Önly fans of Hiphop

kwa waliopo kwenye game now anaefaa kuitwa MC ni FID Q peke yake ila tukiongeza na wasiokuepo ndo wenge sana..
Yes, jamaa anajua kuandika na kuimba real hardcore hiphop. Baada ya huyu nadhani wanafuata:-
1. Solo Thang (naye anaweza sana kuandika)
2. Jay Mo (anaweza kuandika)
 
Yes, jamaa anajua kuandika na kuimba real hardcore hiphop. Baada ya huyu nadhani wanafuata:-
1. Solo Thang (naye anaweza sana kuandika)
2. Jay Mo (anaweza kuandika)

Hivi ndugu zanguni, kuna wimbo gani ambao Fid
Q kasimama na mashairi yake bila kushirikisha
misemo ya kwenye Kanga, Methali na nahau
ambazo zilishatungwa na akina Andanenga way
Back? Acheni kuwapa watu sifa wasizostahiri.
Ni uvivu wa watanzania waliowengi kushindwa
kujisomea vitabu vinavyozungumzia misemo,
nahau, methali, semi nk nk nk... Fid Q anakuja na kutumia misemo kama
''usidharau nazi, embe tunda la msimu'' then watu
wanampa bigup coz ameandika msemo
ulioshiba...
Je msemo huo ni mgeni mwa wanaosoma
misemo ya kiswahili?
 
we una beef na Ngosha!!
 
Huwezi mtaja Faza Nelly kama real Mc, pasipo kuwataja K-Single, Faza Nelly anaanza game K-Single, D-Rob, Adili(Nigga One), tayari walikua wana run game hii kwa bongo.
Bamiza inamtoa Faza Nelly 99 lakini Kwanza Unit walikua tayari wanafanya game, na nina uhakika hata Faza Nelly wali muinsnpire!
JCB bado hajafiki level hiyo ya real MCs
Jay Moe wakawaidaa sana
Pia hahis haujaelewa maana ya MCs, sio kuaaandika mashairi tu zingatia nguzo 5 za hip hip
Maana kama MCs ni kuandika mashairi hata FA atakuwemo!
Na MCs sio kukaza sauti kama JCB maana hata Chindo Man, Kala Pina na Msema Kweli watakuwemo!
Kifupi MCs wa ukweli Bongo
1.Sugu - bado yupo
2.Faza Nelly - R.I.P
3.Adili(Nigga One) - R.I.P
4.Kibacha(K Single) - bado yupo
5.Hashim Dogo -bado yupo
6.D-Rob - R.I.P
7.Chief Ramso - bado yupo

Well!
Ukizumgumzia HIPHOP, kimsingi mkoa wa Mbeya tunaweza kuita ndio JIKO. Nilivyopitia historia za wanamuziki wa kileo wa rap/hip hop (unaweza kucheki facebook pages zao) wengi wameanzia kuimba wakiwa shule Mbeya. Hapa naongelea
1. Mr II (sugu)
2. Joseph Haule (Jay)
3. Adili Nkwela
4. Juma Mohamed Mchopanga (Jay Mo)
5. Jafari Mshamu (Jahfarai)
6. Ilinga Khalifa (C Pwaa)
7. Anselm Ngaiza (Soggy)
8. OCG (sijajua kapotelea wapi)
9. Taikuni Ally (Mchizi Mox)
10. Vivian Tilya (RIP)
11. Zainab Lipangile (Zay B)
12. Castro Komba (Caz T)

na kadhalika. Walio wengi walikutana shuleni na kuanzisha makundi yao ya kuimba, hasa wakiwaiga Naughty by Nature, BIG, Tupac nk.
Ni historia flani tamu hivi
 
Chamber Squad muziki wamejifunzia kwa Prodyuza Expera wa Tushikamane Records pale Moro,kipindi hicho wanajiita CF Boyz..na wale hawakuwa wote watoto wa Dom sema walikutana tu shuleni Mazengo Sec,Mangwea alikuwa anaishi Forest Hill Morogoro ndipo wazazi wake wanaishi sema anapenda kuiwakilisha Dom zaidi ata Noorah Kwao ni Shinyanga...ata ivyo hawa wote ni wa juzi tu.
Moro kuna hazina kubwa ya historia ya huu muziki,sema haijawai kuwekwa kwenye maandishi watu wakaijua.

Ni vema ukajifunza mengi kuliko kujifanya unajua kila kitu!

