Pendekezo: Madaraka Nyerere awe mgombea urais wa CCM

Marehemu CHADEMA, Hamuji tu kuwa nyie ni marehemu, subirini mwone. CCM Gari kubwa huliwezi wewe nyangau.
ivi ccm inaingia ktk uchaguzi bila kujivua gamba, we kada washauri magamba wenzako ata leo akifufuka nyerere akasimamisha, kichapo kipo palepale, chadema lazima itang'ara, chura we........
 
mnatuahidi hivyo hivyo hapa kila wakati lakini baada ya chaguzi huwa mnakuja na mabegi ya sababu kwanini ccm magamba wamewashinda ikiwemo ile sababu maarufu "wamechakachua",Yani kutwa mnachakachuliwa nyie tu,wapinzani tuache maneno tujipange kikweli ka sivyo kila siku tutakua tunapeana moyo kwamba tulishinda lakini tumechakachuliwa,tukae tujiulize hivi ccm wanatushindaje?

wewe hujui kitu kuhusu madarka nyerere mbona unakulupuka kama umeguswa kunako masaburi.?
 
Nani kamnyima kugombea..

ajue atapambana na wanachama halfu wananchi..jina la nyerere does not work in his favour nowdays.

Labda aache siasa za kale za baba yake..we will fight within
 
Alikuwa Waziri wa Fedha, alikuwa Waziri Nishati na Madini, alikuwa Ministry of foreign affairs.

Madaraka kashika cheo gani mpaka apewe urais

Suali bado liko pale pale. Kikwete alipochaguliwa alikuwa amelifanyia nini taifa? Kwenye nishati na madini si ndipo aliposaini mikataba
inayotuumiza hivi leo? Huyu jama alipaswa kuwa jela ni si Magogoni.
 
Aisee,
Amefanya mengi sana lakini wewe huwezi kuona ya JK bali ya nyerere na Slaa tu..

Wanajumuiya wenzako bana! kazi kwelikweli
 
Suali bado liko pale pale. Kikwete alipochaguliwa alikuwa amelifanyia nini taifa? Kwenye nishati na madini si ndipo aliposaini mikataba
inayotuumiza hivi leo? Huyu jama alipaswa kuwa jela ni si Magogoni.
Hujajibu swali bado! Au ndio umejitia kulisahau kama hujaulizwa vile eeenh?
 
Nchi yetu hatuna Mawazo ya kurithiana Uongozi, sasa wewe unataka kutuletea hayo kwa Misingi gani

1. Umetumwa na Prince?
2. Au Umetumwa na mtoto wa Mzee rukwa

Hayo ndio masuala mawili na kwa Prince lazima amekupa one of petrol station jijini Dar then one running 24hrs - U damn cheap
 
This is one of those interesting ideas. Sasa tukizungumzia mtu ambaye ni "outsider" ndani ya CCM bila ya shaka Madaraka ni mmojawapo. Kinyume na inavyidhaniwa jina lake limsaidia sana na litagawa taifa vizuri sana. Katika orodha yangu kwa upande wa CCM ameshika namba mbili kwa sasa. Natafuta sababu ya kumfanya namba moja wa CCM.
 
Kwani niwaulize Watanzania si kuna majina mengine si kuna Husssein Mwinyi , Ridhwan Kikwete , Kina Kawawa , Vikarume si Royal family zote hizi si watazania tunapenda majina makubwa tu ?
Watanzania wanaogopa nini kuweka new Royal Family au system inapanga tu na Watanznaia kazi yao kupiga makofi tu.
 
This is one of those interesting ideas. Sasa tukizungumzia mtu ambaye ni "outsider" ndani ya CCM bila ya shaka Madaraka ni mmojawapo. Kinyume na inavyidhaniwa jina lake limsaidia sana na litagawa taifa vizuri sana. Katika orodha yangu kwa upande wa CCM ameshika namba mbili kwa sasa. Natafuta sababu ya kumfanya namba moja wa CCM.

nisaidie CV yake Mkuu.
 
Alikuwa Waziri wa Fedha, alikuwa Waziri Nishati na Madini, alikuwa Ministry of foreign affairs.

Madaraka kashika cheo gani mpaka apewe urais

Urais is cheo cha kupewa ni cheo cha kuchaguliwa na wananchi vyeo vya kupewa ni hivyo ulivyoorodhesha alivyowahi shika JK kabla hajachaguliwa. Kushika vyeo vya kupewa si pre-requisite ya kuchaguliwa urais. Urais anaweza chaguliwa mtu yeyoye yule aliye-qualify. Kama ana-qualify ana haki ya kuchaguliwa, moja ya qualification ni kufanyiwa public vetting. CCM wamekuwa wakituwekea watu ambao hatuwafahamu vizuri matokeo yake wanakimbia hata midaharo ili tusiwajue. This time wasipofanya hivyo itabidi wajiandae vizuri. Maana itakuwa ndoto kupata kura halali.
 
Tuanze kwa kujua sifa za rais tumtakaye kwa mazingira ya sasa kisha tuangalie nani mwenye sifa hizo.

Kwani inatofauti gani na sheria za manunuzi? Mkijadili watu ni sawa na kusema mnataka Richmond ipewe tenda pasi kuangalia vigezo.
 
Tukishaweka mezani sifa za raisi tunayemtaka watanzania hapo ndipo tutaweza kumpima Madaraka Nyerere kama naye anakidhi vigezo.

Lakini hii ya kulipuka tu kwamba kaifanyia nini nchi hii mara katoka familia ya baba wa taifa haina tija yoyote kwa maendeleo ya nchi yetu.

Mwaka 2005 tuliletewa bonge la kabrasha limejaa sifa za mgombea wa ccm, nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya ccm na serikali, na bila kutafakari ili tuone kama kuna lolote la kujivunia alilowafanyia watanzania kwa kuteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, tukaingia mkenge na hadi leo tunalalamika kila siku mambo hayaendi.

Sasa tujifunze kuainisha sifa za mgombea badala ya kuainisha majina ya wagombea.
 
Back
Top Bottom