(PICHA) Mwakyembe: Mjadala wa AFYA yangu UMEFUNGWA 'FULL STOP'

naona kapata nafuu kidogo tu katusahau wananchi napenda ajue kuwa hajapona bado yetu macho na masikio
Mwakyembe kigeugeu, ametugeukia...!
Mwanzoni tulimsapoti amelishwa sumu! Akatukubalia...!
Sasa hivi amerudi bongo keshasahau! Anatukatalia...!
Mwakyembe kigeugeu, ametugeukia....!

 
HENCE SHOW, thanks 4 such conclusion, tujadili vitu vyenye maendeleo kwa taifa sasa NILWAHI KUSEMA SUALA LA MGONJWA NI YEYE NA TABIBU WAKE, KO POLENI MNAOTAKA ENDLESS MIJADALA& ISIO NA MASLAHI KWA MAENDELEO, sasa tujadili yanayotuhusu, elimu,afya,uchumi,makazi na ugumu wa maisha HATUTAKI KUSIKIA FULANI NI FISADI, AMEIBA HELA KAGODA EPA, RIHARD MONDULI ahhhhhahhhh bandu bha kyalaaa
 
Wa-TZ bwana! Sasa ule waraka wake wa siri vipi? Ataturudia tu! Naungana na Manumba kuwa hakulishwa sumu huyu isipokuwa ni wale Viruwiruwi wa gonjwa letu walikuwa wamechachamaa!
 
Tulitendee haki Taifa letu, kuna mambo mengi ya kujadili juu ya mustakabali wa Taifa letu, maadamu yeye binafsi anaendelea vizuri, tumtakie afya njema ili aendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa. Kuendeleza hapa mjadala ni kudumaza fikra zetu kwenye jambo ambalo halina tija ya moja kwa moja kwa wananchi.
 
Hayo maneno hakuyasema mwakyembe ila amebainisha kuwa afya yake inaendelea vizuri na kusema kuwa tume maalum imeundwa kuchunguza suala la madai ya sumu hivyo tume ndo isubiliwe itoe uchunguzi wake.
 
huyu ni mmojawapo wa wasomi wanaotegemewa na walala hoi kuwatoa kwenye shimo la utelezi wa matatizo'hivi anamwogopa nani au anamweshimu nani katika hili'huyu ni mmojawapo wa watanzania wa kutuletea matatizo huko mbele unafiki utawa cost watanzania'bora angekufa aondoke zake
 
Moto na kazi ya kujenga taifa lilimbali na ufisadi na mafisadi linawezekana na hii lazima itimie na hakika watanzania wana hamu kubwa ya kuona nchi yenye usafi na yenye viongozi safi na wenye utu wa kibinadamu,hakika ni bora ukaungana na wazalendo wa nchi hii.

Mh mwakyembe lazima atatimiza jukumu alilotumwa na Mungu la kujenga nchi iliyo huru na iko mbali na rushwa na mafisadi.
 
wewe ndo nafiki mkubwa ambaye huoni jitihada ambazo mwakyembe amezifanya katika kuhakikisha ufisadi na rushwa vinakoma,muulize baba yako kama amaweza hata kumhoji mwenyekiti wa mtaa atakueleza kazi kubwa na kijasili anayoifanya mwakyembe.Elimika na ujihurumie wewe na ndugu zako walau ili ushurika katika kujenga taifa lenye haki na lili mbali na ufisadi na rushwa.
 
Aisee achana na mi freemason! inaweza ikamfuta duniani. yaani kama ni mimi ndiyo nimepukutishwa manyoya ya head sijui kama naweza kuendelea na mapambano ya mdomo tu. kama ni mimi namwendea congo kumletea kabambe ambayo akijaribu ameondoka kuelekea kwa sir GOD.
 
