PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Tukishamjua halafu what next?

Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.
Mkuu umefikiri sawasawa? unataka vyombo vipi vinavyohusika vifanye kazi yake?hawa watu ni vema tukiwafahamu kwa kina tena si majina tu yapaswa tufahamu hata mienendo yao.

 
Hivi marehemu DM alikuwa member humu JF na kama alikuwa je alitumia jina gani? ili tuone alikuwa ktk misimamo na mitazamo gani, na je alipata responses gani pia toka humu JF au any social networks!
 
Huyu anaweza kutoa ushahidi, ndani ya Polisi kuna wazalendo wa kweli akiwemo yule aliyejinyonga Morogoro ambaye alitaja watuhumiwa wanaolichafua jeshi la polisi, nawaachia vionozi hebu cheki huyu:

Askari huyu bila shaka alijeruhiwa na bomu hilohilo lililomuua Mwangosi an hapa alikuwa anasubiri kuondolewa. Tazama kwa makini umri wa askari aliyemfyatulia Bomu Mwangosi, ni Kijana mdogo kabisa, na tabia hii ya jazba ya vijana inahitaji ushauri ama sivyo itatupeleka pabaya. Tatizo la uwezo wa vijana katika kutetea yanayowahusu si la CCM peke yake, CHDEMA pia wako kwenye shida hii ya kumudu hisia za vijana, na wakati mwingine wanatoa msimamo wa chama kusuppport ubaya uliyotendwa na vijana ili mradi tu kulinda support yao vijana kwa chama. Tunahitaji kufanya jambo kuwasaisia viajana wetu kuchukua nchi hii katika umoja na kuheshimu mawazo ya kila mmoja si vitisho na ubabe wa upande wowote ule ukiwemo wa wale wanaosema damu itamwagika au nchi haitatawalika, kwani mimi nisiamini unachoamini si ndugu yako? Kwahiyo Dawa ni kuniangamiza, la hasha. Na wale wanaotumia dola kuwaumiza wenye itikadi tofauti ilimradi tu uufurahishe utawala, unasahau kuwa utawala wa Mh Kikwete hauwezi kukulinda utaumbuka na kustaafu kwako kutakuwa kwa aibu ka isa sijui hamsomi alama za nyakati? Waulizeni akina Mgonja, je wewe ni nani? TUHEHIMIANE NA TUDUMISHE UMOJA hata kama tuna mawazo tofauti.

Kijana aliuwawa na polisi wenzake na hatimae kumwekea kamaba kama kajinyonga ila ukweli ni kwamba walimuua mwenzao.
 
Mtu mwenye kofia (Barret) aliyekumbatiwa na Daudi ambaye anasemekana kuwa ni mkuu wa kituo cha polici Mafinga na ambaye inasemakana pia kuwa huenda ndio alitoa order ya kuua kwa askari waliokuwa na siraha ni nani kwa jina
Uncle wangu alikuwa polisi ila aliacha, ktk kumdadisi niligundua mabo mengi ambayo kama wewe ni MPENDA HAKI hii kazi inahitaji uwe na akili ya ziada, VINGINEVYO HII SIO KAZI YA KUFANYA hasa kwenye nchi zilizojaa watu wenye roho mbaya kama kina mwema, chagonja, manumba, kamuhanda, mahita na wenzao.

Muone huyo polisi aliyekaa hapo pembeni mwa mwili wa D. Mwangosi baada ya kufanyiwa unyama wa kutisha. muone huyo mshikaji (mwenye heliment nyeusi) ambaye naamini anaweza akaacha kazi ya upolisi kwa namna anayoonekana na huruma akiwa haamini kama binadamu mwenzake anaweza kufanyiwa unyama wa kiwango hiki.

Kwa kweli inasikitisha sana. mimi binafsi hii kazi ya upolisi siipendi, kwa sababu kwa hapa Tanzania, hii inatumika kuchuma dhambi tupu kwa uoga wa njaa ambayo unaweza kujikimu hata kwa kulima kuliko kutumiwa kuua
.



Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAJAMBAZI/MAFISADI/WAUAJI.
 
Tukishamjua halafu what next?

Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.


Wamelianzisha, tuwaache tu! Halafu wao wameua, wao wameunda tume, tume iripoti kwao, wao wawachukulie hatua wahusika, wakati wao ndo wahusika! Wapi na wapi?
 
Tukishamjua halafu what next?

Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.

Who cares?

