Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

Ni kweli mkuu, si kwa jimbo la Igunga tu hata katika majimbo mengine kama Sikonge, Tabora Mjini, Kaliua, Urambo, Nzega - CDM inakuwa ya 3 baada ya CCM na CUF. ni kweli kutakuwa na challenge kubwa hasa ukizingatia kambi za CCM katika jimbo la igunga bado ipo thabiti unless RA aamue kutojihusisha na kampeni, maana karibia kila kaya katoa bima ya afya kwa maana hiyo anawajua wapiga kura wake wote wa igunga na kadi zao za kupigia kura zipo kwenye mafaili yake.

Anyway, Pamoja Tutashinda - Sababu Chadema ni mtetezi wa wanyonge, kimbilio la wenye shida na sera zake zinauzika.
Wasiwasi wangu ni yeye kushirikiana na wanasiasa uchwara (gutter politicians) najua mpiga debe mkuu wa CCM atakuwa Nape piga picha hiyo.
 
Acheni mambo yenu bwana
Hatuwezi kuendesha nchi wala vyama kwa misingi ya ajabu namna hii.
na wote ni mashahidi kwamba katika nchi yetu maamuzi yote ambayo
hufanyika kwa misingi hii hayajawahi kuwa na faida kwa upande wowote
ule, hayajawahi kuwa na faida kwa vyama husika vya siasa wala kwa wananchi.

Swala la kumshinikiza Lipumba kugombea halina uhusiano wowote na Chadema
kutogombea, Nchi hii haitoongozwa na vyama vya siasa Imara bali itaongozwa na
Chama cha Siasa Imara. Acheni wote watatu wapambane, CUF, CCM na CHADEMA.

Kama Lipumba hakuona umuhimu wa kumuachia DR amuondoe Jakaya Ikulu kirahisi
hakuna sababu yoyote ya CHADEMA kumuachia Lipumba wala CUF kupata ushindi
bwerere katika nafasi yoyote ya uongozi.

Sitaki kusikia Siasa za Hovyo Hovyo namna hii, tena nimechukizwa sana kuona
kwamba bado kuna watu wanaujasiri wa kutoa hoja za namna hii, nimeichukia
hoja hii sana na nimemchukia mtoa hoja pia.

Wote ni Mashahidi kwamba, kabla, na baada ya Uchaguzi CUF na Lipumba in
person, wametumia nguvu kubwa sana katika kuhakikisha inakichafua CHADEMA
kwa kila namna.

Baada ya Uchaguzi, Wakati Chadema wanaandamana kupiginia mambo ya msingi
kwa watanzania, CUF na Lipumba walianza kuzunguka kote wanakojua wanasikilizika
na kutangaza kwamba Chadema ni Chama cha Udini.

Achana na Patrinership yao na CCM Zanzibar, sababu sijawahi kuona ubaya wake,
as long as Wazinzabar waliona unawafaa wao kama jamii, CUF waliendeleza informal
partinership na CCM Bungeni, ili kufisha vyote viwili, nguvu ya Upinzani Bungeni na
Nguvu ya Chadema pia.

Waoh, where do you get the guts to recommend Chadema not to go for
Igunda for the sake of CUF. come on.

Let them all go for it. Igunda will decide for their own interests.
Umesomeka sana mkuu hata mimi nawashangaa wanaotaka muungano wakati huu
nafikiri hata uongozi wa Chadema utapuuza, kumbuka CUF walivyokuwa wanabeza maandamano
bora kujulikana umeshindwa kwa jitihada zako kuliko kushinda kwa muungano wa kinafiki.
 
..compromise ni Prof.Lipumba kuhamia CDM halafu asimamishwe kugombea ubunge Igunga.

..tatizo la Prof.Lipumba ni kwamba anapenda kujipendekeza na kumchekea-chekea JK. hana tofauti na Zitto linapokuja suala linalomhusu JK, they just cant help themself. They would rather go against their parties.

