Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,543
Wanabodi,

Niko hapa mjini Dodoma, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omar Nundu, anafanya Press Conference saa hizi hapa Dodoma Hotel na amefunguka vilivyo ikiwemo hoja ya kujizulu!.

Amesema yeye ajiuzulu kwa kosa gani?. Ila pia kama kutojiuzulu kwake kunaweza kumgharimu Mkuu wake, Waziri Mkuu Mhe. Pinda, then anatafakari na atafikia maamuzi ya busara kwa maslahi ya taifa!.

Amezungumzia tuhuma mbali mbali zinazoelekezwa kwake na kusisitiza zote ni uwongo mtupu!.

Endelea kufuatana nami kujua tuhuma dhidi ya tuhuma na kuangalia jinsi anavyozipangua moja baada ya nyingine!.

Natanguliza shukrani.

Paskali.

Update!.
Press Co imekwisha Waziri Nundu kashuka na hoja 10 za nguvu zifuatazo.

1. Ujenzi wa Gati No 12 na 14.
TPA wanaipigia chapuo kampuni CCC ya Uchina kujenga kwa gharama za mkopo wa dola appx 600 toka Exim Bank ya China. Waziri Nundu amekiri kuingilia kati sio mpaka sebulen bali hadi chooni kwenye uchafu wenyewe!.

Hiyo kampuni ya CCC ilipatikanaje?.
Waliofanya feasibility study ni hao hao CCC wanaotaka kujenga ni hao hao CCC na mkopo walioomba toka benki ya Exim ya China ni hao hao CCC. Waziri amepinga kwa kutaka ushindani wa wazi!. Wenzetu Mombasa wamejenga gati kama hizo kwa less than 200 millions, kwa nini sisi tujenge kwa dola milioni 600 tena bila ushindani wa wazi, why?.

2. Baada ya kuona waziri anawakwamisha CCC wakaamua kuyapitishia madudu yao kwa Naibu waziri. wakampa paid trips kutembelea miradi mbalimbali ya CCC duniani pote, Naibu waziri yeye hana bei, akaingia kichwa kichwa kuwa kuwadi wao. Alianza kupigwa trips za nje ya nchi bila kibali cha waziri wake, kwa lugha nyingine ni uwezekano wa Ikulu kuhusika kwa Naibu Waziri huyo kusafiri nje ya nchi bila waziri kujua. Mazingira ya safari hizo za naibu waziri zina viashiria vyote vya rushwa ya "free bees" under pretex ya "facility visit" under transparency lazima Naibu Waziri aseme amelipwa shin ngapi amesafirishwa tiketi za ndege za daraja gani na alifikia hoteli za nyota ngapi?.

Wachini huwa hawasafiri 1st Class, hawalipani per diem nono wala hawakai hoteli ya nyota 5!, ila makampuni yao yananayo sololea tenda kubwa kubwa, huwalipa maofisa wa nchi masikini, per diem nene, kuwasafirisha kwa 1st class na kuwalaza hoteli za nyota 5!.

3. Government guarantee hutolewa pale tuu ambapo waziri husika ameridhika na mradi husika shirika husika lipate mkopo, hiyo gvt guatantee ya mkopo kutoka China aliuomba nani?. Niyayo taarifa Tido akiwa TBC aliomba gvt guarantee ili kukopa fedha kumalizia majengo ya TBC mpaka anaondoka hakuna hiyo guaranteeleo vipi MOF wawe kimbelembele kutoa hiyo guatantee ya TPA fasta fasta bila kupitia kwa waziri husika!.
Haya ya TPA ni madudu kuliko hata ya Richmond!.

Mh Nundu amesema haoni sababu ya yeye kujiuzulu na haelewi jinsi kampuni ya CCC ilivyoibuka . Mkanganyiko mkali. Source TBC.

Agoma kijiuzulu adai hajaambiwa ajiuzulu ila atafakari na anedai tatizo ni naibu wake sio yeye. Adai naibu wake kapewa rushwa kibao na wachina na safari za kutosha ili wapewe tender ya kujenga bandari.

Adai CCC ni kampuni na wanaoijua ni Naibu wake na TPA na ndio wanaotaka serikali ikope then iipe kampuni hiyo ya CCC ndo ijenge gati namba 13 & 14 zaidi wao ndo wanapanga bei na serikali iridhie bila discussion

Wana JF nimesikiliza sana utetezi wa waziri Nundu kupitia ITV alipokuwa ameitisha press conference Dodoma nimegundua utetezi wake ni dhaifu na hautoshi kukwepa kumuwajibisha!!!

