Picha: Rais Kikwete ashiriki maombolezo ya Regia Mtema

aee.jpg

Nimeongea mara kadhaa kwamba katika itikadi hatuchukii mtu ila matendo ya mtu. Mtu anabaki na haki yake kwa vile hubadilika na utu unaweza kumrudia baada ya kughafirika na kitu fulani. Picha hii inanipa mwono mwingine nikirudi nyuma mwaka mmoja mambo yalivyokuwa yanaendelea baada ya uchaguzi Mkuu.
 
Candid sasa unaelekea kuharibu ile habari nzuri uliyoleta.
Hapa ni mazishini,msibani,maombolezoni au mazikoni?Watu huenda mazishini kwa hali yoyote atakayokua nayo kwa wakati anapopata taarifa.Mazikoni kuna kujitayarisha kimavazi nk
Nahisi wote uliowaona wamevaa usivyopenda wamekurupuka toka makazini,ferry,kanisani na mitaani.Ni wachache sana walikwenda kwanza majumbani kujitayarisha(wa mjini husema 'kujisoap')
Utakapoudhuria maziko ya huyu mpendwa wetu utaelewa na kuona tofauti.
RIP REGIA
 
Chadema kwa kulazimisha mambo.
maaalim ni makamo wa kwanza wa Rais Znz na ana shughuli nyingi za kitaifa.
Pasi na shaka CUF wataongozwa na Mtatiro, Naibu wake bara.

Na Hamad Rashid atakuwepo pia. Kwani yeye anashinda pale Habari maelezo Dar

Aksante katibu muhtasi wa Maalim Seif!! Bila shaka hata diary yake unaitunza wewe na una orodha ya kazi alizonazo unaijua wewe. Pia kumbe hata JK Pinda na wengineo walijua kuwa Jana wangekuwa Msibani na walishapanga hayo kwenye diary zao. Think LOUD men!! Kwani kuchangia humu ni lazima hata kama unaona huna hoja bali vumbi tuu!!

:focus:
Rest In Eternal Peace our beloved sister! Amen!!
 
aee.jpg

Nimeongea mara kadhaa kwamba katika itikadi hatuchukii mtu ila matendo ya mtu. Mtu anabaki na haki yake kwa vile hubadilika na utu unaweza kumrudia baada ya kughafirika na kitu fulani. Picha hii inanipa mwono mwingine nikirudi nyuma mwaka mmoja mambo yalivyokuwa yanaendelea baada ya uchaguzi Mkuu.

mkuu naona kama huu msiba umekuchanganya sana....nakushauri ukae utulie uomboleze salama......tuliza hisia zako na hisia zako zisikutume katika kufikira mambo ya kisiasa zaid hasa uwaonapo wanasiasa wamejumuika pamoja msibani.....maana naona kama kuna shida flani imekupata
 
Picha hizi sijazipenda kweye maombolezo ya hayati dada yetu Rigia Mtema
r+b.jpg
r+7.jpg
at+3.jpg

Najua wengi hapa watanifutulia macho, lakini watanzania tunatakiwa tuwe na upeo wa kutambua na kuchanganua nafasi za matukio. Hapa si masuala ya chama, ni msiba ambao unatuhusu watanzania wote. Alivyovaa Freeman Mbowe safi kabisa ni vazi la msiba. Picha ya kikwete unamwona kijana kwa mbali na pendera ya Chadema kajifungia huu ni mtazamo finyu, hapa ni msiba wetu sote.

Hali kadhalika Dr. Slaa anatakiwa awe na mabadiliko ya mivao kutofautisha nafasi kama hizi. Vazi hilo hilo ofisini, msibani, kanisani, hotelini nk. hapana, nitaendelea kutoa somo hadi tutakapokuwa mstari mmoja.

