mfereji maringo
JF-Expert Member
- Nov 19, 2010
- 1,037
- 251
lipumba akíombea halafu akakosa si heshima yake itashuka sana jamani? tumwache tu kwa ajili ya 2015 urais.
CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.
Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:
- Ni mzaliwa wa Tabora
- Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
- Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
- CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.
Mkuu,
Tukiweka mbali ushabiki wa Chama tunahitaji mtu kama Lipumba bungeni. Hali ya uchumi wa nchi unaenda kombo na walioko bungeni sio wajuzi wa uchumi waliobobea Lipumba anaweza kuongeza nguvu bungeni kuzidi kuikosoa serikali iliyo madarakani.
Igunga imekuwa wilaya ya mwisho kimaendeleo ukilinganisha na wilaya zingine za mkoa huu wa Tabora. Hakuna maji, zahanati hovyo, shule hazina walimu, hakuna mikakati ya maendeleo. Nashangaa wanaosema rostam kaliliwa na watu si kweli hata kidogo labda kwa wale vibarua waliokuwa wanashiba kwake.
Nahauri Igunga iwatumie vijana hao niliowataja wanaweza kufanikisha maendeleo ya Igunga.
kwani NEC ndio magamba?huo uchaguzi NEC wataubania usifanyike sasa hivi mpaka wapate mtu ambaye wana uhakika atashinda from ruling party