RC Makonda na Mrisho Gambo wajifunze kwa RC Shamshama na Dr Kleruu, uongozi wa visasi haulipi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Hawa vijana wa sasa wanatakiwa wafundishwe "historia za Wakuu wa Mikoa" ili waweze kujifunza na kuishi na jamii husika bila kupandikiza chuki.

Hili Mwalimu alilitambua baada ya tukio la Mkulima wa Kihehe wa Kijiji cha Mkungugu Isimani kumtandika risasi hadharani Mkuu wa Mkoa Kleruu kisa "lugha za kashfa na kukosa heshima".

Lakini vijana wa sasa wanaokuwa wakuu wa Mikoa na Wilaya wanadhani "chuki" ya Mzee Mwamwindi kwa Dr Wilbert Kleruu ilijengwa kwa siku moja;hapana...Ulikuwa ni muendelezo wa chuki za Wakuu wa mikoa waliotangulia kuweka dharau kwa wananchi.

Mwaka 1965- 1968 Mkuu wa Mkoa Iringa alikuwa anaitwa Said Shamshama,huyu alikuwa na maneno ya kejeli sana,dhihaka na lugha ya hovyo kwa wananchi.

Wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya Uhuru 1966 akihutubia wananchi wa Iringa,akahimiza walime mazao ya biashara ili wajipatie kipato cha ziada,hasa chai na kahawa.Wazee wakaitikia,muitiko huo ukasbabibisha mazao ya chakula kupungua,na hatimaye 1967 Iringa kama moja ya "basket of Southern Highlands" ikawa na chakula kichache.

Sherehe za Wakulima 1967,Wakiwemo kina Mzee Mwamwindi kama wakulima wakubwa Iringa walifika,RC akawatukana sana kuwa ni wajinga,walipoambiwa kulima mazao ya biashara wooote walilima bila kukumbuka ya chakula.Bwana Shamshama akatukana sana kama anavyofanya Makonda.Jopo la Wazee Wakulima wa Iringa wakiongozwa na "bepari" Mwamwindi wakachukia sana.

Katikati ya hotuba akaonekana Mzee mmoja anapanda jukwaani,watu wakajua ni mzee wa TANU anakwenda kuchukua itifaki.Kumbe Mzee ana yake,alipofika Jukwaani alimuwasha RC Shamshama "kerebu" kadhaa za maana.Akamwambia mwaka jana ulituambia tulime mazao ya biashara,mwaka huu unatukashifu.Yule Mzee alifungwa gereza la Isupilo.

Nyerere akamtoa RC Shamshama akamleta RC John Mwakangale,ambaye hakukaa sana ndio akaja Dr Kleruu 1970-1971.

Dr Kleruu kaja kama kijana,damu inachemka,akiwa na PhD ya mambo ya Kilimo toka nje.Akataka kuwakomesha wale wazee waliompiga kerebu RC Shamshama.Matokeo yake akaingia anga za Mzee Mwamwindi akapigwa shaba,na siku hiyo Iringa nzima watu walisherekea kwa kunywa pombe kwenye vijiwe vya ulanzi vya Isoka na Mlandege.

Lakini chuki kwa Kleruu ilianzia kwa RC Shamshama,watu wakawa wanaona hawa RC's mbona wanakuwa "waonezi" sana.Na ndio maana hata Mwamwindi ktk kujieleza kwake,inasemwa aliwahi kujibu "Siwezi kuomba msamaha,na hata mkiniachia,naweza kumfuata huyo aliyemleta huyu Gavana(RC) huku,na hakumwambia kuwa huku kuna wanaume wenye mkoa wao"

Nyerere akaona isiwe tabu,ngoja apige sahihi jamaa apigwe kitanzi kuwatisha Wazee wengine wa mji.Sasa hawa vijana kama kina Makonda na Gambo wajifunze.Hatuombei yatokee ya Shamshama na kina Kleruu,wala si vyema,lkn binadamu ni mnyama;ana kiwango cha mwisho cha uvumilivu.Wasiongoze kwa kupandikiza chuki na visasi vya hadharani,bali kwa weledi,haki,kanuni,sheria na taratibu.