Anasema hana uhusiano mzuri na naibu waziri wake, eti naibu waziri wake alikuwa anajifanyia ya kwake bila ya yeye kujua!!!!!

Kwa jinsi alivyojitetea ni wazi hana siri na shinikizo hilo limemchangana.

Naomba kwa ambao mmesikia sijui kama mmemuelewa?

Ningelikuwa JK ningemfuta kazi kwa jinsi alivyojidhalilisha yeye mwenyewe na serikali yake kwa ujumla!!!!

Ni kweli hapa madudu ni kuliko Richmond maana Waziri anaingilia TPA kama walivyofanya wenzake kuingilia Tanesco!!! Hahaaa!! Richmond kumbe ilikua mbaya Pasco?!! I like that!!! Hawakuonewa kumbeeee!!!
Mkuu Halisi, mimi daima najitahidi kusimama kwenye kweli na haki.

Kuhusu Richmond sijawahi kusema Richmond ilikuwa safi, ili ni kweli Richmond walionewa na hili nasimama nalo mpaka kwesho kwa sababu ndio ukweli wenyewe!.
1. Japo ilikuwa ni kampuni hewa, na mkataba ulikuwa ni mkataba batili, ile mitambo waliyoileta sio mitambo hewa, na umeme walioufua sio umeme hewa!, hivyo kuwatendea haki, Tanesco walipaswa kulipia umeme waliotumia!, na hapa nahalalisha ile tozo na piga ua galagaza, lazima italipwa!, hakuna pa kutokea!.

2. Baada ya kuipiga chini Dowans, tulikumbatia IPTL kwa gharama mara 10 ya Dowans!, hii ni akili au matope?.

3. EL alijiuzulu kuwajibika kwa madudu ya Richmond, nikawasisoitiza humu, aliwajibika klu save faces za wahusika wakuu!.

4. Zitto alishauri au tutaifishe mitambo, au tuinunue, alipigwa vita mpaka kuitwa fisadi, leo ameinunua Simbion, tunauziwa umeme na tunalipa
gharama mara 10 zaidi ya kama tungeinunua!, hii ni akili au matope?!.

5. Mwenye nchi akakiri hawajui Dowans, Mwarabu zuga akaja mpaka Ikulu to "make belive", Simbion wakaingilia Ikulu, leo ni sisio sisi
tunaishangilia Simbion tukinunua umeme kwa gharama kubwa kuliko Dowans mitambo inayofua umeme ni ile ile ya Richmond, ememe
unaofuliwa ni uleule wa Dowans, kama juzi tulikataa na kupiga kelele na leo tumenyamaza, kuna tofauti gani ya kujilia matapishi yetu?!.

6. Wizi wa hii CCCC ni afadhali ya Richmond!. Hakuna ajuaye walijuaje, wakajitolea kufanya feasibility study bure!, hawa ni waendeshaji na
sio wajenzi, wala sio wakopeshaji, lakini waendeshaji hawa, baada ya feasibility study, wakajigeuza ni wajenzi, lazima wajenge wao!,
serikali yetu haina fedha, hivyo sasa wakajigeuza wao ni wakopeshaji kwa kuitumia Exim bank yao kwa sharti mkopo huo utatolewa only
if ni CCCC ndio watajenga, na wangeshamaliza ujenzi ndipo wangefanya kazi yao ya uendeshaji mpaka mkopo ule ulipwe!, tena wanatupa
grace period ya miaka kadhaa bila kulipa na kweka very low interest ya asilimia 3% per annum!, mabingwa wa hesabu pigeni hesabu
mkopo huu ungemalizika kulipwa baada ya miaka mingapi? (life time)

7. Thamani halisi ya ujenzi ni dola milioni 200 +!, wakaweka other costs na vya juu vyote ikafika
milioni 400!, kina Mgawe waka top up zao milioni 100!, ikafika na Mkulo akatop zake milioni 27!, ikafika milioni 527!. Deni lote lilikuwa
lilipwe na sisi Watanzania!.

