(PICHA) Mwakyembe: Mjadala wa AFYA yangu UMEFUNGWA 'FULL STOP'

Kuna mambo mawaili tu nayaona kwa Mwakyembe.
Ama ni mnafiki kiasi cha kutisha au ubongo umeathirika kiasi cha kutisha.
 
teh politics is wat we tanzania are really experiencing. ivi yeye kusema mjadala umefungwa manake nini? In tz ndo nchi pekee inayofikiri wananchi ni mbumbumbu sana. yaaani kama huyu huyu ndo aliekuwa analalamikia uhuni aliofanyiwa leo hii haki yake kaipatia wapi? NI WACHACHE SANA IVI TUNAOFAHAMU KUWA LOWASSA NA MWAKYEMBE WALIKUTA LONDON MWANZONI MWA MWEZI HUU BAADA YA LOWASSA KUTOKA UJERUMANI NA MWAKYEMBE KUTOKA INDIA ATUAMBIE KIKAO CHAO WALIJADILI NINI PASIPO KUMTAJA MTU ALIYE WAKUTANISHA..... WA?????????? TANZANIA INAPOELEKEA TUKAE MKAO WA KUKIMBIA INCHI COZ TIME YA KUSEMA ENOUGH IS ENOUGH INAAPROACH MNOOOOO... ANYWAY UMRI WANGU UNANIRUHUSU KUENDELEA KUSHUHUDIA MENGI KWA NEEMA YA MUNGU, KANAANI NITAINGIA.

Alaah kumbe! I did not know about this....

Mungu wa Ibrahim; Isack na Jacob wewe ni Mungu wa kweli kando yako wewe hakuna mwingine..Watupa jua, mvua na hewa vitu vya msingi watenda uovu na wema bila ubaguzi..ulimtumia Sauli (aliyekuwa na juhudi ya kuliangamiza kanisa lako) kama chombo safi cha kupeleka injili yako kwa mataifa..Hakika njia zako si njia zetu na mawazo yako yako juu sanaaaa..Uhimidiwe mwokozi na jina lako kuu liinuliwe heshima na adhama zina wewe Mungu wangu; unastahili kuitwa Mungu na kuabudiwa milele!


Warning! Anything to do with personal interests (Kama kweli kuna ukweli katika hili) zitakuwa dealt with accordingly nimesha weka amri ya milele ufisadi Tanzania lazima uwe concluded whether people like or dont hili halihitaji democracy bali uamuzi wake yeye aliye na nguvu zote na anayedhani anaweza ku counteract hizi nguvu asonge mbele.
 
everybody has a price na Mwakyembe ameshafikiwa bei aliyokuwa anataka!i had this feeeling right from th start that unafiki utaendelea kichwani mwake ili kujipatia chochote toka kwa bwana mamvi!this is very dissapointing
 
Mwakyembe unafanya siri hujalishwa sumu kuinusuru ccm sasa kifo ndicho kitakachokuumbua
 
huyu jamaa watakuja kumla hata kiboga na bado ataficha, kwahiyo suluhu yake na wale alossema wamemuwekea sumu ndo washapatanishwa au inakua vp????
huyu jamaa ni mnafiki sana, sasa tutaamini vipi kama ile barua yake ya ulalamishi aloipeleka kwa mwema hakuizuia wasiitolee au wasiifanyie kazi?????????
ndumi la kuwili mkubwa kweli huyu, hata hivyonakutakia afya njema
 
Mficha maradhi kifo humfichua! alificha maradhi ya richmond sumu ikamfichua. na sasa anawaficha waliomuwekea sumu mauti lazima yamkute! labda kama atazidi kuimarisha safari zake za kwenda kanisa la ufufuo na uzima ili akafufuliwe upya baada ya mafisadi wenzake kumpa sumu!
 
mzee wa kufuchua mambo pole sana kwa yalio kusibu ila tunakuokmba
utullie sasa usiwe unafichua mabomu yaliyotegwa kwani matokeo yake umeyaona
nadhan mungu alijua huna hatia kwa vile uanatetea wanyonge
 
Jonson panashaka wewe ni msengerema na ni mzalendo wa usengerema!

hoja au swali halijibiwi na matusi labda ttu kama wewe ni punguani!!!
 
acha tabia za kike wewe ndio mnafki mkubwa kenge wa mwisho wee.dr yupo fiti kwa lolote.

hivi ni hii post yake tu ndio imekufanya umtukane mwenzio namna hii au kuna kingine mkubwa??ustaarabu kazi....
 
