Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Kwanza, Dowans ina kosa lipi?

Halafu, kumbuka kuwa Nyerere hakuweka misingi mizuri katika nyanja zote, na haya matatizo ya umeme, maji, elimu, umasikini, maradhi, yote yanatokana na Nyerere, ni lipi jema na lililofanikiwa alilifanya Nyerere? Nakuhakikishia hakuna! Mpaka haya matatizo ya katiba ni yake, katiba zake alikuwa akitunga yeye na watu wake wa karibu kwa siku mbili tatu anazi-implement kidikteta na hakuna wakukataa, na ukiuliza tu, kosa.

Sasa unachokataa nini? Mtoa mada hajaona jema kwa Nyerere nami namuunga mkono, hata mimi sijaliona jema lolote, na kumbuka, nilikuwepo wakati wa Nyerere, kabla yake na sasa awamu ya tatu baada yake.
ukisubiri kuonyeshwa mema wakati yapo, basi hautayaona maishani kwako kamwe...
 
Nakubali mkuu mimi sijui naomba unisaidie hivi na kile chakula cha farasi marekani nadhani unakumbuka Unga wa njano tumekula sana UGALI wake mzuri kweli wewe ndio uliomletea Nyerere? nisaidie mkuu
wewe mwenyewe unasema ni chakula cha farasi na mkapewa ninyi binadamu(ila sio mimi) , je maana yake nini? huyo mtu anawapenda au alikuwa anawadharau?
akutukanaye hakuchagulii tusi hata siku moja
 
Haaa haaa haaa! Nafikiri nimeshaanza kuelewa mjadala huu unaelekea wapi, maana kuna notion kwamba Waislamu ndio walioleta uhuru wa nchi hii na ndio sentensi kwamba eti Nyerere "alipewa tu nchi na hajui uchungu wake!" We jaribu kuwatafuta wapinzani wakuu wa Nyerere utakuta ni Waislamu!
kume umewaona hao, hao ni vipofu na ni watu wa kulaumu siku zote maishani mwao.
Hawana kitu kizuri chochote kile..kila kitu wao ni watu wa kuonewa tu
Ukiwaambia kuhusu madudu ya Kikwete wala hawayaoni kabisa.......this are new nazi's
 
ishu hapa sio kikwete ni mzuri au mwinyi ni better kuliko nyerere

ishu hapa ni kuwa nyerere hakuwa kiongozi mzuri mtakatifu anaestahili sifa zote hizo
anazopewa.............
 
Hata mimi ningeshangaa sana kama ungemkubali Nyerere wewe na kundi lako wenye akili finyu za kufikiri zaidi ya kulalamika tu kwamba tunaonewa, hatuna vyuo vingi, hatupewi madaraka, ila ukumbuke kuwa Roma haikujengwa siku moja! ni juhudi za za ziada zinahitajika ili angalau uweze kuwa mshindani siyo mshiriki badala ya kulalama kama Juha! mfano mzuri angalia matokeo ya kidato cha nne mwaka huu, sasa hapo sijui utamlaumu nani, kwani hata huko wizarani mmejitahidi kupenyeza watu wenu angalau waokoe jahazi lakini wapi hambeeki nyinyi, sasa hayo malalamiko yenu sijui mnayatoa kwa kutumia kigezo gani, huyo huyo Nyerere unayemkandia ndiyo alijitahidi angalau kutaifisha shule za dini yake mwenyewe ili na nyinyi muweze angalau kufurukuta, na kama kweli alikuwa na nia mbaya na nyie sijui mungekuwa wapi kwa sasa kwani hizo shule zenu zenyewe sijui mnazo ngapi, na hata zilizopo zinafanya nini kama siyo kambi za umbeya tu na uhuni. Na huyu Zumbukuku wa sasa hivi ndiyo bure kabisaaaaaaa, afadhali hata ya mwinyi pamoja na elimu yake ndogo lakini alikuwa msikivu siyo huyu anayejifanya anajua wakati hajui kitu!, haiingii akilini nchi yake mwenyewe maji ya shingo mambo yamemwelemea leo anajifanya kwenda kuwa msuluhishi nyumba ya jirani, watu wamekufa hata kuzikwa hawajizikwa leo anakurupuka kwenda kuwa msuluhishi kwa wengine, Arusha kwenyewe hakueleweki lakini anajifanya kuvaa pamba masikioni, ni matuamaini yangu kuwa watanzania hawatakaa wafanye makosa makubwa kama haya tena kuchagua mtetea mafisadi.
 
