Hapa tupo pamoja! Katika analogy hii, tunaweza kusema katiba ndio 'ukweli'?
Mimi kama sijaelewa vizuri labda, lakini mi navyoona niboro kama inawezekana Pinda aendelee amalize tu ngwe hii ilobaki kwa CCM.
Sheria hii inavunja katiba, katiba katika ibara yake ya 66 inaainisha jinsi mtu anavyopata ubunge. Sheria hii imevunja ibara ya 66 ya katiba.
Sidhani kama hiyo interpretation ni sahihi. Kwani Pinda ni Mbunge wa kuteuliwa? Kateuliwa na nani? Nafikiri kwa kuwa amepita bila kupingwa ina maanisha ni mbunnge wa kuchaguliwa.
Imevunja pia na haki ya msingi ( Basic right) ya wakazi wa majimbo yote ambayo watu wamepita bila kupingwa , haki ya kushiriki katika shughuli za umma inayosema:
Uhuru wa kushiriki shughuli za umma:
(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na
kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya
kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa
hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au
yanayolihusu Taifa.
Tume ya uchaguzi imewachagulia wananchi wabunge na kuwanyima haki yao ya msingi kwa sababu tu vyama vya siasa havikuweka wagombea (au wagombe waliowekwa waliwekewa pingamizi)
Gaijin, nadhani shida ilianzia bungeni wakati wa kutunga sheria. Tume ya uchaguzi inafuata sheria ambayo supposedly imeopitishwa/kubaliwa na wananchi (kupitia wawakilishi wao, wabunge!).
Gaijin, nadhani shida ilianzia bungeni wakati wa kutunga sheria. Tume ya uchaguzi inafuata sheria ambayo supposedly imeopitishwa/kubaliwa na wananchi (kupitia wawakilishi wao, wabunge!).
Hapo sasa!...wengi huwa wanachapa usingizi tu mjengoni. Ningetegemea vitu kama hivi kuleta debate kubwa tu mjengoni kabla havijapitishwa.hivi bunge linawezaje kupitisha sheria ambayo inapingana na katiba?
hivi bunge linawezaje kupitisha sheria ambayo inapingana na katiba?
Gaijin, nadhani shida ilianzia bungeni wakati wa kutunga sheria. Tume ya uchaguzi inafuata sheria ambayo supposedly imeopitishwa/kubaliwa na wananchi (kupitia wawakilishi wao, wabunge!).
Hatuwezi kujua mpaka tujaribu, unaweza kusema hutashinda halafu ukawa surprised na independent minded justices huko kwenye high courts.Unaweza kusema utashinda ukaenda kukutana na politics mahakamani.
Kinachoniuma ni ukweli kwamba hakuna mwanasheria aliyefuatilia hili. Na kuna watu wanaweza kuona hili jambo kama pedantic legalese zisizo na practical effect, nimetoa youtube clip ya Masha hapo juu, ilikuwa bado kidogo tu Masha apitishwe kwa style hii, baada ya kushindikana wananchi walipopiga kura tumeona kumbe Masha hakupendwa hivyo na wananchi, kiasi kwamba hata kama angekuwa mgombea pekee katika kura ya ndiyo/ hapana kuna uwezekano angeshindwa.
Kwa hiyo ni muhimu kubadilisha hii habari ya kupita bila kupingwa, even if it is only to ensure the integrity of our system. Ama sivyo Rostam anaweza kununua viti kibao vya ubunge akacontrol bunge lote.
Tunataka wawakilishi wa wananchi wawe wamechaguliwa na wananchi kweli, sio usani sanii fulani fulani tu.
"Sehemu hii ya Katiba hii" haimaanishi katiba yote counsellor, mwananchi ana haki ya kuishitaki sheria ya uchaguzi kwamba ime violate ibara ya 66 ya katiba.
Right tatizo la sheria tumeshaliona. So what is your recommendation? Iongezwe aina nyingine ya mbunge, i.e mbunge wa kupitishwa kwenye ibara husika? Au wananchi wapewe haki ya kumchagua hata mbunge ambaye hana mpinzani? Je hapo watakuwa wanachagua kweli kama atakuwepo mgombea mmoja?
Sheria yoyote ambayo inakinzana na Katiba haiwezi kuitwa sheria, uwezo wa bunge kutunga sheria uko limited kuwa watunge sheria ambazo zinaendana na katiba.
Ndio maana Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa ya Tanzania zinawajibika kufuta kifungu cha sheria kinachoenda kinyume na katiba. Ingawa mara nyingi kwa kuogopa the powers who are wanakwepa kufanya hiyo kazi waliyopewa kikatiba, mfano halisi kesi ya Mtikila ya mgombea binafsi