Ataka mjadala kuhusu ugonjwa wake ufungwe
headline_bullet.jpg
Akataa kueleza anachoumwa, aachia serikali



Mwakyemb(1).jpg


Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akiingia kwenye ofisi za wizara hiyo tayari kuanza kazi jana na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari. Dk. Mwakyembe, alirejea nchini Ijumaa iliyopita akitokea nchini India alikokwenda kutibiwa.(PICHA: OMAR FUNGO)



Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema waliokuwa wanataka kuandika kichwa cha habari kuwa amekufa sasa wajue yuko hai, na ametaka mjadala kuhusu kuugua kwake ufungwe kwa sababu umekuwa unaiumiza na kuiathiri sana familia yake.

Alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa katika makao makuu ya Wizara ya Ujenzi, jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuripoti ofisini kwake kuendelea na kazi baada ya afya yake kuimarika kutokana na kuumwa kwa miezi kadhaa.

Dk. Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela (CCM), aliingia ofisini kwake jana saa 3.57 asubuhi na baadaye kuzungumza na waandishi kwa dakika zisizopungua 10, kuanzia saa 4.20 asubuhi.
Alisema mjadala kuhusu kuugua kwake, umekuwa ukishupaliwa na baadhi ya magazeti kwa kuupamba kwa vichwa vizuri vya habari ili kufanya biashara.

“Lingine tu ambalo pengine waandishi wa habari niwaeleze, lakini niwaombe vilevile, jamani sasa suala la Mwakyembe kuumwa basi lifike basi mwisho,” alisema Dk. Mwakyembe, ambaye alirejea nchini Ijumaa iliyopita kutoka kwenye matibabu nchini India.

Aliongeza: “Unajua kwenye Journalism (uandishi wa habari) lazima mtu pia ujali hali inayowahusu watu wengine. Nina watoto. Sasa kila siku huyu baba ambaye anategemewa kufa kesho asubuhi hata kama inaleta headline (kichwa cha habari) kizuri kwenu na kuuza gazeti inaumiza.”

“Mliopenda kupata headline (kichwa cha habari) kwamba nimekufa, basi niko hai na nitaendelea kuwa hai. Kwa hiyo nawaombeni jamani yaishe tafadhali, nawaombeni sana,” alisema.

Alisema alikuwa anaumwa, lakini sasa amerudi kutoka nchini humo alikokuwa amekwenda kupata matibabu akiwa mzima na anaendelea na kazi.

“Nilikuwa naumwa, kwa kweli nimerudi sasa mimi ni mzima kabisa, naendelea na kazi, mmenikuta ofisini kwangu. Na sasa hivi ningependa nifanye kikao kiwe kifupi zaidi maana nina mafaili lundo yananisubiri kuweza kuyapitia,” alisema Dk. Mwakyembe.

AWASHUKURU JK, MAGUFULI, WATANZANIA

Aliishukuru serikali, hasa Rais Jakaya Kikwete, kwa kubeba jukumu hilo hadi kwenda kumuona nyumbani kwake na kushinikiza apata matibabu haraka iwezekanavyo.

Pia aliishukuru serikali kwa kuhakikisha amepata usafiri uliomuwezesha kwenda hospitali nchini India.
Vilevile, alimshukuru Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu, Balozi Herbert Mrango na Naibu Katibu Mkuu

Wizara hiyo, Dk. John Ndunguru, kwa kuendesha wizara peke yao bila msaada wake.
Kadhalika, aliwashukuru wananchi wote nchini, wakiwamo Wakristo na Waislamu, waliojitolea kumuombea apate afya njema.

“Maombi yao hayakuwa ya bure, yamezaa matunda, mimi sasa hivi ni mzima na naendelea na kazi,” alisema Dk. Mwakyembe.


Akijibu swali kwamba uchunguzi wa madaktari umeonyesha alikuwa akisumbuliwa na tatizo gani, alisema anaiachia serikali kupitia tume iliyoiunda kueleza suala hilo.


“Kwa sababu nilipokuwa India nikaambiwa kuwa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ameunda tume inachunguza. Tuiache serikali. Kwa hiyo, kama kuna lolote ninalo nitaieleza serikali, na kama kuna taarifa yoyote nitaipa hii tume ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani amesema,” alisema Dk. Mwakyembe.

AWATAKA WAPIGAKURA KYELA
KUSITISHA MAANDAMANO

Aliwashukuru wapigakura wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, ambao walipanga kuandamana kwenda jijini Dar es Salaam kumuona Rais Kikwete ili waelezwe maradhi yaliyokuwa yanamsumbua Dk. Mwakyembe.

