Pinda kukutana na Madaktari Dar, Je anaingilia mamlaka ya Bunge?

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,217
1,259
Pasco mwenzako anataka kukutana na watu aliosema wamefukuzwa kazi kesho saa tatu asubuhi kwenye ukumbi wa CPL Muhimbili. Unasemaje hapo?

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YUPO DAR ES SALAAM KUTOKA DODOMA KUSHUGHULIKIA MGOMO WA MADAKTARI AMBAO UMEKUWA UKIENDELEA KWA LENGO LA KUUPATIA UFUMBUZI.

LEO AMEKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PAMOJA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA WASTAAFU.

KESHO SAA 3 ASUBUHI ATAKUTANA NA MADAKTARI BINGWA, MADAKTARI WALIOSAJILIWA (REGISTRALS) NA MADAKTARI WALIOKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS) NA BAADA YA HAPO SAA 4 ATAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD NA WAWAKILISHI KUTOKA HOSPITALI ZA MKOA WA DAR ES SALAAM, KWENYE UKUMBI WA CPL, MUHIMBILI.

MATARAJIO YA SERIKALI NI KWAMBA MAZUNGUMZO HAYO YATAWEZA KUMALIZA
MGOGORO HUU NA MADAKTARI WOTE KUREJEA KAZINI NA HIVYO KUREJESHA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HALI YA KAWAIDA KWA WANANCHI WA TANZANIA.

HIVYO SERIKALI INAWAOMBA WOTE WANAOHUSIKA WAFIKE KATIKA MIKUTANO HIYO BILA YA KUKOSA.

(IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
 
Habari itakuwa confermed kwenye habari TBC.tafadhali madaktari tushikamane kutetea haki yetu na profession yetu tusishawishiwe kwa maneno na vitisho vya serekali kamati kuu tafadhari be there
 
Waziri mkuuu,asalimu amri yupo dar sasa kusolve issue ya madakatri wote ,internspamoja watumishi wengine muhimbili,si alichimba mkwara atawafukuza sasa asalimu amri
 
Shart.# 1.selikali isifukuze dr. Hata mmoja. 2. Wizara ya afya ipigwe chini na kusukwa upya ndo wakubali kuingia ktk mazungumzo.
 
Tatizo siyo kukutana na madaktari; mazungumzo yoyote na madaktari hayawezi kuwa na maana kama Waziri wa Afya, Naibu, Katibu na Mganga mkuu bado wapo madarakani. Kanuni ya kwanza ya kujenga imani kwa madaktari ni kwa wanne hawa kuondolewa kwanza. That is a pre-condition ya mazungumzo yoyote ya maana.
 
wamebaaana wameachia,wamebaaana wameachia
che che che sisimizi kambeba tembo..
kazeni hivyohivyo wakuu!
 
Waziri mkuuu,asalimu amri yupo dar sasa kusolve issue ya madakatri wote ,internspamoja watumishi wengine muhimbili,si alichimba mkwara atawafukuza sasa asalimu amri

Kuna thread nimesoma inasema kuwa rais Kikwete ameenda Finland. Sikutaka kuiamini hiyo habari lakini inawezekana ni kweli maana sioni sababu ya Waziri mkuu kuacha shughuli za bunge na kuja Dar kama rais angekuwepo nchini!

Pamoja na blunders za watu wengine, naamini kwa dhati kabisa Speaker wa Bunge Anne Makinda anatakiwa awaombe radhi watanzania. Kwa zaidi ya week huyu mama amekataa huu mgogoro usijadiliwe bungeni. Watu wanataabika wengine wamepoteza maisha lakini yeye ameendeleza siasa. Leo kwa mara ya sita Mh Serukamba amesimama kutaka bunge lijadili, naibu katoa maelezo kuwa atapata ushauri ya kamati ya uongozi ya bunge!

Ule ujasiri anaotumia Speaker, naibu wake na wenyeviti kutoa hukumu na hata kutoa nje wabunge wa upinzani mbona unapotea kwa mambo muhimu yanayohusu uhai wa raia wasio na hatia? Kama wameruhusu watu watoe matusi bungeni badala ya kujadili hoja za wananchi wanashindwa nini kuruhusu mjadala kuhusu mgomo wa madaktari?
 
nakumbuka intern walipodai fedha zao wakapewa na kutimuliwa nikasema serikali inataka kuanza vita ambayo mshindi tushajua ni nani ..?
 
jamani mimi nilikuwa nadhani PM amemaliza share yake. Walianzia waziri wa afya likaja jopo la mawaziri na kisha waziri mkuu. Madaktari hawakutokea na yeye akatoa tamko la serikali nadhani share yake ikaishia hapo. Ilitakiwa sasa ije ngazi ya juu sasa kwa ama kukazia tamko la waziri mkuu ama kulirekebisha.

Mkanganyiko ni mkubwa sasa! Mara kamati ya bunge mara kamati ya serikali mara waziri mkuu! Nimebaini kwamba serikali serikali.imejichanganya na inaendelea kujichanganya. Mimi ni muumini wa kauli thabiti, nilikuwa naamini kabisa kwamba kauli ya serikali iliyotolewa na waziri mkuu ilikuwa thabiti na kulikuwa na mpango mbadala; kumbe hakuna. Najua katika kuokoa maisha ya watanzania hakuna mshindi kati ya serikali na madokta; kwa macho ya kawaida inaweza kuwa it is a win win situation, lakini ndani ya moyo wangu naona pigo kwa serikali.
 
Back
Top Bottom