Obama: Tanzania ni mfano wa kuigwa

Sawa Tanzania is better off than some or many other African countries but are we really better off. Kabla ya kuanza kufurahia sifa lazima tuangalie tume linganishwa na nani. Kwa bara letu lenye nchi kama Susan. Somali, Sierra Leon, Liberia. Congo etc. Kobe akilinganishwa na konokono ataonekana ana mbio zaidi. Sawa tukubali kupokea sifa lakini tujue tu kwamba we have been compared to countries which have hit rock bottom. Tujiangalie sisi wenyewe hali yetu ikoje si kufurahia kuwa kuna wenye hali taabani kuliko sisi.

Let us be realistic mkuu, wewe kwa maono yako unataka kumwona kila mtanzania katika hali ipi? na je ataifikia hiyo hali kwa namna gani? na kwa kipindi cha muda gani? Je, hayo unayoyafikiria unadhani yatategemea resources zipi na zitafanikisha vipi?
Nimeuliza hivi ni kwa sababu umeweka maneno ambayo hayakutamkwa na hata huyo Obama sasa inawezekana labda una mawazo mengine tofauti na yale aliyoyaeleza Obama lakini unataka yawe ni sehemu ya hoja zako.
 
Mkuu what I have said has nothing to do na maneno yaliyo tamkwa directly na Obama. Ninacho sema mimi ni kwamba tusifurahie tu kuwa better off than someone. Tujiangalie wenyewe. Siyo kufurahia tu kuambiwa we are better off. What do you mean nina taka kumuona kila mtanzania katika hali gani? Kwani nimesema anything kuhusu mtanzania? You are right we have to be realistic. The countries we are told we are better of than are not doing that well. Ndiyo maana nikataja baadhi ya nchi zenye matatizo Africa. Tujiangalie sisi wenyewe na how better off we really are. I don't see the point ya kulewa sifa wakati hata wewe I'm sure you know hali halisi ya mwananchi Tanzania. And that's why i said tukubali kusifiwa lakini tusi ridhike. Au wewe uliaka nisemeje mkuu?
 
Last edited:
Ni Huduma gani za jamii ambazo ni mfano wa kuigwa? Elimu hamna kitu, Afya ndo usiseme, Mawasiliano mabovu, maji vijijini, yaani unajua hawa wakubwa wanapelekewa maendeleo kwenye karatasi lakini ki uhalisia hali ni mbaya. Ngoja hao jamaa waje kujifunza watapigwa changa lamcho tu. Unacheza na wabongo...................

Unaongea nini wewe?

1) Elimu wakati wa JMK, over 2000 secondary schools, haijatokea kwa rais yeyote aliopita, hata ukichanganya wooooooote na shule walizojenga kwa awamu zoooooooooooote, hawajafikia shule alizojenga JMK kwa muda mfupi.

Vyuo vikuu, zaidi ya 11, na vingine nane vipo njiani, kwa kipindi kifupi cha JMK. Kimoja kimevunja record ya dunia, toka kitangazwe mpaka kijengwe, mpaka kianze kuchukuwa wanafunzi, less than 2 years, si kingine bali ni UDOM. Hakuna ilipowahi kutokea namna hii na kwa muda huo.

2) Hospitali, uliza uambiwe, Huduma zinahamia hospital za wilaya, nenda hospital ya wilaya yako ukaone, hivyo ndivyo ilivyokuwa miaka minne nyuma? na sasa mkakati wa kujenga vituo vya afya kila kata umeanza, hayo huyajuwi? au huyaoni? Ni juzi tu, nilikuwa Aga Khan Hospital (Dar) kwa shughuli zangu, viongozi wa hiyo hospital wanalalamika, wauguzi na madaktari wanaacha kazi wanaenda hospital za serikali, kwa sasa zinalipa kuliko private tena kama Aga Khan inayosifika kwa kulipa. Jee, hayo huyajuwi? au huyaoni? au huyasikii?

3) Maji, nenda katizame miradi ya maji iliyopo sasa hivi katika kila wilaya, utalia kwa furaha, haijawahi kutokea. Kila wilaya inatakiwa ihakikishe wananchi wanapata maji safi na ya kutosha na mihela ipo teletele kwa miradi ya maji. Jee huyaoni hayo? au huyasikii?

4) Mabarabara, Singida - Babati - Minjingu (ilipoishia lami ya kiutoka Arusha) inajengwa tena kwa spidi ya hali ya juu. Dodoma - Babati hali kadhalika. Mkata - Handeni - Korogwe. Tayari imeanza juzi, nilikuwa huko. Na mengine kibao.

