Kenya haimtambua kama raia

Kuhusu pingamizi la Nassari hata mimi nimeliona lina makosa kwenye kunukuu vifungu muhuhimu vya shauri hili linaloweza kupelekea shauri kutupiliwa mbali mapema tu.

Kuna sheria ya uhamiaji THE IMMIGRATION ACT No 7 of 1995(inahusu muundo na shughuli za uhamiaji)
Kuna sheria ya uraia THE TANZANIA CITIZENSHIP ACT No of 1995(inahusu uraia tu)

Sasa Nassari kuqote kifungu cha sheria ya uhamiaji(Immigaration Act) kifungu 5(2)(b) badala ya sheria ya uraia(Tanzania Citizenship Act)kifungu 5(2)(b), ni makosa makubwa sana, maana ukienda kwenye kifungu hicho kwa mujibu wa barua ya pingamizi kifungu hicho hakipo.

Mwisho barua ya Afisa uhamiaji Mkoa ipo shalo sana, haina maelezo ya kutosha kabisa na ndio maana Nassari ameshawishika kuandika pingamizi hilo kwa kigezo cha barua ya Afisa uhamiaji ambaye kimsingi amechemka aliposema eti Nassari alipofikisha umri wa miaka 18 alipaswa kuukana uraia wa Kenya. Kwani alikuwa na Dual Citizenship?... how?
Nahisi alishinikiza kuandika barua hii wakati ule ili wapate sababu wamtose Sioi, na sasa imevuja na Huyo Afisa Uhamiaji ataonekana bogas tu
 
Back
Top Bottom