8. Kwa vile hatujui CCCC wameingiaje, ila ni hakika kwa asilimia 100% kwa mia, wameletwa!, kama mpaka leo tunapigizana kelele kuhusu
Kagoda, hao wanaotajwa ni ma ajenti tuu, wenyewe wapo na ni untouchables!. Kwenye Richmond na Dowans mpaka Simbioni, hao wote
mnaowaona ni ma agenti tuu na na middle men, wenyewe wapo!, na sasa kwenye CCCC, hao waChina wanatumiwa tuu lakini wenyewe
wapo!. Nundu hakujua ana deal na kina nani!, he has to go!

9. Kuna watu wanajipambanua kupiga vita ufisadi hata humu jukwaani tunao, na kuna akina sisi tunaonyooshewa vidole kutetea mafisadi,
utakuja kukuta kumbe hao wapinga mafisadi ndio wanaokula na mafisadi na ndio wanategemea fedha za mafisadi kukamilisha agenda
yao ya kupinga ufisadi kwa maneno!, na sisi tunao onekana kutetea mafisadi, ndio tunawasiadia zaidi Watanzania kujua ukweli, kama
sisi wakosoaji wa Chadema humu jukwaani huishia kutukanwa sana, lakini kuna uwezekano, ndio tunaisadia zaidi Chadema, kuliko
wasifiaji kwa sifa shanhwe na mapambio!.

10. Tanzania inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wewye meno, ila iko siku iso jina, itafika na
]u kweli utasimama!.
My Take.
Kwa Press Conference hii, naona Waziri Nundu kaamua kujilipua liwalo na liwe, kitendo cha kugoma kujiuzulu kutapelekea kumlazimisha JK kumfukuza kazi!. Tena ni bahati ameyasema haya leo Jumapili ikulu yetu haifanyi kazi, lakini ingekuwa ni siku ya kazi, angefutwa kazi leo leo!.
wenye press conference nilikuwepo, kiukweli, upepo haumwendei vizuri waziri Nundu kaamua liwalo na liwe, kausema ukweli wa moyoni mwake na kuna uthibitisho beyond reasonable doubt, kuwa Waziri Nundu sio fisadi ila amezungukwa na mafisadi left right and centre, hivyo yeye kuishia kuonekana an enemy of the people and soon atafanywa kondoo wa kafara kwa kufutwa kazi kwa mtindo ule ule wa "funika kombe mwanaharamu apite".
Hili la uzalendo wa Nundu kutanguliza mbele maslahi ya taifa dhidi ya maslahi ya mafisadi, itamcost.

Iliwahi kutokea kule nyuma kwenye kisa cha IPTL aliyekuwa Katibu Mkuu wa Madini, Patrick Rutabanzibwa alipelekewa rushwa nene na Rugemalila siku ya Xmas Ave, na siku ya Boxing Day akairudisha kwa Rugemalila na kwenda kumripoti Waziri wake Kikwete kwa rais Mkapa, kilichofuatia Rutabanzibwa akahamishwa fasta, IPTL ikapitishwa juu kwa juu!.

Sasa ni zamu ya Nundu, subirini kama atafikia J.4!.

Hivyo wewe mwana jf be the first to know kuna Waziri kesho atafutwa kazi!.

Paskali
 
Pasco wewe ni mchumia 2mbo,othertim we don undestand u..aneitishaje press kama hana hoja wakati nchi ipo ktk tension..hoja angeachia ngazi..na Ester Bulaya je?
 
Pasco taratibu Brother,
Kule kwenye ile Thread ya Easter Bulaya umeanzisha thread halafu umekimbia na unakuaj huku kuanzisha thread nyingine wakati Press conference haijaisha!!........ni kwa nini usingecomment tu au kui update thread ya Crash Wise?
 
Asante kwa taarifa mkuu Pasco.
Endelea kufuatilia kila kinachojiri hapo utuhabarishe.
Kulikua na taarifa za JK kuwepo huko,una lolote?
 
we ni pasco au pascal?... Lakini we jamaa unakawaida ya kutuacha kwenye mataa kumbuka kwa yule mama hujamaliza kiporo. tena umeanzisha nyingine hapahapa na yenyewe umeleta juujuu bado unataka tukufatilie.
 
Asante Pasco endelea kutujuza kinachoendelea.
Hakuna kinachoendelea ujinga mtupu, Press Conference imeshakwisha na Wazii Nundu amesema bado anatafakari kama kuna ulazima wa yeye kujiuzulu.
The same blah blah, wala hakuna jipya.
 
Press Co imekwisha Waziri Nundu kashuka na hoja 10 za nguvu zifuatazo.

