Pamoja na 'makaratasi' ya JK, zipo ripoti zinatoka Ubalozi wa Marekani nchini mwetu kuhusu Tanzania. Kwa jicho la 'jumla' Tanzania ni nchi ya Amani na Tulivu na yenye kutafuta maendeleo ya wananchi wake tangu nchi ilipopata Uhuru. Hilo peke yake linaweza kupelekea Rais yeyote anayelinganisha Tanzania na nchi zingine za Bara letu kuweza kusifia na kusema ni mfano wa kuingwa. Ukiweka kando uozo unaojitokeza hapa na pale bado nchi yetu ni mfano mzuri barani Africa. Obama hajakosea!
"alisema jana kuwa kila atakakopita ataziambia nchi hizo za Afrika ziige mfano wa Tanzania."
Kama habari hii ni ya kweli kabisa na si kwamba anatupiga changa la macho, naanza kudoubt credibility ya Obama. Hivi kweli Marekani inaye balozi hapa nchini, ina mashushushu kibao na vifaa vya kuangalia matukio yote duniani Rais wake anaweza asiwe makini kiasi hiki?
Eti nchi zingine ziige mfano wa TZ ; kwa yafatayo!:
-Viongozi walio madarakani kutokubali kushindwa? (angalia uchaguzi wa Biharamulo, Zanzibar) nk.
-Kuacha sumu ikawaua wananchi wake kwa kuthamini mno wawekezaji?(Angalia North Mara -au naye ana hisa humo?)
-Kufisadi hela za wananchi na kuwaacha mafukara wa kutisha?
Kufisadi hela za wafadhili? (angalia zile za maliasili)
-Kubwa zaidi ni kuitumbukiza nchi katika vita na migogoro ya kidini. Ebu asubiri islamic courts kama za Somalia zianzishwe Tz ndipo atajua kuwa kauli yake ilikuwa ya kipuuzi.
Nawasihi viongozi makini wa Africa, msiige Tanzania. Hata hiyo inayoitwa amani haipo bali ni ujinga tu. Msiige TZ kwa kuwafanya wananchi wenu wajinga na makondoo kama TZ.
Masatu,nawasiwasi na credibility yako! kati yako wewe na mchukia ufisadi nani amefanya reflection ya post hapo juu?Nahisi mzee hukuwa na haja ya kuamua tu kumkosoa Mchukia ufisadi, kwa critical thinking yake na ndiyo maana tuko kwenye hii forum.Hujaelewa! soma kasome tena bandiko, kwa kifupi issue sio "utajiri" kama ni utajiri angezungumzia SA, Botswana, Nigeria etc.Kibaya zaidi issue pia sio yeye kazaliwa wapi!
Yaani huwezi kuchangia bila kuonyesha rangi yako.You are prejudicative really you are!
Huyo Mzungu wako Masatu,
Amenyongwa au kajinyonga? Maana watu wamemzunguka na mama anamfokea utafiikiri jamaa alimuharibia mtoto wake wa Kiume (mambo ya UK na u-Pedo...).
Kama umejihangaisha kuweka picha ya mtu anajinyonga basi tafuta ya kweli na si MTU ANANYONGWA. Wee vipi bwana, yaani WWW zote hizi duniani umekosa picha hata moja ya mtu anajinyonga?
Juu ya Kikwete kusifia Obama au ukitaka geuza na kuwa Obama anamsifia Kikwete/Tanzania, si kila mara yuko kule? Anatoa ajira kwa USA kwenye mahoteli, Airports, highways, parkings etc. Pia investment zao kibao zipo pale Tz.
Labda niungane na Mtanzania. Nilishakutana na Lawyer mmoja kutoka Nigeria (mzee na umri wake) na nikaanza kupaka juu ya Tanzania. Akaniuliza kama nilishawahi kufika nchi yoyote ya Africa zaidi ya Tanzania, nikasema hapana (kumbuka Gabon niliishia Airport tu), akacheka kidogo na kuniambia:-
" I was in Tanzania, Dar es salaam. I have visited a lot of countries in Africa and i must tell you that, Tanzania you are much better than many other countries in Africa..."
Nikamwambia kuwa, wee uliishia Dar na hukuenda huko madongo kuinama.... akaongeza kuwa nchi nyingine hata hiyo Dar yao kwa kweli ni mzinga wa soo, sasa itakuwa huko Madongo kuinama??
Ila still sisi Watz tungelipenda walau tuwe tunalinganishwa na nchi kama SA, Egypt, Botwsana etc na siyo Sudan, Somalia, Ethiopia etc...
Sasa Masatu, maadamu tunajua tunachosema/kushutumu na tunafahamu kuwa mambo uozo upo pote, nani anyongwe? Wewe au sisi? Wahiwahi uje Tabora, ntakuandalia kabisa Ngoye ya Myombo chini ya Mangle tree pale shule ya Kanyenye itakusaida sana kukupunguzia hasira kwani siye ndiyo tumego.... tumegoma baba yangu kujinyonga wala kunyongwa.....
MkamaP, heheee , Lyongo (mhogo mchungu) anasema karoti wajinyinge. Walau angelisema Mpare Magimbi....... (maana yake ni Masatu hujambo?)
Kwa kusema ukweli kuwa Sisi tuna matatizo yetu hivyo wao hawajui kiundani yaani mfumo na Bunge letu hata demokrasi ya Kweli, Hata Ben naye walisema hivi hivi
Haya ni matamshi ya mvinyo ya Obama. Naweza kukusoma na kukuelewa MasatuWenzetu wanapotoa kauli kama hizo huwa hawa kurupuki kua mechanism in place. Kwa kuwa tumezoea siasa za Mwembe yanga na kupayuka ovyo tunadhani na wenzetu nao ndio hivyo hivyo
You know the Italian Prim Minister already told them he got the h***s lines up, just say the word...
mhhhhh
Wenzetu wanapotoa kauli kama hizo huwa hawa kurupuki kua mechanism in place. Kwa kuwa tumezoea siasa za Mwembe yanga na kupayuka ovyo tunadhani na wenzetu nao ndio hivyo hivyo