Nini tofauti ya Waziri anayetokana na Wabunge wa Kuchaguliwa na Wananchi na yule wa Kuteuliwa na Rais?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,283
2,043
Wajuzi wa mambo naomba kuelemishwa tofauti ya utendaji kazi uliopo kati ya Waziri anayetokana na Wabunge wa Kuchaguliwa na Wananchi na Waziri anayetokana na kupewa Ubunge na Rais.

Kama utendaji wa kazi zao za Uwaziri zinafanana basi nashauri Mawaziri watokane na Wabunge wa kupewa Ubunge na Rais.

Mbunge wa kuchaguliwa na wananchi asipewe Uwaziri. Kutokuwapa Uwaziri kutawafanya Wabunge hao kujikita kwenye majimbo yao na kutatua kero zinazowakabili wapiga kura wao kama walivyokubaliana wakati wa kuomba kura.

Wabunge hawa ni wa wananchi kwani wamewachagua kuwapa Uwaziri kunawafanya kuwa mbali na majimbo yao na wapiga kura wao. Wabunge wa kuchaguliwa na Rais hawana makubaliano na wapiga kura pia hawana majimbo yao hivyo kuwapa uwaziri ni sahihi ili wawatumikie wananchi wote kama ilivyo kwa Rais.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Swali la ziada kidogo. Kwa mfano mbunge wa kuteuliwa na Rais akawa waziri. Ikitokea akaupoteza uwaziri na tuseme akabakia na ule ubunge wake, anakuwa anawajibika kwa namna gani au anatumikia watu gani haswa?
 
Tofauti ipo kwenye title ya uzi wako.

Usituchoshe kukujibu majibu.
 
Kwa uchaguzi huu huu wa kiccm ccm.
Wajuzi wa Mambo naomba kuelemishwa TOFAUTI YA UTENDAJI KAZI uliopo kati ya WAZIRI anayetokana na Wabunge wa kuchaguliwa na Wananchi na WAZIRI anayetokana na kupewa UBUNGE na RAIS
Kama Utendaji wa Kazi zao za UWAZIRI zinafanana basi nashauri MAWAZIRI watokane na WABUNGE wa Kupewa UBUNGE na RAIS. MBUNGE wa Kuchaguliwa na Wananchi ASIPEWE UWAZIRI. Kutokuwapa UWAZIRI kutawafanya Wabunge hao KUJIKITA kwenye Majimbo yao na Kutatua KERO zinazowakabili Wapiga kura wao Kama Walivyokubaliana wakati wa kuomba Kura.Wabunge hawa ni Wa Wananchi kwani wamewachagua kuwapa UWAZIRI kunawafanya kuwa Mbali na Majimbo yao na Wapiga Kura wao.Wabunge wa Kuchaguliwa na RAIS hawana Makubaliano na Wapiga kura pia hawana Majimbo yao hivyo kuwapa UWAZIRI ni sahihi ili wawatumikie Wananchi wote Kama ilivyo kwa RAIS.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Swali la ziada kidogo. Kwa mfano mbunge wa kuteuliwa na Rais akawa waziri. Ikitokea akaupoteza uwaziri na tuseme akabakia na ule ubunge wake, anakuwa anawajibika kwa namna gani au anatumikia watu gani haswa?

Anakua kama viti maalum tu kama Bashiru.
 
Swali la ziada kidogo. Kwa mfano mbunge wa kuteuliwa na Rais akawa waziri. Ikitokea akaupoteza uwaziri na tuseme akabakia na ule ubunge wake, anakuwa anawajibika kwa namna gani au anatumikia watu gani haswa?
Anamtumokia raisi.
 
Back
Top Bottom