(PICHA) Mwakyembe: Mjadala wa AFYA yangu UMEFUNGWA 'FULL STOP'

mkuu wangu sikubaliana na mtazamo wako wa kutaka kutetea na kulinda ujinga,majungu,chuki,fitina na uchonganishi ktk jamii! huyu jamaa yako hafai kubakia ktk ofisi ya umma kwasababu kuna siku atakuja singizia wafanyakazi wengine kwamba wamemwekea sumu ama wanapanga njama za kumuua! ni mtu hatari kwa umoja na mshikamano wetu kama taifa!
Nasikitika kuwa unaliona tatizo hili kwa msimamo wa kuweka miguu juu ya stuli na kuagiza pop corn ili kuangalia the next episode.
Ni mtu wa mawazo ya kijinga tu asiyewe na upeo wa kuona hapo kuwa kombe limefunikwa ili wanaharamu wapite, na wewe ukiwa mmoja wapo.
Kama tatizo lina wakanganya hata vigogo wa serikali na kuishia kutoa taarifa zinazo kinzana, than I am at loss to understand your sense of reasoning.
 
Sasa ivi anadai amepona na mjadala umefungwa. Sawa aendelee tu kuwalinda hao waliotaka kumuua asije tena baada ya mwezi moja ooh waliotaka kuniua wameanza tena. Aendelee ivyo ivyo kama alivyowaficha wezi wakuu wa Ritchmond. Ila historia itamhukumu ngoja tuone
 
Hakika kwa wanaokumbuka hadithi ya mtoto mtukutu aliyekuwa anatoka nje kidogo ya kijiji na kupanda kwenye jiwe la kilimani nje ya kijiji chao na kupiga kelele iliyoleta mwangi wa sauti kijijini inayosikika ikisema "imweeeeeeeee Jamani Chui,Nafwaaaaaaaaaaa Jamani Chui !!!!!!!!!!!" hakika wanakijiji kila mmoja na rungu,panga,gobole hao mbio kuelekea eneo inakotoka sauti,wakifika cha kustaajabu wanamkuta kijana wao kijana wa kijijini mtoto wa Mwanakijiji mwenzao amekaa juu ya jiwe anawacheka.Kila Mwanakijiji anaanza kunungunika na panga lake mkononi wanalalamika upunguani wa kijana huyo wa kijijini kwao, kwa kuwa na kelele zote hizo hakuna chui wala chochote kinachodhuru kijana huyo bali ananchofanya ni mchezo mbaya wa dhaihaka kwa jamii yake.

Siku ya siku toto tukutuku limeelekea kwenye jiwe lile kama kawaida yake kufika huko kweli bahati mbaya kakumbana na chui wa kweli,akaanza kupiga kelele kama kawaida,hakika kama kawaida wanaanchi kwa kujua ni lile toto tukutu hakuna alie inua mguu kwenda popote zaidi kila mmoja aliendelea na shughuri zake.Ilipofika jioni mzazi wa mtoto tukutu alishaanga kutomuona mtoto wake akaenda kutoa taarifa kwa mjumbe kisha mjumbe akapiga mbiu kumsaka mtoto tukutu yaliyojili ni kukuta mabaki ya mwili wa toto tukutu.

Lugha aliyotumia Mwakyembe kutengeneza propaganda ili ajiwekee mazingira binafsi wakati anajua alishaualika umma kwenye jambo lake kutoka kuwa lake binafsi na kuwa la umma liliitaji umakini sana na si kama hivi alivyopanga ama walivyopanga,iliitajika elimu ya ufahamu wa umma kubwa sana.Uzuri wa jambo ili ni kuwa IMEKULA KWA MWAKYEMBE NA WALE ALIOJENGA MAZINGIRA UMMA UKAWAWEKEA TUHUMA SASA WAMEPATA MTELEMKO KAZI KWAKE, WANANCHI SASA WATAWASUPPORT IKIBIDI KUMFIKISHA MAHAKAMANI KUPITIA BARUA YAKE.
 
Huyu Dr. Mwakyembe ni mtu wa kuogopwa maana anazo sura mbili.
Tangu alipotoa ripoti ya Richmond bungeni na kuficha taarifa nyingine alionekana hafai machoni mwa wengi kuficha ukweli ulioonekana. Alipoumwa marafiki, jamaa zake wamehangaika sana kuhakikisha anapata nafuu ya kuumwa naye jana kawatosa.
Kawafedhehesha hata waliokuwa wanamuombea apone ili aseme amepatwa na masaibu gani kumbe mambo yake ni hayo, inawezekana kapewa kitu kidogo ili anyamaze, kwetu tunasema YAITWA KAKE NKE'MBEBA yaani amedanganywa na chambo kama panya
 
au PhD yake ni ya American International University kama ya Makongoro Mahanga?
 
