Paukwa... Pakawa!

"Kutokana na mambo yanavyokwenda inabidi na rais pia ajiuzuru ili kupisha haki itendeke kwa kila anayeusika,kama alinyofanya mbeki baada ya kushutumiwa kua anaingilia mwenendo wa kesi ya zuma.lakini kwa kiasi kikubwa kikwete hizi kesi zote zinamgusa kwa namna moja au nyingine,hivyo ili haki iweze kupatikana ni lazima na yeye hajiuzuru ktk hili."
Talk of Day Dreaming!....
 
"Rev Kishoka and other 'skepticists' ningependa kujua ni nini hasa mlitaka Rais afanye kwa sasa? Ajipeleke yeye mwenyewe mahakamani au? Nafikiri hata kama hatuamini sincerity ya Rais kwa sasa tutoe basi alternative wakati tunapom-critique! Inachukiza mtu aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote mafisadi kupelekwa mahakamani, hadi kuamini kuwa kamwe hawatapelekwa mahakamani sasa anabadilika baada ya kuona wamepelekwa. Process inapoanza anadai hakubaliani na hilo kwa sababu anayeisimamia hiyo process naye ni muhusika katika ufisadi. Kwa hiyo afanyeje sasa! aache?"

Mkuu mchungaji,
analysis yako nzuri sana kwa kuisoma. Mkuu Nurujamii amekuuliza maswali hapo juu...Ningeomba kujua majibu yako Mkuu.

Binafsi mtazamo wangu ni kua pragmatic, sasa ntapokutana na idealists phylosophies (ambazo ndio zime shamiri hapa jamvini),...napata tabu kidogo kuelewa ni nini hasa mkuu unachotaka kifanyike, under the contemporary Tanzanian political environment ili ufurahi kuwa kuna kazi ya kupambana na ufisadi inafanyika?
 
Waberoya,
Mkuu sasa na wewe unatoka nje kwa sababu anayewashitaki hao watu sio Kikwete isipokuwa ni serikali ya Tanzania. Sasa tunapojaribu kusema kuwa mhusika wa mipango ya kesi hizi ni Kikwete moja kwa moja tunakuwa tunapotosha Umma..
Kikwete ameruhusu vyombo vya sheria vichukue hatua kuhusiana na watuhumiwa na sidhani kama ni kazi yake kufungua ama kupanga mashtaka gani yafunguliwe wala sidhani kama ni yeye aliyefanya uchunguzi, tujaribu kutafuta kiini cha vitu hivi badala ya kulaumu tuuu..Mfano kwa nini Kuhujumu Uchumi haikuwa sababu kubwa ya viongozi hawa kupandishwa Kisutu..

Nimefurahi kusikia wanaowashtaki Mramba na Yona si Kikwete ila serikali, na wanafanya kazi pale Kikwete anapotoa go ahead!

So hatuna serikali, ila mpaka iambiwe na Kikwete!!!!!

hapa kutakuwa na uonevu, kuwa wezi fulani waende na wengine wasiende

Waberoya:

Inabidi utumie the following doctrine; "You go to war with the Army you have but not with the Army you might want or wish to have at a later time."

Unaposema JK jiuzulu, je hiyo process ya kuwapata watakatifu wa kuongoa mafisadi itafanyika wapi?

Na nani ame-guarantee kuwa atakayechukua baada ya JK kujiuzulu atakuwa bora zaidi?

Politics ni ku-seize the moment.

Kwa hiyo mwizi yeyote awe raiskwa sababu hatuna imani na atakayekuja!

Yaani katika watanzania milioni 40, we can not trust someone to lead us???

ina maana una confirm jamii ya watanzania ni fisadi wote, so siyo kosa kabisa Kikwete kuwa rais hata kama naye aliingia mikataba mibovu na kuua watu!!

Inabidi tuwe clean, siyo kusema huyu afadhali msafi kuliko huyu?? kichekesho hiki.

Mchakato mzima wa kumpata rais Tanzania ni kichekesho kwenye vyama vyetu, wanampata ka presha za muda huo na sio nini alifanya siku za nyuma.

UKIFIKA WAKATI UKAONA KIKWETE ANAFAA KWA URAIS NA UKAONA HAKUNA WA KUM-REPLACE BASI FORGET CCM WILL RULE FOREVER!!!!!!
 