“Kwanza nitangulie kwa kuwashukuru sana. Kwanza kwa maombi yao na vilevile subira kubwa waliyokuwa nayo katika kipindi chote ambacho mbunge wao nimekuwa sipo,” alisema Dk. Mwakyembe.
Aliongeza: “Naomba niwahakikishie tu wana Kyela hawana haja ya kuandamana tena, nimekuja. Napanga kwenda

Kyela mimi mwenyewe katika wiki moja mbili zijazo kufuatana na lundo la kazi litakalopungua hapa wizarani.”
Kuhusu kupishana kauli kati yake na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba,

Dk. Mwakyembe alisisitiza kuwa hawezi kurejea tena suala hilo kwa vile linashughulikiwa na serikali.
“Serikali imeamua kulichunguza hili suala. Sasa hatuwezi kuendesha parallel systems (mifumo sambamba). Serikali

inachunguza halafu sisi huku kama waandishi wa habari tunaongea haya, haitokuwa sahihi,” alisema Dk. Mwakyembe.
Aliongeza: “Tuiache serikali iangalie hili suala, maana nikisema serikali ni pamoja na hata yeye DCI Manumba, polisi wote wanahusika. Kwa hiyo, hebu tuipe nafasi serikali ije na taarifa ambayo pengine itaturidhisha wote.”
“Lakini kwa upande wangu mimi kama Mwakyembe, mimi kama nilivyosema siku nyingi namuachia Mungu. Na tuiachie serikali.”

‘UGONJWA WAKE NI WA KITAALAMU’

Alisema hawezi kuwaeleza Watanzania ugonjwa unaomsumbua hawataelewa kwa sababu ni mambo ya kitaalamu.
“Hata kama watu watakimbilia kuuangalia (ugonjwa huo) kwenye kamusi hawawezi kufanikiwa kupata chochote,” alisema Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo Oktoba 9, mwaka jana, yalimlazimu kupelekwa katika Hospitali ya Appolo, India kwa matibabu zaidi.
Maradhi hayo yalizua utata mkubwa baada ya kudaiwa kuwa yametokana na kuwekewa sumu, huku kukiwa na kauli

mbalimbali zinazotofautiana kutoka kwake na baadhi ya watendaji wengine wa serikali.
Kauli tata zaidi ziliibuka baada baadhi ya viongozi, akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta,

kudai kuwa maradhi yanayomsumbua Dk. Mwakyembe yametokana na kulishwa sumu.
Hata hivyo, Kamishna Manumba alijibu madai hayo aliposema kuwa uchunguzi wa polisi umebaini kuwa Dk. Mwakyembe hajaugua kwa sababu ya kulishwa sumu na kutishia kuwachukulia hatua waliotoa kauli hizo.

Ripoti ya uchunguzi aliyoisoma Manumba katika mkutano wake na waandishi wa habari Februari 16, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, inaonyesha kuwa Dk. Mwakyembe hakulishwa sumu huku akisema kwamba pia ilijumuisha taarifa kutoka hospitalini India ambako alikuwa anatibiwa.

Alisema uchunguzi huo unalipa Jeshi la Polisi picha kuwa waliotoa taarifa hizo hadharani wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Baada ya kauli hiyo, Dk. Mwakyembe aliibuka na kutoa kauli nzito iliyoonekana kumjibu Kamishna Manumba akielezea kushangazwa kwake na majibu hayo, huku akisisitiza kuwa madaktari waliokuwa wakimtibu walikuwa wakitafiti chanzo

cha ugonjwa wake na walikuwa hawajafikia hitimisho, hivyo si sahihi kwa Manumba kusema kuwa hautokani na kulishwa sumu, kwani sumu si lazima ikudhuru kwa kulishwa tu.

Mbali ya Dk. Mwakyembe, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, kwa nyakati tofauti walikana kuijua ripoti hiyo ya Kamishna Manumba.
Hata hivyo, katika kile kilichoonekana kudhamiria kuchukua hatua, Kamishna Manumba aliwasilisha jalada la mashtaka

kwa watu hao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, ambaye alithibitisha kupokea jalada hilo, lakini alisema ni vigumu kufahamu ni lini atakapopeleka mahakamani jalada la kesi dhidi ya watu hao.




CHANZO: NIPASHE
 
Kama hamjui propaganda ndo kwisha kabisa, mwakyembe ametumia kodi za watanzania kukimbia india, sasa ili kuisafisha ccm anajidai kunyamaza, huku ni kuwakosea haki wapiga kura, anawafanya waonekane vichaa, mbumbumbu na hayawani kwa kushabikia jambo ambalo yeye kajidai kulipiga kufuli. MUNGU HAKWEPESHI, MWAKYEMBE ATAPATA MSHAHARA WAKE MNONO KWA UNAFIKI ANAOUFANYA. KAMA KWEL HAJAFANYA UNAFIKI, BASI UBONGO WAKE UMEATHIRIKA, HIVYO TUNAMRUHUSU TENA ATUMIE PESA ZETU AKAPIMWE AKILI. KWAN HAJUI AFANYALO
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom