Kuchapisha Fomu Moja 2025 Kwa mgombea wa CCM, Demokrasia imezingatiwa?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,110
22,563
Salaam, Shalom!!

Jana 2/1/2024, wamesikika viongozi wawili wa chama Cha MAPINDUZI Mzee Kinana na Ndugu Majaliwa Kassim,wakiibua HOJA ya kuzuia wagombea na watia Nia wengine ndani ya chama kutokudiriki kuchukua fomu ya ugombea urais, Kwamba itachapishwa fomu Moja tu Kwa Sa100.

Kwa kuwa hatukuwahi kufiwa na Rais aliyepo madarakani, na Kwakuwa sa100 hakupita mchujo ndani ya chama kama mgombea urais2020 Bali kama mpambe wa mgombea Urais, IPO haja ya kuruhusu wagombea wengine wamchukue fomu na mchujo upite.

HOFU ya HOJA ya kuchapisha Jina Moja Kwa mgombea wa CCM inatoka wapi ilhali mkt ana kofia mbili?

Hivi ikitokea mgombea huyo ameghairi kugombea, mtarudisha vp mchakato wakati mmeshapiga stop watia Nia wengine?

Tukiendelea na mawazo haya, vyama vya upinzani IPO siku wagombea Urais watazuiwa kuchukua fomu Ili kumrahisishia njia mgombea wa CCM mwenye HOFU ya changamoto ya upinzani ndani na nje ya chama.

Karibuni 🙏
 
Salaam, Shalom!!

Jana 2/1/2024, wamesikika viongozi wawili wa chama Cha MAPINDUZI Mzee Kinana na Ndugu Majaliwa Kassim,wakiibua HOJA ya kuzuia wagombea na watia Nia wengine ndani ya chama kutokudiriki kuchukua fomu ya ugombea urais, Kwamba itachapishwa fomu Moja tu Kwa Sa100.

HOFU ya HOJA ya kuchapisha Jina Moja Kwa mgombea wa CCM inatoka wapi ilhali mkt ana kofia mbili?

Hivi ikitokea mgombea huyo ameghairi kugombea, mtarudisha vp mchakato wakati mmeshapiga stop watia Nia wengine?

Tukiendelea na mawazo haya, vyama vya upinzani IPO siku wagombea Urais watazuiwa kuchukua fomu Ili kumrahisishia njia mgombea mwenye HOFU ya changamoto ya upinzani ndani na nje ya chama.

Karibuni 🙏
Ndio demokrasia yenyewe hiyo. Siyo kila siku kukopi kwa wengine
 
Salaam, Shalom!!
Hivi ikitokea mgombea huyo ameghairi kugombea, mtarudisha vp mchakato wakati mmeshapiga stop watia Nia wengine?
Karibuni 🙏
Mkuu Rabbon , hii ndio demokrasia ya CCM, ni utaratibu wao wa ndani, na hiki ndicho kinachokwenda kutokea 2025, fomu itatolewa moja, ila haitaandikwa jina, Mama Sa100 ataichukua na kumpatia amtakaye kama tulivyo shauri kwenye mada HII

Mpaka sasa nimeishapewa majina ya watu 3 wa 2025
Wa kwa ni mtarajiwa Maza mwnyewe!. Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Wa pili ni Kama Sauti Hii ni Sauti ya Kweli, Nimeelezwa Mpango Ndio Mpango Mzima!. Swali ni... Akiwa Mkristo, Kwanini ni Lazima Awe Mkatoliki?!

Wa tatu ni Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

P
 
Mkuu Rabbon , hii ndio demokrasia ya CCM, ni utaratibu wao wa ndani, na hiki ndicho kinachokwenda kutokea 2025, fomu itatolewa moja, ila haitaandikwa jina, Mama Sa100 ataichukua na kumpatia amtakaye kama tulivyo shauri kwenye mada HII

P
Pasco hata kwenye IGA ya DP World, ulishauri kuwa HGA zitakuwa wazi na kujadiliwa bungeni.

Baada ya lengo lako kutimia, kimyaaaa!!
 
Mkuu Rabbon , hii ndio demokrasia ya CCM, ni utaratibu wao wa ndani, na hiki ndicho kinachokwenda kutokea 2025, fomu itatolewa moja, ila haitaandikwa jina, Mama Sa100 ataichukua na kumpatia amtakaye kama tulivyo shauri kwenye mada HII

P
Na bado kuna watu wanasema Mbowe amekaa sana katika uenyekiti wakati CCM hata mwenyekiti Taifa hashindanishwi na yeyote!
 
Na bado kuna watu wanasema Mbowe amekaa sana katika uenyekiti wakati CCM hata mwenyekiti Taifa hashindanishwi na yeyote!
Pamoja na yote, mwisho ni miaka 10!. Chadema katiba original iliweka ukomo wa miaka 10, kwenye marekebisho ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006, hicho kipengele kiliyeyushwa na watu 2, huku aliyekuwa Katibu Mkuu, Dr. Wibroad Slaa hajui, wala John Myika hajui!. Angalia michango yao kwenye hoja hii Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
P
 
kwenye marekebisho ya katiba
Mkuu unaheshimika sana humu JF usifanye misinformation.... 2006 iliandikwa katiba mpya maana chama kilizinduliwa upya (rebranding) 2004. So yalikua maoni mapya kabisa yaliyoandika katiba mpya sio eti ammendments!!

Hili limeshakua clarified na Dr slaa pamoja na Mnyika tokea 2011 na nyuzi zipo humu humu msipotoshe.
 
Back
Top Bottom