Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

Chadema tunaamini ktk mabadiliko, na vijana ndio nguvu ya mabadiliko, Vijana makini na mahiri ndani ya chadema wapo wengi sana! Chamsingi Dr. asimamie na ashiriki kisawasawa katika upatikanaji wa kamanda
 
The parliament is one of the most important platforms for a political party to portray itself. If Chadema thinks it is unlikely to win Igunga with another candidate then Slaa should go for that. By the way, Igunga is also going to send signals of the future of Tanzania's politics.
 
Bora Dr.Slaa asiende Kugombea!Akidondoshwa kwenye Kinyang'anyiro atachuja ile mbaya!
 
Dk. Slaa asiende kabisa. Ila kwa Lipumba angefaa sana lakini siku hizi CUF hawaaminiki kabisa.
 
great idea! nadhani tukiacha ubinafsi wazo hili ni zuri.tunahitaji upinzani wenye nguvu zaidi ili kuwakomboa watanzania dhidi ya utawala dhalimu wa ccm.tukumbuke kuwa hata jirani zetu kenya hawakuweza kumpindua dikteta moi hadi pale walipoamua kuacha tofauti kikabila Raila (mjaluo)akakubali kumuachia kibaki(mkikuyu).tuache ubinafsi wa vyama.........uzalendo kwanza.kwani wote si tunalala gizani?
 
Prof. Lipumba awe mgombea wa Upinzani Tabora.
Labda kwanza ahame CUF ajiunge na Upinzani.
Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.
Ni kweli lakini faida zipi umeziona zimeletwa na Wabunge wa CUF ? Nitajie hata moja tu.
Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga.
Kwa nini ashinikizwe ? Unataka kuniambia huwa anashinikizwa kugombea Uraisi - mara nne zote !
Ni mzaliwa wa Tabora
Toka lini Tabora imetoa mbunge wa Upinzani pamoja na Pro. Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF na mgombea Uraisi wa kudumu ?
Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Hii CUF iliyojitoa Upinzani ikidai wapinzani wahuni ?
  • Hii CUF ambayo mgombea wake wa Uraisi Zanzibar anagonga whisky Ikulu ?
  • Hii CUF ambayo toka uchaguzi uliopita imeshirikiana na CCM kukihujumu Chadema ?
  • n.k., n.k.
Come on, be serious please !
Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
You must be kidding !
CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.
  • Chadema itajijenga lini pale ambapo hakina nguvu kama lengo ni kukijenga CUF ?
  • Wengine tunakumbuka Chadema ilivyoiunga mkono CUF mwaka 2000 lakini CUF ikaitolea nje Chadema mwaka 2010.
  • Watu wa Igunga watawaelewaje wana Chadema kama badala ya kukinadi Chadema wanakinadi CUF ?
  • Sikubali na ni heri kuukosa Ubunge kuliko kuwasalati wapiganaji wa kweli wenye kiu cha mabadiliko ya kweli.
  • Kama Mwenyekiti wa CUF, Lipumba ameshindwaje kukemea usaliti unaofanywa na wabunge wa CUF bungeni ?
Hapana Mafia Yetu, sikubaliani na wewe kata kata.
 
CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:

  • Ni mzaliwa wa Tabora
  • Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
  • CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.

CUF has been playing a passive role in the parliament. hapo kwenye red sidhani kama kweli ataimarisha upinzania. Mapambano yote ya Chadema hajawahi kuyaunga mkono.
 
Naomba nieleweshwe kwenye hili: CUF si wamesema wamejitoa kambi ya upinzani bungeni? Sasa mnaunganisha nguvu ipi tena mnavyosema Lipumba anafaa? Nionavyo mimi wapinzani wote waunganishe nguvu kupambana na chama tawala lakini Lipumba au CUF hapana; isije ikawa mnaongeza another Shibuda in the building. Wapinzani msiangalie tu nani atashinda, lakini muangalie huyo mtu atakuwa productive bungeni?. CUF kwakweli hawajawa na uhakika wanataka nini hasa kutokana na matamshi yao, nahisi pia wao wenyewe hawajielewi. CUF Zanzibar inaonekana kuwa ni chama ndani ya CCM so it is hard kwa CUF bara kujiita wapinzani. That being said, sioni kwanini (wapinzani bara) m-take risk yakumuweka Lipumba in these critical times.
 
Hao CUF ni lini wamekuwa tayari kuwasaidia CHADEMA? na ni lini wanashirikiana na CHADEMA? tusijisahau mambo wanayowafanyia CHADEMA Bungeni
Lipumba alikabidhi katiba yao CCM, sasa CDM aje kutafuta nini? CUF ni demu wa CCM inamaana wanataka amiliki wanamme wawili?
 
Slaa ninayemjua mimi hawezi enda kugombea ila Lipumba aende tuu ili nae aonje ubunge unakuwaje na uchumi wake utusaidie kurekebisha mambo!
 
duhu naona dk slaa tayari ashakubali kutogmbea. cdm iwaachie cuf yaani pro lipumba
 
"Ameshakubali kutogombea"!!! hiki ni kiswahili cha wapi? umeshindwa hata kusema Dr Slaa amekataa kugombea Igunga?

tz ni kubwa baba/dada. ndio maana ukiwasikia wamasai, wasukuma, wanyamwezi. wagogo, wanyiramba, waturu, wahaya, wamakonde, wamangati, wazanaki. wanavyoongea na kuandika kiswahili utaanguka. lkn ukiwasikia wahariri wanavyoandika kiswahili chetu utazimia. basi tuvuliane tu
 
Back
Top Bottom