ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,116
- 49,840
Nimewahi kuhoji kwanini hizi pesa ambazo hawa wanaojiita asasi zisizo za kiserikali wasiwe wanazitumia ku compliment mipango ya Serikali badala yake nao wanakuwa na mambo yao ambayo hakuna tija yoyote inaonekana kwenye jamii.
Kama hawataki Serikali iwapige marufuku sio lazima wawepo maana kwa pesa zao kutoratibiwa zinaingia kwenye uchumi kinyemela na pia ndio hutumika kufadhili mambo ya ushoga, utakatishaji pesa, Madawa ya kulevya na kuingiza silaha kienyeji.
Ukisoma Takwimu zake ni pesa zaidi ya Trilioni 3 zinaingia Nchini kwa njia ya hawa NGOs lakini hakuna impacts inayoonekana kwenye jamii.
Laiti kama wao wangekuwa wana compliment mipango ya Serikali tungekuwa mbali ila hawataki jwa sababu wanazozijua wao.
Kwanini Mwendazake alishindwa kuwapiga marufuku Hawa? Wanajifanyaga kutoa Elimu, Elimu ipi ya maana wanatoa?
My Take
Serikali Wasajilini Upya na Kila NGOs ihakikishe Ina complements mipango ya Serikali Kwa Kila Moja na usajili wake vinginevyo wapigwe marufuku hakuna kitu Cha maana wanasaidia jamii.
======
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Seif Shekalaghe akizungumza. Picha na Mtandao
Dodoma. Wakati mashirikia yasiyo ya kiserikali yakizungumzia namna fedha za wafadhili zilivyowanufaisha Watanzania, wadau wameonyesha wasiwasi wao kama zote zinafika maeneo husika.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana kuhusiana na fedha hizo, Mhadhiri wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Dk Nasibu Mramba alisema huenda kuna fedha ambazo huishia kwenye mifuko ya watu binafsi kwa sababu wanaoweza kuwakagua ni wafadhili waliotoa fedha hizo pekee.
Chanzo: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Kaya (NPS)
Mwenendo wa fedha za NGOS zinazoingia nchini
Ongezeko la fedha zinazopatikana nchini kupitia ufadhili wa NGOs
Imeandaliwa na: George Helahela
Mchanganuo wa fedha za NGOs
“Hizi NGO zinapaswa kuangalia thamani ya fedha kwa kuhakikisha zinakwenda kwa wale waliokusudiwa, tumeshashuhudia fedha hizi za ufadhili wa mradi zikiishia mifukoni mwa watu na Serikali haina nguvu ya kutia mkono huko,” alisema Dk Mramba.
Kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto inaonyesha Sh2.24 trilioni zilizopatikana nchini kupitia mashirika hayo zimewanufaisha watu milioni 119.69 katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka 2022.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa fedha hizo ni ongezeko la Sh1.05 trilioni na asilimia 88.3 ya mapato ya mashirika ikilinganishwa na mwaka 2021.
Mapato hayo ni asilimia 5.3 ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/23, yanatokana na mashirika 1,257 yaliyowasilisha taarifa zao serikalini kati ya mashirika 6,635 yaliyopo.
Imeainisha kati ya fedha hizo Sh2.14 trilioni zilitokana na wafadhili kutoka nje ya nchi, ndani wametoa Sh18.77 bilioni huku michango kutoka sekta binafsi ikiwa ni Sh7.58 bilioni.
Michango ya jamii ni Sh4.20 bilioni, malipo ya huduma Sh5.64 bilioni, mapato ya vitega uchumi Sh3.40 bilioni, michango ya wanachama Sh29.23 bilioni, ruzuku Sh290.65 milioni, msamaha wa kodi Sh540.49 milioni, bakaa Sh37.18 bilioni.
Katika fedha hizo zilizopatikana kupitia mashirika yasiyo Serikali kiasi kikubwa kimeenda katika kutekeleza miradi ya sekta ya afya ambayo ilipata Sh72.82 bilioni ikifuatiwa na uwezeshwaji wa jamii ambayo ilikuwa na Sh57.51 bilioni.
Maeneo mengine ni ulinzi wa jamii Sh39.92 bilioni, Kilimo (Sh29.28 bilioni), Elimu (Sh26.83 bilioni), mazingira (Sh26.11 bilioni), Utawala Bora (Sh13.18 bilioni), nishati (Sh3.50 bilioni), maji (Sh3.06 bilioni) na haki za binadamu (Sh1.47 bilioni).
Ajira na wanufaika
Ripoti hiyo inaonyesha ajira 15,479 zilitolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali 1,257 kwa mwaka huo huku 9,974 wakiwa ni Watanzania na wageni walikuwa 156.
Kati ya ajira hizo 8,627 zilikuwa ni za wanawake na 6,852 zilikuwa ni za wanaume.
Pia katika ripoti hiyo inaonyesha waliojitolea kwenye mashirika hayo walikuwa 5,505, kati yao Watanzania ni 5,255 na wageni 250.
Kwa upande wa wanufaika, jumla ya watu milioni 119.69 walinufaika na miradi iliyotekelezwa kupitia fedha hizo huku sekta ya afya ikichukua zaidi ya theluthi mbili ya wanufaika.
Sekta ya afya ilikuwa na wanufaika milioni 83.03 huku waliobakia wakiwa kwenye sekta nyingine tisa ambazo ni uwezeshaji wa jamii, ulinzi wa jamii, mazingira, kilimo, elimu, utawala bora, maji, haki za binadamu na jinsia.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Seif Shekalaghe alisema kuna mashirika ambayo hayajawasilisha taarifa zake katika mwaka huo, idadi ambayo ni robo tu ya mashirika yaliyopo.
Kwa mujibu wa Dk Shekalaghe, kuna jumla ya mashirika 6,635, lakini 1,257 tu ndiyo yaliyotoa taarifa zake.
“Kutokuwasilisha kwa taarifa kunapunguza utambuzi wa mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya Taifa,” alisema.
Wadau wazungumzia
Akizungumzia hilo, Dk Mramba alisema ni jambo zuri la kuchangia katika maendeleo ya Taifa lakini fedha hizo nyingi zinatoka kwa wafadhili wanaopanga ni wapi ziende kutumika.
Alisema mara nyingi fedha hizo zinatolewa kama makubaliano kati ya mtoaji na mpokeaji na Serikali haihusiki, hivyo anayezikagua mara nyingi anakuwa ni aliyezitoa.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Paul Loisulie alisema wafadhili wamejenga minyororo yao kwa nchi walizozitawala na hata ufadhili wanaoufanya ni njia ya kuendelea kuboresha uwepo wao.
“Kuonyesha kwamba wao ni muhimu kwa nchi za Afrika kwa kuhakikisha kuwa minyororo yao haikatiki nchini. Na pia misaada hiyo ni njia ya kuendelea kuweka utegemezi,”alisema.
Alisema kutegemea kwa kiasi kikubwa ufadhili ili kujiendesha inamaanisha hata kimawazo na kisaikolojia hakuna wakati NGOs zitawaza kuja kufanya kazi kwa kujitegemea.