Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Huwezi kuboresha mfumo wa afya unaohudumia watanzania mil. 45 kwa usiku mmoja hii ni work in progress serikali imeshasema nini inaendelea kukifanya; madaktari wenyewe wanahusika kuuhumu mfumo wanaouhudumia ; miongoni mwao ndio wadai wakubwa wa rushwa kabla hawajakuhudumia uzalendo huu leo wameutoa wapi? kama wanataka kuwa wanasiasa na wawe wasitutie mchanga wa macho kwa kujifanya wanawatetea watanzania
Chama
Gongo la Mboto DSM
Chama, sikuzaliwa jana wala juzi. Nimezaliwa kabla hata Tanganyika haijapata uhuru, kwa hiyo nina uwezo wa kuona maendeleo ya nchi yanakwenda vipi. Kitu nilichokiona ni huduma kwa jamii kupungua mwaka hadi mwaka na watu wachache sana kutajirika kupita kiasi, ukijumuisha viongozi wa nchi. Hii ina maana kwamba rasilimali za mchi hazituiki ipasavyo. Zingekuwa zinatumiwa ipasavyo, uboreshaji wa huduma ungetendeka siku hadi siku. Unachokisema wewe ni maneno ya propoganda wanazoelezwa watu ambao hawajui ni kitu gani kinaendelea. kwa bahati mbaya sana kwenu, idadi ya watu kama hao inazidi kupungua.