Serikali yasaini Mikataba 4 ya Msaada wa Tsh. Trilioni 1.4

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Tanzania na Global Fund zimesaini mikataba minne ya misaada yenye thamani ya dola za Marekani milioni 606.9 sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.4 kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na uimarishaji wa mifumo ya afya nchini.

Mikataba hiyo imesainiwa Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha, Dkt. @mwigulunchemba1 na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Linden Morrison.

Waziri Nchemba amesema msaada kutoka Global Fund umepangwa kutekelezwa kwa miaka mitatu ambapo mpaka sasa Tanzania imepokea misaada kwa vipindi vinne ambavyo ni Julai 2012 – Desemba 2014, Julai 2015 – Desemba 2017, Januari 2018 – Desemba 2022 na Januari 2021 -Desemba 2023.

"Miradi inayotekelezwa kupitia msaada wa Global Fund kwa kipindi cha kuanzia Januari 2024 hadi Desemba 2026 itatekelezwa na Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha inaendelea kuwa Mpokeaji Mkuu wa Sekta ya Umma na Management and Development for Health (MDH) ni Mpokeaji Mkuu wa pili kwa Sekta Binafsi," amesema Waziri Nchemba.

WIZARA YA FEDHA
 
🌝🌝🌝
 

Attachments

  • 20240129_123832.jpg
    20240129_123832.jpg
    140 KB · Views: 2
Wizara ya Afya imesaini makubaliano ya Msaada wa Shilingi Trilioni 1.4 kutoka Global Fund Kwa Ajili ya Afya mbalimbali za Afya ambazo ni Ukimwi,malaria na kifua Kikuu.

Fedha hizo zitatolewa ndani ya miaka 3 ijayo kuanzia mwaka wa Fedha 2024/2025 Hadi 2027/2028.

Ikumbukwe Tanzania ni namba 4 Dunia kupokea pesa nyingi miongoni mwa Nchi zinazopata Fedha za mambo ya Afya kutoka Global Fund.

View: https://www.instagram.com/p/C2u_AFgqMMq/?igsh=MWpwcGtuem05ODdocA==

Angalizo.
-Hatutegemea kuwe na dollar crisis kuanzia mwaka wa Fedha ujao.
-Pamoja na vipaombele vya Global Fund ni vyema Serikali ikawa inawashawishi hao Watoa pesa wakubali vipaombele vya Serikali
-Mapesa hayo yatumike Kwa malengo stahiki badala ya semina zisizoisha,kampeni ambazo haziachi alama na miradi hewa Kupitia NGOs.

Mwisho
Serikali iwe inadai mrejesho tangible kutoka Kwa Wizara ya Afya Ili kufanya assessment ya value for money.Hizo pesa ni nyingi kuliko za Uviko 19 lakini Uviko Imetoa matokeo makubwa ,tunataka tuone mtokeo na huku.
 
......afya mbalimbali za afya.......

By the way huu ni pure msaada au mkopo wa namna fulani?
 
Zamani nikiangalia wazee wanaacheza bao utasikia anaeonewa anaitwa TUTUSA😂
@tunaupiga_mwingi_2024
 
Si mmesema ni msaada, hivyo, sitarajii deni la Taifa kuongezeka kwa nchi kupokea fedha hizi.
 
watalipana posho pekee na kununua majumba yao Dubai
Huu mfuko wa Global Fund ulianzishwa mwakanl 2002 na Koffi Annan akiwa SG wa Umoja wa Mataifa. Ni mfuko ulioanzishwa kukabiliana na magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria katika nchi za Africa, Asia na South America.

Kabla ya Mfuko huu wagonjwa walikuwa wanashindwa ku afford matibabu hasa ya UKIMWI kwa kuwa bei dozi ya mwezi mmoja ilikuwa inakaribia Tsh 300,000. Hivyo basi ni watu wengi hasa wa Third World waliokufa kwa ugonjwa wa UKIMWI.

Vyanzo vya mfuko huu ni michango ya fedha kama msaada kutoka nchi za USA, United Kingdom, Sweden, Canada, EU na makampuni makubwa kama Cocacola, Gates Foundation, etc

Misaada hii hutolewa kwa nchi ambazo zinakidhi vigezo na siyo mkopo.

Kuhusu ku-miuse hela za mfuko huu siyo rahisi kwa kuwa wasimamizi wa fedha hizi ni makampuni makubwa ya ukaguzi wa mahesabu. Kwa Tanzania zinakaguliwa na PWC
 
Back
Top Bottom