BoT: Unaporudishiwa fedha chakavu usikatae

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kufuatia kuwepo kwa mivutano katika huduma mbalimbali za umma pindi mwananchi anaporudishiwa pesa iliyo chakavu, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeshauri wananchi kutokataa pesa hizo ikiwa ni halali badala yake itumike utaratibu wa kuzipeleka benki ili ziweze kubadilishwa.

Akizungumza na Swahili Times, Meneja Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano, Noves Moses amesema jukumu la Benki Kuu ni kusimamia mabenki (commercial banks) hivyo zinapaswa kuzipokea na wao hufanya mchakato wa kuziharibu na kurudisha pesa mpya.

“Inapokufikia noti ambayo unaona ni chakavu, basi tumia utaratibu uliopo kuipeleka kule inakohusika ili iweze kuchukuliwa na kwenda kufanyiwa utaratibu unaouhusika kufanyiwa kwa maana ya kuwa destroyed [kuharibiwa] ili tuweze kupata noti mpya kwenye mzunguko wetu,” amesema.

Adha, amesema pesa inaweza kukataliwa benki kutokana na kutokuwepo kwa alama mbalimbali muhimu ambazo zinaainisha uhalali wa noti, hivyo wananchi wanapaswa kutambua alama hizo kabla hawajapeleka katika mahali husika kwa ajili ya kubadilishwa.

Mkuu wa Wilaya ashitakiwa kwa kutusi na kuwaweka mahabusu watumishi
Amesema pia kuwepo kwa pesa nyingi chakavu ni kutokana na wananchi kutokuwa na elimu ya utunzaji wa pesa na kutotilia umakini wa umuhimu wa kutunza noti.

Ameongeza kuwa Serikali inatumia gharama kubwa kutengeneza pesa hizo, hivyo ni vyema wananchi watambue umuhimu wa kutunza noti na sarafu vizuri ikiwemo kuepuka kuzikunjakunja wanapozihifadhi ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
 
Sasa kwanini yule anayempa mwenzie pesa mbovu asiipeleke mwenyewe kubadili?? Sababu bank kwenyewe wanaringa sana Mimi nilienda kubadili pesa chakavu, vile vidada vikanisumbua sana! Inachosha , Bora uikatae tu
Hapa inabidi mtu uende BoT moja kwa moja iliyo karibu na ulipo. Bank hao watumishi lazima wazingue tu
 
MImi nlipeleka coins kama za laki 3 CRDB. kUfika pale, kale kadada kakaniambia hizi ku deposit tutakata hela kias flan.
Nliwasha moto wa tanuru.
Walivozidi kukaza nkawaambia mimi nauza barafu shuleni, nionyesheni wanafunzi wanaokuja na noti. Kwanza account ni yangu msinipangie cha kufanya.
Bladihenken wakaenda kumuita jamaa mmoja huko ndani ndani akaja akahesabu zooote na wakadeposit bila kukata.
 
Hata baadhi ya benki hukataa pesa chakavu wakati BOT wanataka pesa chakavu zipelekwe huko sasa sijui inakuwaje.
 
Nina hizi buku tano ngoja niende benki wakazisafishe

download (1).jpeg
 
Kuna matawi mengi tu ya benki huwa hawataki kupokea pesa chakavu, na hayo matawi machache yanayopokea hupokea kwa masharti kibao (kuna vitu kadhaa wanataka viwepo kwenye hiyo noti, uwe na akaunti benki husika) au kwa shinho upande nk.

Upande wa pili, utata upo maeneo haya.
1. Watanzania wengi hawaendi benki, na ujio wa mawakala wa benki mitaani (mawakala hawataki noti mbovu) unawafanya wafisike kabisa benki.

2. Matawi mengi ya benki hayapo karibu na maeneo ya watu wa chini wanapoishi.

3. Benki hazifunguliwi kila siku wala masaa yote.

4. Benki kuna foleni na mlolongo mrefu.

5. Watu hawana pesa mifukoni za kukaa nazo bila matumizi, hivyo pesa unayomuona nayo mtu mkononi ndio hiyo hiyo pekee aliyonayo, na anataka kuitumia muda mchache ujao. Sasa kukaa na pesa chakavu mkononi hakumsaii katika matumizi.
 
Noti mbovu ni ya elfu 5, nauli kwenda bank na kurudi elf 4. Muda masaa6 na hujafanya kazi. Bora uikatae
Naona kuna fursa hapa, inabidi ichangamkiwe.

Mtu unaweza kuwa unazikusanya hizo hela chafu kwa thamani pungufu mfano, hela chafu ya 5000 wewe uipokee kwa kumpa hela safi 4000.

Then ukikusanya nyingi uende BoT ukapewe hela safi.

Nimewaza tu, wazee wa fursa kazi kwao
 
Back
Top Bottom