Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere alikuwa puppet.Hakuwa genius.Waliokuwa wanamtumia ndio waliokuwa genius!

WAKINA NANI WALIKUWA WANAMTUMIA? Sidhani kama una maana ni wananchi maana wananchi bado wamelala
Nyerere ni mfano wa kuigwa hata hata kama kuna dini zinapinga hiyo
 
Rejea habari zilzochapishwa katika gazeti la Msemakweli toleo nambari 013 la Jumapili Juni 7-13, 1998 yenye kichwa cha habari,"Nyerere adai Ujamaa na Ukristo vimeshindwa" likinukuu mahojiano yaliyofanyika katika kipindi cha maswali na majibu katika television ya CNN.

Nyerere alisema, "Ujamaa umeshindwa kama vile Ukristo ulivyoshindwa.

Ukristo ulianza yapata miaka 2000 iliyopita na kila Jumapili niendapo Kanisani nakuta watu bado wanahubiri. Na kwa kweli sina hakika kama kuna nchi hata moja tunayoweza kuiita taifa la Kikristo."

Katika toleo hilo mwandishi wa Msemakweli akiripoti maoni ya Wakristo mbalimbali juu ya madai ya Nyerere.
Wakristo wengi, wakiwemo Maprofesa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo,walijitahidi sana kuutetea Ukristo kuwa haujashindwa bali Ujamaa ndio ulioshindwa peke yake.
Moja ya sababu zilizotolewa ni kuwa Ujamaa umeshindwa kwa vile umetokana na mawazo ya mtu (Nyerere), wakati ukristo haujashindwa kwa sababu haukuanzishwa na mtu bali na Yesu (ambaye Wakristo wengi hudai ni Mungu aliye hai).

Nyerere anaitwa baba wa Taifa na ni mtu wa kimataifa na hivyo maneno yake yanakuwa na uzito wa aina yake katika jamii. Sidhani kama Nyerere alitoa madai haya kwa mzaha tu.

Nyerere ni muasisi wa ujamaa wa Tanzania na amebahatika kushuhudia ukisambaratika mbele ya macho yake, pamoja na juhudi zake za kuhakikisha ujamaa unadumu.

Vile vile Nyerere ameshuhudia waasisi wa mfumo huu duniani Urusi au Soviet Union ya zamani ikisambaratika bila hata risasi moja kufyatuliwa.

Sina sababu yoyote ya kutilia mashaka matamshi ya Nyerere ambaye, pamoja na kuwa ni muumini mzuri sana wa kanisa Katoliki, vile vile ametoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya Ukristo hapa Tanzania.

Naamini ametoa matamshi hayo kwa kutumia uzoefu wake wa kitaifa na wa kimataifa katika masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa. Kutokana na uzoefu huu Nyerere alikuwa katika nafasi nzuri sana ya kuchambua na kuongelea masuala haya.

Imeleweka wazi kuwa Ujamaa ni mfumo wa maisha ambao uliasisiwa na kina Karl Marx na Lenin, hawa ni binaadamu kama mimi na wewe.

Je, Ni kweli kuwa Ukristo (Christianity) ulianzishwa na Yesu, Mungu aliye hai?

Biblia inatueleza kuwa Ukristo kwa mara ya kwanza ulianza pale Antiokia ambayo iko katika bara la Ulaya (soma Matendo ya mitume 11:26) miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa amekwisha kamilisha kazi aliyotumwa na Baba yake hapa duniani.

Ikumbukwe hapa kuwa Yesu hakuwahi kufika Antiokia katika maisha yake yote ya hapa duniani. Na aliwakataza kabisa wanafunzi wake kupeleka mafundisho yake nje ya Israel (soma Mathayo: 10:5-6).

