Pinda hastahili kuwa PM, si mbunge wa kuchaguliwa

Kupita bila kupingwa ni sawa na ushindi wa 100% , hive pined Ana Kilauea sifa ya kuwa PM. Watusi woe waliojiandikisha indigo assumed kura alizopata

For real? Unaweza kutuonyesha kura hata moja aliyopigiwa Pinda? Kama huwezi kuonyesha kura hata moja utasemaje "ni kama ushindi wa 100%"

Hatutaki kuzugana kwa ushindi wa "kama", ukiongelea ushindi wa 100% either umeshinda 100% au hujashinda, hakuna "kama".

Na Pinda hajashinda hata 1%, achilia mbali 100%.
 
Luteni, sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985, katika ibara yake ya 44 inasema hivi;

Sheria hii inavunja katiba, katiba katika ibara yake ya 66 inaainisha jinsi mtu anavyopata ubunge. Sheria hii imevunja ibara ya 66 ya katiba.
 
Hapa kuna swala la tasfiri linawasumbua,nini maana ya kupita bila kupingwa? alichukua form za kugombea hapakujitokeza mshindani sasa ulitaka watu wakapige kura kwa ule mtindo wa mwaka 90,ndiyo/hapana huku pembeni kuna kivuli.Kutokana na mazingira hayo haikuwa na sababu ya kupiga kura maanake hapakujitokeza mpinzani na ingekuwa ni uharibifu wa rasilimali tu.Hivyo Pinda ni mbunge wa kuchaguliwa.
 
Kupita bila kupingwa ni sawa na ushindi wa 100% , hive pined Ana Kilauea sifa ya kuwa PM. Watusi woe waliojiandikisha indigo assumed kura alizopata

Uhalali hautokani na percentage pekee. Nadhani hii ni issue ya kisheria zaidi. 'Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi', kisheria ni nani? Katiba haisemi mbunge anachaguliwa vipi au kivipi anakuwa amechaguliwa. Sheria ya uchaguzi ndio imeweka wazi zaidi hiyo ni kwa vipi mtu atahesabika kuwa 'mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi'.
 
"Sehemu hii ya Katiba hii" haimaanishi katiba yote counsellor, mwananchi ana haki ya kuishitaki sheria ya uchaguzi kwamba ime violate ibara ya 66 ya katiba.

Atakuwa mwananchi toka katavi though. Na basi ya argument yake lazima ianzie ibara ya 5. Pia Pinda anaweza kurely Ibara ya 30(1) inatosema Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma. Pinda alikuwa na haki ya kugombea ubunge. Kama vyama vingine havikuweka mgombea basi haki yake ipotee?
 
Hapa kuna swala la tasfiri linawasumbua,nini maana ya kupita bila kupingwa? alichukua form za kugombea hapakujitokeza mshindani sasa ulitaka watu wakapige kura kwa ule mtindo wa mwaka 90,ndiyo/hapana huku pembeni kuna kivuli.Kutokana na mazingira hayo haikuwa na sababu ya kupiga kura maanake hapakujitokeza mpinzani na ingekuwa ni uharibifu wa rasilimali tu.Hivyo Pinda ni mbunge wa kuchaguliwa.

Vipi kama mtu ambaye watu hawampendi anapendekezwa na chama kugombea ubunge katika jimbo ambalo chama kimoja tu kina mgombea, huoni kwamba kumpitisha bila wananchi kupiga kura angalau hiyo ha ndiyo/hapana kutawanyima wananchi nafasi ya kumchagua/ kumkataa ?

Uwakilishi gani huu unaotunukiwa bila ridhaa ya wananchi ?
 
Sheria hii inavunja katiba, katiba katika ibara yake ya 66 inaainisha jinsi mtu anavyopata ubunge. Sheria hii imevunja ibara ya 66 ya katiba.

Kitanga do you really think ukiargue mahakani kwa kutumia kifungu cha 66 utashinda kesi?
 
Atakuwa mwananchi toka katavi though. Na basi ya argument yake lazima ianzie ibara ya 5. Pia Pinda anaweza kurely Ibara ya 30(1) inatosema Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma. Pinda alikuwa na haki ya kugombea ubunge. Kama vyama vingine havikuweka mgombea basi haki yake ipotee?

