Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu

Wana JF nimesikiliza sana utetezi wa waziri Nundu kupitia ITV alipokuwa ameitisha press conference Dodoma nimegundua utetezi wake ni dhaifu na hautoshi kukwepa kumuwajibisha!!!

Anasema hana uhusiano mzuri na naibu waziri wake, eti naibu waziri wake alikuwa anajifanyia ya kwake bila ya yeye kujua!!!!!

Kwa jinsi alivyojitetea ni wazi hana siri na shinikizo hilo limemchangana.

Naomba kwa ambao mmesikia sijui kama mmemuelewa?

Ningelikuwa JK ningemfuta kazi kwa jinsi alivyojidhalilisha yeye mwenyewe na serikali yake kwa ujumla!!!!

Nawasilisha.
 
kama naibu alikosea kwa nini amemlinda siku zote hizo?tusikwepe uwajibikaji!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Mkuu ni aibu yaani Nundu anasema kwamba CCC walimfuata wakamwambia aende kuangalia miradi yao na wangemlipia yeye akakataa wakamfuata naibu wake (Mfutakamba) wakampeleka Uchina na Mauritania wakamlipia kila kitu na aliporudi akaandika taarifa ya kuipendelea CCC!

Hizi ni tuhuma nzito sana. Ina maana Naibu Waziri kwa lugha nyepesi alihongwa!
 
Mkuu ungeangalia Itv ungemsoma zaidi kamrushia kombora naibu wake bwana mfutakamba kwamba anahusika na madudu yanayoendelea ya kampuni ya ccc kupewa tenda.Kwani wamemgharamia safari za nje ya nchi bila idhini yake.
 
kama naibu alikosea kwa nini amemlinda siku zote hizo?tusikwepe uwajibikaji!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Duh Mkuu ndio maana Nundu alikuwa mbishi kumbe ana ya moyoni! Asingemwajibisha kwa kuwa yeye si mamlaka ya kinidhamu.
Tutaona mengi mwaka huu! Naibu waziri na waziri wake hawaelewani sijui wanafanyaje kazi pamoja?
 
Afadhali wameanza kuumbuana, tutasikia mengi sana,macho na masikio yetu ni kwa mzee wa kaya atafanya maamuzi magumu?
 
Yani migogoro yake na naibu wake anatupa sisi raia for what? ndo maadili ya utumishi wa umma.
Kwa maneno kama yale anategemea akibaki ofisini wataelewanj na naibu?
Nimemskiliza sijapata picha.
 
Halafu anaongea dizaini yuko maji (amelewa)..!

Swali la msingi kwa nini aongee saizi kwani suala hilo la kuhitalifiana na naibu waziri wake limetokea jana au majuzi?

Ni wazi anatafuta huruma wa watanzania. Pamoja na kutia huruma lakini ameonyesha hana uwezo wa kuongoza.
 
Hta mm nimeona knywn habari ch.ten Nundu akijitetea kwamba ni naibu wke ndo anahusika. Kweli mawaziri wetu wa ss ni bogus, ina maana wanakaangana wenyewe!.its tym now tuipige chni ccm haina jipya kwa watz.
 
Mkuu ungeangalia Itv ungemsoma zaidi kamrushia kombora naibu wake bwana mfutakamba kwamba anahusika na madudu yanayoendelea ya kampuni ya ccc kupewa tenda.Kwani wamemgharamia safari za nje ya nchi bila idhini yake.

Hii ni hatari sana mkuu. Na baba mwanaasha yuko Malawi anahudhuria mazishi. Hawezi kumtuma naibu akabaki kuangaikia matatizo ya nchi?
 
huyu jamaa hana la maana lakujieleza,wao waendeleze tu madudu yao peoples power inakuja!!!
 
Mr Nundu kweli amekereka.. Maana ameamua kumwaga ugali sasa baada ya wao kumwaga mboga..! Amesema waziwazi kuwa naibu wake Dr. Athumani Mfutakamba anamhujumu.. Yeye (Mfutakamba) ndo alikuwa anazungushwa na Wachina sehemu mbali mbali za Dunia kwa gharama za hao wachina.. Na amesema Dr. Mfutakamba alikuwa anasafiri bila ya kibali toka kwake.. Nundu amedai Dr. Mfutakamba alikuwa anapewa kibali ofici nyingine ambayo hakuitaja..
So amehitimisha kwa kudai kuwa Kamati yote ya Bunge inashirikiana na Naibu wake kumtoa kafara..
Ama kweli ukistaajabu ya Musa....
 
nimemuelewa kwamba naibu waziri wake alikula rushwa! Hivyo viongozi wetu huwa wanaliana timing kwenye kula rushwa!
 
Engineering na Siasa wapi na wapi? mshikaji na uhandisi wake anafanya press conference mbovu kiasi kile? shame on him hawa ndio wameiua Air Tanzania
 
Back
Top Bottom