(PICHA) Mwakyembe: Mjadala wa AFYA yangu UMEFUNGWA 'FULL STOP'

Mwakyembe: Jamani imetosha
Imeandikwa na Halima Mlacha (Habarileo); Tarehe: 19th March 2012

[TR]
[TD]

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe, amerejea rasmi ofisini na kuanza kazi huku akivitaka vyombo vya habari nchini kuachana na suala la ugonjwa wake, akisema sasa imetosha.

Waziri huyo alikaa nje ya ofisi kwa takribani miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa ngozi unaodaiwa kupukutisha ngozi yake na kukimbizwa India kwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuingia ofisini kwake, Dar es Salaam jana, Dk. Mwakyembe alisema hali yake sasa inaendelea vizuri na ndiyo maana amerejea kazini.

"Naomba nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa nilikuwa naumwa kwa muda mrefu ugonjwa uliojulikana kitaalamu baada ya vipimo kama Populia Thrulema yaani matatizo ya ngozi, lakini sasa naendelea vizuri," alisema Dk. Mwakyembe ambaye alionekana mchangamfu huku akiwa bila glovu mikononi kama ilivyozoeleka tangu aanze kuugua.

Awali akiwasili eneo la ofisi za Wizara ya Ujenzi, alikutana na kundi la waandishi wa habari hali iliyomfanya ashuke haraka kwenye gari na kuingia ndani kwa mwendo wa kasi sana, huku akiishia kuwasalimia waandishi hao na kupanda ngazi akikimbia.

Alirejea nchini Jumamosi kutoka India. Hata hivyo, baadaye alipozungumza na waandishi hao, aliviomba vyombo vya habari vipumzike kuandika na kuchokonoa kuhusu ugonjwa wake na badala yake waiachie Serikali ambayo imeunda tume kuchunguza chanzo cha ugonjwa huo, ikamilishe uchunguzi wake.

"Naomba jamani sasa ugonjwa wa Mwakyembe ufike mwisho kuandikwa. Watu walitarajia na kusubiri mengine, lakini nawaambia mliotaka kuandika vichwa vya habari vya kifo changu mjue tafadhali niko hapa sijafa, naomba yaishe sasa," alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema alipokuwa India kwa mara ya pili kuendelea na matibabu, alitaarifiwa kuwa suala la utata wa ugonjwa wake kuwa ama amelishwa sumu au la, limeundiwa timu na Serikali ambayo Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na polisi wamo ndani yake.

Alisema sasa suala hilo anamwachia Mungu na Serikali inayolichunguza, ambapo alikataa kuzungumzia zaidi kwa nini anahisi alilishwa sumu. "Hili mnalolihoji nitalizungumza kwenye timu hiyo itakayokuja kunihoji, nawashauri muwe na subira ikikamilisha uchunguzi wake, itasema na hata mimi nitasema."

Kuhusu ugonjwa huo alisema ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuuelewa, ingawa alivyopimwa India baada ya uchunguzi, aligundulika kuwa na tatizo hilo la ngozi. Aliishukuru Serikali na hasa Rais Jakaya Kikwete aliyemtembelea nyumbani kwake na kushuhudia hali ilivyokuwa na kushinikiza apewe matibabu haraka na Serikali upande wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kufanikisha safari yake ya India ambako alitibiwa na sasa anaendelea vizuri.

Aidha, alimshukuru Waziri wa Ujenzi, John Magufuli na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Herbert Mrango, kwa kufanya kazi katika kipindi chote alichokuwa peke yake. "Lakini pia nawashukuru Watanzania na wananchi wa Kyela kwa maombi yao na subira katika kipindi ambacho nilikuwa sipo, na Kyela nilisikia wanataka kuandamana kujua hali yangu, nawaomba wasiandamane kwani nimesharudi na nitakwenda huko nikimaliza mzigo wa kazi unaonisubiri," alisisitiza.

Awali Dk. Mwakyembe alidaiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaomsababishia uvimbe katika baadhi ya maeneo mwilini na kitaalamu ugonjwa huo unajulikana kama Exfoliative Dermatitis.

Ugonjwa huo unadaiwa kuathiri wanaume na wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 55 na dalili zake ni kuwashwa, mwili kuishiwa nguvu na sehemu ya juu ya ngozi kupukutika.

