nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Askafu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Dk. Alex Malasusa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutoa tamko la maaskofu kutokana na kuchomwa kwa
makanisa katika vurugu zilizotokea Mabagala jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Katibu wa Mkuu wa Baraza Maaskofu Tanzania, Padri Anton Makunde na Padri Silvester Gamanywa .
Katibu wa Mkuu wa Baraza Maaskofu Tanzania, Padri Anton Makunde akisoma tamko la maaskofu kutokana na kuchomwa kwa makanisa katika vurugu zilizotokea Mabagala jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Picha na Mdau Dande Francis
Sisi maaskofu na viongozi wa makanisa ya kikristo kutoka CCT, TEC na PCT baada ya kusikia na kuona katika vyombo vya habari juu ya uvamizi wa makanisa tumechukua fursa ya siku hii ya leo ili;-
1)Kujionea wenyewe madhara yaliyotokea
2)Kutoa pole kwa waumini wetu
3)Kushiriki pamoja uchungu wa madhara yaliyotupata
4)Kuwepo kwa pamoja namna ya kukabiliana na uvamizi huo
Baada ya kutembelea maeneo yaliyovamiwa na kujionea uharibifu uliotokea
1)Tumeona uchungu na masikitiko ya kwamba watanzania tumefikia kiwango hicho cha kumtendea jirani yake
2)Tunatambua subira na uvumilivu mkubwa uliooneshwa na wakristo kuepusha majibizano ambayo yangeweza kuleta athari kubwa zaidi.
3)Tumeziona juhudi za jeshi la polisi katika kudhibiti hali ya vurugu na kuepusha kupoteza uhai wa raia.
Katika wakati huu
1) Tunawaalika wakristo wote kutolea sala na maombi kwa Mungu aliye mlinzi wet,usalama na ulinzi wetu uko mikononi mwa Mungu pekee.
2)Tunatambua kuwa usalama wa wafuasi wa Kikristo ni haki ya msingi kama raia wengine wowote, ni mategemeo yetu kwamba wakristo na nyumba zao za ibada vinastahili kuhakikishiwa usalama.
Tunapenda kuwaambia Wakristo wenzetu kwamba kikao chetu cha leo kimetupa fursa ya kujionea wenyewe hali halisi ya uvamizi, kwasasa tunajiandaa kuchukua hatua muafaka. Tutawarudia hivi karibuni mbele ya vyombo husika yale yaliyo maamuzi yetu.
Kwa wakati huu tunawaomba muendelee kuwa wavumilivu na watulivu na muwe macho katika kulinda mali na nyumba zetu za ibada kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.
Tunawapa pole wote na kuwatakia Baraka za Mungu.