Hakuna uongozi wa kisasi na kukomoana uliowahi kushinda;kila palipo na hulka ya kisasi na kukomoana chuki hujengeka.Matukio ya Iringa kwa Kleruu na kwingine ambapo nyakati hizo hayakuripotiwa sana kutokana na "uhuru wa habari" kuwa finyu,yalimfundisha Nyerere.Na baadae alimleta RC Mohamed Kissocky kutuliza hali ya hewa.

Ndio maana ya kuwa na Chuo kama Kivukoni,zaidi ya kufundisha itikadi ya chama na TUNU za mwana-TANU,kiliwafunza vijana namna ya uongozi na maadili yake.Hapa ndipo tuliwapa watu kama Jakaya Kikwete,Nikodemus Banduka,Jaka Mwambi,Hussein Shekilango,Horace Kolimba nk.

Tuwafunze vijana,kuepuka siasa za visasi na kukomoana.Na huko upinzani,jengeni vijana katika utaasisi.Maana wanasema "A leader is born at home,and be made at School".Lets istitutionalize the leadership skills of our young generation for the coming line of leadership.
 
Hawa vijana wa sasa wanatakiwa wafundishwe "historia za Wakuu wa Mikoa" ili waweze kujifunza na kuishi na jamii husika bila kuoandikiza chuki.

Let me consider this as a thread of the week! Heshima kwako, mkuu!
 
Umeandika ushauri mkubwa sana mkuu, hasa kwa kuwakumbusha huko nyuma tulipitaje na tuliishije na hawa 'Magavana'.

Wajifunze pia hata kwa Wakuu wa Mikoa Waliopita walifanyaje kazi zao.

Lakini kwa bahati mbaya unaowapa Ushauri wameshalewa Madaraka na hivyo akili na busara zitawajia wakiwa nje ya Uwanja.
 
Vijana wanajisahau sana na haya madaraka!!Watuulize sisi tutawapa dondoo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hawa vijana wa sasa wanatakiwa wafundishwe "historia za Wakuu wa Mikoa" ili waweze kujifunza na kuishi na jamii husika bila kuoandikiza chuki.

Hili Mwalimu alilitambua baada ya tukio la Mkulima wa Kihehe wa Kijiji cha Mkungugu Isimani kumtandika risasi hadharani Mkuu wa Mkoa Kleruu kisa "lugha za kashfa na kukosa heshima".

Lakini vijana wa sasa wanaokuwa wakuu wa Mikoa na Wilaya wanadhani "chuki" ya Mzee Mwamwindi kwa Dr Wilbert Kleruu ilijengwa kwa siku moja;hapana...Ulikuwa ni muendelezo wa chuki za Wakuu wa mikoa waliotangulia kuweka dharau kwa wananchi.

Mwaka 1965- 1968 Mkuu wa Mkoa Iringa alikuwa anaitwa Said Shamshama,huyu alikuwa na maneno ya kejeli sana,dhihaka na lugha ya hovyo kwa wananchi.

Wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya Uhuru 1966 akihutubia wananchi wa Iringa,akahimiza walime mazao ya biashara ili wajipatie kipato cha ziada,hasa chai na kahawa.Wazee wakaitikia,muitiko huo ukasbabibisha mazao ya chakula kupungua,na hatimaye 1967 Iringa kama moja ya "basket of Southern Highlands" ikawa na chakula kichache.

Sherehe za Wakulima 1967,Wakiwemo kina Mzee Mwamwindi kama wakulima wakubwa Iringa walifika,RC akawatukana sana kuwa ni wajinga,walipoambiwa kulima mazao ya biashara wooote walilima bila kukumbuka ya chakula.Bwana Shamshama akatukana sana kama anavyofanya Makonda.Jopo la Wazee Wakulima wa Iringa wakiongozwa na "bepari" Mwamwindi wakachukia sana.

