Nyumba aliyoishi RC wa Iringa Dr. Kleruu kabla ya kuuawa na Said Mwamwindi

Huyu Mwamwindi alizikwa wp? nataka nikaone Kaburi lake...... mtu madhubuti huyu

Nilipokuwa chuo kikuu nakumbuka lecturer wetu wa Development studies alitwambia siku ya kesi yake kutajwa mahakamani ilikuwa ni kama shujaa anapita barabarani, yaani watu walikuwa wakijipanga barabarani kumsubiria apite.

Natamani mtu angeandika hadithi ya ukweli kuhusu huyu Mwamwindi. Sijui Maggid Mjengwa aliishia wapi nilikuwa nakisubiri kwa hamu kitabu ambacho alisema angeandika.
 
Siyo kweli! Mwamwindi aliua kwa vile alikuwa provoked na huyo RC. RC alimfuata shambani kwake akiwa anasimamia vibarua, shamba ambalo lilikuwa kubwa sana na wakati huo ndo siasa ya ujamaa na kujitegemea ilikuwa imeshika kasi, Mwamwindi wakawa wanamwona kama bepari fulani hivi. Maana jamaa alikuwa amejiimarisha sana katika maswala ya kilimo, ieleweke kwamba enzi hizo watu waliokuwa na combine harvester walikuwa wa kuhesabika na Mwamwindi akiwamo. RC alipofika shambani kwa Mhehe akawa anamchomachoma tumbo kwa fimbo yake (kama ya Nyerere) huku akisema hili tumbo lina mirija ya unyonyaji. Hapo hapo Mhehe akahamaki ndo akaenda kuchukua riffle yake na kummiminia risasi hapo hapo shambani. Wacha niishie hapo maana hadithi ya Mwamwindi ni ndefu sana! Wewe kijana wa jana nawe unajidai kutuletea hadithi ya Mwamwindi?

Na mimi ndivyo nilivyo adithiwa, wa lisema siku yenyewe ilikuwa ni Chrismas kama nakumbuka vizuri.

Inaelekea Dk. Kleruu (RIP) alipata taarifa kuhusu Mwamwindi kuwepo shambani kwake akiwa na wafanyakazi wake - nadhani mwaka huo ndio itikadi za ujamaa zilikuwa zimepamba moto nchini, mabepari wakawa wanafananishwa na wanyama,wakaitwa wanyonyaji, wanaibwa kwa nyimbo za kejeri na chuki - yaani wananchi walikuwa primed kuwaona mabepari kama ni wabaya kuliko wakoloni.

Misimamo ya kuchukia Ubepari nchini ilikuwa ina walakini sana, kuna baadhi ya wananchi waliokuwa na uwezo kifedha walipata wakati ngumu sana kwa kunyaganywa mali zao walizo chuma kwa jasho lao!!

Atittude zilizokuwa zimejengeka wakati huo ndizo zilimpa jeuri Dk.Kleruu kwenda kumudhihaki/dhalilisha Mr.Mwamwindi skiwa shambani kwake - kisa? Mwamwindi ni bepari, eye witness walisema walimuona Dk.Kleruu ameshikilia kifimbo akikisukuma sukuma kwenye tumbo la Mwamwindi - hakuna mwanamume worthy his salt angeweza kuvumilia provocation ya kiwango hicho - alicho kosea Mwamwindi ni kule kwenda kuchukua Rifle kutoka nyumbani kwake na kurudi shambani kumpiga risasi Dk.Kleruu - sasa time lag ya kutoka shambani kwenda nyumbani kuchukua bunduki na kurudi tena shambani hasira zilipashwa kuwa zimepungua ndio maana mahakama ilimuhukumu kunyongwa kutokana na kuonekana kwamba iliuua kwa kukusudia "murder case"

Kama Mwamwindi angekuwa na bunduki shambani alafu Dk.Kleruu akaja akamu-provoke hapo angehukumiwa kuua bila ya kukusudia akafungwa kwa muda.
 