Dk. Mwakyembe alikwenda kutibiwa mara mbili katika Hospitali ya Apollo ya nchini India kwa ajili ya matibabu kufuatia hali yake kuzidi kuwa tete na alirejea nchini hivi karibuni huku akionekana kuwa katika hali nzuri na kuripoti ofisini jana saa 3.40 asubuhi.
[/TD]
[/TR]
 
anaweza sana tukimuunga mkono na kuandaa akina mwakyembe wengine wengi,wewe ukiwamo

Anaweza sana kitu gani? tumuunge mkono kwa lipi? kuandaa mwakyembe wengine? hapana, one mwakyembe is already one too many, mimi simo! Hivi Dr. Mwakyembe anapigania nini vile na ili iweje. Uwanja wa Arumeru umezidi kutufungua macho, ama uko nao au hauko nao, wanafiki hawana nafasi tena katika mabadiliko tunayoyatafuta. If you cant fight them, join them na Mwakyembe amekubali yaishe na sasa ameungana nao na kuweka silaha, kama kweli alikuwa nayo, chini. Kama huamini kamuulize Nape.
 
Hiyo ni kuzima moto wa kuzongwa na waandishi wa habari cz nchi hii journalist wamekuwa mahakimu wa kesi zinazofanana na hizo baada ya mahakama kutawaliwa na magamba!
 
Ngonjela za huyu mgonjwa hazijawahi kuwa na tija katika mijadala ya Tz tunayoitaka!
Tusipotezeane mida kutaka kufanya vita za maslahi binafsi katika kundi (chama) eti ionekane ni vita ya kitaifa.

Hivi hebu na mtueleze huyu jamaa mapambano yake yalikuwaje kabla ya mchakato wa uchaguzi wa ccm wa mwaka 2005?
Vp pia alikuwa ni kamanda wa kupinga ufisadi??
Au ndio tusahau yaliyopita?
 
Anaweza sana kitu gani? tumuunge mkono kwa lipi? kuandaa mwakyembe wengine? hapana, one mwakyembe is already one too many, mimi simo! Hivi Dr. Mwakyembe anapigania nini vile na ili iweje. Uwanja wa Arumeru umezidi kutufungua macho, ama uko nao au hauko nao, wanafiki hawana nafasi tena katika mabadiliko tunayoyatafuta. If you cant fight them, join them na Mwakyembe amekubali yaishe na sasa ameungana nao na kuweka silaha, kama kweli alikuwa nayo, chini. Kama huamini kamuulize Nape.

Mkuu Mag, wanataka kujua upepo unapotoka waufuate!
Lol
 
strategically Mwakyembe anaweza kupigana na magamba na wengi tunamshukuru kwa kufanikisha kuweka wazi maswala mengi yawahusuyo magamba! safari bado ni ndefu congrtln for nice job brother!
 
Nimejizuia nisimtukane! siku atakapolalamika nitamkogesha matusi hata kama anachunguli kaburi!!!!! hivi? kuwatumikia wananchi ni lazima uwe kwenye serikali ya kikwete? nayahifadhi hayo matusi kwa siku aliyoiandaa muumba tukijaaliwa
 
strategically Mwakyembe anaweza kupigana na magamba na wengi tunamshukuru kwa kufanikisha kuweka wazi maswala mengi yawahusuyo magamba! safari bado ni ndefu congrtln for nice job brother!
 
Tangu napata akili timamu ikitokea jambo lina utata na ukweli ndani yake utasikia viongozi wa nchi hii ya Wadanganyika Mjadala ufungwe usiongelewe kokote WHY, KWANINi? Kuna nini nyuma ya pazia

Ni kwa kuwa Wadanganyika hatujui haki zetu? Au sheria zilizopo mkubwa akiongea hakuna wa kuhoji kama serikali ya kikolini na si ua kidemokrasia.

Kwa mfano;

Mjadala wa Balali, richmond, kifo cha Nyerere, kiwira, meremeta nk cha ajabu hata Marehemu mtarajiwa Dr. Mwakyembe nae kafanya yaleyale.