5) Mawasiliano ya simu, hii leo Tanzania mpaka vijijini unakula mtandao, wa simu na wa internet. Mimi ni shahidi wa hili, nna ki E61 changu, aaah, sijakosa mawasiliano, na nnasafiri karibu Tanzania nzima. Jee huyaoni hayo? Huyasikii?

Wengine huwa tunatazama wapi sijui, maendeleo hatuyaoni, wamerekani wanayaona sisi tupo hapa ndio tusiyaone? labda hatutaki kutazama.

6) Police Force, kwa sisi tunaesafiri sana, tunaona mabadiliko kutoka hata kwa ma trafiki waliopo barabarani. Sasa trafiki akikusimamisha anaanza kukusalimia, kwa sisi tunaamkiwa, tunaulizwa habari za safari, tunaambiwa samahani kwa kukuchelewesha tunataka kuhakikisha usalama wako na raia wengine tunaomba tukaguwe gari yako. Si mabadiliko hayo, wakati wa Nkapa polisi hawa walikuwa kama mbogo, hutaki hata kuongea nao. Sasa unaona raha wanavyoonyesha kujali.

Ama kweli asiyeona haambiwi tazama.
 
Duh...DSM wewe Mjumbe wa NEC ya CCM nini Mkuu...? Naona mshaandaa Mafanikio ya ya Miaka 5....si Mbaya mkiwaambia wananchi pia ndani ya Miaka 5 wapi Mmefeli na mnajiandaa vipi kurekebisha next 5years to come!!!
 
Swali kubwa ambalo huyo aliyekuwa anamhoji Mr. Obama angeliuliza na lingeleta maana kubwa katika mjadala huu ni: Je, Tanzania ni nchi ya kuigwa kama mfano na nchi zipi?!

Katika kuendeleza diplomasia baina ya mataifa, tumeshindwa kujiuliza, ukiacha nchi za Iran, Iraq, Zimbabwe, Somalia, North Korea na Sudan ambazo zina matatizo baina yake na nchi nyingi, je, Rais wa nchi gani hapa duniani atasimama hadharani na kuibondea nchi nyingine pasipo na uhasama wowote baina yake na hiyo nchi?!
 
Nadhani Kikwete, Pinda, Ngeleja, Chenge, Ballali, na wenzao waende wakagombee uongozi wa Marekani, wawaongoze jinsi wanavyotuongoza sisi, halafu sisi Watanzania tuwasifie kwa kazi nzuri na kuwataka Waingereza wawaige wao!
Mkuu hapa umekwenda very low.....
 
Aje Tz ajione, VIONGOZI WETU WAKIENDA ULAYA WANADANGANYA Tu, Nenda north Mara, nenda singida hakuna maji, nenda DSM hakuna maji, Hospitali zenyewe hazina vifaa vya kisasa watu wakubwa wanaenda kutibiwa nje why?? Jicho tu LOWASA LIMEMPELEKA MAREKANI. Nchi kubwa hizi zinaisifia hii nchi sana kwa sababu wanapata dhahabu, Tanzanite na almasi. Mfano bush alikuja alipelekwa Manzese anapelekwa pazuri tu kama ARUSHA, Wangempeleka KIGOMA, Kigoma wana miaka nenda rudi hakuna UMEME barabara hazipitiki. Ni noma wala OBAMA AKAE KIMYA NA MATATIZO YETU. Kikubwa TZ HATUUAN NDO WANACHOSFIA. Be a think Tank

Tatizo la maji Singida ni la zamani, nenda kaone sasa, au Singida gani unayoongea wewe? kwani kuna Singida Usanda pia.

Tatizo la majii La Dar limeshapatiwa ufumbuzi wa kudumu na tenda zinatangazwa hivi karibuni kabisa. Kimbiji kuna maji ya kuinywesha Dar kwa miaka 200 ijayo bila tatizo. Na ni safi kabisa. Sijui uko wapi hili hulijuwi.

Umeme, hujaona mikakati ya JMK? hilo ni tatizo linalopatiwa ufumbuzi kwa Tanzania nzima kila kukicha na hivi karibuni, kabla hajamaliza kipindi chake utasikia ni nini kinafanyika/ Umeme Kigoma umeshatatuliwa au hulijuwi hilo?