Wivu wa kike. RIP Regia!!!
 
katika kitu ambacho kimenifurahisha ktk msiba huu,ni jinsi wabunge na wananchi walivyoweka pembeni utofauti wao wa vyama,tumekuwa wamoja pasi shaka kuwa kama mwelekeo huu ungekuwa hata ktk maswala ya maendeleo basi Tz tungekuwa mbari
Nawapongeza watz na tutambue kuwa wtz kama ukifanya jema watakuunga mkono,ebu oneni msiba huu ulivyo gusa hisia za wengi,msiba umeunganisha nyoyo za akina engmtolera, maleria sugu,faiza na wanaCDM,CUF CCM, safi sana huu ndio umoja tunao utaka

tuzidi kumwombea mpiganaji mwenzetu popote pale alipo kwa wakati huu
 
Heshima mbele kiongozi, Thanx alot kwa updates za picha and even your comments upon what we shoud dress on sympathetic occassion like that.
My question ni kweli Dr. Slaa na Dr Kikwete wanakwepana ama hukufanikiwa kupata picha yao ya pamoja? Kwa ufahamu wangu sehemu kama hiyo tofauti za kiitikadi na mtazamo wa kisiasa ama uongozi huwekwa pembeni.
Mhn!

I can just speculate kuwa Dr Slaa anaamini kabisa kuwa Dr Kikwete stole the elections.
 
Aksante katibu muhtasi wa Maalim Seif!! Bila shaka hata diary yake unaitunza wewe na una orodha ya kazi alizonazo unaijua wewe. Pia kumbe hata JK Pinda na wengineo walijua kuwa Jana wangekuwa Msibani na walishapanga hayo kwenye diary zao. Think LOUD men!! Kwani kuchangia humu ni lazima hata kama unaona huna hoja bali vumbi tuu!!

:focus:
Rest In Eternal Peace our beloved sister! Amen!!

Ahali yangu.

Kumbuka si lazima kwa viongozi wote wa Serikali kuhudhulia msiba huo. Kumbuka Bi Regia alikuwa mbunge tu na si waziri katika Serikali na kuwa Bunge ndilo linahusika na maziko yake lakini sio Serikali.

Kumbuka kuwa Bunge ni muhimili unaojitegemea kama ilivyo Serikali au Mahakama.

Sasa wahusika wakuu hapo ni Bunge na watendaji wake na sio Serikali. Sasa usilazimishe viongozi wa kitaifa Znz waje wahudhulie msiba huo.

Tusifikiri kuwa Bi Regia alikuwa waziri au mtendaji mkuu wa Seikali iliyoko madarakani. Jifunze mbunge ni nani na mipaka yake utalijua ninalonena.

Picha hizi sijazipenda kweye maombolezo ya hayati dada yetu Rigia Mtema
r+b.jpg
r+7.jpg
at+3.jpg

Najua wengi hapa watanifutulia macho, lakini watanzania tunatakiwa tuwe na upeo wa kutambua na kuchanganua nafasi za matukio. Hapa si masuala ya chama, ni msiba ambao unatuhusu watanzania wote. Alivyovaa Freeman Mbowe safi kabisa ni vazi la msiba. Picha ya kikwete unamwona kijana kwa mbali na pendera ya Chadema kajifungia huu ni mtazamo finyu, hapa ni msiba wetu sote.

Hali kadhalika Dr. Slaa anatakiwa awe na mabadiliko ya mivao kutofautisha nafasi kama hizi. Vazi hilo hilo ofisini, msibani, kanisani, hotelini nk. hapana, nitaendelea kutoa somo hadi tutakapokuwa mstari mmoja.

Hapa nakuunga Mkono kabisa mdau. Basi na Nape na JK wangeingia na kijani na njano si pasingetosha...all in all RIP Regia
 
DSN, natumia kamchina, nitadadavua maandiko nikikaa kwenye pc kuzijibu hoja zako. ingawa umekimbia swali umejitutumua sana kujaribu kumvisha utukufu kikwete ambaye damu za watu zamlilia kuzimu, wakiwemo waliopigwa risasi arusha, wafao kwa kemikali inayotiririshwa na washkaji wa kikwete kwenye mto tigite, wanaokufa kwa kukosa huduma stahiki mahospitalini au kwa kukatika umeme na tiba kuchelewa, mpaka twiga wanamlaani kikwete, kahudhuria msibani ghafla kawa malaika? hujanishawishi bado! nauliza swali tena, P. W. BOTHA, wakati wa zama zake, akihudhuria maziko ya mpigania uhuru wa ANC aliyekufa kwa malaria kwenye kambi ya mazimbu, itamfanya awe mtaifa sanaaaa na kumuondolea ukaburu????
 