..naomba mrejee concession speech ya Prof.Nguyuru Lipumba. yaani ukimlinganisha na JK siku ule utaona kabisa kwamba Prof.Lipumba would have made a better president.

Kujipendekeza si ni hulka na sifa za kwetu nani kati yetu asiyejipendekeza kwa bosi wake??? Mnazungumza tu katika keyboard ila ukweli ndio huo. Hiyo nyekundu is absolutely true hatuzungumzi udini, ukabila ila tunazungumzia competence.

Kuwa na mbunge kama Lipumba ni better off than wabunge kama kina Zainab Kawawa na wengineo wa CCM. Wabunge wa CCM 100 wanafaa kwa Lipumba moja.

Pia na mazingira tuliyonayo tunahitaji wabunge makini bungeni badala ya wabunge wanaenda kuongeza idadi ya namba bungeni. Bunge imara la upinzani linaweza kuhimili serikali hii iliyopo venginevyo ufisadi hautaisha nchini. Mfano ni USA Obama anavyopata tabu na upinzani marekani hivyo na Tanzania inahitaji bunge imara la upinzani.

Mtu mwenye ujuzi wa kama Lipumba anafaa kuwamo bungeni kwa maendeleo na faida ya nchi yetu tukiweka unazi wa chama pembeni.
 
Mdondoaji said:
Kujipendekeza si ni hulka na sifa za kwetu nani kati yetu asiyejipendekeza kwa bosi wake??? Mnazungumza tu katika keyboard ila ukweli ndio huo. Hiyo nyekundu is absolutely true hatuzungumzi udini, ukabila ila tunazungumzia competence.

Kuwa na mbunge kama Lipumba ni better off than wabunge kama kina Zainab Kawawa na wengineo wa CCM. Wabunge wa CCM 100 wanafaa kwa Lipumba moja.

Pia na mazingira tuliyonayo tunahitaji wabunge makini bungeni badala ya wabunge wanaenda kuongeza idadi ya namba bungeni. Bunge imara la upinzani linaweza kuhimili serikali hii iliyopo venginevyo ufisadi hautaisha nchini.

Mtu mwenye ujuzi wa kama Lipumba anafaa kuwamo bungeni kwa maendeleo na faida ya nchi yetu tukiweka unazi wa chama pembeni.

Mdondoaji,

..Prof.Lipumba angetusaidia sana bungeni.

..huyu anatakiwa azoeleke kwenye masikio ya wa-Tanzania kwa michango yake bungeni.

..personally naamini anaweza kuja na nguvu kubwa zaidi ktk kugombea Uraisi akitokea bungeni.

..hakuna ubishi kwamba Prof.Lipumba ni kichwa ktk masuala ya uchumi. mwingine ninayemkubali ni Prof.Wangwe.

..Raisi pia anaweza kuwateua kuwa wabunge. bora angeteuliwa Lipumba kuliko Jussa na Hamad Rashid.​

Msema ukweli mpenzi wa mungu, [/FONT][/COLOR]
Pale Igunga Chadema hawana mtandao na hata katika uchaguzi mkuu ulliofanyika miezi 9 iliyopita CDM hawakusimamisha mgombea ubunge na kwa wale wasiofahamu Mgombea wa CUF Leopold Maona alimtikisa sana RA na wagombea ubunge walikuwa wawili peke yao, Matokeo yalikuwa RA (CCM) kura 35,674 na Leopold Maona (CUF) kura 11,321 lakini kwa waliofuatilia uchaguzi ule vizuri, Leopold Maona angeshinda kama siyo RA kutumia pesa nyingi na wizi wa hali ya juu.