"Rev Kishoka and other 'skepticists' ningependa kujua ni nini hasa mlitaka Rais afanye kwa sasa? Ajipeleke yeye mwenyewe mahakamani au? Nafikiri hata kama hatuamini sincerity ya Rais kwa sasa tutoe basi alternative wakati tunapom-critique! Inachukiza mtu aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote mafisadi kupelekwa mahakamani, hadi kuamini kuwa kamwe hawatapelekwa mahakamani sasa anabadilika baada ya kuona wamepelekwa. Process inapoanza anadai hakubaliani na hilo kwa sababu anayeisimamia hiyo process naye ni muhusika katika ufisadi. Kwa hiyo afanyeje sasa! aache?"

Mkuu mchungaji,
analysis yako nzuri sana kwa kuisoma. Mkuu Nurujamii amekuuliza maswali hapo juu...Ningeomba kujua majibu yako Mkuu.

Binafsi mtazamo wangu ni kua pragmatic, sasa ntapokutana na idealists phylosophies (ambazo ndio zime shamiri hapa jamvini),...napata tabu kidogo kuelewa ni nini hasa mkuu unachotaka kifanyike, under the contemporary Tanzanian political environment ili ufurahi kuwa kuna kazi ya kupambana na ufisadi inafanyika?

Sober,

Nurujamii ni mmoja wa watu ambao hushabikia na kulipa uzito ninaloliandika. Katika hili la mashitaka, anaonelea kuwa mbona sifurahi kinachotokea ambacho sikutegemea kitokee?

Jibu langu kwake na kwako ni hili;

Nikipima na kusoma kilichofanyika na hata "nia" ya kufikisha Mramba, Yona, Patel na Lukaza, natatizwa na lilelinalojionesha kwangu kuwa hawa wamepelekwa mahakamani si kwa nia au madhumuni ya kweli kuwa wachukuliwe hatua, bali ni kutokana na mashinikizo na sababunyingine za kufanya kuonekane kuwa sasa Serikali inafanya kazi yake.

Tumeshajiuliza sana hapa kuhusu suala la EPA kuwa Deloitte and Touche walifanya audit, wakatoa ripoti moja mbaya sana kuhusu BOT. Ripoti hiyo, hata Utoah ambaye ni mdhibiti na mkaguzu mkuu wa Serikali aliafikiana nayo na kutoa tathmini kuwa BOT imefanya kwa makusudi au kwa uzembe wa kupindukia kuruhusu hujuma za EPA.

Dr. Slaa akatoa kauli bungeni na sis tukapiga kelele, lakini Serikali yetu kwanza ikatoa kauli kukanusha kuwepo hujuma kubwa kama hiyo. Ni mpaka pale mabalozi wa nchi tajiri walipoanza kupiga kelele wakiongozwa na Mark Green wa USA, yule jamaa wa Neatherlands, Norway na Ujerumani na mpaka nchi moja wafadhili walipotoa kitisho kusitisha misaada (unakumbuka Membe alvyojibu kwa kiburi kuwa sisi ni nchi huru tusiingiliwe?) ndipo taratibu Serikali na Bunge la CCM likakubali kuna tatizo nao wakaipa kazi ya uchunguzi kampuni ya Earnst and Young.

Kina E&Y wakaja na majibu yale yale ya Deloitte Touche na Utoah, wakawasilisha serikalini. Rais na Serikali, wakaundia tume chini ya IGP, DPP, AG na Takukuru ambao walikuwa wanalipwa laki moja kwa siku. Kamati hii teule, ikapewa muda, nayo ikashindwa kumaliza uchunguzi ikabidi iombe iongezewe muda.

Kamati ilipomaliza utafiti na uchunguzi wake, ikawasilisha ripoti ikulu na kusema inasubiri uamuzi wa Rais.

Wabunge wakahoji, ripoti iko wapi? Ikulu ikasukuma ripoti kwa Sitta na wabunge watoe maamuzi, Bunge likajivua jukumu hilo, hivyo faili likarudi Ikulu.

Sasa wakati wa danadana hizi, Mama Killango akatoa kauli hapendwi mtu, wakaja kina Serukamba, Kisumo na Kingung'e kutoa kauli kali na chafu na kudai kuwa hakuna la msingi kuhusu EPA. Zaidi, CCM ikabadilisha kibao na kuanza kuhodhi sakata lote la EPA kwa kudai kuwa eti, wao ndio walioliibua na si mtu mwingine.

Wakati E&Y wanafanya uchunguzi wao, Manumba ambaye ni DCI alitoa kauli kuwa wao Polisi hawawezi kuanza kufanya uchunguzi wowote mpaka E & Y wamalize uchunguzi wao.