Nilitaka nishangae tangu lini Mwafrika akawa tayari kuuwa kwa ajili ya kutetea kile anachokiamini yaani itikadi? Sana sana ukisikia Mwafrika kaua ujue ni mapenzi tu hapo hamna kingine, ngono ndiyo namba moja!
lol!
 
Na mimi ndivyo nilivyo adithiwa, wa lisema siku yenyewe ilikuwa ni Chrismas kama nakumbuka vizuri.

Inaelekea Dk. Kleruu (RIP) alipata taarifa kuhusu Mwamwindi kuwepo shambani kwake akiwa na wafanyakazi wake - nadhani mwaka huo ndio itikadi za ujamaa zilikuwa zimepamba moto nchini, mabepari wakawa wanafananishwa na wanyama,wakaitwa wanyonyaji, wanaibwa kwa nyimbo za kejeri na chuki - yaani wananchi walikuwa primed kuwaona mabepari kama ni wabaya kuliko wakoloni.

Misimamo ya kuchukia Ubepari nchini ilikuwa ina walakini sana, kuna baadhi ya wananchi waliokuwa na uwezo kifedha walipata wakati ngumu sana kwa kunyaganywa mali zao walizo chuma kwa jasho lao!!

Atittude zilizokuwa zimejengeka wakati huo ndizo zilimpa jeuri Dk.Kleruu kwenda kumudhihaki/dhalilisha Mr.Mwamwindi skiwa shambani kwake - kisa? Mwamwindi ni bepari, eye witness walisema walimuona Dk.Kleruu ameshikilia kifimbo akikisukuma sukuma kwenye tumbo la Mwamwindi - hakuna mwanamume worthy his salt angeweza kuvumilia provocation ya kiwango hicho - alicho kosea Mwamwindi ni kule kwenda kuchukua Rifle kutoka nyumbani kwake na kurudi shambani kumpiga risasi Dk.Kleruu - sasa time lag ya kutoka shambani kwenda nyumbani kuchukua bunduki na kurudi tena shambani hasira zilipashwa kuwa zimepungua ndio maana mahakama ilimuhukumu kunyongwa kutokana na kuonekana kwamba iliuua kwa kukusudia "murder case"

Kama Mwamwindi angekuwa na bunduki shambani alafu Dk.Kleruu akaja akamu-provoke hapo angehukumiwa kuua bila ya kukusudia akafungwa kwa muda.
hasira hasara!
 
Haya mambo ya Mwandindi kuchukuliwa mke wake mara sijui ikawaje au ndio mdada Lady Jay D ameii
Chukua hii Ndi ndi ndi toka kwa Mwamwindi sijui Mwandindi ikimaanisha ukicheza na ndindindi ya mtu anakusepesha kama Dr.Kileruu
 
Ni Mwamwindi siyo Mwandindi
 
Dr.Kleruu alipigwa Risasi Shambani kwa Mwamwindi akiwa Kaenda kumzuia asilime Mazao anayoyataka badala yake alime zao la biashara kwa Gharama zake halafu akawauzie vyama vya ushirika kwa bei waliyojipangia serikali halafu watalipa siku wakijiskia, hata Risasi alipigiwa shambani sio gesti wala kitandani.
Enzi zile ni enzi za Propaganda kama uliweza kuaminishwa Iddi Amin anakula watu na wewe ukaamini huwezi kuacha kuamini uongo eti kisa Kilikuwa uzinzi!
Ilikuweje aende peke yake bila mtu mwingine yeyote, dereva, askari, mkuu wa Wilaya.

Unajua ni kwa nini wakuu wa mikoa waliandamana Ikulu baada ya hukumu ys awali?

Usikurupuke mkuu, kuna kitu zaidi ya hicho ulichoaminishwa
 
Back
Top Bottom