Hakuna hata sehemu moja katika Biblia tunapofahamishwa kuwa Yesu alileta mfumo mpya wa maisha hususan Ukristo. Yesu mwenyewe anatufahamisha kuwa hakuja kutangua mfumo alioukuta uliokuwepo toka wakati wa nabii Musa (ambao sio Ukristo), bali kuutimiliza (Mathayo: 5:17-20). Na kwa Wayahudi peke yao, na wala sio kwa Wazungu au Waafrika au Wahindi au makabila mengine (Gentiles) ya ulimwengu huu (Mathayo 14:21-28).

Ukristo umeasisiwa na Sauli ambaye ndie Paulo. Katika mazingira ya kutatanisha bila ya kuwepo ushahidi wa kuaminika, Paulo alidai kupewa Utume na Yesu mwenyewe katika Njozi.

Kwa ajili ya majadiliano hayo naomba tukubali kuwa ikiwa Paulo alikuwa Mtume. Lakini bado hii haimpi hadhi ya Uungu, bado anabaki kuwa binaadamu kama wengine.

Katika nukta hii tukumbuke kuwa Paulo hakuwahi kukutana na Yesu katika uhai wake. Na ni vema vile vile tukakumbuka kuwa huyu ndio yule Paulo aliyekuwa mstari wa mbele katika kuwatafuta na kuwaua wanafunzi wa Yesu.
Vile vile tisisahau kuwa huyu ndie Paulo aliyekufa kwa kukatwa kichwa karibu na Roma kati ya mwaka 61B.K. na 68 B.K.

Bibilia haituelezi kuwa Paulo baada ya kufa alifufuka na hivyo kuushinda umauti kama inavyodaiwa kwa Yesu, hivyo kupata hadhi ya uungu.
 
Inanipa matumaini kuona mtu kama Gavana akiipinga biblia kwa yale yanayosadikisha uungu,uana na uBwana wa Yesu, maana natambua kuwa ni mtu wa aina gani. Akiisha maliza kupinga kwa nukuu za vitabu mbali mbali vya wasioamini, hurudi kuprove kile anachoamini yeye kwa nukuu za biblia ile ile aliyoipinga punde. Imenifundisha kuwa huyu yupo kwenye kundi la wale waalimu wa mihadhara ya usiki. Ni wa aina ya maandishi na mafarisayo waliokuwa wakimkataa yesu kwa nukuu za kitabu wanachofundishia dini yao. Ni dini hiyo ya kiyahudi gavana anayojifariji kwayo ampingapo Yesu na ni hiyo hiyo anayojifariji nayo ateteapo ungo wake wa kumchomeka Muhamadi mahala fulani katika historia ya wayahudi. Ni huyu huyu anaejifariji na nukuu za nyerere kuhusu kushindwa kwa ukristo, na ni huyu huyu anayemwita nyerere kafiri anapotaka kutetea uislamu wake.Gavana hebu tusaidie ikiwa mitume na manabii wote hata zamani za Yesu wote ni waebrania(wayahudi). Ni wapi wewe mmatumbi unapatikana na muongozo nje ya hawa? Torati, zaburi, na injili zinamtambua muhamadi? Usituletee nukuu za q'uran ya mhamadi maana hiyo kajinenea mwenyewe tu bila shahidi yeyote kati yake na Mungu. Maana ndani ya kitabu kisicho shaka, Amosi 3 anasema Mungu hatafanya jambo lolote bila kuwafunulia, watumishi wake, manabii..
 