mkuu naona kama huu msiba umekuchanganya sana....nakushauri ukae utulie uomboleze salama......tuliza hisia zako na hisia zako zisikutume katika kufikira mambo ya kisiasa zaid hasa uwaonapo wanasiasa wamejumuika pamoja msibani.....maana naona kama kuna shida flani imekupata

Kama umeshawahi kuhudhuria misiba na maombolezo ya misiba, watu hatuzungumzii mkasa uliotokea kupoteza maisha ya mpendwa wetu tu, tunakuwa na mengi ya kuongelea kupoza machungu, na katika nafasi hizi tunajadili mengi yanayojilia kwani aliyetukutanisha katika safu hii na katika maombolezo haya ni dada yetu mpeendwa Rigia Mtema. Mwenyezi Mungu ampunmzishe katika amani milele.

Dada Regia sasa yuko nyumbani kwa baba wa milele na kama angali njiani akisubiri kufunguliwa mlango, tuelekeze sala zetu za maombi kwa nguvu na zile sala za mishale amalize adhabu anazostahili na kupata rehema kamili, kisha Malaika afungue mlango kumkaribisha nyumbani kwa Baba wa milele. Amen
 
kumbe unapoza machungu!!!! kwenye maandishi ya zamabaru hapo sasa naona kweli unaomboleza.....
 
DSN, natumia kamchina, nitadadavua maandiko nikikaa kwenye pc kuzijibu hoja zako. ingawa umekimbia swali umejitutumua sana kujaribu kumvisha utukufu kikwete ambaye damu za watu zamlilia kuzimu, wakiwemo waliopigwa risasi arusha, wafao kwa kemikali inayotiririshwa na washkaji wa kikwete kwenye mto tigite, wanaokufa kwa kukosa huduma stahiki mahospitalini au kwa kukatika umeme na tiba kuchelewa, mpaka twiga wanamlaani kikwete, kahudhuria msibani ghafla kawa malaika? hujanishawishi bado! nauliza swali tena, P. W. BOTHA, wakati wa zama zake, akihudhuria maziko ya mpigania uhuru wa ANC aliyekufa kwa malaria kwenye kambi ya mazimbu, itamfanya awe mtaifa sanaaaa na kumuondolea ukaburu????

Botha na ukatili wake wote Mandera na Power yote aliyokuja kupata baada ya kifungo alikuwa na uwezo wa kuwanyonga na kuwafunga watesaji na wauaji wote wa vifo vya soweto na vinginevyo vilivyofanyika wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Lakini kwa kuwa Mandera ni mwamini Mungu alichofanya alimpa Askofu desmond Tutu umwenyekiti wa kitu kinaaitwa kamati ya maridhiano [RECONCILIATION COMMITEE] huko alichokifanya desmond tutu ni kuakikisha wale wote waliokuwa watesaji na wauaji kwa niaba ya utawala wa kibaguzi wanakaaa meza moja kuomba msamaha kwa wale wote waliohai na kwa ndugu za walikokufa kwa matokeo ya matendo ya kidhalimu ya kikaburu walio wafanyia mateso hayo.Na watendaji wa matokeo hayo hawakuwa makaburu kwa rangi bali pia baadhi ya weusi nao walitumika na utawala huo.

Kwenye kamati hiyo ya maridhiano kama ulibaatiika kuiona,nashukuru nyumbani nilibahatika kuiona kila siku kupitia DSTV,it was a painful moment sana kwa pande mbili mtesaji na mteswaji, na mbaya sana mteswaji kwa kuwa yeye kwake ni kukumbuka machungu aliyoyapata kwa kupoteza ndugu, rafiki na jamaa na pia kwa yeye binafsi kupitia matesoa yale kwa upande wa pili ilikuwa ni kilio kisicho na mwisho.Kama ungebahatika kuwaoana ama kweli mwisho wa ubaya ni aibu,na mbaya sna kuwa kama tunaamini kuna Mungu je siku ya hukumu utamjibu nini.

