Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Taarifa ya kukamatwa kwa Mwandishi wa habari Shagata Suleiman na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza.
.................................................
Ndugu waandishi wa Habari na Taasisi za kihabari Nchini Tanzania, nasikitika kuwataarifu kuwa, Mwandishi wa habari mwenzetu na mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza, Bwana Shagata Suleiman, ambaye pia anafanya kazi na Gazeti la Daily News na Habari Leo anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza na sasa ni zaidi ya masaa matatu tangia amekamtwa.
Mwandishi huyu amekamatwa kwa sababu alikwenda kituo cha polisi kati cha Mwanza kwa lengo la kutafuta mizania / ku balance habari ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kushikiliwa na Jeshi la Polisi.
Cha kushangaza alipofika kwenye lango kuu la kuingilia kituoni hapo alikamatwa kwa kuambiwa yeye ni msumbufu kwani alifika kituoni hapo zaidi ya mara tatu.
Klabu ya waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) imefuatilia kwa mhariri wa Chombo anachofanyia kazi mwandishi huyo na kubaini kuwa, Mwandishi huyu alikwenda awamu ya kwanza na aliambiwa arudi baadaye lakini aliporudi tena akiwa na wenzake aliambiwa yeye ni msumbufu, alikamatwa yeye pekee na kuwekwa chini ya ulinzi hadi sasa.
Nilipopata taarifa hii nilijitahidi sana kumtafuta RPC wa Mwanza Ramadhan Ngh'anzi kwa njia ya simu bila mafanikio, pia nilimtuma ujumbe mfupi ambao pia hakujibu.
Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza tunaliomba Jeshi la Polisi kumwachia Mwandishi huyu na pia kutambua wajibu wa Mwandishi wa habari kwenye kutekeleza majukumu yake.
Kutafuta mizania ya habari ni jambo jema zaidi kuliko kurusha habari ya upande mmoja inayoweza kuzusha taharuki.
Hakuna sheria inayomkataza mwandishi wa habari kufuata chanzo mamlaka/ authoritative source kupata taarifa.
Mwisho MPC inatoa wito kwa RPC wa Mwanza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Saimon Sirro kulishughulikia jambo hilo na kuzingatia azma ya Serikali ya sita ya kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari Tanzania kwa kuwashughulikia askari waliohusika kwenye kitendo hicho.
Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza tupo tayari kuacha kufanya kazi na Jeshi la Polisi kama vitendo vya kuwadhalilisha waandishi wa habari vitaendea kuungwa mkono na jeshi la Polisi Mkoani Mwanza.
Mwisho tunaomba taasisi za kihabari na watetezi wa haki Tanzania kuingilia jambo hilo.
Edwin Soko
Mwenyekiti
MPC
20.07.2021