Inanipa matumaini kuona mtu kama Gavana akiipinga biblia kwa yale yanayosadikisha uungu,uana na uBwana wa Yesu, maana natambua kuwa ni mtu wa aina gani. Akiisha maliza kupinga kwa nukuu za vitabu mbali mbali vya wasioamini, hurudi kuprove kile anachoamini yeye kwa nukuu za biblia ile ile aliyoipinga punde. Imenifundisha kuwa huyu yupo kwenye kundi la wale waalimu wa mihadhara ya usiki. Ni wa aina ya maandishi na mafarisayo waliokuwa wakimkataa yesu kwa nukuu za kitabu wanachofundishia dini yao. Ni dini hiyo ya kiyahudi gavana anayojifariji kwayo ampingapo Yesu na ni hiyo hiyo anayojifariji nayo ateteapo ungo wake wa kumchomeka Muhamadi mahala fulani katika historia ya wayahudi. Ni huyu huyu anaejifariji na nukuu za nyerere kuhusu kushindwa kwa ukristo, na ni huyu huyu anayemwita nyerere kafiri anapotaka kutetea uislamu wake.Gavana hebu tusaidie ikiwa mitume na manabii wote hata zamani za Yesu wote ni waebrania(wayahudi). Ni wapi wewe mmatumbi unapatikana na muongozo nje ya hawa? Torati, zaburi, na injili zinamtambua muhamadi? Usituletee nukuu za q'uran ya mhamadi maana hiyo kajinenea mwenyewe tu bila shahidi yeyote kati yake na Mungu. Maana ndani ya kitabu kisicho shaka, Amosi 3 anasema Mungu hatafanya jambo lolote bila kuwafunulia, watumishi wake, manabii..

Kibby mbona umenikimbia katika ule mjadala wetu JEE YESU NI MWANA WA MUNGU ?????

AU WEWE NI KIBBY MWENGINE????

HIVI KULETA MAKALA HAYA NIMEFANYA UBAYA GANI ???? MIMI SIKUTOA KICHWANI MWANGU.
NYERERE AMBAYE KULIKUWA NA MAJADILIANO YA KUFANYWA SAINT NA KANISA NDIO KAYASEMA HAYO

WEWE TAFAZALI ANGALIA HOJA SIO MIMI .

BIBLIA WALA QURANI SIKUANDIKA MIMI WALA WEWE , TUSOME NA TUTAFAKARI TUSIBURUZWE

SAMAHANI KAMA POST NA THREAD ZANGU ZINA KUPA TAABU, NDIO KUSOMA HUKO , POLE SANA

NAKUKARIBISHA TENA KWENYE THREAD YA JEE YESU NI MWANA WA MUNGU???
 
nashangaa hii imekujaje huku, kwani mimi nilikuwa nachangia kwenye ile tread ya Yesu ni mwana Mungu.
.
 
Ilituendelee Mwl Nyerere alisema tunahitaji vitu 3 , watu , siasa safi na uongozi bora, (wanauchumi wanasema na Mtaji pia unahitajika). Kwa upande wa wanasiasa wa ccm wanasema ilituendelee POSHO KWA WABUNGE inahitajika na kwa wana-CHADEMA wanasema posho HAPANA. Je nani anamuenzi Mwalimu kisanii na nani anamuenzi kwa dhati, kivitendo na dhamira safi???????
 
Mwl Nyerere aliacha kuchimba madini akidai kwamba watanzania wakipata akili watachimba wenyewe. Hivyo basi nakaa chini najiuliza je, watanzania wa sasa hv washapata akili ya kuchimba hayo madini? Inasikitisha kuona madini yetu yanachimbwa na bado tunaendelea kunyanyaswa, mfano katika urenium inayoenda kuchimba dodoma, mwekezaji atapata zaidi ya USD 200 milion kwa mwaka na tanzania itapata USD 5 milion kwa mwaka. (source BBC). Kwa upande wangu haya yote yanasababishwa na viongozi wetu, kila mwaka tunapata ufadhili wa kuwasomesha wanafunzi nje ya nchi. Je wanajifunza nn huko? Au wanachoenda kujifunza ni siasa? Ni kwa nn sasa serikali yetu isione haja ya 'kuomba' sponsorship kwa vitu vya muhm sana kama madini!? Viongozi wetu sasa mmetuchosha, ina maana tutaendelea kuomba mpaka lini? Ni lini tutaacha kuwategemea wazungu kwenye rasilimali zetu wenyewe? Nasema hivi mm nitaendelea kumkubali Gadafi siku zote kwa sababu ni kiongozi aliyewafanya walibya kufaidika na rasilimali zao(mafuta), na ndo maana wamarekani wanamping!
 