Ataacha kukaa kimya na yeye ni mchumia tumbo tu. Sasa hapo ndio amejua yeye si kitu mbele ya mafisadi. Tena inabidi akae kimya vinginevyo hata huo unaibu ataukosa wakati wa baraza litakapo badilishwa hivi karibuni na hamna kitu atafanya. Ukishakuwa chama cha wanafiki na wewe unakuwa mnafiki +

Huyu bwana bado ni mgonjwa lakini kwavile amesikia huyu ****** karibu anabadillisha baraza la mawaziri na yeye angetemwa kwasababu ya ugonjwa imebidi ajikaze kuonekana kuwa amepona ili asiachwe!! Hopefully, hiyo sumu itakuwa imetoka mwilini.
 
hapana sio rahisi kiivo! mwakyembe ashinikizwe kusema otherwise ashitakiwe kwa kuudanganya uma. watanzania sio wajinga ivo. wanasiasa wanatakiwa kuelewa hiyo fact! this sucks
 
Wanafki sasa mmeumbuka,mnafkiri madaktari wangethibitisha kuwa kalishwa sumu angekaa kimya? Lowassa njia nyeupe kuelekea pale white house as kete yenu ishaliwa kabla ya kufika 'king',mliokuwa mnamshambulia mzee manumba sasa mjitokeze tena mje na taarifa hiyo ya madaktari mliyodai eti imeonesha kalishwa sumu,na nyie ma JF feki mjifunze kulalia kwenye ukweli badala ya kugeuka mashabiki kwa kila ishu,sasa mwakyembe kamshukuru sana jk mnasemaje kawasaliti?? Na je vile vibabu vya kinyakyusa bado vina nia ya kwenda kwa baba miraji kujua hali ya mgonjwa?
 
Jiulize ndugu yangu hivi usipobadilisha mitazamo duni uliyonayo hakika hautakuwa msaada hata kwa familia yako,nisamehe kusema kuwa unaishi nyakati zisizo zako ulitakiwa uishi wakati wa ukoloni na mawazo yako haya yangewafurahisha sana wakoloni na ungekuwa kibaraka mzuri sana kwao.na kwa sasa unafaa kuwa kibaraka wa mafisadi.
 
for the sake of peace, national unity and stability he is right.Hakuna marefu yasiyo na ncha,busara imetumika kutuliza bomu ambalo lingalipuka,coz we were divided into two parts(Opposing & Supporting)
Hakuna cha peace,national unity wala stability,hakuna marefu yasio kuwa na ncha nihili ni kweli tulitegemea kuwa marefu hayo yamefikia ncha kwa maana ya ukingoni kwa kuttueleza wazi wazi ni genge gani linafanya unyama huo,ni yepi aliyo yaficha kwenye richmond,kina nani wanahujumu uchumi,kina nani wanawanyonya walipa kodi wa nchi hii amabo pesa zao wengine wanazitafuta kwa shida san,kwa jasho sana,tena kwa kuumia sana,hivi wewe unae-support ukimya wa Mwakyembe ulishawahi kulala njaa kwa kukosa pesa?ulishawahi kwenda kuomba kibarua ufanye kazi yoyote ili ulipwe upate pesa ya kujikimu?hivi unaposema hayo ya unity,mara stability una maanisha nini wakati huu ulikuwa ni muda muafaka wa kuwajua hao au hilo genge la walisha sumu wenzao tena kwa lugha sahihi ni wauji kabisa,leo hii ukiambiwa fedha iliyotumika kumtibu unadhani ingeweza kununua vitanda vingapi vya mahospitali,pesa hiyo ingeweza kunua delivery kits ngapi ili wamama wajawazito wajifungue kwa usalama,je watoto wanaokaa chini kwa kukosa pesa za kununua madawati yangelinunuliwa mangapi?na je huoni kuwa hilo genge la wauaji waliomlisha sumu Mwakyembe kama alivyotuambia yeye na mnafiki mwenzie kwa nini tusiambiwe tukawajua?kuwa hawa ndio wanaosababisha pesa nyingi za walipa kodi zitumike kwa matumizi yasiyo ya lazima kama genge hili lisinglikuwa linalisha sumu wenzao?na kwa kuwafichia siri hao watia sumu na hao magwiji wa Richmond watanzania tuanafaidika au ndio kwanza tunapata hasara na kutoa mwanya wa genge hili kuimarika?No way naungana na wenzangu wanaosema kuwa hawa ni wanafiki kabisa,na kwake yeye hakuna kitakachosaidia maana mbona madaktari wengine wanasema kama sumu iliingia kwenye borne marrow hapo ndio mwisho wa reli kigoma?anapoficha ni kwa faida ya nani?ya Magamba,no way wandugu mnisaidie jibu
 
Nahisi unapaswa kumuunga mkono kama kweli wewe unachukizwa na mafisadi na ufisadi wao unaolimaliza taifa.
 
Huyu anasema amepona lakini angalia kucha zake mbona nyeusi hivyo?

attachment.php
 
Back
Top Bottom