Na kwa wale wasiojua chochote huyu Kijana Leopold anakubalika sana na kama CHADEMA watataka kutumia umaarufu wa ZITTO, Dr Slaa(Phd) na Helkopta kumshinda Leopold itakuwa vigumu sana. Kwa ujumla watu wa Igunga wanaiamini zaidi CUF kuliko CDM na kutokana na hali hizi zote CDM wataangushwa vibaya wakijaribu kumweka mtu yeyote kupambana na kijana yule.

My take; Kama CUF watajipanga na mgombea wao mapema watachukua jimbo la Igunga kama vile kumsukuma mlevi, ilimradi wajipange mapema.
 
Hakuna sababu kulazimisha ndoa hiyo waende kila mtu kivyake, wananchi watachagua mahali ambapo wanahisi kura zao zitatendewa haki. Mimi si kubali ndoa ambayo makusudio yake ni kushinda uchaguzi, napenda ndoa ambayo inamizizi ya mitizamo na itikadi vinginevyo ni kulazimisha mapacha kwa mwanamke tasa
 
..personally naamini anaweza kuja na nguvu kubwa zaidi ktk kugombea Uraisi akitokea bungeni.

Yaani tanzania hatuna mtu mwingine zaidi ya Lipumba kuwa rais,
hivi akigombea tena itakuwa mara yake ya ngapi kushindwa
inabidi sasa tuanze kuhesabu idadi ya kushindwa badala ya idadi ya kugombea
na ukijumlisha kura zake zote toka aanze harakati hafikii za Dr. wa ukweli aliyegombea mara moja.​
 
Msema ukweli mpenzi wa mungu,
Pale Igunga Chadema hawana mtandao na hata katika uchaguzi mkuu ulliofanyika miezi 9 iliyopita CDM hawakusimamisha mgombea ubunge na kwa wale wasiofahamu Mgombea wa CUF Leopold Maona alimtikisa sana RA na wagombea ubunge walikuwa wawili peke yao, Matokeo yalikuwa RA (CCM) kura 35,674 na Leopold Maona (CUF) kura 11,321 lakini kwa waliofuatilia uchaguzi ule vizuri, Leopold Maona angeshinda kama siyo RA kutumia pesa nyingi na wizi wa hali ya juu.

Na kwa wale wasiojua chochote huyu Kijana Leopold anakubalika sana na kama CHADEMA watataka kutumia umaarufu wa ZITTO, Dr Slaa(Phd) na Helkopta kumshinda Leopold itakuwa vigumu sana. Kwa ujumla watu wa Igunga wanaiamini zaidi CUF kuliko CDM na kutokana na hali hizi zote CDM wataangushwa vibaya wakijaribu kumweka mtu yeyote kupambana na kijana yule.

My take; Kama CUF watajipanga na mgombea wao mapema watachukua jimbo la Igunga kama vile kumsukuma mlevi, ilimradi wajipange mapema.

Hii imeshajibiwa katika thread nyingine leo- -- CUF hawawezi kwa sababu wamaekuwa sehemu ya magamba kutokana na uswahiba walifikiana. CUF imeshapoteza hadhi kama chama cha upinzani, achilia mbali kama chama cha upinzani chenye nguvu. Maelewano huko Zanzibar umemfanya POrofesa Lipumba kuonekana kalowa sasa hivi ni kama hana tena hamu na siasa.

Ingekuwa ni kipindi kile cha CUF jino kwa jino, ningesema CUF ingeshinda, lakini siyo leo hii. Mgombea wa CDM au NCCR aweza kushinda, siyo wa CUF.
 
Asante kwa kuonesha wazi hofu yako kubwa juu ya CHADEMA.
Kama Igunga wana akili hawawezi kuwapa CCM "A" wala CCM"B".
 