Tutakukumbuka daima mileleeeee....mbele sisi nawewe tutaonana tena mwalimuuuuuuuuuu.......
 
Huyo mtu sio wakumjibu anamatatizo na mwalimu nyerere.
Matatizo gani mkuu? Kama unayaona/kuyajua yasema hapa! Acha kufikiria kwa kutumia miguu kama viongozi wako wanaotawala. Huwezi hata siku moja kutumia hata akili alokupa Mwenyezi Mungu? Huna hoja, kaa kimya
 
kabla watanzia hawajapata akili ya kuyachimba tayari fisadi mmojo kayakabidhi kwa wazungu, mtanzania kapata akili tayari mikataba imembana na hajui ataivunjaje kwani fisadi anasidia mikataba isivunjwe ili aendelee kupata 10% yake..dah kiongozi wa ukweli alikuwa nyerere tu....
 
Leo mtanisamehe waungwana, mimi napenda sana kujua historia ya taifa hili tatizo ni kuwa hata vitabu vyetu vimeandikwa kishabiki kuliko ukweli, kuna hili swala la mwalimu nyerere kunusurika kupinduliwa mara kadhaa, nimesoma mahali kuhusu Tanganyika mutiny of 1964 na habari kadha wa kadha kuhusu uhaini wa kuiangusha serikali ya mwalimu ambao hata hivyo ulishindwa.

Naomba kufahamu ukweli kuhusu taarifa hizi za mwalimu kunusurika kupinduliwa, na vipi kuhusu marais wengine waliomfata nao walikumbwa na zahama ya aina hii?
 
Leo mtanisamehe waungwana, mimi napenda sana kujua historia ya taifa hili tatizo ni kuwa hata vitabu vyetu vimeandikwa kishabiki kuliko ukweli, kuna hili swala la mwalimu nyerere kunusurika kupinduliwa mara kadhaa, nimesoma mahali kuhusu Tanganyika mutiny of 1964 na habari kadha wa kadha kuhusu uhaini wa kuiangusha serikali ya mwalimu ambao hata hivyo ulishindwa.Naomba kufahamu ukweli kuhusu taarifa hizi za mwalimu kunusurika kupinduliwa, na vipi kuhusu marais wengine waliomfata nao walikumbwa na zahama ya aina hii?
Kwa ufahamu wangu hili mutiny 1964 lilikuwa bonge la soo hadi kusabisha Mwalimu kuomba msaada tena shingo upande kwa yule yule mkoloni mungereza.Kwa ufupi ni Her majesty Army ndio lilozima uasi vinginevo leo tungehadithia mengine.
 
fanya utafiti wanao mtukana nyerere wengi ni dini moja hapa bongo kwa kisingizi aliwadandamiza
halafu sijiamini kwani mimi nyerere

siyo kweli maneno yako. Na huyu mwandishi je?


Kama si Nyerere, tusingekuwa na ombwe hili la uongozi!