Katikati ya hotuba akaonekana Mzee mmoja anapanda jukwaani,watu wakajua ni mzee wa TANU anakwenda kuchukua itifaki.Kumbe Mzee ana yake,alipofika Jukwaani alimuwasha RC Shamshama "kerebu" kadhaa za maana.Akamwambia mwaka jana ulituambia tulime mazao ya biashara,mwaka huu unatukashifu.Yule Mzee alifungwa gereza la Isupilo.

Nyerere akamtoa RC Shamshama akamleta RC John Mwakangale,ambaye hakukaa sana ndio akaja Dr Kleruu 1970-1971.

Dr Kleruu kaja kama kijana,damu inachemka,akiwa na PhD ya mambo ya Kilimo toka nje.Akataka kuwakomesha wale wazee waliompiga kerebu RC Shamshama.Matokeo yake akaingia anga za Mzee Mwamwindi akapigwa shaba,na siku hiyo Iringa nzima watu walisherekea kwa kunywa pombe kwenye vijiwe vya ulanzi vya Isoka na Mlandege.

Lakini chuki kwa Kleruu ilianzia kwa RC Shamshama,watu wakawa wanaona hawa RC's mbona wanakuwa "waonezi" sana.Na ndio maana hata Mwamwindi ktk kujieleza kwake,inasemwa aliwahi kujibu "Siwezi kuomba msamaha,na hata mkiniachia,naweza kumfuata huyo aliyemleta huyu Gavana(RC) huku,na hakumwambia kuwa huku kuna wanaume wenye mkoa wao"

Nyerere akaona isiwe tabu,ngoja apige sahihi jamaa apigwe kitanzi kuwatisha Wazee wengine wa mji.Sasa hawa vijana kama kina Makonda na Gambo wajifunze.Hatuombei yatokee ya Shamshama na kina Kleruu,wala si vyema,lkn binadamu ni mnyama;ana kiwango cha mwisho cha uvumilivu.Wasiongoze kwa kupandikiza chuki na visasi vya hadharani,bali kwa weledi,haki,kanuni,sheria na taratibu.

Hakuna uongozi wa kisasi na kukomoana uliowahi kushinda;kila palipo na hulka ya kisasi na kukomoana chuki hujengeka.Matukio ya Iringa kwa Kleruu na kwingine ambapo nyakati hizo hayakuripotiwa sana kutokana na "uhuru wa habari" kuwa finyu,yalimfundisha Nyerere.Na baadae alimleta RC Mohamed Kissocky kutuliza hali ya hewa.

Ndio maana ya kuwa na Chuo kama Kivukoni,zaidi ya kufundisha itikadi ya chama na TUNU za mwana-TANU,kiliwafunza vijana namna ya uongozi na maadili yake.Hapa ndipo tuliwapa watu kama Jakaya Kikwete,Nikodemus Banduka,Jaka Mwambi,Hussein Shekilango,Horace Kolimba nk.

Tuwafunze vijana,kuepuka siasa za visasi na kukomoana.Na huko upinzani,jengeni vijana katika utaasisi.Maana wanasema "A leader is born at home,and be made at School".Lets istitutionalize the leadership skills of our young generation for the coming line of leadership.

Hamna lolote nyie wala msiwatishe watu.
 
Kama Uzazi ni kuzaa Watu Majasiri Kama Said Mwamwindi basi Kizazi kipya kimejaa Wagumba.

Kama Makamanda wa Vita wanamkimbia Kidada Kimbaumbau kama Tulia Ackson kwa kuvaa Makaratasi Mdomoni unategemea kwny level ya Wafuasi wao tut apate Said Mwamwindi?

Sifa kuu ya Majasiri Uchwara ni kupenda sana kujifananisha na Makamanda wa kweli Mara aitwe Mandela Mara aitwe Arafat, Mara aitwe Castro n.k kila kukicha zinazaliwa a.k.a Mpya
 
Back
Top Bottom