Barabara za Kigoma hujuwi kama wakati wa JMK zimeshaanza kutengenezwa na hata Kabwe akajidai kuwa yeye ndio aalieishinikiza serikali? akaambiwa kijana tulia, tafuta jingine hizo ni ahadi za JMK anazitimiza.

Tafuta Jingine.
 
Swali kubwa ambalo huyo aliyekuwa anamhoji Mr. Obama angeliuliza na lingeleta maana kubwa katika mjadala huu ni: Je, Tanzania ni nchi ya kuigwa kama mfano na nchi zipi?!

Katika kuendeleza diplomasia baina ya mataifa, tumeshindwa kujiuliza, ukiacha nchi za Iran, Iraq, Zimbabwe, Somalia, North Korea na Sudan ambazo zina matatizo baina yake na nchi nyingi, je, Rais wa nchi gani hapa duniani atasimama hadharani na kuibondea nchi nyingine pasipo na uhasa wowote baina yake na hiyo nchi?!

SteveD,
Kama umesikiliza kwa makini na kufuatilia ile interview, hilo swali lako unalo suggest kamwe lisingeweza kuwa kama swali la ziada kwa sababu mahojiano hayakujikita katika kuongelea maswala ya Tanzania. Obama alitumia mfano wa Tanzania kama sehemu ya kuimarisha hoja yake ya msingi kwamba nchi za Africa inabidi zitatue matatizo yake yenyewe na nchi wahisani au wafadhili watasaidia tu pale ambapo wenyewe tumeonesha nia ya kutatua matatizo yetu.
 
Duh...DSM wewe Mjumbe wa NEC ya CCM nini Mkuu...? Naona mshaandaa Mafanikio ya ya Miaka 5....si Mbaya mkiwaambia wananchi pia ndani ya Miaka 5 wapi Mmefeli na mnajiandaa vipi kurekebisha next 5years to come!!!

Hayo ni machache ya kuwakumbusha wasiyoona na wasiyosikia. Nikianza kuyaandika mafanikio ya JMK ya hii miaka michache itabidi nikeshe hapa. Tutawakumbusha wasiyoona japo kidogo kidogo.

Hakuna ujumbe wa NEC wala nini. na wala mimi si mwanachama wa CCM wala chama kingine chochote. Lakini 'mnyonge mnyongeni haki yake mpeni'
 
Tatizo la maji Singida ni la zamani, nenda kaone sasa, au Singida gani unayoongea wewe? kwani kuna Singida Usanda pia.

Tatizo la majii La Dar limeshapatiwa ufumbuzi wa kudumu na tenda zinatangazwa hivi karibuni kabisa. Kimbiji kuna maji ya kuinywesha Dar kwa miaka 200 ijayo bila tatizo. Na ni safi kabisa. Sijui uko wapi hili hulijuwi.

Umeme, hujaona mikakati ya JMK? hilo ni tatizo linalopatiwa ufumbuzi kwa Tanzania nzima kila kukicha na hivi karibuni, kabla hajamaliza kipindi chake utasikia ni nini kinafanyika/ Umeme Kigoma umeshatatuliwa au hulijuwi hilo?

Barabara za Kigoma hujuwi kama wakati wa JMK zimeshaanza kutengenezwa na hata Kabwe akajidai kuwa yeye ndio aalieishinikiza serikali? akaambiwa kijana tulia, tafuta jingine hizo ni ahadi za JMK anazitimiza.

Tafuta Jingine.

Pamoja na matatizo makubwa aliyoanza nayo Mh Kikwete aliposhika ofisi kama vile ukame, upungufu wa chakula, uhaba wa umeme, kupanda kwa bei ya nishati ya petroli, kuyumba kwa uchumi wa dunia, lakini amekuwa very steady na issues za wananchi, ukweli ni kwamba ni kiongozi imara na mzuri.
Wakati wote amejikita katika kuhakikisha kuwa matatizo ya wananchi yanatafutiwa ufumbuzi, ni kiongozi anayeangalia mbali.
 
kwa kweli Mh.Rais wetu anajitahidi mabo mazuri hayataki haraka nothing can come overnight.

wahenga walisema baniani mbaya lakini kiatu chake dawa.

Raisi wetu anajitahidi sana ingawa mwanzo mgumu ipo siku wale wasio appreciate wataanza kukubali.

bravo JK Bravo Tanzania yetu
 
SteveD,
Kama umesikiliza kwa makini na kufuatilia ile interview, hilo swali lako unalo suggest kamwe lisingeweza kuwa kama swali la ziada kwa sababu mahojiano hayakujikita katika kuongelea maswala ya Tanzania. Obama alitumia mfano wa Tanzania kama sehemu ya kuimarisha hoja yake ya msingi kwamba nchi za Africa inabidi zitatue matatizo yake yenyewe na nchi wahisani au wafadhili watasaidia tu pale ambapo wenyewe tumeonesha nia ya kutatua matatizo yetu.

Yep good point Sir!
Lakini unaweza kukubaliana nami kuwa habari hii imeletwa hapa kwa nia nyingine kabisa...na huo ndiyo mwanzo wa haya malumbano. Nimependa sana lile swali ulilo muuliza MwanaFA1 hapo juu.

Ukweli wa mambo ni kwamba ni viongozi wawili tu wa Kiafrika wa ngazi za juu ambao amekutana nao tayari. Mh. Kikwete na PM wa Zimbabwe to be precise. Katika hayo mahojiano Mr. Obama asingekuwa na mfano mwingine wowote ulio bora wa kutoa kati ya Tz na Zimland ili kuleta maana katika maongezi ili kuweka msisitizo uliopo kwenye mwendelezo wa diplomasia baina ya Afrika na Marekani.
 
kwa kweli Mh.Rais wetu anajitahidi mabo mazuri hayataki haraka nothing can come overnight.

wahenga walisema baniani mbaya lakini kiatu chake dawa.

Raisi wetu anajitahidi sana ingawa mwanzo mgumu ipo siku wale wasio appreciate wataanza kukubali.

bravo JK Bravo Tanzania yetu

Hoja yako na fadhila kwa Mh. Rais wetu nazikubali na kuziunga mkono. Hata hivyo kuna mengi ambayo yangeweza kumalizika ndani ya mwaka mmoja wa ngwe yake ya madaraka. Na haya ni mengi na ndiyo yanayo gusa mboni za Watanzania walio wengi kama kipimo cha ubora wa uongozi.
 
Wewe ni kachero wa Chama Cha Mafisadi? (Simaanishi CCM lakini..) Hivi mtu mpumbavu akisifiwa kuwa ni mwelevu na ana akili unaelewaje? Utakuwa na akili ghafla simply bkoz umeambiwa una akili?
Mara ngapi tumesifiwa kuwa tu mfano wa kuigwa na uchumi unapanda? Unajua kuwa wenzetu huwa wanaishia Kariakoo na Jijini Kati na kututathmini kwa hiyo mijengo inayojengwa kwa hela za rushwa?
Kuna tofauti gani kuonekana viwanja umepiga pamba kali wakati nyumbani hakuna uhakika wa kula?
Hii ndiyo siasa ya Tanzania lakini kwa kada wa CCM kama wewe hauko tayari kukubaliana na hilo. Umeambiwa kuwa Obama is the first and last na kwamba akisema basi ndo tumereflect anachosema? Bado watu wanasafiri siku 6 kuja Dar kwa treni tena tumshukuru Mungu hawa WAJERUMANI walituachia hata hiyo reli..cjui ingekuwa je kwa walalahoi wanaokuja huku mjini kutafuta huduma!
Tumeona jana Mheshimiwa anafungua hoteli ya Kempinski Serengeti ambayo hata wanaotarajiwa kulala humo si wananchi isipokuwa wageni wnaokuja kuchuma hapa na wenye hela za kutapeli sorry mafisadi wanaoweza kumudu gharama ya chakula na usiku mmoja hapo!
Unachojivunia ni nini sasa au kwa kuwa wewe ni miongoni mwa waliokuwa blinded na keki ya serikali na ambao hamjui linaondelea uraiani tunakoishi tulio wengi?

TAFAKARI...Fikri kabla ya kujitokeza kwenye forum kama hii..HUNA JIPYA na usituchanganye sisi!!! Kama tungekuwa mfano wa Obama si angeanzia hapa kwetu mbona kasusa..pamoja na Mh kujipendekeza kwenda kwake akiwa wa 1 toka huku Afrika akitafuta favour ambayo bado wameichukua watu wa Ghana!

Huku kwetu hawamjui zaidi ya kumwona kwenye magazeti yalipitwa na muda make hata TV na redo hazikamati..ona tunavyotaabika sasa..hakuna maji, umeme, afya na elimu tumeshindwa kulipia kwa sababu ya sera mbovu ambazo zinatungwa kwa ajili ya maslahi yao wenyewe na nyie mlio karibu nao..huko huko..na OBAMA WENU..nna hasira miye we acha tu!
 
kwa kweli Mh.Rais wetu anajitahidi mabo mazuri hayataki haraka nothing can come overnight.

wahenga walisema baniani mbaya lakini kiatu chake dawa.

Raisi wetu anajitahidi sana ingawa mwanzo mgumu ipo siku wale wasio appreciate wataanza kukubali.

bravo JK Bravo Tanzania yetu

For the sake of Tanzania I pray he succeeds. Kama raisi wetu mafanikio yake ni mafanikio ya nchi.
 
Do you have priorities in terms of countries or regions? For instance, West Africa is extremely important in terms of oil; East Africa in terms of some of the strategic concerns of the United States?

But as you point out, there are strategic, national security, economic, environmental reasons why we think this region is important. And part of the reason we wanted to - although we're only going to one country this time, I actually thought that it made sense for us to connect a trip to Ghana to a previous trip with the G8. We'll be meeting a number of African countries in Italy during the G8 meeting - before that, a meeting in Russia - to show that Africa is directly connected to our entire foreign policy approach; that it's not some isolated thing where once every term you go visit Africa for a while to check that box, but rather it's an ongoing part of a broader discussion about how we move many of these international challenges forward.
"To check that box..." :)
Ha-ha-ha-hah!
Swali kubwa ambalo huyo aliyekuwa anamhoji Mr. Obama angeliuliza na lingeleta maana kubwa katika mjadala huu ni: Je, Tanzania ni nchi ya kuigwa kama mfano na nchi zipi?!
Nigeria, South Africa and Libya?

A quote from wikipedia,
Africom ,
It was reported in June 2007 that African countries were competing to host the headquarters because it would bring money for the recipient country.

....
Wafula Okumu, a research fellow at the Institute for Security Studies in South Africa, testified before congress about the growing resistance and hostility on the African continent. Nigeria, has announced it will not allow his country to host a base and opposed the creation of a base on the continent. South Africa and Libya have also expressed reservations of the establishment of a headquarters in Africa.
Follow the oil
 
[/QUOTE]
Mmarekani ni mmarekani tu hata awe ana rangi ya kijani! Obama anaendeleza yaleyale aliyoyaanzisha Bush kwa Jakaya (US ARMY'S MILLITARY BASE). Na wabongo tunavyopenda MISIFA tutaachia tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
we obama,acha kuijaza ujinga tz...hamna lolote linaloendelea hapa..
ukitaka kujua reality ya bongo tuulize sisi wabongo sio politicians..watakuuzia chai then u'll think that its true..
hamna lolote la maana linaloendelea hapa..labda wizi wa hela za epa na ufisadi uliopindukia tu.
 
Sasa ikiwa mnanyanganywa ushindi na kuibiwa kura halafu mnakaa kimya ,jamani kila mtu atatusifia serikali yetu ,ila kama watu watasimama kidete na kuisakama serikali hii iwache ubabe wa kutumia nguvu na kuiba matokeo ya uchaguzi.

Ni lazima kutokee msuguano ili walioko nje watambue kuwa chini ya majivu kuna moto ,nasema harakati zilizotokea Pemba kama zitaimarishwa Nchi nzima basi hatakuwepo wa kuisifu Tanzania ,lakini kama ni piga tajame basi hata wanyama pori watatusifu.
 
Mmarekani ni mmarekani tu hata awe ana rangi ya kijani! Obama anaendeleza yaleyale aliyoyaanzisha Bush kwa Jakaya (US ARMY'S MILLITARY BASE). Na wabongo tunavyopenda MISIFA tutaachia tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
SIo hivyo ,unajua nchi za wazungu huwa wanatazama kama hakuna anenyukuliwa akapiga makelele wao wanahesabu kuwa kuna amani na utulivu,sasa ikiwa serikali ya CCM inatupiga na kutuzalilisha halafu tunakaa kimya kama hakuna lolote kwa vipimo vyao wanahesabu kuwa hapo kuna amani na ilivyokuwa Chadema wameibiwa na hawakurusha hata jiwe basi huachwa hivyo hivyo na wala huwasikii kutia na kusema lao ,inakuwa kwao bado ni green hali haijawa mbaya ,hivyo tunahitajika kuifikisha hali iliyopo kwenye orange ili waanze kufanya wasiwasi na ikiwezekana ifike red ,hapo ndipo wataelewa kuwa serikali ilikuwa imejivalisha ngozi ya kondoo.
 
Back
Top Bottom