Evarist Chahali
Uskochi
29 Jun 2011
Toleo na 192












WIKI hii ninazungumzia jambo linaloweza kuwakera baadhi ya wasomaji wa safu hii; ninajaribu kumkosoa mwasisi wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere na itikadi yake ya Ujamaa na Kujitegemea, na jinsi ilivyojenga msingi wa ufisadi na utapeli wa kisiasa.
Nimetahadharisha kuwa mada hii inaweza kuwakera baadhi ya wasomaji kwa sababu kuu mbili. Kwanza, hata baada ya kifo chake, Nyerere ameendelea kubaki na heshima ile ile aliyokuwanayo katika siasa za nchi yetu, na neno lolote baya dhidi yake linaweza kukusababishia hasira kubwa.
Kimsingi, kumsema Nyerere vibaya kunaweza kutafsiriwa sio tu kama ukosefu wa heshima; bali pia sawa na “kutafuta laana.”
Sababu ya pili ni ukweli kwamba kwa mujibu wa mila na desturi zetu za Kiafrika, si vyema kumsema vibaya marehemu. Sifahamu kwa nini jamii inapendelea kuzungumzia mema tu ya waliofariki na kuepuka mabaya yao, lakini inawezekana ni miongoni mwa njia za kuwaliwaza wafiwa.
Kumzungumzia Nyerere na Ujamaa kunahitaji zaidi ya makala moja, na kwa minajili hiyo nitaelemea zaidi kwenye hoja ninayojaribu kuitengeneza kwamba kwa kiasi fulani (na pengine kiasi kikubwa) kuna mambo ambayo laiti Nyerere angeyafanya vyema, basi, leo hii tusingekuwa tunashuhudia nchi ikipelekeshwa na mafisadi huku uongozi wa nchi ukiwa katika mtindo wa “bora liende”.
Baadhi ya wachambuzi wa siasa wanakwenda mbali na kumtuhumu Nyerere kuwa alipoamua kung’atuka mwaka 1985 hakufanya hivyo kwa minajili ya kupisha wengine waongoze; bali ilikuwa ni dalili ya kukubali kimya kimya kuwa jaribio lake la Ujamaa limeshindikana na nchi ilikuwa imemshinda.
Wachambuzi hao wanafikia hatua ya kumshutumu kuwa, kwa hakika, wakati anastaafu alipaswa kuwaomba radhi Watanzania kwa baadhi ya makosa aliyofanya, na ambayo kwa sasa yanaisumbua sana Tanzania.
Kwa minajili ya makala hii, naomba niweke kando mazuri mengi ya Nyerere. Sifanyi hivyo kwa ajili ya kumfanya aonekane mbaya tu; bali kuepusha mkanganyiko katika uwasilishaji wa hoja yangu. Na kwa upande mwingine, takriban kila Mtanzania anafahamu mema ya Baba wa Taifa, lakini yayumkinika kuhitimisha kuwa “mabaya” yake yameendelea kuwa kama mwiko.
Kosa moja kubwa la Ujamaa wa Nyerere lilikuwa katika namna jamii ilivyotakiwa kuwanyenyekea viongozi. Wengi tunakumbuka kibwagizo “zidumu fikra za mwenyekiti...” Leo hii tunaweza kujiuliza pasi hofu kuwa “zidumu hata kama ni hovyo?”
Ujamaa ulifanikiwa kutengeneza matabaka yasiyoonekana. Kwa vile Chama kilishika hatamu, na uongozi wa Chama kubaki kwa wateule wachache, kilichojitengeneza ni hali ya u-Mungu mtu kwa viongozi wetu. Japo Nyerere alikuwa mcha Mungu, kama Mjamaa alijitahidi sana kupunguza nguvu ya dini kwenye harakati za jamii.
Kimsingi, Nyerere alitaka dini ibaki kuwa suala la mtu binafsi lakini isiwe jambo linaloweza kukinzana na siasa na uongozi wa nchi. Ni kwa minajili hiyo, baadhi ya wachambuzi wa siasa wanaamini kuwa hata “hujuma” dhidi ya taasisi muhimu kwa Waislamu ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) zililenga kuepusha uwezekano wa asasi hiyo kutoa uongozi mbadala kwa jamii (hususan Waislamu).
Kadhalika, baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa hata kile kinachodaiwa kuwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kugeuzwa chombo cha kuwakilisha maslahi ya dola badala ya waumini, ni matokeo ya jitihada hizo za kupunguza nguvu za dini kwenye jamii.
Kwa hiyo, kwa makusudi au bila kukusudia, Ujamaa ulifanikiwa kuzalisha miungu watu ambao fikra zao zilipaswa sio tu kuwa sahihi; bali kunyenyekewa na kuabudiwa kwa nguvu. Ni wazi kuwa laiti dini zingekuwa na nguvu sawa na itikadi, wananchi - ambao pia ni waumini wa dini hizo, wangeweza kumtanguliza Mungu zaidi badala ya kulazimishwa kuwaabudu watawala; hata wazembe na wale wenye mapungufu ya uadilifu.
Tofauti na sasa ambapo baadhi ya viongozi wameamua kujidhihirisha “rangi zao halisi” kwa kutetea hata yasiyopendeza masikioni mwa wananchi (kwa mfano, kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutetea “posho za waheshimiwa,” hii ya Spika Anne Makinda kuwafananisha baadhi ya wabunge na watu (Waswahili) wa Kariakoo, na ile ya Mwanasheria Mkuu, Frederick Werema na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutetea malipo kwa kampuni ya Dowans), enzi za Nyerere tulishuhudia watendaji wake wakituhadaa majukwaani kuhusu Ujamaa; ilhali mioyoni walikuwa mabepari wanaosubiri Nyerere aondoke “waanze kutafuna nchi.”