Ipo siku tuseme INATOSHA SASA
 
Wakati nyie mwamnanga Mwakyembe, mie nawananga nyie ambao mlikubali kushikiwa akili zenu na kuchezeshwa ngoma msiyoijua na Msanii Samwel Sitta!! Msanii bila ya aibu, aliuambia umma kwamba madaktari wamethibitisha kwamba Mwakyembe amelishwa sumu! Hapo hapo, akataja sababu zake (Sitta) nne za kuthibitisha kwamba Sitta amelishwa sumu!!! Kama sio usanii tuite nini? Yaani tayari kuna scientific evidence kwamba Mwakyembe amelishwa sumu. Wewe unatoa imaginative evidence kuonesha kwamba Mwakyembe amelishwa sumu! Sasa kama kweli kulikuwa na scientific evidence kwamba Dr amelishwa sumu kulikuwa na sababu gani tena ya kutoa imaginative evidence?! Nilishasema awali, kama mtua anatoa vigenzo visivyo vya kisayansi ku-support scientific evidence, basi lazima kutakua na mkanganyiko kati ya hizo scientific evidence na uhalisia! Mathalani, Mwanariadha Samenya alipkuja kuleta utata juu ya jinsia yake ni kwavile kulikuwa na mkanganyiko juu ya uwezo wa jinsia ya kike na uwezo wake ktk riadha! Kila mtu anafahamu Dr Mwakyembe ni mwanaume! Sasa pakitokea mtu akataja sababu kadhaa za kuthibitisha kwamba Mwakyembe ni mwanaume, basi ujue jinsia yake hiyo haiendani na hali halisi ya uanaume! Tusema, anapaka poda, shedo, anabana sauti, anavaa nguo za kike, anatembea kwa maringo, na mambo yote ya kike! Hapo lazima atokee mtu atoe sababu zingine kuthibitisha kwamba, pamoja na yote hayo, huyo mtu ni mwanaume.....!! Hivyo basi, suala la Sitta kutoa sababu za kuthibitisha ulishwaji sumu, inaonesha wazi kwamba palikuwa na mkanganyiko wa hicho alichoita kwamba Madaktari wamethibitisha vinginevyo hapakuwa na haja!! Tafsiri rahis ni kwamba, pamoja na kwamba ripoti haioneshi kupewa sumu lazima tu atakuwa amepewa sumu, na anayebisha basi azi-digest sababu zilizotolewa na Sitta!!! Kama Sitta alifikia kutamka wazi wazi kwamba Mwakyembe amelishwa sumu kutokana na ripoti ya madaktari; alishindwa nini kuitoa hadharani ripoti hiyo?! Jibu simpo tu, hiyo ripoti inayosema hivyo, hakuiona!
 
Mkuu hiyo ni ngonjera, mashairi au taarabu!!
 
Na sasa turudi kwenye huo upambanaji tunaoshawishiwa kwamba Mwakyembe ni mpambanaji anayewasaliti Watanzania kwa kutosema ukweli! Hivi ni upambanaji gani ambao mnaosifia? Ni ule wa Sakata la Richmond? Kwani Sakata la Richmond aliibua Mwakyembe?! Amfahamu role ya Mwakyembe kwenye lile sakata au mnajifanya hamnazo?! TUKUMBUSHANE! Mwakyembe si kwamba ndie aliibua Sakata la Richmond! Role ya Mwakyembe pale ilikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ambayo iliundwa kuchunguza sakata lile! Na kama nitakumbuka vizuri (correct me if am wrong), yeye hakuwamo kwenye lile jopo ambalo lilienda Marekani. Hivyo basi, baada ya kamati kuwa tayari imeshakamalisha uchunguzi, Mwakyembe kama Mwenyekiti wa Kamati akawa na role ya kuisoma ripoti ile bungeni! PERIOD! Na kwavile ripoti ile alikuwa anaisoma kwa mbembwe kwelikweli; ikaja kuonekana ni kama ufichuaji ule ulifanywa na Mwakyembe! Na kimsingi, kitu ambacho kilitokea ni kama mchezo wa filamu! Chachu kuu ya utamu wa filamu ni mwandishi wa story, script, director. Hata hivyo, kila siku Mcheza filamu ndie anaonekana ni shujaa na mwerevu kupita wote hao ingawaje kimsingi yeye anakuwa tu ameelekezwa "fanya hivi, fanya vile!" Na hapa ndipo anapokuja kuonekana Mwakyembe ni shujaa kwenye filamu ile….!! Na kwa bahati, Mwakyembe ni mjanja sana! Ripoti ile ikamtoa kisiasa! Makamu wake, Selelii akajaribu kutoka kupitia ripoti ile; hata hivyo alishindwa, may be tayari stelling wa mchezo alimzidi kwa kila kitu.
 
amwambie mshkaji wake sita e nae aache kuropoka,wakienda kawe wasali tu,sio washike mic
 
Hapa mwakyembe akiwasili kwa nguvu zote

DSC_0043.JPG

Hapo mwakyembe akielekea ofisini

DSC_0087.JPG

Mwakyembe akiongea na waandishi wa Habari na kunena kuwa mjadala
umefungwa full stop hakuna mtu kujadili tena afya yake inaendelea vizuri
DSC_0081.JPG

Anyway, tumshukuru Muumba siku za maisha yetu hapa duniani. Nimeumia sana kwani kazeeka ghafla na ninavyomwona hakika hajapona, naye anakiri kuwa "anaendelea vizuri"
 
Hapa mwakyembe akiwasili kwa nguvu zote

DSC_0043.JPG

Hapo mwakyembe akielekea ofisini

DSC_0087.JPG

Mwakyembe akiongea na waandishi wa Habari na kunena kuwa mjadala
umefungwa full stop hakuna mtu kujadili tena afya yake inaendelea vizuri
DSC_0081.JPG

Safi sana Mwakyembe, Kweli wewe Mwanasiasa aliyekubuhu. Wachonga midomo wote kimya sasa.
 
Back
Top Bottom