Sasa najiuliza, ikiwa karibu miezi 18 tumekuwa tukiimba EPA, EPA, EPA na kwanza Serikali na Waziri wake Meghji wakakanusha hakuna wizi au hujuma, Manumba akasema anasubiri Ikulu impe maelekezo ya nini cha kufanya, unategemea kufikishwa kwa hawa jamaa Mahakamani kutanipa furaha zaidi ya kuhoji kwa kuangalia mashitaka waliyosomewa?

Zakumi anadai kuwa ni heri basi tuwafunge hata kwa hayo makosa madogo madogo, je hiyo ndiyo suluhisho na njia ya kuhakikisha kuwa hakuna tena uhujumu?

Sasa hivi, minong'oni ni kuwa ili CCM ishinde kwa kishindo, inabidi suala la EPA na ufisadi yapatiwe japo namna ya kufanana na ufumbuzi. Zaidi ni ukweli kuwa wahisani wamesema hawatoi pesa zao kusaidia bajeti yetu mpaka kieleweke.

Sasa kwa nini mnamkasirikia au kufadhaishwa na Mchungaji anaposema kuwa hili ni changa na hakuna nia ya kweli kutafuta ufumbuzi?

Ama nikupeni mfano mwingine. Lowassa, Karamagi, Chenge na Msabaha. Hawa walifanya uzembe na wanatuhumiwa kuwa wamekula mlungula. Lakini baada ya wao kujitoa kwenye madaraka, hata ndaniya CCM yenyewe hawajachukuliwa hatua, hawajapewa karipio badala yake wanafanywa ni wafalme, wamepewa maandamano kuwapokea, bado wananyenyekewa ndani ya chama na v=hivyo kuonyesha umma kuwa wao wana nguvu na Serikali haina nguvu.

Ni mpaka pale matatizo yetu yatakapotatuliwa kwa nia ya kweli na usahihi wa kutatua, ndipo nitapata faraja. kinyume na hapo, ni changa mbalo nimelivalia miwani.
 
Nurujamii,

Mkuu haya maneno mazito sana na sidhani kama kweli Rev, Kishoka amefika huko isipokuwa nadhani tatizo linalowasibu wengi hapa ni kesi zenyewe zilizowakilishwa dhidi ya viongozi waliotajwa zinaonekana kuwa ni DHAIFU sana kiasi kwamba zinaacha mwanya na penyo za ushindi kwa watuhumiwa. Jana tu nilikuwa naongea na mshikaji akanambia kwa nini anaona kuwa hili ni changa la macho!

Kama unakumbuka hapa JF sote tumepiga kelele kuwa hawa jamaa ni WAHUJUMU uchumi kwa hiyo tulitegemea kesi zenyewe ziwe ktk kundi hilo la mashtaka lakini inaonyesha wazi kuwa ni swala la Negligence or misconduct ktk ofisi zao...Jambo ambalo linapunguza nguvu ya mashtaka ya Hujuma walizofanya..

Kwa hiyo sio kwamba JF hakuna watu wanaoweza kumuunga mkono Kikwete isipokuwa kilichotakiwa haswa kufanyika sio tu kufikishwa watu hawa mahakamani isipokuwa kesi dhidi yao ziwe zile ambazo sote tunazijua..
Hadi sasa hivi namuunga sana mkono at least kaweza kuinua kidole!...Sasa hivi ndio baadhi ya Wadanganyika wanaanza kujua Mkapa alifanya nini..yet nashangaa bado wapo wanaosema alikuwa kiongozi bora!.. Yale yale ya Mugabe na wafuasi wake.
Kweli Mkandara na mimi ningependa kuweka msisitizo, mashtaka yanayo faa ndio hayo ya hujumu uchumi, ambayo hayana dhamana, kwa hiyo hapa DPP anatuchezea na pia kama wapo walio mpa huo uamuzi wakuchukua. Inabidi Donors waambiwe hili changa macho tunalotaka kufanyiwa.
 
Rev Kishoka and other 'skepticists' ningependa kujua ni nini hasa mlitaka Rais afanye kwa sasa?

Mimi ni 'other' na sijui labda ulikuwa na maana ya 'skeptics' - sasa kwenye hilo wewe unajiweka kundi gani. Mimi nataka Raisi aliyechaguliwa kwa asilima 80% ya wapiga kura na akaapa kuiheshimu, kuilinda na kuitetea katiba, aache kwanza usanii na atimize wajibu wake kulingana na sheria.

Ajipeleke yeye mwenyewe mahakamani au? Nafikiri hata kama hatuamini sincerity ya Rais kwa sasa tutoe basi alternative wakati tunapom-critique!

Je wewe unaamini kuwa yuko sincere maana kama ni hivyo aanze kwa kuwaomba watanzania msamaha kwa kuwahadaa halafu akubali kazi imemshinda. Hizi za kusema mara nchi itayumba akitimiza wajibu wake itakiwavyo ina tafsiri moja tu - Uraisi umemshinda.

Inachukiza mtu aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote mafisadi kupelekwa mahakamani, hadi kuamini kuwa kamwe hawatapelekwa mahakamani sasa anabadilika baada ya kuona wamepelekwa. Process inapoanza anadai hakubaliani na hilo kwa sababu anayeisimamia hiyo process naye ni muhusika katika ufisadi.
Wizi wa EPA ulipangwa na CCM na serikali yake - wafanya biashara ni wazi walitumiwa tu kama zana za kufanikisha wizi huo. Hii maana yake ni kuwa serikali ya sasa haiko madarakani kihalali kwa kutumia pesa za wizi kushinda uchaguzi. Wengine tunasubiri waliokula njama na kupanga wizi wakichukuliwa hatua na si dagaa wa benki kuu au kusubiri mpaka wafe.

Kwa hiyo afanyeje sasa! aache?
Awajibike na ikiwezekana ajiuzulu, uchaguzi mpya ufanyike. Siyo rahisi uchunguzi huru ukawezekana chini ya hii serikali kwa sababu ni 'part and parcel' ya tatizo.

Sio kama nakataa kwamba kuna uwezekano wa kupigwa changa la macho, lakini kinachotakiwa sasa is to critique constructively.
Hapa tuko pamoja na yaonyesha na wewe huamini kuwa kuna dhamira ya kweli. Mfano mdogo tu - Hosea aliifagilia Richmond lakini bado yuko kazini kwa nini. Kigunge alisema EPA ni uzushi - jeuri aliipata wapi. Waziri Masha kawatembelea Mramba na Yona - kwa misingi ipi and on and on....

Pia kumbukeni sio lazima kubisha kila kitu ili uonekane unayajua mapambao sana au wewe ndio mwenye uchungu na nchi yetu kuliko wengine. Nimefikiria sana nini kinatakiwa Rais afanye ili apate support hapa JF lakini nimegundua hakuna. Labda ajipeleke mahakamani mwenyewe na kujiuzulu uraisi tu!
Raisi mwanzoni alikuwa na watanzania asilimia 80% nyuma yake akawaangusha. Rejea post za nyuma hapa JF hasa mwanzoni 2006 alivyokuwa ana support kubwa. Yeye ajiulize kwa nini chati yake imeanguka na bila shaka atapata si jibu tu bali anachotakiwa kufanya hivi sasa.

Nadhani sasa hapa hakuna logic bali ni chuki binasfi kwa Kikwete. Kwamba humtaki tu, basi!
Sasa hapa unaingia kwenye anga mbaya na unaanza kujianika usivyo makini. Aliyeomba kazi akisema hana ubia na mtu, atakuwa na 'zero tolerance' na mafisadi sasa kazungukwa nao. Wengine tunasema Raisi anayumba and it happens tuliye naye anaitwa Kikwete. Sipendi vitendo vya serikali na ayeiongoza ni Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM ambayo imeunda hiyo serikali.

Haya ni maoni yangu tu and I am open and flexible to change my position!
Afadhali wewe maana kuna wanaosema watakufa wakiwa CCM iwe kwa mabaya au mazuri. Be flexible but first make sure you have the elasticity otherwise you can easily break.
 
Nimefurahi kusikia wanaowashtaki Mramba na Yona si Kikwete ila serikali, na wanafanya kazi pale Kikwete anapotoa go ahead!

So hatuna serikali, ila mpaka iambiwe na Kikwete!!!!!

hapa kutakuwa na uonevu, kuwa wezi fulani waende na wengine wasiende

Kwa hiyo mwizi yeyote awe raiskwa sababu hatuna imani na atakayekuja!

Yaani katika watanzania milioni 40, we can not trust someone to lead us???

ina maana una confirm jamii ya watanzania ni fisadi wote, so siyo kosa kabisa Kikwete kuwa rais hata kama naye aliingia mikataba mibovu na kuua watu!!

Inabidi tuwe clean, siyo kusema huyu afadhali msafi kuliko huyu?? kichekesho hiki.

Mchakato mzima wa kumpata rais Tanzania ni kichekesho kwenye vyama vyetu, wanampata ka presha za muda huo na sio nini alifanya siku za nyuma.