Mimi siongelei kumnyima Pinda haki yake ya kugombea ubunge, Naongea sio tu kumpa mwananchi haki yake ya kupiga kura, bali pia hata kumpa Pinda haki yake ya kupigiwa kura.

Hata ukisema uachane na hivyo vifungu vya ibara ya 30 kuhusu haki za binadamu, ukiambiwa umtafutie Pinda aina ya ubunge wake kutoka ibara ya 66 huwezi kuipata, maana Pinda hakuchaguliwa, amepitishwa.

Kwa hiyo sio tu Pinda hana sifa za kuwa Waziri Mkuu, Pinda hana haki za kuwa mbunge period. Labda aende kuteuliwa.
 
Sheria hii inavunja katiba, katiba katika ibara yake ya 66 inaainisha jinsi mtu anavyopata ubunge. Sheria hii imevunja ibara ya 66 ya katiba.

66.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, Pinda ni 'mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi'. Binafsi, sioni mgongano kati ya sheria ya uchaguzi na katiba katika jambo hili hasa ukizingatia katiba haijasema 'kwa undani' ni vipi mbunge anachaguliwa.
 
Bado Pinda ni mbunge wa kutokana na jimbo. sheria iko wazi kwamba mbunge aliyepita bila kupingwa ni mbunge sawa na waliopita baada ya kupingwa Sifa ya kuwa mbunge anayo na hivyo sifa ya kuteuliwa anayo kwa mujibu wa katiba anaweza kuwa waziri mkuu.
 
Kitanga do you really think ukiargue mahakani kwa kutumia kifungu cha 66 utashinda kesi?

Hatuwezi kujua mpaka tujaribu, unaweza kusema hutashinda halafu ukawa surprised na independent minded justices huko kwenye high courts.Unaweza kusema utashinda ukaenda kukutana na politics mahakamani.

Kinachoniuma ni ukweli kwamba hakuna mwanasheria aliyefuatilia hili. Na kuna watu wanaweza kuona hili jambo kama pedantic legalese zisizo na practical effect, nimetoa youtube clip ya Masha hapo juu, ilikuwa bado kidogo tu Masha apitishwe kwa style hii, baada ya kushindikana wananchi walipopiga kura tumeona kumbe Masha hakupendwa hivyo na wananchi, kiasi kwamba hata kama angekuwa mgombea pekee katika kura ya ndiyo/ hapana kuna uwezekano angeshindwa.

Kwa hiyo ni muhimu kubadilisha hii habari ya kupita bila kupingwa, even if it is only to ensure the integrity of our system. Ama sivyo Rostam anaweza kununua viti kibao vya ubunge akacontrol bunge lote.

Tunataka wawakilishi wa wananchi wawe wamechaguliwa na wananchi kweli, sio usani sanii fulani fulani tu.
 
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, Pinda ni 'mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi'. Binafsi, sioni mgongano kati ya sheria ya uchaguzi na katiba katika jambo hili hasa ukizingatia katiba haijasema 'kwa undani' ni vipi mbunge anachaguliwa.

Kachaguliwa na nani? Kapata asilimia ngapi? Unaweza kutuonyesha mfano wa kura hata moja aliyopigiwa Pinda ?
 
Bado Pinda ni mbunge wa kutokana na jimbo. sheria iko wazi kwamba mbunge aliyepita bila kupingwa ni mbunge sawa na waliopita baada ya kupingwa Sifa ya kuwa mbunge anayo na hivyo sifa ya kuteuliwa anayo kwa mujibu wa katiba anaweza kuwa waziri mkuu.

Kwa mujibu wa ibara ya 66 Pinda si mbunge. Wewe katiba unayoisema ibara gani hiyo ?
 
Kwa hiyo ni muhimu kubadilisha hii habari ya kupita bila kupingwa, even if it is only to ensure the integrity of our system. Ama sivyo Rostam anaweza kununua viti kibao vya ubunge akacontrol bunge lote.

Hapa nakubaliana na wewe. Kimsingi kwa sheria na katiba ilivyo sasa (pamoja na kuwa ni mbaya!) hakuna shaka kwamba Pinda ni 'mbunge wa kuchaguliwa'. Katiba inaweza kubadilishwa ili iwe ni lazima kwa mbunge na rais kuchaguliwa kwa kupigiwa kura (hata kama hana mpinzani). Lakini ni wazi hili nalo lina challenges zake. kwa sheria ya sasa mtu anashinda kwa simple majiority tu hivyo kama hana mpinzani hata akijipigia mwenyewe tu kura moja inatosha yeye kushinda.
 
