William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Ukorofi wa Mchungaji unafikia hatua ya kuuliza, je tunashangilia nini cha msingi ikiwa ukweli ni kuwa hili ni changa la macho na Kampeni za CCM kushida uchaguzi wa 2010 kwa kishindo cha tufani ya Katrina umeanza?
Mkulu Kishoka,
Heshima mbele bro, kwa kweli kinachoendelea so far ni mapema mno kusema wazi kwamba exactly ni nini hasa, between sheria na siasa, lakini:-
1. Wananchi wa Tanzania, tumeonewa vya kutosha na tumenyanyaswa na viongozi hasa wezi kwa muda mrefu sana, wakati wa Sokoine na uhujumu uchumi tumeona dagaa wakiswekwa lupango, huku papa wakiendelea kunawiri na kutucheka, tunasikia Sokoine alitaka kufanya kweli lakini Mwalimu alikataa kabisa, sasa this time is for real tunaona papa wakiswekwa lupango.
- Tena ninaaambiwa kwamba hata kuwaweka rumande hii week end nzima imefanywa kwa makusudi makubwa na "someone", kwa sababu siku ya Ijumaa baada ya kuwakilishwa kwa kesi yao ya kuomba dhamana kule mahakama kuu, mawakili wa serikali walipotea kwa makusudi na kutoonekana kwa muda mrefu sana knowing kwamba ruling haiwezi kutolewa bila ya wao kuwepo. Familia ya Yona did all they could kuwatafuta ikiwa ni pamoja na kuwapelekea gari kama watakwua wamekwama mahali lakini nowhere they could be found!
- By the time wamepaetikana ilikuwa late tena wakajitokeza wenyewe mahakamani na kupelekea the judge kuwakaripia sana, wao wakiwa wanatabasamu tu as if nothing happened, sasa unajiuliza ni kwa nini hasa kwa sababu ninaambiwa kuwa kuchelewa kwao ni moja ya sababu kubwa zilizopelekea kutoachiliwa kwa watuhumiwa.
2. Binafsi ninaamini kwamba this thing is for real kwa angalau 75%, kwa sababu ukishawafikisha Mramba na Yona, kwenye sheria ni lazima uende all the way to the end huwezi kuwaacha wengine kama the Richimonduli waliotutia hasara kubwa bongo kuliko all hawa wengine combined. Ni kweli in private mawaziri wengi wanadai kuwa uamuzi wa kutoa msamaha ulikuwa wa cabinet rais included, lakini let sheria take its mkondo kwanza, na besides ninaambiwa kwamba Yona na Mramba they are in for a long shit kwa sababu wana kesi nyingi sana pending na hasa Mramba.
- Lets say hawa tu wawili ndio watafikishwa mahakamani, can you imagine huko NEC na CC itakuwaje, kwa sababu unafikiri hawa wawili hawana wajumbe wa kuwatetea huko ndani na kutaka kujua kwa nini wengine hawajafikishwa kwenye sheria? Tayari kumeshaanza maneno ya udini, ukabila, na u-mtandao kuhusiana na kushikwa hawa Yona na Mramba, sasa rais kweli anaweza ku-take hiyo risk, jawabu kwangu ni kwamba hawezi tena hawezi kabisaa ni lazima wote watinge kwenye sheria tena soon, nasikia by next week kutakua na big news, infact tayari kuna habari za el kutafuta njia ya kukimbia!
