Mawaziri wa elimu na legacy zao ambazo haziridhishi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Joseph Mungai
Chini ya uongozi wake huyu masomo ya biashara na kilimo yalifutwa kwa baadhi ya shule za sekondari, Physics na Chemistry ikafanywa kuwa kipindi kimoja halafu wizi au uvujishaji wa mitihani ya NECTA ulitamalaki sana.

Shukuru Kawambwa
Huyu chini ya uongozi wake mikopo ya vyuo vikuu ilianza kusuasua na kutolewa kwa vigezo vingi vya ajabu ajabu sana na pia viwango vyenye mkanganyiko mtupu, pia wakati wake ungeweza kukuta wanafunzi wengi tu wenye uhitaji wa mikopo wamekosa na wale ambao hata hawana uhitaji wa hiyo mikopo wamepata mikopo.

Joyce Ndalichako
Huyu akumbukwe zaidi kwa upande wa makato kupanda kutoka 8% hadi 15% kwa wanafunzi waliochukua mikopo ya vyuo vikuu.

Adolf Mkenda
Huyu wa sasa yeye legasi yake kubwa inaweza kuwa kuundwa kwa tahasusi rasmi za kidini katika elimu ya juu ya sekondari.
 
Prof. Ndalichako alikuwa Waziri bora kabisa wa Elimu. Shukuru Kawambwa sijui aliokotezwa wapi na JK, mzee wa division zero aka BRN.
 
Mkuu hii sio rocket science,jiulize hao uliowataja watoto na wajukuu wao wamesoma wapi? Ukipata jibu ndio utaelewa kulalama humu hakusaidii chochote,super minister ni Jackson Makweta (MHSRIP)wengine wote ni mafisadi na walafi
 
Kwa yule jamaa we ungepinga????

Kipindi kile ilikuaga hakuna namna, mi nlikuaga najua hadi Doroth gwaji ana tatizo la akili kwa mambo aliyokua akifanya chini ya bwana yule. Ila siku hizi ni mtu makini kama sio yeye kabisa
 
Joseph Mungai
Chini ya uongozi wake huyu masomo ya biashara na kilimo yalifutwa kwa baadhi ya shule za sekondari, Physics na Chemistry ikafanywa kuwa kipindi kimoja halafu wizi au uvujishaji wa mitihani ya NECTA ulitamalaki sana.

Shukuru Kawambwa
Huyu chini ya uongozi wake mikopo ya vyuo vikuu ilianza kusuasua na kutolewa kwa vigezo vingi vya ajabu ajabu sana na pia viwango vyenye mkanganyiko mtupu, pia wakati wake ungeweza kukuta wanafunzi wengi tu wenye uhitaji wa mikopo wamekosa na wale ambao hata hawana uhitaji wa hiyo mikopo wamepata mikopo.

Joyce Ndalichako
Huyu akumbukwe zaidi kwa upande wa makato kupanda kutoka 8% hadi 15% kwa wanafunzi waliochukua mikopo ya vyuo vikuu.

Adolf Mkenda
Huyu wa sasa yeye legasi yake kubwa inaweza kuwa kuundwa kwa tahasusi rasmi za kidini katika elimu ya juu ya sekondari.
Ongea yote lakini Ndalichako ndiye waziri bora wa elimu kati ya wote hao uliowataja. Anaweza kuwa na mapungufu yake ktk utendaji lakini alikuwa so objective
 
Joseph Mungai
Chini ya uongozi wake huyu masomo ya biashara na kilimo yalifutwa kwa baadhi ya shule za sekondari, Physics na Chemistry ikafanywa kuwa kipindi kimoja halafu wizi au uvujishaji wa mitihani ya NECTA ulitamalaki sana.

Shukuru Kawambwa
Huyu chini ya uongozi wake mikopo ya vyuo vikuu ilianza kusuasua na kutolewa kwa vigezo vingi vya ajabu ajabu sana na pia viwango vyenye mkanganyiko mtupu, pia wakati wake ungeweza kukuta wanafunzi wengi tu wenye uhitaji wa mikopo wamekosa na wale ambao hata hawana uhitaji wa hiyo mikopo wamepata mikopo.

Joyce Ndalichako
Huyu akumbukwe zaidi kwa upande wa makato kupanda kutoka 8% hadi 15% kwa wanafunzi waliochukua mikopo ya vyuo vikuu.

Adolf Mkenda
Huyu wa sasa yeye legasi yake kubwa inaweza kuwa kuundwa kwa tahasusi rasmi za kidini katika elimu ya juu ya sekondari.
Umesahau wengine mkuu..
HEBU TUCHAMBUE LEGACY ZAO..
Mimi kipindi naanza shule Alikuwa Mweshimiwa Nicholaus Kuhanga

  • OSCAR KAMBONA (1961 - 1962)
  • SOLOMON ELIUFOO(1962 - 1967)
  • CHEDIEL MGONJA (1968 - 1971)
  • REV. SIMON CHIWANGA (1972 - 1974)
  • THABITA SIWALE (1972 - 1974)
  • MHE. THABITA SIWALE (1972 - 1974)
  • NICHOLAUS KUHANGA (1977 - 1982)
  • JACKSON MAKWETA (1983 - 1986)
  • PROF. KIGHOMA MALIMA (1987 - 1988)
  • PROF. PHILEMON SARUNGI (1993 - 1994)
  • PROF. JUMA KAPUYA (1995 - 1999)
  • AMRAN MAYAGILA (1989 - 1990)
  • CHARLES KABEHO (1990 - 1992)
  • BENJAMIN WILLIAM MKAPA (1992 - 1995)
  • MARGRETH SITTA (2005 - 2007)
  • PROF. PETER MSOLLA (2006 - 2008)
 
Joseph Mungai
Chini ya uongozi wake huyu masomo ya biashara na kilimo yalifutwa kwa baadhi ya shule za sekondari, Physics na Chemistry ikafanywa kuwa kipindi kimoja halafu wizi au uvujishaji wa mitihani ya NECTA ulitamalaki sana.

Shukuru Kawambwa
Huyu chini ya uongozi wake mikopo ya vyuo vikuu ilianza kusuasua na kutolewa kwa vigezo vingi vya ajabu ajabu sana na pia viwango vyenye mkanganyiko mtupu, pia wakati wake ungeweza kukuta wanafunzi wengi tu wenye uhitaji wa mikopo wamekosa na wale ambao hata hawana uhitaji wa hiyo mikopo wamepata mikopo.

Joyce Ndalichako
Huyu akumbukwe zaidi kwa upande wa makato kupanda kutoka 8% hadi 15% kwa wanafunzi waliochukua mikopo ya vyuo vikuu.

Adolf Mkenda
Huyu wa sasa yeye legasi yake kubwa inaweza kuwa kuundwa kwa tahasusi rasmi za kidini katika elimu ya juu ya sekondari.
Huyu wa sasa anapokea maelekezo kutoka juu na juu inapokea maelekezo kutoka uarabuni
 
Back
Top Bottom