lifeofmshaba
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 867
- 219
MKUU wa Polisi wa Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, jana alishikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumpiga risasi sehemu ya makalio, Mkufunzi wa Sanaa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Dadie Kitururu (42).
Hata hivyo, baadaye ofisa huyo wa polisi aliachiwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Adolphina Chialo, alithibitishwa kutokea kwa tukio hilo.
Alisema inadaiwa kuwa jioni ya siku ya tukio Kitururu alimgonga kwa gari mpanda baiskeli aliyetambuliwa kuwa ni Salumu Chiga (58), mfanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Kamanda huyo alisema ajali hiyo ilitokea karibu na ofisi za Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kilichoko katika eneo la Kilakala, mjini Morogoro.Chialo alisema wakati ajali hiyo inatokea ofisa huyo wa polisi alikuwa nyuma ya Kitururu, akiwa anaendesha gari lake.
Alisema baada ya ajali hiyo, Kitururu alikimbia kuelekea eneo la Forest.
Alisema baada ya kumuona Kitururu akikimbia Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kigoma, alifyatua risasi kwa kutumia bastola yenye namba PA06897 aina ya Chaineez na kupasua tairi la mbele la gari la Kitururu.
Kamanda huyo alisema hata hivyo risasi hiyo ilipenya na kumfikia Kitururu kwenye makalio yake."Baadaye, OCD alimkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika kituo Kikuu cha Polisi cha Morogoro na kumweka rumande. Hata hivyo baadaye polisi waligundua kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na majeraha na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi zaidi," alisema kamanda Chialo.
Alisema baada ya kufikishwa hospitalini mtuhumiwa alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa sababu hali yake ilikuwa mbaya na kwamba katika uchunguzi, aligundulika kuwa na kipande cha risasi katika makalio yake.
Alisema hata hivyo madaktari walifanya jitihada kuondoa kipande hicho cha risasi.Kamanda Chialo alisema baadaye polisi walimshikilia OCD huyo kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.