Papa Francis amtimua Askofu anayempinga kuhusu kuruhusu ndoa za jinsia moja, kutoa mimba na waliobadili jinsia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,048
49,731
Ikumbukwe huyu Papa wa Vatican anaeongoza Kanisa la RC almaaufu Kanisa Takatifu la Mitume kama wanavyojiita wao ameamua kuwaburuza wenzake wafuate msimamo wake.

Baadhi ya mambo ambayo anataka Kanisa lake lifuate ni

- Kuwatambua Mashoga bila kukemea akisema wenye dhambi ndio wanatakiwa kwenda kanisani

- Kubariki Ndoa za mashoga

- Kufuhusu utoaji Mimba

- Kutambua watu Waliobadili Jinsia kinyume na maumbile Yao ya Asili

- Kuwa na msimamo legelege na kuficha taarifa za watawa wanaokumbwa na kashfa za kulawiti Watoto wadogo.

- Kufuhusu Baadhi ya Maaskofu wa RC huko Amerika ya Kusini kuoa kinyume na msimamo wa Kanisa lao Hilo la Mitume.

Haya wenye Kanisa lenu johnthebaptist mnaitwa huku 😁😁

======
Papa Francis amemfuta kazi askofu Joseph Strickland, ambaye ni mkosoaji mkubwa aliyeibua maswali juu ya uongozi wa Papa katika Kanisa Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Jimbo Katoliki la Tyler, huko Texas, Marekani alilokuwa akiliongoza .

Askofu Strickland ni mmoja kati ya sauti kinara katika tawi la uongozi wa Kanisa Katoliki nchini Marekani ambalo linapinga vikali mabadiliko yanayopigiwa chapuo na Papa.

Kuondolewa kwake kunakuja baada ya Papa kuzungumzia juu ya hali “ya kuwa nyuma” kifikra ya baadhi ya viongozi wa Kikatoliki nchini Marekani.

Askofu Strickland mara kadhaa ameshambulia hatua za Papa kutaka kubadili msimamo wa Ukatoliki katika masuala kadhaa ya kijamii ikiwemo kutoa mimba, haki za waliobadili jinsia na ndoa za jinsi moja.

Mwezi Julai mwaka huu, alionya kuwa mafunzo mengi ya Ukatoliki ambayo ni ya “ukweli wa msingi” yalikuwa yanapingwa, ikiwemo kile alichokiita majaribio ya “kudunisha” ndoa “kama ilivyoundwa na Mungu” baina ya mwanamume na mwanamke tu.

Askofu huyo pia amekosoa majaribio hayo aliyoyaita ya “kuvunja miiko” na kusema wanaoyapigia chapuo “wanapinga utambulisho wao wa kibailojia waliopewa na Mungu”.

Katika barua yake ya mwezi Julai, askofu Strickland amedai kuwa majaribio “kubadilisha visivyobadilika” yatasababisha mfarakano mkubwa ndani ya Kanisa. Na wale wanaotaka mabadiliko, ameonya kuwa “ndio hasa wanaofarakanisha [Kanisa]".

Askofu Strickland alikuwa chini ya uchunguzi wa Vatican na hapo awali alitupilia mbali uwezekano wa kujiuzulu, na katika barua ya wazi mwezi Septemba alimtaka Papa amfute kazi.

"Siwezi kujiuzulu kama Askofu wa Tyler kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ninawatelekeza wana kondoo,” alisema.

Kwa mujibu wa Vatican, uamuzi wa kumfukuza umefikiwa baada ya “ziara ya kitume katika Jimbo la Tyler iliyoagizwa na Papa mwezi Juni".

Vyombo vya habari vya Kikatoliki vinaeleza kuwa uchunguzi huo pia uliangazia masuala ya kifedha katika jimbo hilo.

Askofu Strickland, 65, aliteuliwa kuwa askofu mwaka 2012, wakati wa Papa Benedikto XVI.

Vatican imesema kuwa Jimbo la Tyler kwa sasa litaongozwa kwa mpito na Askofu Joe Vasquez wa Jimbo la Austin.

Hatua hii inafuatia hatua mahususi zinazochukuliwa na Papa ili kulifanya Kanisa Katoliki kuendana na wakati kwenye utawala wake.

Siku ya Alhamisi, Vatican ilitangaza kuwa watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa katika Kanisa Katoliki ilimradi kwa kwa kufanya hivyo hakutazua kashfa ama “mchafuko”.

Mwezi Oktoba Papa alisema kuwa Kanisa linaweza kukubali kubariki wanandoa wa jinsi moja, huku akiwaeleza makardinali kuwa "hatuwezi kuwa majaji ambao tunachofanya ni kukana, kukataa na kutenga tu".

Akizungunza katika mkutano wa Siku ya Vijana Duniani jijini Lisbon Papa alisema kuwa mgando wa fikra wa baadhi ya watu “hauna manufaa”.

"Kwa kufanya hivyo unapoteza utamaduni halisi na utategemea itikadi ili kuungwa mkono. Kwa maana nyingine, itikadi inachukua nafasi ya imani,” aliongeza kusema.

Mabadiliko ya tabianchi pia imekuwa ni moja ya ajenda kuu ya utawala wa Papa Francis - ambapo mwaka 2015 alitoa chapisho muhimu kuhusu mazingira ambalo lilionya kuwa dunia ilikuwa inaelekea hatua mbaya zaidi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Papa pia amewashutumu vikali wale wote wanaokanusha mabadiliko ya tabianchi na anatazamiwa kuwa katika mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP28 baadae mwezi huu huko Dubai.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kuhudhuria toka mikutano hiyo ianzishwe mwaka 1995.

Chanzo: BBC
 
Maoni ya Papa Francis Dhidi ya Muelekeo Mpya wa Kanisa kwenye masuala ya Kijamii.

Kwamba Kuna Baadhi ya Viongozi Wana mgado wa Kifikra hivyo Kanisa haliwezi kuendelea kuwa nyuma kifikra Kwa kile alichoita Haina manufaa Kwa Kanisa.

Hali hii imepelekea kuanza kutoa sakramenti Kwa watu wa Jinsia Moja,Kuruhusu utoaji Mimba na watu Waliobadili Jinsia.

Waumini wa RC mnasemaje?

View: https://twitter.com/bbcswahili/status/1723590466598309996?t=FG7rQLomW2Is3DgSfrBz3Q&s=19
 
bibisii ni wazushi.
hakuna chombo chochote cha Vatican kilicho report habari za papa kukubalina na mashoga..

na kwa hulka ya kanisa moja, takatifu, Katoliki na la mitume, siyo kujibizana na vyombo vya habari..
Hawana muda wa kujibu upuuzi na uzushi.
 
bibisii ni wazushi.
hakuna chombo chochote cha Vatican kilicho report habari za papa kukubalina na mashoga..

na kwa hulka ya kanisa moja, takatifu, Katoliki na la mitume, siyo kujibizana na vyombo vya habari..
Hawana muda wa kujibu upuuzi na uzushi.
Askofu wa USA katimuliwa kisa kupinga mambo ya ajabu ambayo papa wenu anayashadidia 😂😂
 
Maoni ya Papa Francis Dhidi ya Muelekeo Mpya wa Kanisa kwenye masuala ya Kijamii.

Kwamba Kuna Baadhi ya Viongozi Wana mgado wa Kifikra hivyo Kanisa haliwezi kuendelea kuwa nyuma kifikra Kwa kile alichoita Haina manufaa Kwa Kanisa.

Hali hii imepelekea kuanza kutoa sakramenti Kwa watu wa Jinsia Moja,Kuruhusu utoaji Mimba na watu Waliobadili Jinsia.

Waumini wa RC mnasemaje?

View: https://twitter.com/bbcswahili/status/1723590466598309996?t=FG7rQLomW2Is3DgSfrBz3Q&s=19

Duh!
Makubwa
 
Uzi huu unaweza kufutwa au kuhamishiwa sehemu ambayo huwezi reply.

Nafikiri kuna kitu kinaendelea humu kwa hawa moderators katika kulinda image ya dini fulani habari,ushauri hata maoni yakiletwa humu yanayo onekana yana kinzana na dini hiyo yanafutwa kwa haraka sana.

Tuupe muda nafasi wa kuamua.
 
Mambo ya 1378 yanajirudia. Papa Gregory XI anakufa, Urban VI anateuliwa na baraza huko Rumi.

Wakati huohuo Clement VII anateuliwa huko Avignon Ufaransa kuwa papa.

1409 baraza la usuluhishi huko Pisa Italy linafikia hatua ya kubatilisha uteuzi wa wote wawili -- Urban VI & Clement VII, na kuwatimua.

Alexander V anateuliwa kuwa papa mpya. Lakini wale wengine 2 wanaendelea kushikilia misimamo yao na kukataa kuachia ngazi.

Kwa kipindi cha miaka 6 iliyofuata Ukatoliki ukawa na mapapa 3 kwa wakati mmoja, hadi Baraza la Constance mwaka 1414 Iilipowatimua wale wawili mahasimu na kumvua mamlaka papa wa tatu, kisha likamteua papa mwingine Martin V.

👉Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe. ~Mathayo 23:15
 
Kanisa Katoliki na Baba Mtakatifu (Maarifa wa Petro) haliwezi kuruhusu dhambi.

Nyie mashoga nendeni mkasali kwenye makanisa yanayowaunga mkono. Yapo mengi.

Mafundisho ya Kanisa hayaamuliwi na Papa (kama mtu binafsi) bali taasisi. Upapa hauwezi kuunga mkono dhambi. Kamwe.
 
Hili kanisa linataka kunifanya nielekee kuamini kile wasabato wasemacho juu ya Papa na RC kwa ujumla
 
Kanisa Katoliki na Baba Mtakatifu (Maarifa wa Petro) haliwezi kuruhusu dhambi.

Nyie mashoga nendeni mkasali kwenye makanisa yanayowaunga mkono. Yapo mengi.

Mafundisho ya Kanisa hayaamuliwi na Papa (kama mtu binafsi) bali taasisi. Upapa hauwezi kuunga mkono dhambi. Kamwe.
Unajua hoja mama ya Padre Martin Luther kuasi RC?.

Ukitambua hilo utaelewa kuna nyakati kanisa lilihalalisha baadhi ya maovu.
 
Uzi huu unaweza kufutwa au kuhamishiwa sehemu ambayo huwezi reply.

Nafikiri kuna kitu kinaendelea humu kwa hawa moderators katika kulinda image ya dini fulani habari,ushauri hata maoni yakiletwa humu yanayo onekana yana kinzana na dini hiyo yanafutwa kwa haraka sana.

Tuupe muda nafasi wa kuamua.
Waliufuta wakaurudisha,kinachoknekana ni post yangu ya kwanza hapo Juu ilikuwa ni content ya mada kama hii ila baada ya kubadili heading.

Cha ajabu wakaurudisha huu Uzi wa Sasa na heading yake so sitarajii wafute tena Kwa sababu ni una chanzo rasmi na habari za Papa kumfuta kazi huyo Askofu wa USA ziko wazi na sababu ndio hizo hapo Juu.
 
Back
Top Bottom