Mwisho wa yote Baba wa Taifa la South africa Mzee Madiba aka Mandera akawasamehe kwa niaba ya Taifa, kama walisamehewa na na kiongozi aliyepitia machungu makubwa kwa kufungwa miaka 27 hivi bado ujajua kuwa Mungu anafanya kazi in a mysterious way,hivyo muache Mungu aitwe Mungu.Wanafalsafa wa sasa duniani wanasema a true judgement ambayo ndiyo itatawala duniani katika siku zijazo huko mbele,ni pale mkosewaji anapo ombwa msamaha na mkoseaji with a true and sincearity from the hurt yani honestly basi, mkosewaji akishasema napokea msamaha wa matendo yako basi hiyo ndiyo hukumu ya Mungu juu yako wewe mkosaji,na sio hizi zetu za kidunia za kufungana Jera na kutoana roho, kwa kuibiana simu ya mchina hata kama kwa kuibiwa mke.

Regia R.I.P
 
Botha na ukatili wake wote Mandera na Power yote aliyokuja kupata baada ya kifungo alikuwa na uwezo wa kuwanyonga na kuwafunga watesaji na wauaji wote wa vifo vya soweto na vinginevyo vilivyofanyika wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Lakini kwa kuwa Mandera ni mwamini Mungu alichofanya alimpa Askofu desmond Tutu umwenyekiti wa kitu kinaaitwa kamati ya maridhiano [RECONCILIATION COMMITEE] huko alichokifanya desmond tutu ni kuakikisha wale wote waliokuwa watesaji na wauaji kwa niaba ya utawala wa kibaguzi wanakaaa meza moja kuomba msamaha kwa wale wote waliohai na kwa ndugu za walikokufa kwa matokeo ya matendo ya kidhalimu ya kikaburu walio wafanyia mateso hayo.Na watendaji wa matokeo hayo hawakuwa makaburu kwa rangi bali pia baadhi ya weusi nao walitumika na utawala huo.

Kwenye kamati hiyo ya maridhiano kama ulibaatiika kuiona,nashukuru nyumbani nilibahatika kuiona kila siku kupitia DSTV,it was a painful moment sana kwa pande mbili mtesaji na mteswaji, na mbaya sana mteswaji kwa kuwa yeye kwake ni kukumbuka machungu aliyoyapata kwa kupoteza ndugu, rafiki na jamaa na pia kwa yeye binafsi kupitia matesoa yale kwa upande wa pili ilikuwa ni kilio kisicho na mwisho.Kama ungebahatika kuwaoana ama kweli mwisho wa ubaya ni aibu,na mbaya sna kuwa kama tunaamini kuna Mungu je siku ya hukumu utamjibu nini.

Mwisho wa yote Baba wa Taifa la South africa Mzee Madiba aka Mandera akawasamehe kwa niaba ya Taifa, kama walisamehewa na na kiongozi aliyepitia machungu makubwa kwa kufungwa miaka 27 hivi bado ujajua kuwa Mungu anafanya kazi in a mysterious way,hivyo muache Mungu aitwe Mungu.Wanafalsafa wa sasa duniani wanasema a true judgement ambayo ndiyo itatawala duniani katika siku zijazo huko mbele,ni pale mkosewaji anapo ombwa msamaha na mkoseaji with a true and sincearity from the hurt yani honestly basi, mkosewaji akishasema napokea msamaha wa matendo yako basi hiyo ndiyo hukumu ya Mungu juu yako wewe mkosaji,na sio hizi zetu za kidunia za kufungana Jera na kutoana roho.

Una kiwango cha juu katika mwono wako, u mtume wa kuigwa, hii ni falsafa adimu sana kwa wengi.

Nimekupata na umenipata kwa undani kabisa, ndiyo tunayotaka si visa. Binadamu hubadilika kitabia na matendo kuendana na msukumo wa wakati na mazingira, na hata yaliyojilia ni matokeo ya wakati na yatapita.

Huwezi Jua safari za Clinton na Bush wamemshauri vipi na unaweza kuanza kuona dalili kwa mbali.
 
Back
Top Bottom