UKIFIKA WAKATI UKAONA KIKWETE ANAFAA KWA URAIS NA UKAONA HAKUNA WA KUM-REPLACE BASI FORGET CCM WILL RULE FOREVER!!!!!!

Nashukuru Rev kwa kuweza ku-justify argument yako, hivyo wengi wetu au doubting Thomas, watakuwa/tutakuwa tumeelewa na si chuki binafsi against the Goverment au mtu fulani. Infact sasa inabidi tujue cost za investigation ya EPA ni ngapi from Delloite, Ernest and Yound to Kamati Ya IGP etc etc, ili tuone kama Value for Money Ipo, au ndio tunazidi kuumizwa.Na pia kama tunaelekea katika mstari unaofaa, maana kwa mambo yanavyo kwenda inawezekana tunakwenda kushoto badala ya kwenda kulia, sasa fikiria tutakapo gundua hiyo time na cost ya kurudi kwenye barabara ifaayo itakuwaje? Si mamuvi yatazidi.
 
a. Je hii ni mara ya kwanza kwa watumishi wa serikali na hata mawaziri kufikishwa mahakamanni?
b. Je hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushuhudia kesi zenye "high profile"
c. Je Katika kesi za huko nyuma kuna watu waliokuwa na nyadhifa kubwa ambao leo hii wanatumikia kifungo (nazungumzia wanasiasa)
d. Je tunazo sheria za kutosha kukabiliana na changamoto za uhalifu unaohusisha viongozi wa kisiasa?
 
Sheria zipo , sema hakuna Utashi. hata kabla ya sheria hizi mpya za TAKUKURu/PCB etc walikuwa wana uwezo wa kufunga watu. Na hata sasa hivi kinacho gomba ni utashi, ndio maana Donors/wafadhili wameamua kuchukua hatua mbadala ili serekali/ au vyombo vyake vichukue hatu zinazo faa, maana bila kushinikizwa ungekuta vithibitisho vinapotea au unaambiwa hakuna ushaidi wa kutosha/ ama kesi inafunguliwea kwa weak points au uendeshaji wa kesi unatibuliwa ili asifungwe mtu.
Mimi ninamkumnbuka kuna Mzee mmoja wa NASACo MD/GM enzi za 1974/76 alifungwa kwa rushwa kwa zilezile sheria wanazodai zilikuwa na mapungufu.
Mzee wa watu alionekana na Mali kushinda uwezo wake licha ya utetezi wake wa kufuga kuku etc alishindwa kuthibitisha upatikanaji wake
 
...
Zakumi anadai kuwa ni heri basi tuwafunge hata kwa hayo makosa madogo madogo, je hiyo ndiyo suluhisho na njia ya kuhakikisha kuwa hakuna tena uhujumu?

...

Rev:

Nakuelewa msimamo wako lakini una ka-extremist fulani. Unaposema hakuna tena uhujumu, unakwenda kwenye extreme ambayo ina-exist kwenye theory au principal tu.

Sir, kuwa pragmatic kidogo.
 
Yap! sasa nimewapata kwa pande zote mbili za shilingi..
Kusema kweli ndugu zangu tusiwe wanafiki kwa kauli zetu, mtanisamehe kutumia neno hilo....
Kikwete kama rais wa nchi yetu kafanya mambo ambayo hayakutegemewa kabisa pamoja na kwamba kuna mapungufu ktk kuwasilisha....
Ukitazama maswali ya Mwanakijiji, kusema kweli sikumbki ni lini kiongozi ngazi za waziri kama kina Yona na Mramba walisimamishwa mahakamani..sikumbuki zaidi ya kesi za Uhaini. Hii haijatokea tanzania labda kidogo wakati wa Sokoine na aliboronga kwa sababu ilitumika nguvu badala ya akili.

Kwa hiyo serikali ya Kikwete tunaipa point moja kubwa sana kwani haya yote tunayodai yalitokea sii wakati wa utawala wake hata kama alikuwa waziri, bado nasema hakuwa rais kwa sababu sote humu tunafahamu nguvu ya rais wa nchi za Kiafrika. Mkapa kama rais tumeyapokea yote haya na hakuna hata mmoja wetu aliyediriki kufungua mdomo acha mbali kukisia tu kwamba kuna baya linaendelea watu tulivumilia alipofungua Ujasiriamali Ikulu, akibuya pombe kali hadi Ofisini akiingia Bwiii!..

Kinachonitatiza mimi ni pale tunapomlaumu Kikwete moja kwa moja wakati tunafahamu kabisa kuwa Kikwete mara zote amekuwa akipelekewa habari za Uongo na tungo za kinamna kuonyesha kuwa serikali yake inafanya kazi. Tumeona hadi Hotuba zake akisema mambo ambayo sii kweli, alikataa hata kutokea kwa tatizo la samaki Mkoani Mwanza na watu kuuziwa Mapanki..Lakini baadaye chini ya uvungu ameweza kusafisha kabisa biashara ile kiasi kwamba mapanki sasa hivi ni chakula cha kuku..Ni rais pekee aliyeweza kufanya mambo tunayoyachukia hata kama kachukua muda mrefu, hana kiburi wala Uungu.

Yote haya ameyarithi toka kwa Mkapa na kwa uhakika amefanya mengi kurekebisha hali iliyokuwepo pamoja na kwamba bado analishwa habari za UONGO kiasi kwamba ni vigumu kufahamu kuna kiongozi chini yake mwenye nia nzuri.

Kwa hiyo nasi nawaomba kwanza tukubali kwamba kuruhusu kkesi hizi zifike mahakamani ni kazi nzuri aliyoifanya. Kuwaondoa viongozi kama Lowassa na Rostam ambaye alikuwa mweka hazina wa CCM chini ya Utawala wa Mkapa amefanya kazi nzuri.. Trust me I can't imagine Tanzania ingekuwa vipi kama mawaziri wote wa Mkapa na wale wa Mtandao wangekuwa bado serikalini tungekuwa wapi leo hii..

Na pengine nitamrudia Rev. Kishka mwenyewe aliyesema kuja kwa Kikwete inawezekana kuwa ni baraka!.. hiyo pekee ni goal la mwananchi kwani ni wakati wa Kikwete pekee tumeweza kusimama na kutoa malalamiko kama haya yakatingisha serikali..
Ni wakati pekee tumeona baraza la Mawaziri likiangushwa kutokana na lawama za wananchi na ushahidi kutolewa ambao leo hii tumeusimamia, Kikwete angeweza kabisa kupiga marufuku tuhuma hizi na kuweka vikwazo kwa wapinzani kama Mugabe..
Ni hatua moja mbele wakuu zangu na sasa nadhani ni wakati wetu kuongeza nguvu za mashambulizi kwa vyombo vya serikali ambavyo vimekabidhiwa kesi hizi..
Sii Kikwete anayewakilisha mashtaka haya mahakamani, kuna watu aliowaamini kufanya kazi hii.. Hivyo kama walivyokosea kina Yona, Mramba, Karamagi, Rostam na wengine wote kutumia madaraka yao vibaya kuna uwezekano mkubwa kuwa hata hawa viongozi wa taasisi hizi za sheria wanaweza kutumia vibaya madaraka yao..
Na tusije kusubiri tena kaa tulivyosubiri wakati wa Mkapa, ikiwa kuna matumizi mabaya ya madaraka kwa hawa DPP ama Takukuru ni jukumu letu sisi kujipanga kama mashahidi ktk vyombo hivyo..Nina hakika kabisa kuwa hii mipango inachezwa na watu wengine kabisa nje ya Kikwete na analikishwa limbwata la Wapambe (Kusifiwa) unajua tena Kikwete muungwana lakini ni mtu wa sifa...(misifa).

Kwa hiyo waungwana badala ya kulalamika tu kuhusisana na mwenendo wa hizi kesi, haijalishi muda na wakati ulikwisha pita kinachotakiwa ni sisi kufahamu kwamba hawa watu hatimaye wako ktk sheria na kinachotakiwa ni uwezo wetu ku prove kwamba hawa jamaa walihusika kwa njia moja ama nyingine kulihujumu taifa. Green light imekwisha tolewa, tusifikirie sana kuwa Kikwete hawezi kufanya hili ama lile wakti haya macheche ambayo yalikuwa hayawezekani yamefanyika..
Tuwe sote pamoja ktk hili kuijenga nchi badala ya kupotezana nguvu..Let's all play our part ikishindikana ndipo tunaweza kutoa hukumu zetu..Yeye binadamu na tumeona mapungufu yake kama binadamu hivyo tumsaidie kuondoa hiki kiwingu..
 
Kwenye nyekundu ....................unamjua Kiula aliyekuwa ujenzi.!?
 
Mkuu Mkandara, heshima mbele.

Mkuu Nurujamii aliuliza na narudia, watu walitaka JK afanyeje(i.e alternative course of action) ili watu waone anashughulikia ufisadi???... So far sijaona jibu.

Sanasana nimeona elaborate background info za what happended mpaka hapa tulipofikia.
Lakini STILL, no alternative course of action bearing in mind the realities on the ground.

Mwanzoni ilikua,... JK hana ubavu wa kuwashitaki EPA,... EPA walipofika mahakamani ..ikawa, mbona hakuna hata kigogo mmoja wa serikalini aliefikishwa? ...walipokamatwa mapapa wawili na mpaka sasa wako ndani....ikawa mbona kesi hizi tu na wakati kuna makesi mengine kibao makubwa kama Kagoda?....walipoona kua in the next few days/weeks kuna high possibilty ya hizo kesi heavyweight kufikishwa mahakamani .... Sasa imekua mbona na yeye mwenyewe rais hajifikishi mahakamani?... I mean ukitazama vizuri pengine ndiyo nature ya human society. Tukubali tu mitazamo.

Kuna post hapa zinamlaumu JK,...kwanini so far ni kesi hizi tu ndiyo zipo mahakamani(kwa maana ni chache),...na ukisoma sehemu nyingine hapahapa jamvini kuna post zinamlaumu JK, kwanini anapeleka makesi makubwa mengi kwa pamoja(kwa maana nyingi), na kuwa ni lazima zitakua zimeandaliwa vibaya tu, ilibidi azichague kwanza za kushinda.... Hapa utaona JK hawezi kufanya chochote bila kuparuwiwa na makucha!

Sasa ukifikiri vizuri ndipo unapoelewa kuwa huu hapa ni mjadala tu, na penye mjadala kuna angle mbali mbali za kujenga hoja. Lakini vilevile kuna kupick positions. Wengine watakua flexible based on hoja na wengine hawataweza kubetray their positions regardlesss....

Kule U.S hata katikati ya the best of times za U.S, as a country, hakuna rais aliyewahi kupata job approval ratings za 100% kwenye opinion polls,... kwahiyo mkuu mkandara nafikiri inabidi tukubali tu kuwa mitazamo ndio nature ya human society.
 
Kwanini Cabinet yote isifikishwe kwenye mkono wa Sheria? au ndio ina nguvu sana haiwezi kufikishwa huko.

Ninavyo fahamu mimi hata kama watu mia wakakaa na kukubaliana jambo kuna mmoja anae wajibika moja kwa moja..kama baraza wangepitisha halafu yeye akapinga na yeye ndiyo wizara yake angejiuzuru....
 
Mkandara umejibiwa hapo juu kuhusu Kiula. Kusema kuwa haijawahi kutokea ni denial of the historic facts.

Kukamata watu kwenda mahakamani is a commendable step in scaring the potential fisadi, but doesn't make the system incoruptible. You need to address the systemic causes of corruption if you are to address the problem in the longer term and sustainable way. Wewe umeshaona kuna mabadiliko yoyote ya sheria kuhusu rushwa? Msingi mkubwa wa rushwa katika nchi yetu ni uchaguzi wa kisiasa. Je, umeona serikali hii ikihangaika ku-address rushwa katika siasa? Kama mfanyabiashara anachangia chama cha siasa, tena tawala, sh 400m, kesho akiomba msamaha wa kodi utashangaa akisamehewa?

Again, tunashangilia watu kupelekwa mahakamani wakati hatujajua hata specific makosa wanaoshitakiwa. Kuna watu walishangilia sana kuhusu Kiula, lakini ikaja gundulika baadaye kwamba ilikuwa ni katika jitihada za Mkapa kumkomoa Kiula kwa maugomvi yao binafsi waliyokuwa nayo wakati wakiwa mawaziri wote wakati wa Mwinyi. Na sasa tunaanza kuona watu wa mtandao akina Karamagi mafaili yao yakifungwa kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwashtaki.

We need to be more watchful than celebratory, vinginevyo tutakuwa tunashangilia mafanikio hewa!
 
"Kukamata watu kwenda mahakamani is a commendable step in scaring the potential fisadi, but doesn't make the system incoruptible. You need to address the systemic causes of corruption if you are to address the problem in the longer term and sustainable way. Wewe umeshaona kuna mabadiliko yoyote ya sheria kuhusu rushwa? Msingi mkubwa wa rushwa katika nchi yetu ni uchaguzi wa kisiasa. Je, umeona serikali hii ikihangaika ku-address rushwa katika siasa? Kama mfanyabiashara anachangia chama cha siasa, tena tawala, sh 400m, kesho akiomba msamaha wa kodi utashangaa akisamehewa?"