Msema ukweli mpenzi wa mungu,
Pale Igunga Chadema hawana mtandao na hata katika uchaguzi mkuu ulliofanyika miezi 9 iliyopita CDM hawakusimamisha mgombea ubunge na kwa wale wasiofahamu Mgombea wa CUF Leopold Maona alimtikisa sana RA na wagombea ubunge walikuwa wawili peke yao, Matokeo yalikuwa RA (CCM) kura 35,674 na Leopold Maona (CUF) kura 11,321 lakini kwa waliofuatilia uchaguzi ule vizuri, Leopold Maona angeshinda kama siyo RA kutumia pesa nyingi na wizi wa hali ya juu.

Na kwa wale wasiojua chochote huyu Kijana Leopold anakubalika sana na kama CHADEMA watataka kutumia umaarufu wa ZITTO, Dr Slaa(Phd) na Helkopta kumshinda Leopold itakuwa vigumu sana. Kwa ujumla watu wa Igunga wanaiamini zaidi CUF kuliko CDM na kutokana na hali hizi zote CDM wataangushwa vibaya wakijaribu kumweka mtu yeyote kupambana na kijana yule.

My take; Kama CUF watajipanga na mgombea wao mapema watachukua jimbo la Igunga kama vile kumsukuma mlevi, ilimradi wajipange mapema.
maneno yako yalikuwa na ukweli miezi 8 iliyopita lakini sio hivi leo tena maana hali ya kisiasa imebadilika sana, CUF ya kabla ya uchaguzi siyo cuf ya leo hii tena kwani cuf ya leo ni sehemu ya serikali hawana tena nafasi wliyokuwa nayo kabla ya uchaguzi, wabunge wa cuf bungeni wengi ni inactive bungeni na ukiangalia chadema ya kabla ya uchaguzi siyo chadema ya leo hii tena kwani chadema ya leo ni chama kilicho na watu makini na resources za kutosha ukilinganisha na chadema kabla ya uchaguzi na pia ccm hivi sasa imechoka kuliko ya ile ya kabla ya uchaguzi kwani utendaji wake umeshuka mno bungeni wamekuwa kutwa kucha wakitetea posho na maslahi yao binafsi badala ya kushugulikia matatizo ya wananchi na wananchi tumewaona chadema wakipigania maslahi ya umma siku hadi siku. kwahiyo kama upo karibu na huyu leopold kama kweli anataka ubunge basi agombee kupitia chadema na si cuf tena.
 
mgonjwa huyo...hata wana igunga jana wakati wanalia walisema kuwa sasa tegemeo lao ni dr slaa
 
ukiangalia kwa makini leopold alikuwa very weak candidate na hasa ukizingatia aliachiwa jimbo peke yake na chadema ukilinganisha na maneno yako unayosema kwani alipata asilimia 32 ya kura alizopata RA kwahiyo huo ushindani unausema siuoni ukiangalia takwimu zako amepata kura chache mno kwani amepata low tenth afadhali angekuwa higher twenth hapo kidogo ningesema lakini ukiangalia hizo namba kwa makini pamoja na wizi still bado leopold alikuwa weak candidate.
 
Huyu naye sijui ni wa wawapi .Huyo mgombea wao labda anaweza kuingia Chadema kesho unajuaje ?Hofu tuuuuuuuuuuuu jamani .
 
Hapa mtoa mada hana ajenda, kwani ukweli ni kuwa CDM imeshinda nafasi za udiwani Igunga na wana madiwani 3 katika halimashauri hiyo.
Diwani wa klata ya Igunga Mjini ni wa CDM sasa mtu anaposema kuwa CUF ina nguvu ilipata diwani? kura za urais zilikuwaje kwani Lipumba alipata ngapi na Dr.Slaa alipata ngapi na hivyo tujue kuwa CUF ina nguvu?

CDM imeshafanya siasa Igunga baada ya uchaguzi Mkuu uliopita , ila CUF hawajaenda tena huko sasa leo watakuwa nan nguvu kutoka wapi?
 
mnaodai kuwa lipumba ana nguvu sana igunga mnatumia vigezo gani ?? kigezo kizuri ni data je mnazo data kuthibitisha maneno yenu??
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom