Nyoka na fimbo kwenye Noti ya Tsh 500 ina Maana gani? BoT yatoa ufafanuzi

Habari waungwana naomba kujua kwenye noti ya shilingi Mia tano kuna Picha ya nyoka kajiviringisha kwenye mti sasa naomba kujua maana yake kwa yeyote anayejua
 
Habari waungwana naomba kujua kwenye noti ya shilingi Mia tano kuna Picha ya nyoka kajiviringisha kwenye mti sasa naomba kujua maana yake kwa yeyote anayejua
 
Dogo yule nyoka nilimkuta ghorofani kwangu kajikunyata nikamwonea huruma nikamwekea mti akaukumbatia kwa kujiviringisha kisha nikamwita kihakazi wangu akampiga picha halafu nikamwita bosi wa BOT anayeishi jirani akaipenda hiyo picha hivyo ikawekwa rasmi kwenye noti
 
Yule Ni nyoka wa Shaba ambaye Mungu aliwaambia wana wa Israel wamtazame Kwa uponyaji soon waking'atwa Na nyoka wa kawaida
 
Yule ndio hasa anakushawishi kusaka noti Kama ilivyokuwa kwa Adam na Eva
 
Habari wana jf! Naombeni kufahamishwa kuhusu picha ya nyoka aliyejizungusha kwenye fimbo, nilishaiona kwenye Taasisi kubwa za Afya kama Muhimbili kisha nimeiona tena kwenye noti ya Tshs. 500 upande wa nyuma kushoto. Ina umuhimu gani mkubwa mpaka kutumika kwenye mahospitali na kwenye noti? Kama kuna mwingine aliyebahatika kuiona kwenye kitu kingine naomba atujuze!
Habari Nataka kutoa tofauti ya alama ya nyoka
 
Yule anaeonekana kwenye mahospitali na kwenye Pharmacy mbalimbali Duniani yule siyo nyooka Bali ni aina ya mnyoo ambao miaka ya nyuma ulikua unasumbua sana na ulikua tishio na dawa zakuutibu zilikua hazijapatikana na uliua watu wengi sana katika inchi za ukanda wa Jangwa la Saharah, Jambo ambalo lilipelekea shirika ala afya duniani likatangaza vita zidi ya huo mnyoo.
 
TZ35.JPG

Wana Jf,naomba mnijuze Ile picha ya nyoka aliejiviringisha kwenye fimbo pembezon wa Noti ya Tsh 500 ina wakilisha nini?




View attachment 846438
======

UFAFANUZI

========

MAELEZO KUHUSU BAADHI YA ALAMA KATIKA NOTI NA SARAFU
Kumekuwa na mijadala kuhusu alama zilizopo katika noti na sarafu za Tanzania, hususan alama ya nyoka inayoonekana kwenye noti ya shilingi 500.

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

Utengenezaji wa noti na sarafu za nchi yoyote ile huanza baada ya kukamilika kwa mchakato wa usanifu na michoro ya fedha husika.

Usanifu huo unahusu, michoro na alama mbalimbali ambazo zinaelekeana na nchi husika.

Katika kutekeleza jukumu la kuamua nini kitumike au kisitumike katika kutengeneza fedha, nafasi ya wananchi huzingatiwa. Hapa nchini, Benki Kuu ya Tanzania ina jukumu kubwa katika maamuzi hayo.

Alama za kawaida katika noti na sarafu nyingi hapa duniani ni kama picha za watu mashuhuri, picha zinazoonesha shughuli za kiuchumi, mali asili kama milima na maziwa, majengo marefu na wanyama.
Alama na michoro inayokuwa katika noti na sarafu ina maana halisi ili kuepusha tafsiri potofu ambazo zinaweza kutokea.

Ni wajibu wa Benki Kuu ya Tanzania kuhakikisha kwamba picha, michoro na alama zozote zinazoleta ukakasi zinaepukwa.

Kiwango cha elimu na namna ya utunzaji wa pesa kinachangia namna fedha ilivyo pamoja na alama zake.

Inatakiwa namna fedha ilivyo na alama zake ziwe zinaelekeana na kuwa rahisi kuzitambua.

Hivyo, alama ya nyoka aliyejiviringisha katika fimbo ambayo inaonekana na katika noti ya shilingi 500, inamaanisha utoaji wa huduma za afya. Hii ni alama ya huduma ya tiba inayotumika karibu duniani kote, zikiwemo taasisi za afya za hapa nchini na za kimataifa. Benki Kuu ya Tanzania iliweka alama hiyo katika noti ya shilingi 500 kuonesha umuhimu ambao serikali inaweka katika huduma za afya.

Upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, wakiwemo watoto, ni suala ambalo linapewa kipaumbele na Serikali. Hili linajidhihirisha wazi katika mgawanyo wa bajeti ya serikali ambapo sekta ya afya inapata rasimali ya kutosha.

Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
24 Agosti 2018
Uhusiono wa Nyoka, fimbo na huduma za afya ni upi sasa hapo,,,tujuavyo mfano kwenye bendera yetu ya Tz kila rangi ina aksi uhalisia wa vitu vinavyopatikana hapa nchini,,mf..njano-madini,,blue-bahari n.k,,,sasa hapo kwenye nyoka na fimbo ni ukakasi kwa kweli
 
Back
Top Bottom