Nyumba ya Mbunge Kapteni John Komba yaungua moto

MMMMMH!!!!!!PUT YOURSELF UNDER KOMBA'S SHOES!!! ACHA HIZO

Asilimia kubwa ya mali za komba zimepatikana baada ya kuimba "nambari wani ni chama kilichotulemaza" kwenye kuomba kura,
Amekua kuwadi wa mafisadi, kupitia TOT kutumika kushawishi watu kupigia kura
magamba kipindi cha uchaguzi.
 
Kuna habari kuwa nyumba ya Mbunge wa Mbinga Magharibi Kpt John Komba iliyopo Litui-Mbinga inaungua. Tafadhali kwa mwenye taarifa zaidi au aliyeko-site.&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
Source: Radio Wapo
<br />
<br />
Sema polepole mwenyewe amelala afu ana Buladi Puresha... Lol
 
Poleni. Nadhani nyumba hiyo ndiyo yenye hoteli na guest kubwa na nzuri kuliko zote Lituhi.
Pasco unajua maana ya Hotel au unamaanisha mgahawa maana kwa watanzania wengi akiona sehemu wanauza chai na vitumbua ataita hotel.
 
Cpt:Komba anatakiwa Kuchukua Magari ya Zimamoto ya Jiji la Dar es Salaam then ayapeleke kwake Kuzima huo Moto! sababu Pesa anayo sana tu!.
 
CAPT.JOHNDAMIANOKOMBAMBUNGEMBINGAMANG.CCM.TEL.07442845.jpg

John Komba Mbunge wa Mbinga

WATU wasiojulikana wanadaiwa kuchoma moto nyumba ya Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, katika kijiji alikozaliwam, Lituhi, kata ya Lituhi wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma. Habari zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea Agosti 14 mwaka huu majira ya usiku katika kijiji hicho ambapo nyumba hiyo imeteketea kabisa.​

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu mmoja kati ya ndugu wa jirani na Bw. Komba ambaye alikuwa katika eneo la tukio, alijitambulisha kwa jina moja la Malumba, alisema kuwa moto huo umesababisha hasara kubwa ya kuteketeza nyumba na vitu vyote vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo.

"Ndugu yangu hapa ninavyosema, nyumba na vitu vyote vya ndani vimeteketea kwa moto lakini hakuna vifo vilivyojitokeza tupo salama," alisema. Aliongeza kuwa mbunge huyo alikuwa katika ziara ya kutembelea wapiga kura wake katika jimbo hilo na kwamba taarifa za kuunguliwa nyumba hiyo alizipata usiku akiwa katika mji mdogo wa Mbambabay na kuamua kurejea nyumbani.

Kadhalika Majira lilipomuuliza Bw. Malumba ni kitu gani hasa kilichosababisha moto huo kuunguza nyumba, alisema inadaiwa kuna watu wasiojulikana wametumia mafuta aina ya petroli kuchoma nyumba hiyo. Vilevile alipotafutwa kwa njia ya simu Bw. Komba hakupatikana kwa kuwa simu yake muda mwingi ilikuwa imefungwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba jeshi la polisi linafanya uchunguzi na litatoa taarifa kamili mara baada ya kukamilisha kazi yake. Bw. Kamuhanda alisema polisi wamekwenda huko katika kijiji cha Lituhi, kwa lengo la kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo.

Majira
 
Kinachonishangaza nyumba hiyo imchomwa moto wakati yeye akiwa ziarani huko huko jimboni kwake, inaashiria nini hasa na wakati nyumba yake iko pale kijijini Lituni kando ya mtu Ruhuhu alikozaliwa mkoani Ruvuma wilayani Mbinga, kuvuka mto Ruhuhu upande wa pili ni mji mdogo wa Manda katika wilaya ya Ludewa. Niliwahi kupita hapo mara moja miaka michache iliyopita wakati hayati Laurance Gama alipowahamisha wakazi wa hapo Lituhi palipokuwa na hospitali kubwa tegemeo la pekee la Ukanda wa Nyasa kwa kisingizio cha mafuriko ya mto huo Ruhuhu.
 
itakuwa ni peoples' power hiyo, watu wana njaa wewe unahanjahanja na tumbo lako wao wakuangalie tu, who are u.
 
Back
Top Bottom