Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eliuterius Hyera, aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi Chiungutwa wilayani Masasi, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na askari mwenzie.
Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicodemus Katembo leo Februari 03, 2024, imeeleza kuwa askari hao walikuwa kwenye jukumu la ukamataji wa mtuhumiwa anayedaiwa kuvunja ofisi (Haikutajwa) na kuiba.
“Mtuhumiwa huyo alianza kukimbia ili asikamatwe ndipo Askari aliyekuwa na bastola alipofyatua risasi kwa lengo la kufanikisha ukamataji na ikapelekea kumjeruhi Mkaguzi huyo.
Juhudi za kuokoa maisha yake zilifanyika kwa kupelekwa Hospitali ya Ndanda ambapo alifariki dunia akiendelea na matibabu.” Imeeleza taarifa ya ACP Katembo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi, huku mtuhumiwa akiendelea kushikiliwa kwa hatua zaidi za kisheria.
Source - CloudsTv