3. Kwa taifa letu haya yanayoendelea sasa hivi hatukutegemea hata siku moja kuwa yanawezekana, lakini hatimaye sasa ni clear kua yanawezekana meaning kwamba from now on hakuna kiongozi atakayekua immune na sheria tena asilani, rais anahitaji pongezi nzito sana kwa hili ambalo hata Mwalimu hakuwa na ubavu nalo, WHY ninasema hivyo:-
- Sokoine alikuwa tayari ana list ya viongozi wa juu mawaziri wakiwemo aliotaka wakamatwe, kwa kuhujumu uchumi na pia alimuhakikishia Mwalimu kwamba ana ushahidi wa kutosha, kati ya viongozi hao walikwemo Barongo, na Kahama, katika kutayarisha ushahidi wake Sokoine alishikirikiana sana na Kaisi, na Kolimba. Lakini Mwalimu alipokataa wasishikwe, Kaisi ambaye sasa alikuwa RC Bukoba was so upset kwamba akaamua kwa hasira kumuweka ndani Barongo alipofika Bukoba, na hata Kahama pia lakini Mwalimu akamlazimisha kumuacha haraka sana the minute alipojaribu kule Bukoba uwanja wa ndege, wakati sir George anashuka kutoka Dar. Kina balozi Magombe wamefanya mambo ya aibu sana huko majuu, kina Maryogo na wengine wengi sana, lakini ninampa heshima rais kwa kuimaliza hii tabia ya kulindana kwa viongozi, rais ameweka mfano sasa ni wajibu wetu wananchi ku-take it form there!
3. Kwa wale wote wanaomjua muungwana kwa karibu, watakubaliana nami kwamba wakati wa kampeni zake za urais, pembeni pembeni kabla ya kufikia kwenye uwazi siku zote alikuwa na hoja nyingi sana zinazomsumbua kuhusu utawala wetu, lakini za muhimu zilikuwa tatu, (1). Viongozi mafisadi kuwafikisha kwenye sheria, (2). Nyumba za serikali walizouziwa viongozi, (3). Viongozi waliokaa kwenye power kwa muda mrefu sana. Hizi ni ishus nimesikia mwenyewe akizilalamikia sana kwa pembeni na leo nimeona akizigusa zote, ingawa kwenye la nyumba bado anasua sua, lakini haya mengine amejitahidi sana na hasa hili la viongozi na sheria.
4. Dataz zaidi nilizozipata jana ni kwamba kabla ya kufikiria kuanza kwa hii operation, kuna watu wetu walienda Zambia kula darasa kidogo on how to go about it, kwa hiyo kuna ka-muongozo flani hivi, ingawa ninaambiwa kwamba hata kule Zambia, operation ilikwenda safi sana mpaka ilipofikia kumkamata mstaafu wao wa idara ndipo mchezo ukasimama hapo hapo maana Mwanawasa, naambiwa aliiba uchaguzi na aliyeuiba ni huyu bwana mstaafu anayeitwa Chungu. Sasa je hapa Tanzania itakua hivyo hivyo kwamba hatutafika kwa mstaafu wa idara? Maana tusipofika huko kazi yote ni bure!
- Again ninaomba ksuema kuwa tuko kwenye the right track, na huu ni wakati wa kumpa rais ushirikiano wetu, na hasa ningetegemea kuwaona upinzani waki -take charge, maana huu ndio hasa wakati wao, pale tunapoambiwa hakuna ushahidi wao ndio wanaopaswa kujitokeza na ushahidi mzito, maana sisi wananchi walipa kodi tunawalipa ruzuku kila mwezi, sasa tunawalipa ruzuku for what kama sio watusaidie wka mambo kama haya?
- Kuendelea kumlaumu rais after all this kwa kweli sioni kama ni productive, kwa sababu rais anatakiwa afanye nini zaidi ya haya aliyokwisha fanya tayari? Amefungua mlango sasa sisi wananchi tu-take a charge na pia tu-take advantage, Mramba na Yona wako rumande sio kwa sababu ya kushindwa dhamana, isipokuwa ni kuthibitisha kwamba wahusika wa ushitaki wako serious, binafsi ninataka kutoa pongezi nzito sana kwa rais na wahusika wote wa hii operation, na ningependa kuwapa moyo kwamba baadhi yetu wananchi tuko nyuma yao na tuko tayari kuwapa msaaada ikibidi, lakini nasema hvi rais amefanya ya kwake, sasa ni zamu yetu wananchi kumalizia na hasa ninategemea Upinzani kutuongoza hapa, maana ndio hasa sababu ya kuwapa ruzuku.
Ahsante Rev!