kama nyerere alikuwa kiongozi bora kwa nini hakufuata ushauri wa edwin mtei aliyekuwa gavana wake? Refer mkutano wa Nec pale arusha na akithibitisha udikteta wake kwa kumvua ugavana, then baada ya muda kupita akasema mtei was right, julius hakuwa kiongozi bora bali dikteta mwenye kauli nzuri thats why alimprefer kawawa aliyekuwa yes man kama pinda afu jiulize why sokoine hakulast long. Tumsikuuze saana nyerere hakuwa kiongozi kivilee ndo ametufikisha hapa tulipo now

You are too young to understand
 
Ametunyima elimu. Ana dhambi kubwa sana huyu mzee. Na ndio maana mpaka leo Mitanzania inaongoza duniani kwa ujinga

Mitanzania ikiwemo na wewe!

TZ during Mwalimu's era was 2nd to Cuba when it came to literate rates. Hiyo ilianza kuanguka wakati wa Mwinyi,then Mkapa kisha mkwere ndo amefanya wewe na hao unaowaita mitanzania,muwe wajinga!
 
wewe mwenyewe unasema ni chakula cha farasi na mkapewa ninyi binadamu(ila sio mimi) , je maana yake nini? huyo mtu anawapenda au alikuwa anawadharau?
akutukanaye hakuchagulii tusi hata siku moja

Mbona tena unaleta mipasho! wewe unajua tusaidie tupate faida, wewe mwenyewe unasema Nyerere alikuwa mtu anaesimamia msimamo wake, hakutetereka hata siku moja, na Marekani aliwapinga kwa nguvu zake zote hakutaka kudharauliwa na Marekani, sasa mbona huyo huyo unaesema mwenye msimamo kaomba msaada wa chakula Marekani wakamwambia chakula amna yapo mahindi ya farasi na mifugo mingine, Nyerere akapewa hayo mahindi ya njano Watanzania tukawa tunakula UGALI wa yanga, Nyerere kimya miaka ya 85 ndio tukajua kumbe tulikuwa tunakula chakula cha Farasi, huwo ndio msimamo? simkubali Nyerere hongera wewe ukula Ugali wa yanga
 
kama nyerere alikuwa kiongozi bora kwa nini hakufuata ushauri wa edwin mtei aliyekuwa gavana wake? Refer mkutano wa Nec pale arusha na akithibitisha udikteta wake kwa kumvua ugavana, then baada ya muda kupita akasema mtei was right, julius hakuwa kiongozi bora bali dikteta mwenye kauli nzuri thats why alimprefer kawawa aliyekuwa yes man kama pinda afu jiulize why sokoine hakulast long. Tumsikuuze saana nyerere hakuwa kiongozi kivilee ndo ametufikisha hapa tulipo now

Nimesikitishwa na hoja mfu ambayo mtu aliyeanzisha mada hii ametoa. Kusema Nyerere hakufanya mambo ya maana katika nchi yetu ni matusi kwa wale ambao wanaelewa nchi yetu ilikuwa wapi na nini kilisababisha uchumi wetu kudorora mwaka 1979-hadi miaka ya tisini. Niliona upungufu mkubwa wa uelewa wa historia ya nchi yetu pale tulipokuwa tukijadili uamuzi wa Mwalimu kuitambua Biafra na kwa kweli wale ambao wanapima maendeleo kwa wingi wa vitu ambavyo wachache wanavyo na si jinsi ambavyo wengi wanavyo.