1. Ujenzi wa Gati No 12 na 14.
TPA wanaipigia chapuo kampuni CCC ya Uchina kujenga kwa gharama za mkopo wa dola appx 600 toka Exim Bank ya China. Waziri Nundu amekiri kuingilia kati sio mpaka sebulen bali hadi chooni kwenye uchafu wenyewe!.

Hiyo kampuni ya CCC ilipatikanaje?.
Waliofanya feasibility study ni hao hao CCC wanaotaka kujenga ni hao hao CCC na mkopo walioomba toka benki ya Exim ya China ni hao hao CCC. Waziri amepinga kwa kutaka ushindani wa wazi!. Wenzetu Mombasa wamejenga gati kama hizo kwa less than 200 millions, kwa nini sisi tujenge kwa dola milioni 600 tena bila ushindani wa wazi, why?.
 
Pasco os a self proclaimed news breaker wa jf.
Yeye hataki kuchangia uzi wa mtu hasa wenye habari ya moto!!
Pasco taratibu Brother,
Kule kwenye ile Thread ya Easter Bulaya umeanzisha thread halafu umekimbia na unakuaj huku kuanzisha thread nyingine wakati Press conference haijaisha!!........ni kwa nini usingecomment tu au kui update thread ya Crash Wise?
 
Press Co imekwisha Waziri Nundu kashuka na hoja 10 za nguvu zifuatazo.

1. Ujenzi wa Gati No 12 na 14.
TPA wanaipigia chapuo kampuni CCC ya Uchina kujenga kwa gharama za mkopo wa dola appx 600 toka Exim Bank ya China. Waziri Nundu amekiri kuingilia kati sio mpaka sebulen bali hadi chooni kwenye uchafu wenyewe!.

Hiyo kampuni ya CCC ilipatikanaje?.
Waliofanya feasibility study ni hao hao CCC wanaotaka kujenga ni hao hao CCC na mkopo walioomba toka benki ya Exim ya China ni hao hao CCC. Waziri amepinga kwa kutaka ushindani wa wazi!. Wenzetu Mombasa wamejenga gati kama hizo kwa less than 200 millions, kwa nini sisi tujenge kwa dola milioni 600 tena bila ushindani wa wazi, why?.
Pasco kulikuwa na haja gani kuanzisha thread hii wakati kuna thread kama hii imeanzishwa na Crashwise? au unaona ni ujiko sana wewe kuanzisha, halafu nenda kwenye thread yako ya Bulaya ukajibu uongo wako kule.
 
2. Baada ya kuona waziri anawakwamisha CCC wakaamua kuyapitishia madudu yao kwa Naibu waziri. wakampa paid trips kutembelea miradi mbalimbali ya CCC duniani pote, Naibu waziri yeye hana bei, akaingia kichwa kichwa kuwa kuwadi wao. Alianza kupigwa trips za nje ya nchi bila kibali cha waziri wake, kwa lugha nyingine ni uwezekano wa Ikulu kuhusika kwa Naibu Waziri huyo kusafiri nje ya nchi bila waziri kujua. Mazingira ya safari hizo za naibu waziri zina viashiria vyote vya rushwa ya "free bees" under pretex ya "facility visit" under transparency lazima Naibu Waziri aseme amelipwa shin ngapi amesafirishwa tiketi za ndege za daraja gani na alifikia hoteli za nyota ngapi?.

Wachini huwa hawasafiri 1st Class, hawalipani per diem nono wala hawakai hoteli ya nyota 5!, ila makampuni yamayo sololea tenda, huwalipa maofisa wa nchi per diem nene, kuwasafirisha kwa 1st class na kuwalaza hoteli za nyota 5!.
 
Pasco kulikuwa na haja gani kuanzisha thread hii wakati kuna thread kama hii imeanzishwa na Crashwise? au unaona ni ujiko sana wewe kuanzisha, halafu nenda kwenye thread yako ya Bulaya ukajibu uongo wako kule.
Easy Fit, Sorry hiyo thread ya Crashwise mpaka sasa ninapo posti hapa, sijaiona kwa vile mimi niko eneo la tukio physically, ninapandisha kitu ninachokiona kwa macho yangu na ninachokisikia kwa masikio yangu nikiripoti live kutoka eneo la tukio.

Mode kama kuna mwana jf mwingine yuko hapa eneo la tukio, naomba uinganishe hii thread na hiyo inayotajwa as long as its the same suject matter!.

Paskali
 
Back
Top Bottom