Personal attacks kwa Dr. Ulimboka zimeanza! Waziri mkuu kadhihirisha utendaji duni

Movie iko hivi wanajamii, pinda alikua anajibu mambo muhimu ambayo madaktari walikua wanataka yatimizwe b4 hawajarudi kazini akaanza kupangua hoja moja baada ya nyingine mwishoni ndo akaanza kuelezea profile ya huyo dr ulimboka kuwa alishawahi kuongoza mgomo wa wa madaktari mwaka 2005,ndo akaanza kumchambua tangu anasoma chuo hadi hapo alipo.pinda anadai mgomo huo ulianzia kwa madaktari waliokua interniship muhimbili(mafunzo kwa vitendo)then baadae umeamia kwa chama ukiwa na taswira tofauti hapo ndo akawa anamchambua ova anasoma mashairi ya taarabu
Inshort mi nimeona km mtoto wa mkulima kaamua kutishia nyau nyama maana yy(ulimboka) km kiongozi wa chama cha madaktari lazima awe ndo mtu wa mwisho kutoa maamuzi magumu ya chama chake yaani maadhimio yanayofikiwa na chama yy ndo anakua mtu wa mwisho kuyaimplement so kumsema yy binafsi naona anajipunguzia mvuto kwa jamii maana ule si msimamo wake binafsi ni msimamo wa chama na yy ni kiongozi anayesikiliza kile kinachoafikiwa na walio wengi kwenye chama.

Well said mkuu!nitaigongea like hii kitu when i get home
 
Msingi wa yote ni kiburi cha madaktari kukataa wito wa mkubwa. Ndipo watanzania tumejulishwa Dr. Ulimboka mtu gani:
1. 2005 aliongoza mgomo Muhimbili
2.. Akasimamishwa na kupewa onyon kali na MAT
3. 2006 Rais akampa msamaha
4. Aliandika barua kwa MAT kuomba msamaha na kuahidi atajihusisha tena na migomo
5. Rekodi zinaonyesha mafunzo ya intern hajamaliza
6. Hana cheti cha udaktari
7. Ni mfanyakazi wa NGO ya UKIMWI

Hapo Pinda asilaumiwe bali Ulimboka ahukumiwe kwa kuwaburuza madaktari

Kwani hao madaktari hawana akili mpaka waburuzwe na Dr. Ulimboka? Hakuna lolote serikali itatue tatizo sio kutafuta mchawi hapa!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ulimboka ni Kiongozi Tu kashikilia Kasia!! Ila wenye uwezo wa kushika Kasia wapo wengi!! Kaza Buti Ulimboka no easy way in achieving expectations!!
 
Huwa simwangalii hilo low perfoming PM likiongea lakini niliamua kumsikiliza leo. Kaongelea jinsi mgogoro ulivoanza na ulipofikia sasa hivi. Maelezo aliyoyatoa nayatilia mashaka hasa kiasi cha pesa ambazo madakatari watachukua kama mshahara ukiongezwa kwa matakwa yao. Nilipochoka ni pale aliposema eti mkutano wa madaktari ni uvunjifu wa sheria ila walikuwa wanaivumilia tu. Nilitegemea mtu tunayemwita waziri mkuu aseme madaktari wanavunja sheria namba fulani ya mwaka fulani kwa kufanya mikutano. Kusema tu kuwa mikutano si halali hivo anaagiza vyombo vya dola kuvizuia ni kutumia utawala wa ubabe na si utawala wa sheria.
Nadhani huyu bwana kama ilivo mambo mengi aliyoshindwa kuyatatua ni kuishia kuwa mwongeaji ameshindwa kutatua mgogoro wa madaktari na antafuta sympathy ya public. kaamuru daktari ambaye hatokuwepo kazini kesho ajihesabu si mtumishi tena.

Mr handsome PM Pinda, sisi watanzania tunataka na tunajua tutapata tu huduma bora toka kwa madaktari walioridhia kazi zao. Kuwalazimisha eti asiyekuwepo kazini kesho si mtumishi hakukupi sympathy yoyote au kwamba tujue umefanya vya kutosha ila madaktari ndio wana makosa. Tunajua fedha za serikali zinavoliwa na wajanja ambao hawana hata digrii moja ila degree ya ujanja ujanja na uwizi ambao ndio fani inayolipa kwenye serikali yenu chovu na ilokoswa fikra. Waiteni madaktari mwongee nao. Uliyokuja kuongea hayaingii hata akilini ukizingaltia kuwa ulishawahi kutudanaganya wananchi kupitia bunge na kuishia kulindwa na spika kuvuliwa nguo. Ni wajinga tu wasiojiuliza maswali mengi watakaokuamini haraka haraka hivo. Hilo pozi lako kujifanya unasema ukweili halitushawishi make mara nyingi umelitumia na kuishia kutudanganya mr handsome.
 
Bado sijaona kosa la Pinda

Huwezi kuona maana wewe u mmoja wa watu wa aina hiyo ambao badala ya kujibu na kujadili hoja wanaishia kuvamia personality.
Madai ya Madaktari si ya Ulimboka, Pinda kuanza kumjadili Ulimboka ni upotovu, hapo Pinda anachochea mgogoro.
Sasa kesho madaktari wakichagua Kamati nyingine Pinda atatafuta wasifu wake pia na kuutoa hadharani?
 
serikali inajaribu kuwafanya madaktari waonekane walafi na wasio na utu. Pinda ameongea vitu asivyovijua, kama juha kwa wenye uelewa. Yani huyu babu haelewi kabisa Sekta ya afya na mapungufu yake, so wamemjaza urojo kichwani kaishia kutema upupu. Shame on you Mizengwe Kuyundu Mamba Pindi.
Dalili zinaonesha ww ndiye Ulimboka, na kama sio basi mkewe au hawara yake. Maji yapo shingoni eeenh? Dakika chache tu inteligensia imeshusha data zake. Aaah kumbe ni chokoraa tu anasababisha watu wanapoteza maisha. Ingekuwa China angepigwa shaba tu basi, kazi kwisha!
 
Jamani mimi simpendagi waziri mkuu pinda kutokana na upole wake na mwendo wake wakinyonga katika kutatua mambo, lakini kwa hili la hawa madaktari wasiotaka suluhu namunga mkono pinda mimia kwamia, madai wanayotaka madaktari hawa ni magumu mno ni kama kuomba mtu akukatia kichwa chake ataishi kivipi?
 
ulimboka ni daktari by profession,anaweza asiwe na leseni ya kutibu lakini haimuondolei kuwa daktari.MAT ni jumuia ya madaktari tanzania,wote wanaotibu,wanaouza mahindi na wabunge.
Ahsante mkuu. tuwe tunaelimishana namna hii. wengine hata hatujui udaktari unaanzia wapi. Hivi ukiwa hujamaliza ama hukuhudhuria intern unaweza kuwa daktari? MAT ni kwa madaktari wa wanadamu au? Wale wa wanyama nao.wana umoja wao? Wa phamasia nao vipi?

Mkuu mbona madaktari wa Regency na Aga Khan hawagomi? Pia kuna wengine ambao wako Hospitali za Serikali wamegoma lakini huko kwenye Hospitali za Kulipia wanafanyakazi? Jana nimeenda Hospiyali moja ya kulipia kumuona daktari wangu wa pua, koo na masikio ambaye huwa yuko Muhimbili. Muhimbili amegoma lakini huku kwingine anakula vichwa
 
nimeshangazwa sana na kauli wa waiziri mkuu kufuatilia personal profile ya dr. ulimboka.

updates
- alichokisema waziri mkuu:

kaeleza jinsi Dr. Ulimboka alivyowahi kuongoza mgomo wa madaktari nchi nzima mwaka 2005. Aeleza pia kwamba kumbukumbu hazioneshi kwamba Dr Ulimboka alimaliza internship hospitali ya muhimbili. Kaenda mbali pia kusema amepewa barua ya Dr Ulimboka kwenda chama cha madaktari kukiri kutojihusisha na ushawishi wowote kwenye masuala ya migomo mwaka 2005 baada ya kusamehewa na Rais asifutiwe uanachama wake.


MAFILILI
Today 22:22
#9 JF Senior Expert Member Array


Join Date : 28th April 2011
Posts : 489
Rep Power : 341


icon1.png
Re: ni sahii waziri mkuu kusoma profile ya mtumishi hadharani


Msingi wa yote ni kiburi cha madaktari kukataa wito wa mkubwa. Ndipo watanzania tumejulishwa Dr. Ulimboka mtu gani:
1. 2005 aliongoza mgomo Muhimbili
2.. Akasimamishwa na kupewa onyon kali na MAT
3. 2006 Rais akampa msamaha
4. Aliandika barua kwa MAT kuomba msamaha na kuahidi atajihusisha tena na migomo
5. Rekodi zinaonyesha mafunzo ya intern hajamaliza
6. Hana cheti cha udaktari
7. Ni mfanyakazi wa NGO ya UKIMWI

Hapo Pinda asilaumiwe bali Ulimboka ahukumiwe kwa kuwaburuza madaktari

Kama kuna jinsi ya kumjua mtu mwenye akili ya kitumwa kwa urahisi basi ni namna anavyowaadress viongozi. Hili neno 'wakubwa' ni neno la kitumwa, jiepushe nalo. Hao mawaziri wengi wao ni vilaza tu wameingia ofisini kwa siasa na sio taaluma.

Kama Dr. Ulimboka hakumaliza Internship mbona yasisemwe siku zooote mpk leo kwa kuwa mna hasira naye ndio mseme?

Unaposema Dr. Ulimboka kawaburuza madaktari, ina maana wao wenyewe hawana akili na utashi wa kuamua la kufanya? Huo ni ujinga na dharau, wale ni watu wazima. Ama ulivyozoea kuburuzwa na the so called wakubwa ndio unadhani kila mtu anaburuzwa kama wewe?

Kama Dr.Ulimboka hana cheti cha udaktari na bado alikuwa anafanya kazi, viongozi wake woote wanapaswa kushtakiwa kwa uzembe pamoja naye. Nashangaa limeongelewa kwa sifa wkt linaonesha jinsi serikali inavyoongozwa na vilaza.

Kwa kifupi sioni jipya zaidi ya yale yale ya Masaburi na issue ya UDA. Kama mtu unajua kitu na unanyamaza mpk siku uchokozwe, nini kipimo cha uadilifu wako.

Crap crap crap!

Godbless Lema angepewa nafasi atudhihirishie jinsi PM alivyo muongo
 
eti......huyu ulimboka ni nani huyu, katokea wapi......

Badala ya kutoa majibu yeye anatafuta profile ya mtu.....yale yale ya manufacturing of teachers...

Yah..manufacturing of teachers to assemble many doctors....:lol:
 
Yaani Serikali inaendeleza propaganda za magamba kwenye ishu kama hii.............. There must be a problem somewhere.
 
Inshort pinda kakosea maaana ulimboka ni kiongozi wa chama aliyechagulia kiuhalali ss km wanachama wake wanagoma na mgomo unabaraka za chama kwa nn aanze kumshambulia yy?na sio chama?kulikua na ulazima gani kuanza kusoma cv yake wakati alikua anatakiwa kujibu hoja za madaktari?mbona wabunge walivyojipenyezea posho ziongozwe hakusoma cv ya bi kidude makinda kuwa kina shirika la uuma alilokua yalikua yanafilisika?hizo gharama za maisha zimepanda kwa waheshimiwa tu?kiukweli fani ya udaktari haipewi stahiki yake inayostairi,pinda asiwe kama remote control kila button inapokua clicked inafanya kazi
::::Ni style yao na JK. umesahau JK alivyomuattack Mgaya wa TUCTA mbele ya wazee wa CCM?
 
Ahsante mkuu. tuwe tunaelimishana namna hii. wengine hata hatujui udaktari unaanzia wapi. Hivi ukiwa hujamaliza ama hukuhudhuria intern unaweza kuwa daktari? MAT ni kwa madaktari wa wanadamu au? Wale wa wanyama nao.wana umoja wao? Wa phamasia nao vipi?

Mkuu mbona madaktari wa Regency na Aga Khan hawagomi? Pia kuna wengine ambao wako Hospitali za Serikali wamegoma lakini huko kwenye Hospitali za Kulipia wanafanyakazi? Jana nimeenda Hospiyali moja ya kulipia kumuona daktari wangu wa pua, koo na masikio ambaye huwa yuko Muhimbili. Muhimbili amegoma lakini huku kwingine anakula vichwa
kama unataka kufanya kazi ya kutibu tanzania hapa ndio unatakiwa kufanya internship.daktari ni yule aliyesoma na kumaliza med school.usijione mpweke kwani hata waziri wako hajui haya.
 
nimeshangazwa sana na kauli wa waiziri mkuu kufuatilia personal profile ya dr. Ulimboka.

updates
- alichokisema waziri mkuu:

Kaeleza jinsi dr. Ulimboka alivyowahi kuongoza mgomo wa madaktari nchi nzima mwaka 2005. Aeleza pia kwamba kumbukumbu hazioneshi kwamba dr ulimboka alimaliza internship hospitali ya muhimbili. Kaenda mbali pia kusema amepewa barua ya dr ulimboka kwenda chama cha madaktari kukiri kutojihusisha na ushawishi wowote kwenye masuala ya migomo mwaka 2005 baada ya kusamehewa na rais asifutiwe uanachama wake.


mafilili
today 22:22
#9 jf senior expert member array


join date : 28th april 2011
posts : 489
rep power : 341


icon1.png
re: Ni sahii waziri mkuu kusoma profile ya mtumishi hadharani


msingi wa yote ni kiburi cha madaktari kukataa wito wa mkubwa. Ndipo watanzania tumejulishwa dr. Ulimboka mtu gani:
1. 2005 aliongoza mgomo muhimbili
2.. Akasimamishwa na kupewa onyon kali na mat
3. 2006 rais akampa msamaha
4. Aliandika barua kwa mat kuomba msamaha na kuahidi atajihusisha tena na migomo
5. Rekodi zinaonyesha mafunzo ya intern hajamaliza
6. Hana cheti cha udaktari
7. Ni mfanyakazi wa ngo ya ukimwi

hapo pinda asilaumiwe bali ulimboka ahukumiwe kwa kuwaburuza madaktari

sasa pinda badala ya kushughulika na matatizo ya msingi anashughulika na mtu binafsi. Huyo dr ulimboka yeye ni kiongozi wa madaktari hivyo pinda anatakiwa kushughulika na matatizo ya madaktari sio mtu binafsi.
 
na kilicho nishangaza ni kutoa order kwa vyombo vya dola hasa polisi kuhakikisha hao madaktari hawafanyi vikao vyao tena popote ndani ya nchi hii na hiyo iliokuwa inafanyika ilikuwa kinyume na utaratibu,na hajatoa maelezo ya kutosha ni jinsi gani watatatua kero za hao madaktari..,tunahitaji viongozi na sio watawala kwa kweli..
 
Dalili zinaonesha ww ndiye Ulimboka, na kama sio basi mkewe au hawara yake. Maji yapo shingoni eeenh? Dakika chache tu inteligensia imeshusha data zake. Aaah kumbe ni chokoraa tu anasababisha watu wanapoteza maisha. Ingekuwa China angepigwa shaba tu basi, kazi kwisha!
Wewe na serikali yako iliyoua watu kwa uzembe wa kutowasikiliza madaktari ndio mlitakiwa mjiuzulu na kupigwa risasi kwa kukaidi kuwasikiliza madaktari tangu dakika za aawali mnasubili mambo yawafike shingoni ndio muanze kutumia ubabe na huruma ya watanzania safari hii mtaeleweka tu.
 
Back
Top Bottom