Na “dua” zao zilisikilizwa mwaka 1985 pale Nyerere alipoamua kustaafu. Bila aibu wala uoga, Awamu ya Pili chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi, ikaanzisha operesheni ya nguvu ya kuua Ujamaa. Ikumbukwe kuwa hadi wakati huo Ujamaa ulikuwa bado kama ndoto na hadi unauawa, haukuweza kufikia hatua ya kuwa kitu halisi. Ndio maana Mwinyi na wenzake waliopitisha Azimio la Zanzibar hawakupata wakati mgumu kutekeleza “mauaji ya itikadi ya Ujamaa.”
Lakini hata kabla ya Mwinyi na wenzie “kuuzika” Ujamaa, utawala wa Nyerere ulishatengeneza mazingira ambayo yalikwaza utekelezaji kamili wa itikadi hiyo. Kwa mfano, pamoja na kauli kali dhidi ya mabepari na mabeberu, Tanzania iliendelea kuwa tegemezi wa misaada ya mabepari na mabeberu haohao tangu tunapata Uhuru hadi Nyerere anaondoka madarakani.
Utegemezi huo kwa kiasi kikubwa haukuwekwa hadharani pengine kwa kuchelea kuwa ungeleta mgongano na msisitizo wa sera ya Kujitegemea. Lakini hilo ni dogo kulinganisha na ukweli kwamba miaka kadhaa kabla ya kuwekwa hadharani, Serikali ya Nyerere ilikuwa ikifanya mashauriano “ya siri” na mashirika ya fedha ya kimataifa kuhusu mipango ya kurekebisha uchumi (kibepari) ambayo kimsingi ilikinzana moja kwa moja na itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea.
Lakini lililo baya zaidi ni kwamba Nyerere alikuwa amezungukwa na matapeli mbalimbali wa kisiasa (political conmen). Hawa ni watu walionukuu ki-kasuku kila alilosema Nyerere na tukawaamini kuwa ni Wajamaa kama yeye, lakini ukweli ni kwamba walikuwa na mawazo ya kibepari na kinyonyaji. Kwa faragha, walifanikiwa kuwekeza utajiri mkubwa nje ya nchi; huku subira ikivutwa Nyerere aondoke madarakani ndipo uanze kutumika.
Watangulizi wote wa Nyerere, kwa maana ya Mwinyi, na Marais Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, ni watu waliolelewa na Baba wa Taifa. Swali la kujiuliza ni je: Waliwezaje kuficha “rangi zao halisi” na kudumisha imani ya Nyerere kwao hadi walipofanikiwa kupata urais na kubainisha wao ni watu wa aina gani?
Lakini pia tunafahamu udhaifu wa Nyerere ambao umerithiwa hadi sasa ambapo viongozi aliowapenda walipoboronga sehemu fulani waliadhibiwa kwa kuhamishiwa mahala pengine. Kiongozi anavurunda kuongoza shirika la umma; kisha anaadhibiwa kwa kupewa ubalozi!
Kuna wanaodhani kuwa huenda Nyerere hakujua kuwa baadhi ya wafuasi wake ni mbwa mwitu wenye ngozi ya kondoo.Wengine tunadhani kuwa Nyerere alifahamu kuhusu hilo, lakini, kama ilivyo kwa Kikwete na mafisadi, alikuwa na huruma kwao.
Labda aliamini kuwa ni “utoto wao tu katika kuuelewa Ujamaa, wakikua wataacha”. Kwa bahati mbaya hawakuacha, na Nyerere alipoondoka “watoto hao watukutu wa Ujamaa” wakageuka majabali ya siasa zisizojali kabisa utu wa Mtanzania wa kawaida.
Na kwa vile Ujamaa ulikuwa na chembechembe za Ukomunisti - mfumo wa kibabe usioruhusu kukosoa au upinzani, CCM aliyoasisi Nyerere ikageuka taasisi ya ki-Mungumtu ambapo licha ya kiminya fursa ya kukosoana, inawaona wanasiasa wa Upinzani kama maadui wa Taifa. Kila anayejaribu kukosoa anaonekana kama mhaini.
Ugonjwa huo ukahamia na kwenye taasisi za dola (kama Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi) ambapo badala ya kuwekeza nguvu kupambana na maovu katika jamii, raslimali kubwa inaelekezwa kuwadhibiti wazalendo wanaokemea au kupambana na maovu hayo.
Matapeli zaidi wa kisiasa zaidi ya wale waliokuwemo kwenye mfumo wametambua kuwa sehemu salama ya kuifisadi Tanzania, ni kuwemo ndani ya CCM ambapo sio tu watapatiwa ulinzi na vyombo vya dola, lakini pia watafanikisha “madili” yao ya kifisadi (kama ilivyokuwa kwenye skandali za Richmond, EPA, nk), na pindi wakijisikia kujiuzulu watapongezwa kwa “ujasiri” wao na kuambiwa hizo ni “ajali tu za kisiasa” (rejea kujiuzulu kwa Lowassa).
Migongano tunayoshuhudia hivi sasa kati ya wanasiasa na viongozi wa dini ni mwendelezo tu wa jitihada zilizoanzishwa nyakati za Ujamaa. Kadhalika, uzembe wa wabunge wengi wa CCM kupitisha kila kinacholetwa na serikali bungeni (hata kama kina madhara kwa wapigakura wao), ni mwendelezo huo huo wa Chama kushika hatamu.
Na udikteta wa Spika Makinda dhidi ya wabunge wa vyama vya Upinzani, ni utekelezaji tu wa imani hasi kuwa vyama hivyo ni mithili ya maadui wa taifa (na sio umasikini, ujinga na maradhi kama alivyotusisitizia Nyerere).
Hali kadhalika, utetezi wa waheshimwa kuhusu posho kubwa wanazolipwa na zisizoendana na utendaji kazi wao unachangiwa zaidi na imani potofu kuwa stahili zao hazipaswi kwa namna yoyote ile kufanana na za walalahoi.
Kibaya ni kwamba tumebaki kuwa taifa lisilo na mwelekeo. Kwenye Ujamaa hatupo kwa vile ulishazikwa na Azimio la Zanzibar. Kwenye ubepari hatupo kwa vile Ubepari hauhalalishi utapeli wa kisiasa na ufisadi mwingineo unaoshamiri kwenye nchi yetu.

Kama ambavyo tunaotegemea kudra za Mwenyezi Mungu kutusaidia kutatua tatizo la mgao wa umeme, hatma ya nchi yetu nayo inaelekea kutegemea kudra za Muumba.
 
Back
Top Bottom