Mkuu,
Atleast sasa tunaanza kuona other possible courses of action kwenye hili la ufisadi. Lakini tukumbuke hata hayo mapendekezo yako na mengine mengi, hayataweza kuifanya the whole system incorruptible!... Hakuna hata nchi moja duniani iliyoweza kufanikiwa 100%.

Kitu ambacho wengi tumekua tukikipigania ni kuondoa hii culture ya impunity kwa vitendo vya ufisadi, hasa kwenye ofisi za umma, ambayo ilikua imeota mizizi. Sasa kama hatua zinaanza za kushughulikia ufisadi, sidhani kama ni sahihi kubeza kila juhudi zinazofanyika.

Ofcourse itakapodhihirika JK anatuchezea mchezo watanzania na hizi kesi,...kibao kitamgeukia tena kama ilivyokua mbeya...Mwayembe alisema Watanzania si mabwege tena!
 
Wakuu,
Sawa huyo Kiula ambaye kama sikosei alisimamishwa kizimbani akiwa waziri wakati wa Mwinyi lakini kuna kati yenu anayekubali kwa Uhakika kuwa alikuwa Fisadi?..Hata huyo Ngasongwa bado tunaona ni mchezo ndani ya chama CCM kwa sababu hawa wote ni Wapinzani wakubwa wa Ufisadi (navyofahamu mimi)..Ilitakiwa waondolewe na fitna zikasukwa! zaidi ya hapo hakuna Kiongozi fisadi ambaye kesha pandishwa mahakamani..
Labda ningeiweka vizuri lugha yangu kuhakikisha kwamba tunaotaka wapelekwe kizimbani ni hawa wahujumu Uchumi ambao sote tunakubali makosa yao..
Jamani so far Kikwete anakwenda vizuri tatizo linakuja labda kwa wale waliokabidhiwa madaraka hayo!...
Swala la Lowassa Bungeni na hata kujiuzuru kwake ingetakiwa Sitta apinge kujiuzuru kwake hadi hapo atakapo jieleza laa sivyo anavuliwa Ubunge! Kama bunge liliweza kumsimamisha Zitto bila kibali cha Kikwete walishindwa vipi kumsimamisha Lowassa na wengine hadi hapo kesi zao zitakapo wasafisha!...
Wakuu zangu Tanzania kuna makundi na watu wanabebana hivyo inatakiwa rais ambaye anachukiwa na watu wote kwa Ushenzi wake, jambo ambalo Kikwete hawezi na hakuna mtu tanzania anayeweza hivi sasa. hawa jamaa wananguvu ya ajabu sana ndani ya chama na serikali msifikirie kuwa sheria ipo upande mmoja tu.. Sheria imeundwa ili ivunjwe na watu kama hawa na wamejiandaa kuhakikisha sheria haiwakwamishi.
 
Rev Kishoka and other 'skepticists' ningependa kujua ni nini hasa mlitaka Rais afanye kwa sasa? Ajipeleke yeye mwenyewe mahakamani au? Nafikiri hata kama hatuamini sincerity ya Rais kwa sasa tutoe basi alternative wakati tunapom-critique! Inachukiza mtu aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote mafisadi kupelekwa mahakamani, hadi kuamini kuwa kamwe hawatapelekwa mahakamani sasa anabadilika baada ya kuona wamepelekwa. Process inapoanza anadai hakubaliani na hilo kwa sababu anayeisimamia hiyo process naye ni muhusika katika ufisadi. Kwa hiyo afanyeje sasa! aache?

Sio kama nakataa kwamba kuna uwezekano wa kupigwa changa la macho, lakini kinachotakiwa sasa is to critique constructively. Pia kumbukeni sio lazima kubisha kila kitu ili uonekane unayajua mapambao sana au wewe ndio mwenye uchungu na nchi yetu kuliko wengine. Nimefikiria sana nini kinatakiwa Rais afanye ili apate support hapa JF lakini nimegundua hakuna. Labda ajipeleke mahakamani mwenyewe na kujiuzulu uraisi tu!

Nadhani sasa hapa hakuna logic bali ni chuki binasfi kwa Kikwete. Kwamba humtaki tu, basi!

Haya ni maoni yangu tu and I am open and flexible to change my position!
uanjua watu wengine hawajawahi kuajiriwa aidha serikalini au katika mashirika ya umma wanaishi tuu hivyo basi hawaelewi lolote TZ inavyoendeshwa na hao wanajifanya kujua sana kumbe hamna lolote.wao ubishi bila kujua lolote and might be they are paid by....god nows.tuliopo bongo tutafika tuu
 
Back
Top Bottom