Kachaguliwa na nani? Kapata asilimia ngapi? Unaweza kutuonyesha mfano wa kura hata moja aliyopigiwa Pinda ?

Kwani hiyo ibara ya 66 ya katiba inasema ili uwe umechaguliwa kuwa mbunge inabidi utimize masharti/vigezo gani? ibara hiyo ya 66 haisemi hili na ndipo hapo sheria ya uchaguzi inakuwa relevant.
 
Hapa nakubaliana na wewe. Kimsingi kwa sheria na katiba ilivyo sasa (pamoja na kuwa ni mbaya!) hakuna shaka kwamba Pinda ni 'mbunge wa kuchaguliwa'. Katiba inaweza kubadilishwa ili iwe ni lazima kwa mbunge na rais kuchaguliwa kwa kupigiwa kura (hata kama hana mpinzani). Lakini ni wazi hili nalo lina challenges zake. kwa sheria ya sasa mtu anashinda kwa simple majiority tu hivyo kama hana mpinzani hata akijipigia mwenyewe tu kura moja inatosha yeye kushinda.

Unaweza kutunga sheria na kuiweka vitabuni kusema jua linazunguka dunia, ikapitishwa na kukubalika kwa watu wote.

Lakini sheria hii haitabadilisha ukweli kwamba dunia inazunguka jua na jua halizunguki dunia.

Ukweli unabaki kuwa Pinda hakuchaguliwa hata kwa kura moja, hata ufanye sarakasi gani za kisheria na kuita "kupitishwa bila kupingwa ni sawa na kuchaguliwa" na ujanja mwingine kama huo.

Pinda hakuchaguliwa hata kwa kura moja, ukweli ndio huo.
 
Kwani hiyo ibara ya 66 ya katiba inasema ili uwe umechaguliwa kuwa mbunge inabidi utimize masharti/vigezo gani? ibara hiyo ya 66 haisemi hili na ndipo hapo sheria ya uchaguzi inakuwa relevant.

Unajua maana ya "kuchaguliwa"? Unataka habari za kuanza kudefine "what is is" hapa?

Huwezi kuchaguliwa kama huna waliokuchagua, kama Pinda kachaguliwa niambie nani kamchagua ?
 
Ndio maana hapo juu nikasema hili ni suala la kisheria (na sio mantiki). Kimantiki hakuna ubishi kwamba Pinda hakupigiwa kura sio tu na watu wengine bali hata yeye mwenyewe hakujipigia kura!

Lakini uchaguzi unaongozwa na 'sheria' ya uchaguzi ya mwaka 1985 (ambayo inatokana na katiba - 'sheria' mama!). Katiba inaongelea mbunge wa kuchaguliwa....sheria ya uchaguzi inaelezea ni vipi mtu anakuwa 'mbunge wa kuchaguliwa'.
 
Unaweza kutunga sheria na kuiweka vitabuni kusema jua linazunguka dunia, ikapitishwa na kukubalika kwa watu wote.

Lakini sheria hii haitabadilisha ukweli kwamba dunia inazunguka jua na jua halizunguki dunia.

Hapa tupo pamoja! Katika analogy hii, tunaweza kusema katiba ndio 'ukweli'?
 
Ndio maana hapo juu nikasema hili ni suala la kisheria (na sio mantiki). Kimantiki hakuna ubishi kwamba Pinda hakupigiwa kura sio tu na watu wengine bali hata yeye mwenyewe hakujipigia kura!

Lakini uchaguzi unaongozwa na 'sheria' ya uchaguzi ya mwaka 1985 (ambayo inatokana na katiba - 'sheria' mama!). Katiba inaongelea mbunge wa kuchaguliwa....sheria ya uchaguzi inaelezea ni vipi mtu anakuwa 'mbunge wa kuchaguliwa'.

Mark Twain alisema "the law is an ass", you can direct it anywhere and it will go. You can pass a law to call red blue and blue red, but will the actual colors change ?

Katika sheria kuna the letter of the law and the spirit of the law which goes deeper than some technical aspects of the law which can be easily circunavigated. Tunahitaji a precedent setting ruling kurudishs kura ya Ndiyo/ Hapana kwa hawa wagombea pekee.
 
Back
Top Bottom