Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu

Sasa yaani anasubiri kubanwa ndio aseme ukweli ?, anyway hata kama sio yeye atakuwa amefanya kosa la kuficha mwizi, na yeye kama kiongozi wa huyo mwizi, basi hafai kuwa kiongozi
 
hii inaonyesha hakuna team work kwenye wizara, maana kama naibu anasafiri kikazi lzima apate maagizo toka kwa waziri na hata kama anasafiri kibinafsi lazima aage ili waziri ajue shuguli zitaendaje wakati waziri hayupo!!
 
Tatizo kubwa ni kwenye uteuzi. Kikwete kajaza marafiki wake kwenye nafasi zote tatu yaani waziri, naibu waziri na katibu mkuu na hii ni kwa kila wizara. Waziri hawezi kusema chochote mbele ya naibu wake, naibu hawezi kusema chochote mbele ya katibu kwa sababu kila mmoja ni personal friend wa JK na huwezi kusukuma mtu.

Inakuwaje Naibu waziri asafiri nje ya nchi bila waziri wake kujua? Na hata akijue anaweza kweli kumzuia?

Pili, Watanzania tunatakiwa kutambua kuwa China inabebea kwenye 'state corruption' Siongelei rushwa ya mtu mmoja, hapana, ila linapokuwa swala la kampuni ya Kichina kushinda tenda kuna mtandao mkubwa toka kwenye serikali yao wa kusaidia kampuni zao zipate tender. Hili tatizo ni kubwa kuliko maelezo. Wanatumia makampuni makubwa kukopesha nchi masikini lakini ukweli ni serikali ya china iko nyuma yake.

Kikwete angekua ana interest na hii nchi ya Tanzania angevunja baraza lote la mawaziri na kuunda upya. Lakini ninachoona kinaendelea sasa hivi ni maonesho ya kutunisha misuli kati yake yeye (JK) na Lowassa! Maamuzi mengi anayofanya yanalenga kujibu mapigo ya Lowassa! Tanzania kwa sasa ni sawa na yatima! Hivi kweli Kikwete hashutushwi na ubadhirifu uliooneshwa na CAG? Achilia mbali sarakasi za wabunge wa CCM, yeye kama kiongozi mkuu anafikiri nini kuhusu report ya CAG?

Mkuu thanks, una hoja. Tatizo kila mtu ni "kijogoo" mbele ya mwenzake kutokana na uhusiano wao na appointing authority. Ndio maana wenye busara wanapendekeza Rais apunguziwe mamlaka yake na hii si kwa faida ya nchi tu bali hata kwa Rais mwenyewe. Angalia sasa yanayomkuta!
 
Kwenye press conference nilikuwepo, kiukweli, upepo haumwendei vizuri waziri Nundu ila luwalo na liwe, kausema ukweli wa moyoni mwake na kuna uthibitisho beyond reasonable doubt, Nundu sio fisadi ila amezubgukwa na mafisadi left right and centre, hivyo kuishia kuonekana an enemy of the people!.

1-Aondoke Tena bila kuaga,Kama sio anang'ang'ania nini(ni part and parcel)
Ni hawa wafuatao:
2-Omar Chambo-ya kuvulia samaki
3-Athaman Mvuta-kamba
4-Jey Key Ze Great Presidaa:A S 41:

Mkuu thanks, una hoja. Tatizo kila mtu ni "kijogoo" mbele ya mwenzake kutokana na uhusiano wao na appointing authority. Ndio maana wenye busara wanapendekeza Rais apunguziwe mamlaka yake na hii si kwa faida ya nchi tu bali hata kwa Rais mwenyewe. Angalia sasa yanayomkuta!

Kiongozi, wakati Lissu anapiga bungeni kuhusu urais (presidency) wa ki-falme CCM ama kwa makusudi au kutoelewa waliamzomea! Rais yuko kila ngazi, mawaziri, naibu mawaziri, katibu wakuu, wakugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya, Directors wa mashirika ya umma, wenyeviti wa boards za mashirika ya umma, hata kwenye uongozi wa magezeti! Na kwa bahati mbaya kajaza watu (ambao hawakukutana barabarani). Nani amsukume nani? Nani amkoromee nani? Kwa mtu yoyote asiyetambua urais wa kifalme na madhara yake basi aangalie yanayotokea Tanzania kwa sasa! Watu wamefanya uongozi ni 'hobby'.

Pia, ninaamini hata wana-ccm wengi waliochagulia kuwa wabunge kwenye bunge la East Africa wana mkono wa 'kifalme'. CCM wanamwacha mtu kama Dr Mndolwa?
 
Mkuu wangu I salute you kwa kumbukumbu maridhawa. Tatizo ni kwamba ufalme ukishafitinika unakuwa umeishiwa kitu muhimu kinachoitwa MAONO. Uwezo wa kuona na kupambanua mambo ya mbali (kusoma alama za nyakati) unakuwa haupo.

