Picha ya Mwigulu Nchemba na Mwanae yazua mjadala mitandaoni

Hebu acheni ujinga hivi kweli mie niwe na hela nimepeleke mtoto Kayumba?
Wacheni kusomesha mtoto Feza sio kosa maana analipia hela zake
Suala sio kuwa na pesa au kutokuwa na pesa. Suala ni unafiki. Nyerere alikuwa na uwezo wa kupeleka watoto wake nchi yoyote ila walisomea mazingira haya haya.

So, huyu ni bora angekaa kimya kuliko kujifanya yupo nasi kumbe changa la macho.

Aliwahi kusema bungeni anataka kila kitu kiwe kwenye kiswahili hadi job interview. Sasa kama unataka kila kitu kwa kiswahili mbona wanao umewapeleka " hallow dady?"
 
View attachment 321828
Picha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mbunge wa Iramba Mashariki imezua "hisia" tofauti na mijadala mitandaoni.Picha hiyo inamuonyesha Mh.Mwigulu akiwa na mwanae wa kiume,na "Caption" ya picha inayosomeka elimuniufunguo. Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.

Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa, itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu ktk shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya Elimubure na Uboreshwaji wa elimu katika shule za umma wanakimbiza watoto wao katika shule binafsi? Kwanini Mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?

Picha hii imezua mijadala tofautitofauti na wapo wanoona Mh.Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.

Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali
Shule za wanyonge hizo, Huko ni KISWAHILI tu maana ni lugha adhimu na inatumika bunge la Afrika, pia kumuenzi Nyerere tunatumia Kiswahili tu ndio maana MZEE WA KUCHORA MAJABALI kaamua kumpeleka mwanae huko;

Wanyonge acheni ulimbukeni nkupeleka watoto wenu english medium , kingereza si kitu, wala exposure si kitu, mwigeni MWIGULU
 
Hao watoto Feza cha mtoto tuu, Madelu anawalea wachezi thelathini, benchi lote la ufundi na uongozi wote wa Singida Big Stars
Cheza na bwana Tozo wewe. 😎
 
Hao watoto Feza cha mtoto tuu, Madelu anawalea wachezi thelathini, benchi lote la ufundi na uongozi wote wa Singida Big Stars
Cheza na bwana Tozo wewe.
Ilakweli jamaa Kuna familia sinalipwa kwa mikono ya mwigulu Hadi wazungu jamaa anawalipa vzr siyo Chini ya milion ,300 kila mwez jamaa Ana sain Kama mishahara
 
Back
Top Bottom