PICHA; Wanaharakati wa CCM Elimu Ya Juu Wapinga Mgomo wa Madaktari

Huwezi kuboresha mfumo wa afya unaohudumia watanzania mil. 45 kwa usiku mmoja hii ni work in progress serikali imeshasema nini inaendelea kukifanya; madaktari wenyewe wanahusika kuuhumu mfumo wanaouhudumia ; miongoni mwao ndio wadai wakubwa wa rushwa kabla hawajakuhudumia uzalendo huu leo wameutoa wapi? kama wanataka kuwa wanasiasa na wawe wasitutie mchanga wa macho kwa kujifanya wanawatetea watanzania

Chama
Gongo la Mboto DSM

Chama, sikuzaliwa jana wala juzi. Nimezaliwa kabla hata Tanganyika haijapata uhuru, kwa hiyo nina uwezo wa kuona maendeleo ya nchi yanakwenda vipi. Kitu nilichokiona ni huduma kwa jamii kupungua mwaka hadi mwaka na watu wachache sana kutajirika kupita kiasi, ukijumuisha viongozi wa nchi. Hii ina maana kwamba rasilimali za mchi hazituiki ipasavyo. Zingekuwa zinatumiwa ipasavyo, uboreshaji wa huduma ungetendeka siku hadi siku. Unachokisema wewe ni maneno ya propoganda wanazoelezwa watu ambao hawajui ni kitu gani kinaendelea. kwa bahati mbaya sana kwenu, idadi ya watu kama hao inazidi kupungua.
 
Naomba kuweka record sahihi hapa, hawa sio wana harakati wa vyuo vikuu, hawa ni wafuasi wa ccm, huyo kiongozi anasoma Mlimani na ni kada wa chama, hawa wametumwa wala sio mawazo yao, hofu yao hapo ni kuona kama chama chao kinazidi kupoteza mvuto kwa wananchi kwa haya yanayofanyika.
 
Mtoto wa mpuuzi kama hatojiunga na watoto wasikivu basi tegemea upuuzi tu. Wapo wengi tu wanafunzi-mizoga wanaoishadadia serikali ya ccm huku vyuo vikuu.Hawa hawawezi kukemea lolote baya kama vile ufisadi,rushwa,matumizi mabaya ya ofisi za umma n.k hao ni vilaza wanaotegemea promotion ya ukuu wa wilaya,ukatibu taarifa n.k Ni vijana ambao ukiwauliza kuhusu tatizo la ajira wanasema ni kazi ya Mungu bila kuainisha vile serikali ya ccm imeua viwanda na vingine kuuza bila ridhaa yetu. HAKIKA NAAMINI:ni rahisi kwa kijana yeyote aliyehitimu kidato cha nne kuelezea uhalisia wa mambo nchini,kuliko mwanachuo msujudia ccm.
 
Hawana Kazi ya kufanya Maandamano baadala ya kusoma wao wanataka sifa za kijinga.huyo dogo anapenda misifa ya kijinga.Huo muda wa kufanya matembezi ya kijinga wanapata wapi?Ndiye aliyeaanda pia yale maandamano yaliyopokelewa na Nape pale Lumumba.Tupa kule
 
Kilaza akimshauri kilaza kitu naye akafuata anaonekana kilaza zaidi, waliandamana kwenda kwa wagonjwa au kwa madaktari? Ila nawasifu kwa maana maisha ya chuo tight wamepewa perdiem wafanye hivyo its good, je hiyo ndio njia ya kumaliza tatizo, noi sifuri kawashauri akina ziro
 
1.JPG

Kundi la wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu nchini, wakiwa na mabango jana katika hospitali ya taifa, Muhimbili, Dar es Salaam, kushinikiza madaktari waache mgomo.
2.JPG
Kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu Abubakari Assenga (kushoto), akiwa na Katibu wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Edwin Chitange, baada ya maandamano ya wanaharakati hao kufika Muhimbili kushinikiza madaktari kusitisha mgomo
5.JPG
Kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya Juu, Abubakar Assenga akizungumza na waandishi wa habari baada ya maandamano yao kufika Muhimbili kushinikiza madaktari kuacha mgomo.
3.JPG
Mwanamke aliyekuwa akisubiri kuona mgonjwa wake, Katika hospitali ya Muhimbuli, Dar es Salaam, Helen Thomas, akisoma bango lililoachwa na wanaharakati hao wa vyuo vya elimu ya juu.
4.JPG
Wanaharakati wa vyuo vya elimu ya juu, wakihanikiza baada ya kufika Muhimbili kutaka madaktari waache mgomo

MY TAKE; Hivi Wanaharakati wa MAgamba Vyuo vikuu ni hao tu?
ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firahuni
 
2.JPG
Kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu Abubakari Assenga (kushoto), akiwa na Katibu wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Edwin Chitange, baada ya maandamano ya wanaharakati hao kufika Muhimbili kushinikiza madaktari kusitisha mgomo

Huyu dogo Assenga anatafuta kusafisha jina kwa wakubwa wa chama cha magamba ili siku moja wamkumbuke katika ufalme wao.
Amewaokoteza hao wasela sijui kutoka mitaa gani na kuwaita wanaharakati wa vyuo vya elimu ya juu, ukiwaangalia tu unawaona kwamba hawajui wanachokifanya pengine wanatumikia buku mbili tu.
 