Kuna tofauti kubwa kati ya CF Boyz (Albert Mangwea a.k.a Mangwair, Mallo Star a.k.a Nzeku Chipa, QG a.k. Moses Bushagama) na
36 Chamber Squard (Agustino Makale a.k.a Accapaino, David Kabongo a.k.a Dark Master, na Athony a.k.a Tonny Kichwa Ngumu)

CF Boyz wanafanya rekodi morogoro kwa produza Kameta mwaka 1998, album yao iliitwa Heshima kwa wote na ilikuwa na nyimbo 6.

Chamber Squard ya kina Dark Master ilishinda mashindano ya Hi Hop mkoa wa Dodoma mwaka 1995 katika Ukumbi wa NK Disco Teque, Fainali waliingia na Mob Monster na Gz Mob

Hapo Magwea, Mez B na Nzeku wakiwa darasa la 6 shule ya msingi Mlimwa!

So usiseme vitu usivyovijua, Nzeku, Mangwea na Mez B wamekua marafiki toka shule ya msingi Mlimwa wakati wakiishi Area C kabla ya kukutana Mazengo mwaka 1997 wakiwa kidato cha Kwanza na kuamua rasmi kuanzisha kundi la CF Boyz.

Mwaka 1997 Dar Master, Tony na Accapaino a.k.a Tino Makale Designer ndio walikuwa wanamaliza shule Mazengo, kwa hyo baada ya Tino na Nzeku kuacha kujishugulisha na muziki ndipo mwaka 2000 Mez B na Mangwea walipomaliza kidato cha nne wakaamua kuelekea Dar es salaam kuungana na Dar Master na Tonny na kuwa Chamber Squard!
Mwaka mmoja baadae 2001 Malik Haji Nura nae alipomaliza kidato cha 4 akajongea Dar kuugana na Chamber Squard!

Labda pia nikufahamishe maana ya 36 Chamber iliyozaa Chamber Squard, shule ya sekondari mazengo ilikuwa na mabweni 4, ila katika mabweni hayo manne Bweni la Ujamaa ndo lilikuwa kubwa, refu na vyumba vingi kuliko yote!

Miongoni mwa vyumba vya bweni hilo ni chumba namba 36, ambacho asilimia kubwa ya walikoua wakiishi hicho na kushinda walikuwa wanahusudu muziki wa HI HOP.

So ikawa wanafunzi wakikosa kuwaona wenzao darasanai wakiulizana wengine wanajibu atakua 36 Chamber!

36 Chamber Dar Master na Accapaino walikuwa wakiishi Uzunguni na Tony alikua anaishi Kikuyu!

Wakati huo Magwea na Nzeku walikuwa wakiishi Area C na Mez B walihamia Kikuyu.
 
Mkuu mfano miaka hiyo Arusha na Mbeya zilikuwa juu sana kwa Hip hop lakini wasanii waliokuwa wanasikika ni wa Dar tu na si kwasababu ya uwezo wao pekee bali media za Dar zilikuwa bias mno!

mfano imechukua muda mrefu msanii kama Mr Ebbo(kipindi anaishi Arusha) kujulikana lakini jamaa alikuwa anaimba R&B tena kwa kuchanganya English na Kiswahili fasaha sana yaani alikuwa balaa!

Unajua Xplastaz wa Arusha pamoja na kutikisa ughaibuni wakiwa na rapper mkali kama Ruff Nelly lakini nyimbo zao zilikuwa hazipigwi Dar wala vituo vya TV kama Channel 5 havikuwahi kurusha hata nyimbo moja yao.Je unajua wasanii wa kwanza nyimbo yao kurushwa Channel O kutoka Tanzania ni Xplastaz tena hapa Bongo wakiwa hawaonekani ktk TV zetu?

Watu wengi wa muziki hapa Dar hasa wenye vituo vya radio kama hawafaidiki chochote na wewe hutasikika!

Kama unasema kuhusu media itakua unaongelea miaka ya 95 na kuendelea!
Kwa sababu miaka ya 95 kurudi nyuma hapakuwa na media iliyokuwa ikipiga miziki ya HIP HOp, kwa maana hiyo kama wasanii unaosema hawakupata airtime kwa media za channel 5 na zingine waongelea miaka ya 2000.

Tambua Radio One ndio FM station ya kwanza kuanzishwa nchini mwaka 1994 na ilichukua takribani miaka 4 mpaka 1998 kama sikosei ndio ikaja RFA!

Lakini elewa hata kabla ya kuja kwa Redio One wasanii wengi tu tuliwafahamu na kusikia kazi zao japo zilikuwa kwenye Cromo!