Asa mbona alitafuta sana sympathy yetu watanzania kipindi afya yake ilipoyumba? Magamba bwana!
UMEONA EE UZUSHI MTUPU ,ALAFU KUMBE GONJWA LIPO WAZI KABISAA,nxt akiigua mwingine tutafakari kabla ya kushabikia alafu badae eti unatuambia FULLSTOP.
 
Unajua ile sumu aliyopewa mh. Mwakyembe ilikuwa kali mno na huenda imeingia hadi kwenye ubongo ndiyo maana anapingana na kauli zake mwenyewe, rafiki yake sitta na wale wote waliokuwa wanampigania! Msameheni bure jamani siyo yeye bali ni nguvu ya sumu. Mwakyembe kama yeye bila sumu ndani yake ni mtu mzuri na mwungwana.
 
akienda india tena itabibidi arudishe pesa zetu tuliokuwa tunampa akatibiwe kumbe bora ange-ku-f-a kabisa mnafiki huyu
 
Ninawasi wasi sana kama unajua unachokisema.

Fanya tena utafiti Mkuu.

Kwa kweli huyu ndugu ni mnafiki sana,kabla ya kuanza kuugua alitoa report/ttaarifa ya kutaka kuuawa na al shaabab,baada ya kuugua ndio akazidi kubwabwaja pasipo maelezo yoyote yenye rutuba na sasa ndio amekuja na hitimisho la unafiki. Najiuliza:
1) Mwanzo mara zote alikuwa anatoa tuhuma kwa uuma ili iweje kama sio unafiki wa kutoiamini serikali na kutaka huruma ya wananchi??
1)ikiwa mda wote huo amekuwa akitibiwa kwa kutumia kodi za wavuja jasho la wananchi (bare in mind wabunge hawakatwi kodi mishahara yao na masurufu yao kibao wakati hatamfagizi wa ofisi ya umma/binfsi anakatwa kodi), kwa nini wananchi wasipewe taarifa ya sababu na matokeo ya kodi yao??
3) anaendelea kufanya kazi kwa ufanisi upi ikiwa alisema mwenyewe alilishwa sumu ofisini?? Ana uhakika gani wa kutokumbana tena na matatzo ya usalama ikiwa hana imani na kina Manumba??
4) Katika hili kwa nini tu asishitakiwe na kina Manumba,yeye na Sita wake kwa kutoa kauli za kuhatarisha na kuichonganisha serikali/polisi na umma!!

Mwakiembe ni mnafiki na mchumia tumbo!!!
 
Wana JF,
Yaliyo sirini mwa mwakyembe anayajua mwenyewe. Ila kama hatapasua bomu kama alivyowahi kutuahidi atakapohitaji huruma yetu mambo yakimchachia hataipata.

Watakachofanya polisi ni kuchakachua taarifa ya madaktari waliomtibu.Uamuzi ni wake.
 
KJM joto kwako gari full ac na kwa ofisi full AC joto litatoka wapi?
Kama kweli umepona tunashukuru!
 
teh politics is wat we tanzania are really experiencing. ivi yeye kusema mjadala umefungwa manake nini? In tz ndo nchi pekee inayofikiri wananchi ni mbumbumbu sana. yaaani kama huyu huyu ndo aliekuwa analalamikia uhuni aliofanyiwa leo hii haki yake kaipatia wapi? NI WACHACHE SANA IVI TUNAOFAHAMU KUWA LOWASSA NA MWAKYEMBE WALIKUTA LONDON MWANZONI MWA MWEZI HUU BAADA YA LOWASSA KUTOKA UJERUMANI NA MWAKYEMBE KUTOKA INDIA ATUAMBIE KIKAO CHAO WALIJADILI NINI PASIPO KUMTAJA MTU ALIYE WAKUTANISHA..... WA?????????? TANZANIA INAPOELEKEA TUKAE MKAO WA KUKIMBIA INCHI COZ TIME YA KUSEMA ENOUGH IS ENOUGH INAAPROACH MNOOOOO... ANYWAY UMRI WANGU UNANIRUHUSU KUENDELEA KUSHUHUDIA MENGI KWA NEEMA YA MUNGU, KANAANI NITAINGIA.
 
Kama Mungu angekuwa Osama George Bush sijui angefanywaje; kama Mungu angekuwa George Bush Osama sijui ingekuwaje?.......Haraka zenu ziacheni mwacheni Dr. Mwakyembe akabidhi kesi yake kwake mtoa haki ya kweli uone atakavyomtetea!
 
Back
Top Bottom