Sijui ni unafiki au uvivu wa kufikiri? Iweje wasomi wa chuo kikuu wapotoshwe na wanasiasa je wakulima wetu kule kijijini siitakuwa balaa!!nikweli wanavyuo hawa hawajui hoja halisi ya mgomo?ama kweli mpo chuo but hamsomi
 
kuna wawili nimewaona wana soma
datastar training college sasa sijui na chuo hiki ni chuo kikuu
- hila bado kuna post za maafisa mbalimbali kwenye wilaya mpya na mikoa pia kuteuliwa na kuajiliwa, acheni wasafishe njia wapete
hila T2015CDM hikishajiliwa tuwangoe woteeeeeeeeee
 
kuna wawili nimewaona wana soma
datastar training college sasa sijui na chuo hiki ni chuo kikuu
- hila bado kuna post za maafisa mbalimbali kwenye wilaya mpya na mikoa pia kuteuliwa na kuajiliwa, acheni wasafishe njia wapete
hila T2015CDM hikishajiliwa tuwangoe woteeeeeeeeee
 
mambugila hawa, wanachuo gani hawa wasio na akili hata kidogo kwanza hawafananii na wanachuo wanadanganya umma kwa kuwaokota watu mitaani na kuwaita wana chuo waongo wakubwa..........
 
de'levis alisema kuwa sasa hivi vitaibuka vikundi kibao vya kuonyesha kulaani madaktari...ndo hawa sasa nawaona
 
Elimu ya JUU ??? Hawa ninao ona ni wanafunzi wa Elimu ya Juu ? Lakini inawezekana kweli kama wanafunzi 5000 wameingia kidato cha kwanza hawajui kusoma na kuandika unategemea nini ? ndio hao Elimu ya JUU sijui kama wanjua hata nchi inakwendaje ? ni mavuvuzela wa Mr Dhaifu
 
1.jpg

kundi la wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu nchini, wakiwa na mabango jana katika hospitali ya taifa, muhimbili, dar es salaam, kushinikiza madaktari waache mgomo.
2.jpg
kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu abubakari assenga (kushoto), akiwa na katibu wa jumuia ya madaktari tanzania, edwin chitange, baada ya maandamano ya wanaharakati hao kufika muhimbili kushinikiza madaktari kusitisha mgomo
5.jpg
kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu, abubakar assenga akizungumza na waandishi wa habari baada ya maandamano yao kufika muhimbili kushinikiza madaktari kuacha mgomo.
3.jpg
mwanamke aliyekuwa akisubiri kuona mgonjwa wake, katika hospitali ya muhimbuli, dar es salaam, helen thomas, akisoma bango lililoachwa na wanaharakati hao wa vyuo vya elimu ya juu.
4.jpg
wanaharakati wa vyuo vya elimu ya juu, wakihanikiza baada ya kufika muhimbili kutaka madaktari waache mgomo

my take; hivi wanaharakati wa magamba vyuo vikuu ni hao tu?


hawa si wanaharakati ni wana-ccm wa vyuo vikuu,mbona hawakuvaa sare za ccm? Au wanaogopa kibano maana kuvaa nguo ya kijani siku hizi ina kama ume........ea
 
Kwanza kabisa hawa wamepewa kibali cha kuandamana au vipi?Maake wangekuwa wengine duuh hiyo intelejensia ya ya Mwema ingefanya kazi duuh walitumwa na Magamba na wao pia ni Magamba
 
Hawamjui adui yao!!
Eti nao ni watetezi wa serikali wakati yafahamika wazi serikali ina wasemaji,watendaji na watetezi wake rasmi.
Nani anawasemea matatizo yao?
 
Hivi unapowaangalia hawa wanafanana na wasomi wa elimu ya juu? Hata wa magamba hawafanani hivyo. Hawa ni zaidi ya magamba. Hawa ni watu wenye njaa tu. Wamelambishwa halua sasa wanakimbia barabarani wakicheka ovyo. Mwanaharakati gani anachekea huku Watanzania wakidhalilika kwa kulala chini wakiwa hospitali miaka 50 baada ya uhuru. Ona lingine linaonyesha mapengo tu. Kama wako vyuoni lazima ni wale vilaza waliokopa majina ya kuingilia vyuoni. Coconut headed individuals.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom