Personal attacks kwa Dr. Ulimboka zimeanza! Waziri mkuu kadhihirisha utendaji duni

Yani kwenye katiba mpya lazima viongozi wote wapimwe akili, uwezo wa kufikiria na kujitambua, yani bure kabisa anaacha solve tatizo anatoa vitisho, yani huyo sijui huwa anafikiria nini ndio maana mpaka huwa analia lia bungeni
 
huyu ulimboka kama yuko private hosptal anafaidika na mgomo wa madoc wa serikali kwani hivi hospital za binafsi wanapata wateja wakumwaga kwa wasio na uwezo wa kwenda private hata wakifa kwake haimsumbui
 
Yani kwenye katiba mpya lazima viongozi wote wapimwe akili, uwezo wa kufikiria na kujitambua, yani bure kabisa anaacha solve tatizo anatoa vitisho, yani huyo sijui huwa anafikiria nini ndio maana mpaka huwa analia lia bungeni

sio vitisho ni amri ama waende job au wapoteze kazi.wataofannya mikutano wataenda lockup.wataoruhusu kumbi zao kutumika watakiona fulstop
 
Yaani namjutia PM kwa personal attack, kaharibu!! Nilimsikiliza mwanzo mwisho nikiwa bado najaribu kumwelewa akaja na hicho kichekesho na aibu kwa kiongozi mkuu kama yeye.

Hivi watanzania tunawasoma madaktari? Hivi inaweza ikawa wanatufikishia meseji ambayo twatakiwa kuielewa lakini tunakuwa wagumu kuelewa? Mungu saidia sie watanzania tupate meseji madaktari wanayoituma kwetu. Maana maisha yamekuwa magumu sana, hata kitunguu kimoja kinauzwa tsh mia tano. Na hii mishahara ya laki naaa haitoshi tena kabisa. Tupe ujasiri kama madaktari! Tujaze na roho mtakatifu tumshinde shetani ajaye kwa sura kama pm!
 

Serikali yageuka mbogo
• Madaktari wasema hawataenda kazini, kesho kukutana

na Edson Kamukara
Tanzania daima


amka2.gif


SERIKALI imetangaza kuwafuta kazi madaktari wote watakaoendelea na mgomo huku ikiviamrisha vyombo vya dola kuwakamata watakaodiriki kufanya mikutano kwenye maeneo mbalimbali.

Msimamo huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya madaktari kushindwa kufika kwenye mkutano ulioandaliwa kuzungumzia madai na mgomo wa wataalamu hao.

Pinda aliwaamaru madaktari wanaoendelea na mgomo katika mikoa saba nchini kurejea kazini mara moja leo asubuhi huku akiweka wazi watakaokiuka agizo hilo watapoteza ajira zao.

Alisema serikali inatambua madaktari hao wanaongozwa na kamati ya mpito isiyotaka suluhu licha ya juhudi zilizofanywa za kuwaita kushughulikia madai husika.

“Serikali tayari imechukua tahadhari ya kukabiliana na hali hii kwa kuagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kupeleka madaktari wake katika hospitali za mkoa wa Dar es Salaam ili kusaidia wagonjwa walioko hospitalini. Kwa hiyo huduma zitaendelea kama kawaida,” alisema Pinda.

Katika mkutano huo Pinda aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya; Waziri wa Nchi Ofsi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia; Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha; na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika.

Akionekana kukerwa na kitendo hicho cha madaktari hao kushindwa kukutana naye, Pinda alisema kuanzia leo ameviagiza vyombo vya dola kuzuia mikutano yote ya madaktari hao, akisema ni kinyume cha sheria ingawa serikali ilikuwa ikiwavumilia tu.

“Mgomo wao si sahihi kwa sababu haukufuata taratibu za kuuitisha. Wao walipaswa kutangaza mgogoro na kisha kutoa notisi ya siku 60, jambo ambalo hawakufanya,” alisema Pinda na kukipongeza Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (Tughe) kwa kutambua hoja za madaktari hao lakini wakasema njia iliyotumika si sahihi.

Pinda ambaye aliwasili ukumbuni hapo saa 6:12 mchana badala ya saa 4:00 kama ratiba ilivyokuwa, alianza kwa kufafanua chimbuko la mgomo huo na hatua kadhaa zilizochukuliwa na serikali kuutatua.

Alisema tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, kulikuwa na madai ya wataalamu mbalimbali waliokuwa kwenye mazoezi kwa vitendo (interns) kwamba wangeitisha mgomo kwa sababu ya kucheleweshewa posho zao; alisema juhudi zilifanyika na wakalipwa madai hayo yaliyokuwa yakifikia sh milioni 876.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa baada ya malipo kufanyika, mgogoro ulihama kutoka kwa interns na kuwahusisha wataalamu wa kada nyingine za afya wakiwemo madaktari na kwamba kwa kuwa interns hao nafasi zao zilikuwa zimezibwa wakati wakiwa wamegoma, serikali iliona ni vyema kuwasambaza kwenye hospitali nyinge jijini hapa.

“Uhamisho huo ulifanywa kwa nia njema ila wenzetu waliutafsiri kama adhabu ya kuwakomoa interns hao na kupitia Chama chao cha Madaktari (MAT), walileta madai kuwa tuwarejeshe Muhimbili wakitoa sababu nyingi ambazo kimsingi tuliona zina mantiki,” alisema Pinda.

Aliongeza kuwa wakati wakiwa kwenye majadiliano ya hoja hiyo na yeye kuonyesha nia ya kukutana nao, MAT walienguliwa na jukumu hilo kupewa Jumuiya ya Kamati ya Mpito iliyoongozwa na Dk. Stephen Ulimboka, ambayo ilitoa madai nane.

Katika madai yao walitaka posho ya kulala kazini ya sh 10,000 kwa siku, ilipwe kwa kiwango cha asilimia 10 ya mshahara wa mwezi, posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi iwe asilimia 30 ya mshahara wa mwezi; na posho ya nyumba walipwe asilimia 30 ya mshahara wa mwezi.

Madai mengine ni kupandishwa kwa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu zifikie asilimia 40 ya mshahara, kupatiwa posho za usafiri kwa asilimia 10 ya mashajara iwapo itashindikana wapatiwe usafiri wa kwenda na kurudi kazini.

“Wanadai mshahara wa sh 700,000 ni mdogo sana kwa daktari anayeanza kazi, hivyo wanapendekeza alipwe sh 3,000,000 kwa mwezi. Wanataka kupatiwa bima ya afya pamoja na familia zao kwa kupewa kadi za kijani na wanataka interns warejeshwe Muhimbili bila masharti yoyote,” alisema Pinda.

Hata hivyo, akichambua madai hayo alisema serikali haiwezi kuyapatia ufumbuzi mara moja madai hayo ila taratibu za kuyapatia ufumbuzi zinaendelea huku akikanusha kuwa daktari anayeanza kazi analipwa sh 700,000 bali ni sh 957,7000.

Alisema madaktari hao wamependekeza wanaoajiriwa hivi sasa walipwe mshahara wa sh milioni 3.5 wakati watumishi wa kada nyingine kama wahandisi wanaanza na sh 600,000 na wahasibu wanaanza na mshahara wa sh 300,000; kwamba posho zote wanazodai zikijumuishwa zinafikia asilimia 120 ya mshahara wa daktari mmoja.

“Kwa mujibu wa mapendezo yao ina maana kiwango cha kuanzia mshahara wa mhudumu wa afya kitakuwa sh 670,316 na mshahara wa juu utakuwa sh mil. 8.1 kwa mwezi. Utekelezaji wa pendekezo hili utagharimu sh bil 83.5 kwa mwezi ambayo ni sawa na sh bil. 417.5 kwa kipindi kilichobaki cha miezi mitano,” alisema.

Pinda alifafanua kuwa kwa mujibu wa mapendekezo hayo mshahara na posho, daktari anayeanza kazi atapata sh mil. 7.7 na daktari mshauri mwandamizi atapata sh mil. 17.2 kwa mwezi.

“Endapo madai hayo yatatekelezwa kwa mwaka mmoja jumla ya mishahara yao itakuwa sh bil. 799.7 badala ya sh bil. 222. 2 hadi kufika Juni 2012.

Kiongozi wao si daktari
Katika hatua nyingine, Pinda alisema kuwa katika uchunguzi wao walibaini kuwa kiongozi wa mgomo, Dk. Ulimboka alihitimu shahada ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2004 na kupata usajili wa muda No. 2022 wa Baraza la Madaktari mwaka huu na kupangiwa internship Muhimbili.

Alisema kuwa Novemba 2005, aliongoza mgomo wa madaktari nchini na usajili wake ulisitishwa na kushtakiwa mbele ya baraza hilo kwa ukiukaji wa maadili ya taaluma ya madaktari kwa kutishia na kufanya mgomo.

Mwaka 2006 Rais alimsamehe na hivyo kurejeshewa usajili na baraza na kuruhusiwa kuendelea na internship.
“Katika kumpa taarifa za msamaha wa Rais, Wizara ya Afya na Baraza la Madaktari walimtaka Dk. Ulimboka kutojihusisha na migomo au suala lolote kinyume na maadili ya udaktari ambapo Februari 2, 2007 alikiri sharti hilo kwa maandishi.

Hadi sasa hakuna taarifa kama alimaliza internship kwa kuwa hajawasilisha cheti cha kumaliza mazoezi hayo na hatuna taarifa anafanya kazi wapi ila si mtumishi wa serikali na hajasajiliwa kama daktari, alisema Pinda.

Dk. Ulimboka anena
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, alisema hakuna sheria ya kumfukuza mfanyakazi asiyeenda kazini kwa siku moja na hivyo kuwataka madaktari waendelee kukaa nyumbani.

Alisema leo wanafanya taratibu za kisheria ili kesho wakutane kuzungumzia mgomo huo ambao sasa serikali inaonekana kutaka kutumia nguuvu kuwasambaratisha.
Alibainisha kuwa sababu ya wao kushindwa kwenda kukutana na Waziri Mkuu jana ni kuchelewa kupata barua ya wito wa kuitwa kwenye mkutano.

“Sisi tulipata barua saa 11 jioni na tukaandika barua kumjibu Pinda kuwa hawawezi kukutana leo kwa kuwa wenzao wengine wameshatawanyika, pia tulifanya hivyo kwa kuwa jana tulitarajia wenzetu kutoka mikoani wangewasili Dar es Saalam.”

Kuhusu kutohitimu mafunzo ya udaktari, alisema huo ni uongo kwa kuwa alimaliza mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Muhimbili na kutunukiwa cheti chake cha udaktari mwaka 2007.


 
Namjua nje-ndani Dr Ulimboka;ni Dr wa ukweli mwenye cheti;Pinda kama kasema hivyo basi kaongopa tu kufuatia kiwewe cha mgomo!By the way kama hana cheti ilikuaje apelekwe intern?Usipomaliza intern ndiyo unakuwa siyo Dr?Kipi kinatangulia kati ya kuapa kiapo cha uaminifu kuwa Dr au intern?

Pinda hajui asemalo na ni aibu kwa kiongozi wa level ya MP kuwa muongo!
Askofu una Mikwala Sana hebu tuwekeeni Ushahidi tujue nani ni mkweli au tuna Waziri Mkuu Kilaza kama Mkuu wa Kaya... Hii Chichiem imezalisha Mashetani badala ya Viongozi.. Vyombo vya Dini kemeeni hawa Magaddafi ya Tanzania
 
Msingi wa yote ni kiburi cha madaktari kukataa wito wa mkubwa. Ndipo watanzania tumejulishwa Dr. Ulimboka mtu gani:
1. 2005 aliongoza mgomo Muhimbili
2.. Akasimamishwa na kupewa onyon kali na MAT
3. 2006 Rais akampa msamaha
4. Aliandika barua kwa MAT kuomba msamaha na kuahidi atajihusisha tena na migomo
5. Rekodi zinaonyesha mafunzo ya intern hajamaliza
6. Hana cheti cha udaktari

7. Ni mfanyakazi wa NGO ya UKIMWI

Hapo Pinda asilaumiwe bali Ulimboka ahukumiwe kwa kuwaburuza madaktari
Contradicting statements: i. Alisimamishwa kama nani? Muuza mitumba?
ii. MAT ni chama cha Madaktari (Medical Association of Tanzania), angewezaje kuandika kuomba
msamaha kwa jumuia ilyokuwa haimtambui?
iii. Mafunzo ya Intern hufanywa na madaktari waliohitimu ambao baada ya kuwaridhisha wanao-
wakagua huidhinishwa kupewa leseni ya kufanyia kazi kama madaktari. Ilikuwaje huyu jamaa
tunayeambiwa hana cheti cha udaktari kuhudhuria Internship? Kumbe kuna uzembe wa
kuwahudhurisha mafunzo ya Internship hata wasiomadaktari kama mimi teksi dereva?
iv. Pinda ni mwanasheria mwenye rekodi ya uongo uliokithiri kama ilivyothibitishwa Bungeni, na safari
hii anauthibitishia umma tena, eti Ulimboka alisamehewa na Rais, lakini hajamaliza "Internship"
hadi leo! Itakuwaje huyo jamaa akitoa vyeti vyake hadharani? Atajiuzulu?
My take: Si sahii kwa mtu mkubwa kama Waziri Mkuu kutoa taarifa hadharani zisizo sahihi kwani zinaweza kumwonyesha kama mtu asiye makini.
 
Taratibu naanza kuelewa kwa nini hadi dakika hii ninapoandika Raisi wa Jamhuri ya Tanzania ni Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu ni Mizengo Kyanza Peter Pinda!
 
Taaluma si cheti, Ulimboka ana elimu ya udaktari...no matter amepokonywa leseni ya udaktari ila nikienda kwake atanipa tabibu ya maradhi yangu. Kuna mwalimu mmoja alifukuzwa kazi na kufutiwa cheti chake akihusishwa na kuvujisha mitihani. Huyo mwalimu ni hazina kubwa kwangu kwani alikua na darasa la tuition! Amewasaidia watu wengi hasa A'level kanda ya Dsm. Kinachomata hapa si leseni wala vyeti, JE taaluma hiyo ya udaktari anayo kichwani?!
 
Taaluma si cheti, Ulimboka ana elimu ya udaktari...no matter amepokonywa leseni ya udaktari ila nikienda kwake atanipa tabibu ya maradhi yangu. Kuna mwalimu mmoja alifukuzwa kazi na kufutiwa cheti chake akihusishwa na kuvujisha mitihani. Huyo mwalimu ni hazina kubwa kwangu kwani alikua na darasa la tuition! Amewasaidia watu wengi hasa A'level kanda ya Dsm. Kinachomata hapa si leseni wala vyeti, JE taaluma hiyo ya udaktari anayo kichwani?!

Nam challenge aanzishe hospitali yake akachukue mkopo benki halafu awalipe madr. huo mshahara wataacha kazi serikalini watakuja kufanya kazi kwake..

Hapo nitamuona ana kichwa kweli lakini otherwise akagombee ubunge perido..udr..amezingiziwa si fani yake..
 
Hatuhitaji mtu kutuambia kuwa, hata viongozi wetu nao wanataka mabadiliko ila njia ya kufikia ndiyo bado ina mambo mengi ya kupambana nayo ikiwa ni pamoja na kuwatoa watu uoga, kuwajaza hasira wananchi pamoja na kutengeneza mazingira ya kuwatoa kirahisi walio madarakani.
 
Back
Top Bottom