Sasa kwa mtazamo wako wa kubaniwa na media je mwaka 90 mpaka 1996 walikuwa wana hit na nyimbo zipi na warirekodi wapi?
Sio mtu akikuimbia mageton basi unataka jamii nzima imtambue kuwa ni mkali, ilihitajika nguvu za ziada na uwezo kudhihirisha hilo!

Ukiongelea Faza Nelly mimi nilimckia mara ya kwanza mwaka 1996 je jiulize mimi sikua dar lakini niliwezaje kusikia nyimbo zake? Ikiwa unasema hakuwahi kupigwa kwa media yoyote?

Mac Mooger mwaka 1995 alikuwa na album 2 sokoni je ww umewahi kusikia wimbo wake upi redioni?

So lazima utofaitishe waliokuwa wanajifanya wana rap ili kusaka nyap, na waliokuwa wanarap kuonyesha uwezo na vipaji vyao!
 
Mkuu sipingi hata neno moja katika bandiko lako hili lakini msingi wangu mkuu ni Media za Tanzania zilipoanza kupiga Muziki wa Hip hop hazikuwa zikitoa nafasi kubwa kwa wasanii wa mikoani ambako kulikuwa na watu wenye uwezo mkubwa tu.Siwezi kuwalaumu sana radio one maana kipindi walau kilichokuwa kinapiga Hip hop tupu za Bongo cha Mike Mhagama kila jumapili (Rap time) kilikuwa hakizidi saa moja tu.

Hata kipindi media zinaongezeka hadi tunapata TV za muziki bado tatizo lilikuwepo ndio maana nikawataja X plastaz kufanya vizuri bila kupata airtime ya radio na TV zetu.

Tukizungumzia kufahamika kwa Mamcee kipindi media hazijaanza mpaka inaanza radio one ilikuwa inategemea matamasha na hasa kwenye madisko na mashuleni kitu ambacho binafsi sikizungumzii sana maana nataka tuangalie nafasi ya media zetu kuupeleka muziki huu mbele zaidi tofauti na sasa.
 
Sawa sawa hata mimi cjasema kuhusu media, ila rejea kauli yako kwamba mikoani palikua na wasanii wengi wakali ila hawakupata nafasi, ndio nikakuuliza wasanii wengi wakali km Jontwa, Saleh Jabri, WWA, Rough Niggerz, Bob Issa, Gwantaman, Double G (Godwin Gondwe), Unique Sisters, Sound Of Gansters, na nk, waliweza kujulikana nchini hata kabla hakujawa na FM Stations.

Katika hayo matamasha unayoyasema ndiko walikoshiriki na kufanya vizuri hatua iliyopelekea sifa zao kusambaa hata nje ya maeneo yao!

Hivyo nachelea kusema wasanii waliokuwa wakifanya vizuri walickika na kutambulika hata bila ya kupata airtime kwa media
 
popote ulipo Ipycalypse au yeyote atakayemuona naomba amwambie kuwa namuhitaji ili tuje tufahamishane kwa Data, je kati ya Dr Dre na Primo nani nyoko.
Niko jukwaa la Entertainment
 
Na taarab je?
Mbona inaongoza kwa kushabikiwa na mapunga na wasagaji?
Are you among them?
If YES nenda kachukue kopo ukachambe then usirudi hapa kawatafute ushuzi wenzio.

watu tunasikiliza miziki inayoeleweka rnb,jazz fusion,soul,pop,rock n roll,afropop,rhumba..sio iyo miziki ya wasela...ivi huwa ata kuoga wanaoga kweli hao!!!
 
watu tunasikiliza miziki inayoeleweka rnb,jazz fusion,soul,pop,rock n roll,afropop,rhumba..sio iyo miziki ya wasela...ivi huwa ata kuoga wanaoga kweli hao!!!
Ukitaka kujua maana ya neno msela, kuna truck aliimba Ngwea & Nature inaitwa hivyohivyo "MSELA",

Ukiikosa hiyo basi tafuta remix yake ambapo Jay Mo kafanya na Bamboo wa Kenya,

Tafsiri ya neno msela imeelezewa kwa kirefu tu.

Labda we kati ya maudhui ya wimbo na muimbaji wake unaangalia nini kwanza??
 
Jamani Mnakiona Anacho Fanya
  • Nash Mc
Hapo Ndo naendelea Kumvulia Kofi Na Kuamini Kuwa Yeye Ni Real Mc Tz
 
Back
Top Bottom