Ni kweli Mh. Tundu Lissu alitahadharisha hilo lakini kwa ulevi na kupungukiwa maono, CCM na vibaraka wao wakaishia kuzomea mle Bungeni na hata nje ya Bunge. Matokeo yake ndio hayo - CCM haijui ielekee upande upi.
 
Alitakiwa kuchukua hatua mapema huu si muda wakusema mbona na wewe na wewe umeiba. Ulitakiwa kuchukua hatua mapema na kuwambia watanzania ufisadi kama kweli upo other wise Nundu ni mfa maji tu huna lolote,
 
Kiongozi, wakati Lissu anapiga bungeni kuhusu urais (presidency) wa ki-falme CCM ama kwa makusudi au kutoelewa waliamzomea! Rais yuko kila ngazi, mawaziri, naibu mawaziri, katibu wakuu, wakugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya, Directors wa mashirika ya umma, wenyeviti wa boards za mashirika ya umma, hata kwenye uongozi wa magezeti! Na kwa bahati mbaya kajaza watu (ambao hawakukutana barabarani). Nani amsukume nani? Nani amkoromee nani? Kwa mtu yoyote asiyetambua urais wa kifalme na madhara yake basi aangalie yanayotokea Tanzania kwa sasa! Watu wamefanya uongozi ni 'hobby'.

Pia, ninaamini hata wana-ccm wengi waliochagulia kuwa wabunge kwenye bunge la East Africa wana mkono wa 'kifalme'. CCM wanamwacha mtu kama Dr Mndolwa?

juzi bungeni kama ulifuatilia vizuri baadhi ya wabunge wa ccm walikuwa waki address hii nguvu ya uteuzi aliyonayo rais na inavyochangia uozo lkn kutokana na woga wa kushughulikiwa na system pamoja na unafiki wao walibaki wakijiuma uma tu.
Juzi hiyo mwishoni naibu wa spika wakati akitoa muongozo wa mbunge mwishoni aliongea kiutu uzima kuhusu teuzi za wakuu wabovu wa idara.. alipendekeza wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa idara wawe wanafanyiwa usaili na wilaya husika, alikwenda mbali zaidi mpk kugusia wakuu wa wilaya wanaoletewa majimboni from no where na hawafamu lolote khs vituo vyao vya kazi.
 
Ana matatizo mengine kabisa ambayo nina uhakika hakuzungumzia. Je amezungumzia dhulma aliyotaka kuifanya KIA? _

Siku hizi Press Conf waandishi wanakwenda kusikiliza, wachache sana wanafanya utafiti na kuuliza maswali magumu bila ya kuwa na maslahi nayo. Ukiona wanaouliza maswali magumu wana maslahi na jambo husika na si kwa kufanya utafiti. Kama waandishi wangekwenda kwa Nundu wakiwa na taarifa kamili, nadhani Waziri angeanza kumwaga matusi.Bahati mbaya hata mipaka na majukumu ya Waziri watu wanakua hawamuulizi. Tusubiri tuone na wenye mapenzi mema na nchi hii watamwaga humu nyaraka. Sekta ya uchukuzi ni nyeti sana na ikiangaliwa vyema inaweza kubeba uchumi wetu.
 
huyu jamaa alikuwa wapi siku zote kuongea maneno hayo??? yeye si ndo boss si angechukua hatua kuliko kutulalamikia sisi wananchi, anafikiri tutafanya nini???? asitafute huruma ya wananchi
 
Watu wanataka ujiuzulu sio kutuambia kama umeonewa au la
Nilidhani upo Mbeya nasikia boss wetu kapigwa mawe Pasco
OTIS
 
Last edited by a moderator:
Toboa!!!!!!!!!!!
kila waziri aseme lake.

Mh Waziri ulikuwa wapi kumlima mapema??????????
 
Mfutakamba kesho Naye anaita press conference kukanusha tuhuma za Nundu! Wonders shall never end
 
Kwenye press conference nilikuwepo, kiukweli, upepo haumwendei vizuri waziri Nundu ila luwalo na liwe, kausema ukweli wa moyoni mwake na kuna uthibitisho beyond reasonable doubt, Nundu sio fisadi ila amezubgukwa na mafisadi left right and centre, hivyo kuishia kuonekana an enemy of the people!.

kaka tokea asubuhi watu wanakusubiri kule kwa easter bulaya. Au umesahau?
 
Huu ni upuuzi. Alikuwa wapi kumkemea kabla ya yote. Huyu si yupo chini yake? Dhana ya uwajibikaji sio lazima wewe binafsi ufanye kosa hata kosa la mtu wa chini yako linakugharimu, mbona watu wa chini yake akifanya vizuri sifa na cheo anapandishwa BOSS. Atoke tu ili liwe fundishwa kwa viongozi wenye kunyamazia maovu
 
Back
Top Bottom