Tukishamjua tutajua namna ya kuishi nae mtaani. Muuaji lazima aangaliwe kwa jicho la UUWAJI.
 
hivi ulimsikia mandishi aliyeojiwa na itv? anasema wakati marehemu anapigwa rpc alikuwa kwenye gari

samtymz watu wakishuhudia vitu ka hivyo wanapanic so anaweza kujichanganya pia! ctak kulazimisha kuwa huyo ni RPC coz mwenyewe cmfham but kama cyo yeye na akanushe coz naamin aliyemention anamfaham rpc kwa sura!!
 
Mtu mwenye kofia (Barret) aliyekumbatiwa na Daudi ambaye anasemekana kuwa ni mkuu wa kituo cha polici Mafinga na ambaye inasemakana pia kuwa huenda ndio alitoa order ya kuua kwa askari waliokuwa na siraha ni nani kwa jina

Huyo Mkuu wa kituo cha Polisi Mafinga ndiye aliyekuwa akijaribu kuwazuia polisi wenzake wasimuadhibu marehemu kwani alikuwa anamfahamu. Tear gas canister lililomua marehemu pia lilimjeruhi OCS huyo (wana Mafinga watutajie jina lake - mie silifahamu).

Kwa habari zaidi ya tukio hilo tembelea: Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima: DAUDI MWANGOSI UMEKWENDA SISI TUPO NYUMA YAKO
 
Tukishamjua halafu what next?

Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.

Well said mkuu,tuache sheria ichukue mkondo wake kuliko kujifanya ni wapelelezi na kuingilia majukumu!
 
Profesa na Gelange Vidunda mmesema kweli kabisa, kuna askari waliomtetea mwangosi na kuna Watu waliochochea machafuko mahali hapo pasitawalke na ndipo wakakutana na vijana wadogo wa FFU (wanasema ni kati ya wageni waliotoka DSM majuzi kati)

Mwisho jamani Mahakama hapo hakuna kitu ni sawasawa na Dreva katoka nyumbani kaingia kwenye basi anaenda Mbeya mbele kaona digidigi kapeleka gari porini (hakudhamiria kutoka nyumbani ntaenda kumuua fulani leo nipeni switch,

Aau Daktari na operation zake kakata mshipa mgonjwa kafariki hakuna tofauti na POLISI kapewa cha moto, nenda kazini, alichopewa kakitumia sasa kwa nini Boss kamtuma?

Mimi naona ni kumlaani yawafike mabaya, lakini kwa Hukumu ni sawa na dua za kuku kwa mwewe
 
Ombi langu ni kuwa MODS wetu wasije wakaondoa uzi huu. Tumeshajaribu kuweka mambo yenye kufanana na huu lakini imekuwa censored. Please MODS tuvumuliane ili tuweze kutafuta na kupata ukweli. Thanks
 
Tukishamjua halafu what next?
Tuachie vyombo husika vifanyie kazi hili swala, huko itakuwa kuanzisha ugomvi, fujo, mfarakano baina ya raia na askari.

Kwani kuna tatizo gani kwa watu kujulishwa majina ya washukiwa wa uharifu?

Ni muhimu sana kujua majina yao kama vile tulivyopata picha zao,kwa mfano

1/Itatusaidia Kupata historia,mwenendo na tabia zao.

2/Kutaepusha mchezo mchafu wa polisi wa kuwatorosha au kuwalinda wahusika.

3/Kunatupa nafasi na sisi wenyewe kufanya uchunguzi wetu binafsi.

4/Kutaepusha mchezo mchafu wa polisi wa kubambikizia kesi watu wasiohusika.

5/Itatupa nafasi sisi wenyewe kuwafuatilia wahusika mahali popote walipo, ukiwezekana kuwachukulia hatua mbadala sisi kama jamii.

6/Itatupa mwanga wa namna ya kupeleka ushahidi kwenye tume iliyoundwa.

*Kumbuka mpaka sasa serikali na polisi haijawakamata polisi hao waliohusika na hata kuwataja majina yao, zaidi inajaribu kuwakama raia wasiohusika na sasa inajaribu kutafuta namna ya kuwahusisha na tukio hilo. Swali, je inaogopa nini?
 
Nina wasiwasi sana na huyu jamaa alievaa shat la mikono mifupi na kushika bendera. Huyu sio askari wa iringa. Huyu amekuja special kwa kazi ya uuaji. Hapa kuna kitu kizito sana nyuma ya hili. Iweje wammkamate mwandishi tu na sio mwananchi mwingine wa kawaida? Kipindi kidogo nilishawahi kusikia harakati za huyu Marehemu katika tasnia ya habari hapo Iringa
Ilifikia kususia nafikiri ilikuwa kuchukua habari kutioka taasisi mojawapo ya habari iringa. lazima polisi wanasiri kubwa juu ya hili.
 
Back
Top Bottom