Nyumba aliyoishi RC wa Iringa Dr. Kleruu kabla ya kuuawa na Said Mwamwindi

Siyo kweli! Mwamwindi aliua kwa vile alikuwa provoked na huyo RC. RC alimfuata shambani kwake akiwa anasimamia vibarua, shamba ambalo lilikuwa kubwa sana na wakati huo ndo siasa ya ujamaa na kujitegemea ilikuwa imeshika kasi, Mwamwindi wakawa wanamwona kama bepari fulani hivi. Maana jamaa alikuwa amejiimarisha sana katika maswala ya kilimo, ieleweke kwamba enzi hizo watu waliokuwa na combine harvester walikuwa wa kuhesabika na Mwamwindi akiwamo. RC alipofika shambani kwa Mhehe akawa anamchomachoma tumbo kwa fimbo yake (kama ya Nyerere) huku akisema hili tumbo lina mirija ya unyonyaji. Hapo hapo Mhehe akahamaki ndo akaenda kuchukua riffle yake na kummiminia risasi hapo hapo shambani. Wacha niishie hapo maana hadithi ya Mwamwindi ni ndefu sana! Wewe kijana wa jana nawe unajidai kutuletea hadithi ya Mwamwindi?
Asante babu kwa kunipa Mwanga. Naweza kukuamini sasa manake wengi watoto wa tisini wanapotosha kuusu hii case
 
Nyakati ngumu hazipiti ila Watu wagumu wanapita.

R.I.P Mwamwindi hakika wewe ni shujaa wa aina yake.
Very sure. Umenikumbusha hichi kitabu
1540749818195.jpeg
 
Alinyongwa, Mwalimu alimsihii akane awe aliua bila kukusudia alikataa katu. Dr. Kreluu alikua mwasherati wa kutembea na watoto pia wake za watu. Adabu aliipata, shujaa Mwamwindi..
Shujaa wakati aligongewa mke???ushujaa angeuonyesha kwa kumchakaza mkewe p*mb* mpaka mashine iwake moto aache kuruka ruka ila alioufanya ni ushamba.

Nilikuwa namkubali ila sikujua kisa kumbe yalikuwa mapenzi!
 
Dr.Kleruu alipigwa Risasi Shambani kwa Mwamwindi akiwa Kaenda kumzuia asilime Mazao anayoyataka badala yake alime zao la biashara kwa Gharama zake halafu akawauzie vyama vya ushirika kwa bei waliyojipangia serikali halafu watalipa siku wakijiskia, hata Risasi alipigiwa shambani sio gesti wala kitandani.
Enzi zile ni enzi za Propaganda kama uliweza kuaminishwa Iddi Amin anakula watu na wewe ukaamini huwezi kuacha kuamini uongo eti kisa Kilikuwa uzinzi!
Naam umenena ukweli haswa ndivyo ilivyokuwa
 
Dr. Kleruu wapo wengi sana Nyakati hizi ila Majasiri kama akina Said Mwamwindi hawapo!!
Huyu Mkulima alimtandika Risasi RC akamtia kwny Trekta lake akampeleka kwa RPC akamwambia nimewaletea Mzoga Wenu.
Juzi kati hapa Mgambo tu wa TANAPA wameharibu mashamba ya Mahindi zaid ya heka 400 huko Mbeya kisa wamelima kwenye Hifadhi, halafu wanakijiji wanakimbilia ITV !!!
Kwahiyo unataka kusema akina Mwamwindi wanahitajika sana nyakati hizi?
 
Nilitaka nishangae tangu lini Mwafrika akawa tayari kuuwa kwa ajili ya kutetea kile anachokiamini yaani itikadi? Sana sana ukisikia Mwafrika kaua ujue ni mapenzi tu hapo hamna kingine, ngono ndiyo namba moja!
Unakunywa bia gani?
 
Huyu Dr.krelyuu mbali na kusimamia kijinga sera za ujamaa pia aikua anafanya ujamaa kwa Mke wa Mwamwindi
 
Hii haij
Kwa nini mkulima Mwamwindi alimpiga risasi RC Dk. Kleruu? V

Maggid Mjengwa

Toleo la 220

4 Jan 2012

UKIMWONA kwenye mitaa ya Iringa bado anatembea kwa hatua za kijeshi. Ni Mzee David Butinini. Alipata kuwa askari polisi na alishuhudia kwa macho yake, siku Mkulima Said Mwamwindi alipofika kituo cha Polisi Iringa akiwa na mwili wa marehemu Dk. Kleruu kwenye gari aliloendesha.

Dk. Kleruu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliyeuawa na Mwamwindi kwa kupigwa risasi. Mzee David Butinini alikuwa pia mmoja wa mashahidi kwenye kesi ya mauaji iliyomkabili marehemu Mwamwindi.

Mzee David Butinini ni rafiki yangu wa muda mrefu. Jioni ya Jumapili moja tunakutana Soko Kuu Iringa. Namuuliza juu ya kumbukumbu zake ya kilichotokea miaka 40 iliyopita.

Tunazungumza huku kwa pamoja tukikiangalia kituo cha polisi kilicho mbele yetu na ambapo Mzee David Polisi alifanya kazi kama Polisi miaka 40 iliyopita.

“Unasikia Maggid, nilishuhudia kwa macho yangu. Nilikuwa bado kijana enzi hizo. Nilikuwa mwanamichezo pia. Nilikuwa kwenye kikosi cha polisi cha mpira wa miguu. Nakumbuka ilikuwa jioni ya Jumapili ya Krismasi . Ni kwenye saa kumi na moja hivi.

Tulikuwa kama askari watatu hivi tumevalia kiraia na tulisimama pale nje ya kituo,” Mzee David ananieleza huku akionionyesha kwa mkono mahali hapo.

Kelele za makuli wabeba mizigo sokoni zinatufanya mimi na Mzee Butinini tusisikilazane vema. Wote, kutokana na utamu wa simulizi hii tunajikuta tunasogea mbele kidogo na kusimama kando ya kibanda cha rafiki yangu Mwarami. Kijana anayeuza matunda Soko Kuu la Iringa.

“Unajua Maggid, Iringa ya wakati huo ilikuwa na watu wachache sana hapa katikati ya mji. Na magari nayo yalikuwa ya kuhesabika. Na Jumapili ile ya Krismasi ilikuwa tulivu kupita kiasi. Ghafla tukasikia muungurumo wa motokaa kama tulivyokuwa tukiyaita magari enzi hizo.

“Mita mia tano mbele yetu tukaliona gari likitokea kwenye mtaa huu tuliosimama. Ni Mtaa wa Jamatini wengine wanauita Uhindini. Na kama ilivyo sasa, na enzi hizo pia barabara hii ni one way. Gari zinakwenda njia moja tu.

Zinashuka kusini, hazipandi kaskazini.

Je, ni wakati gani mlibaini kuwa ni gari la mkuu wa mkoa? Namwuliza Mzee Butinini.

“Kwanza kama askari tukabaki tukijiuliza; kwa nini dereva wa gari linalokuja anavunja taratibu za barabarani? Lakini, gari lilipokaribia tukabaini haraka kuwa ni Peugeot 404 rangi ya buluu. Ni gari la mkuu wa mkoa. Na pembeni lilikuwa na maandishi ’ RC-Iringa’. Sikumbuki namba za usajili wa gari lile. Tukahisi kuwa mkuu wa mkoa amekuwa na dharura iliyomfanya avunje taratibu za barabarani,” anasema Mzee Butinini anayeonekana kuwa na kumbukumbu nzuri ya tukio kana kwamba lilitokea juzi tu.

Unasema mlihisi mkuu wa mkoa alikuwa na dharura fulani. Je, gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo gani na dereva wa gari alifunga wapi breki ya kwanza? Mbele ya kituo? Nyuma ya kituo au kando ya kituo? Namuuliza Mzee Butinini.

“Kwa kweli hata mwendo haukuwa wa kasi sana. Ni wa kawaida tu. Dereva alipunguza mwendo baada ya kupita kituo cha polisi. Akakata kulia na kufunga breki kando ya kituo pale kwenye ule mnara wa kumbukumbu ya askari waliopigana Vita Kuu ya Dunia,” anajibu.

Nini kikatokea? Namuuliza tena Mzee Butinini ambaye wakati huo alikuwa askari kijana sana.

“Tukamuona mtu ambaye hakuwa mkuu wa mkoa akifungua mlango na kuelekea mlango wa mapokezi. Alikuwa mtu mrefu, mnene kiasi na nakumbuka alikuwa na sharubu kiasi.”

Namkatisha Mzee Butinini kwa kumwuliza; kwa vile mlifahamu kuwa gari lilikuwa la mkuu wa mkoa na dereva hakuwa mkuu wa mkoa wala dereva wake, hamkuona kuwa ni jambo la kushangaza? Mlichukua hatua gani kabla dereva huyo hajafika ‘kaunta’ ya mapokezi pale polisi?

“Bwana Maggid, kila kitu kilikuwa cha kushangaza na kilikwenda haraka sana. Maana, yule Bwana Mwamwindi alikwenda moja kwa moja kaunta na pale alikutana na afande Mbete, nakumbuka alikuwa kijana wa Zanzibar. Mara tukamwona akitoka tena na kurudi kwenye gari. Akachukua bunduki na kuja nayo tena kaunta ya polisi. Alikwenda ‘kuisarenda’ kwa maana ya kuikabidhi,” anasema Mzee Butinini.

Je, nyinyi askari mliokuwa nje mlibaki hapo hapo na umesema mlivaa kiraia. Je, mlikuwa makachero?

“Kazi ya uaskari ni kazi ya ukachero pia, lakini kwamba tulivaa kiraia siku ile ni kwa vile ilikuwa Jumapili na tena siku ya Krisimas. Na kwa kweli hatukuwa na pa kwenda. Tulikuwa tukijiandaa kusafiri kwenda Moshi kesho yake. Nilikuwa kwenye kikosi cha mpira na tulikuwa na mashindano ya polisi kule Moshi.

Kwa sisi askari vijana kituo cha polisi ilikuwa ni kama kijiwe pia cha kukutania na kupiga stori tukiwa nje. Si unaona hata sasa hivi kuna askari vijana pale kituoni wamevalia kiraia wanapiga gumzo. Na sisi ilikuwa hivyo hivyo enzi zetu,” anasema Mzee Butinini huku akinionyesha askari wale vijana nje ya Kituo cha Polisi Iringa, siku ile ya Jumapili jioni.

Namrudisha tena Mzee Butunini kwenye reli ya mazungumzo kwa kumkumbushia swali langu; Je, mlifanya nini baada ya kumwona Mwamwindi akiwapita na bunduki kwenda kukabidhi kituoni?

“Ahaa! Tuliingiwa na shauku ya kipolisi ya kutaka kwenda kuichunguza gari ya mkuu wa mkoa. Nakumbuka wakati Mwamwindi akiandikisha maelezo yake tuliizunguka gari ile ya mkuu wa mkoa kugagua kilicho ndani.

“Mimi nilikuwa wa kwanza kumtambua Mkuu wa Mkoa, Dk. Kleruu aliyekuwa amelazwa kiti cha nyuma akiwa amevalia overall nyeusi na miwani machoni. Nikasema jamani huyu ni RC Kleruu!” Mzee David anaelezea picha yake ya kwanza ya kifo cha Dk. Kleruu. Namwuliza ni kipi kikatokea baada ya hapo.

Anajibu; “Kwa kweli mambo yalikwenda haraka sana. Nakumbuka kulikuwa na pilikapilika nyingi pale kituoni. Mimi nilikuwa mtaalamu wa chumba cha mawasiliano tukiita signals. Taarifa zilianza kusambazwa kupitia chumba chasignals nilikofanyia kazi.

Ilikuwa mshikemshike. Tarumbeta la polisi likapulizwa. Askari wakakusanyika. Tukatangaziwa rasmi kifo cha mkuu wa mkoa. Kuna askari waliotumwa hospitalini kwenda kuchukua kitanda cha magurudumu cha kumlaza Dk. Kleruu na kumpeleka kumuhifadhi chumba cha maiti.

“Gari la mkuu wa mkoa likazungushwa na kuingizwa uani kwenye kituo cha polisi.

Wanamichezo tuliokuwa tukijiandaa na safari ya Moshi kesho yake tukaambiwa tuendelee na mipango ya safari. Tuliondoka asubuhi yake na basi la Relwe.

“Nyuma yetu tuliacha vumbi kubwa. Msako mkali wa kipolisi ulianza usiku ule ule wa kuamkia safari yetu ya Moshi. Iringa ilitikisika na ikaendelea kutisikika kwa wiki kadhaa.

“Kuna jamaa wa mjini na ambao walikuwa ni wakulima na walimchukia sana Dk. Kleruu. Baadhi nawakumbuka kwa majina. Jamaa hawa walipopata habari ya kifo cha Dk. Kleruu, basi, mmoja wao alinunua kreti za bia na kuanza kunywa na wenzake kusheherekea. Kati ya watu wa kwanza kunaswa kwenye msako wa kipolisi ni jamaa hawa.

Maswali kwa askari huyo wa zamani yanaendelea, namuuliza; Je, Dk. Kleruu alikuwa ni mtu wa namna gani?

“Bwana Maggid, na kwa bahati nilimfahamu sana Dk. Kleruu, maana kabla ya kuhamishiwa Iringa alitokea Mtwara. Na mimi nilifanya kazi Polisi Mtwara wakati Kleruu akiwa Mkuu wa Mkoa. Naweza kusema namfahamu Dk. Kleruu. Na ninayo ya kumwelezea hata sasa
Hii haijamalizika kaka
 
Back
Top Bottom