Je, ni nani asiyefahamu kuwa hadi mwaka 1978 nchi yetu ilikuwa na uchumi mzuri sana hadi IMF walidai kuwa Tanzania lazima itumie akiba yake ya nje na ibakie isiyozidi miezi sita hapo mwaka 1977? Najua mbumbumbu wanaotoa hoja mfu humu ndani watakuwa hawajui hilo. Je, ni nani asiyejua kuwa nchi yetu ililazimika kutumia dola milioni moja kila siku katika vita ya Uganda na kuwa vita hiyo ndiyo iliyofilisi nchi yetu? Mbumbumbu wa historia na uchumi watang'aka kama watu waliofumwa ugoni? Je, ni nani asiyejua kuwa mnamo mwaka 1979-80 bei ya mafuta ilipanda sana duniani na nchi yetu ambayo tayari ilikuwa imefilisika kwa vita haikuwa na fedha za kuweza kuendesha uchumi wake? Mazezeta wa historia na uchumi hilo halipo vichwani mwao kwani hawajui na wala hawajawahi kujishughulisha kujua hilo?
Je, ni nani asiyejua mataifa yanayotoka katika vita na ambayo uchumi wake umeyumbishwa navyo yanahitaji msaada/mikopo kutegemeza chumi zao? Watoa majibu ya kijiweni hawajui hilo kwani hawajawahi kujiuliza kuwa historia ya dunia imeonyesha hivyo kwani hata mataifa ya Ulaya yalipata msaada huo kutoka kwa Marekani katika Mpango wa Marshal. Na suala la mgawo na foleni za chakula na bidhaa baada ya vita je wamewahi kujiuliza kuwa Waingereza walikaa katika mgawo kwa miaka saba na siku waliporuhusiwa kula mayai mawili ni siku ambapo Malkia Elizabeth alisimikwa?

Ninaweza kuendelea kuuliza maswali mengi cha muhimu ni kusema kuwa Mwalimu alikuwa na makosa aliyoyafanya lakini huwezi ukaniambia kuwa eti aliporomosha uchumi kwa siasa za Ujamaa bali kukataa kwake masharti ya kijinga ya IMF na Benki ya Dunia yaliyodai eti serikali yake ilikuwa imeshindwa kuendesha uchumi vizuri ni uongo mtupu. Nilikuwepo wakati ule na nilipanga foleni ya sukari, sabuni na vitu vingine na kwa kweli kama kuna wakati serikali iliwahi kutoa sababu za ukweli kuhusiana hali ya uchumi ni wakati ule. Kama mtu aliyepata nafasi ya kusoma si tu sheria bali uchumi na siasa za taasisi za kimataifa za pesa ninathibitisha kuwa hali mbaya ya uchumi ilichangiwa kwa sehemu kubwa na sababu za nje na si za ndani. Kwa bahati mbaya watu wenye kupenda majibu mepesi na kwa kweli ya kijiweni ndio wako mstari wa mbele kupotosha ukweli na kutaka kutufanya kuwa sisi tu mazezeta wasio na uwezo wa kuchambua mambo. Chuki zao kwa Mwalimu kwa kweli huwezi ukazieleza vizuri kwani mtu ambaye alidiriki hata kutaifisha taasisi za kidini na kuzifanya za watu wote hivi sasa anaonekana kuwa alikuwa na ajenda ya kupendelea watu wa madhehebu fulani? Hivi hii kweli inaingia akilini?

Ninamalizia kusema kuwa maamuzi ya Mwalimu mengi yalilenga ustawi wa watu na si wa kutaka kujinufaisha na kama alikuwa mtu aliyependa watu wasisome je si huyu aliyetaifisha shule ili watu wa dini na makabila yote wasome? Je si huyu aliyeanzisha elimu ya watu wazima na kusababisha kiwango cha kujua kusoma na kuandika kupanda na kuwa asilimia 95? Si huyu aliyejenga miundo mbinu kama Tazara na viwanda vingi ambavyo mafisadi wamevigawa bure? Si huyu aliyeweza kushinda mbinu za benki za nje kuua NBC pale ilipotaifishwa? Si huyu ambaye hakutumia madaraka yake ya uraisi kujitarisha na hata watoto wake hali zake ni zinakaribia za Watanzania wengine.

Inanisikitisha sana kuona haya yote lakini watu wenye ajenda ovu ndivyo walivyo na hawatachoka kupotosha historia ili nia zao ovu zifanikiwe. Napenda kusema kuwa watashindwa kwani wale wenye uelewa mzuri wa mambo tutasimama imara kupangua hoja zao mfu.
 
Mmeuza vyote alivyoanzisha mwalimu leo mnaona hata hafai, hao ndio watanzania wa sasa wa kizazi cha bongo freva, hamjui hata mlikotoka. Wewe unaamini kiswahili unachozungumza kutoka Mtwara, Pemba, (Kalya) Kigoma, mpaka Bukoba kimekuja hivihivi. Hospital za Bugando,Maweni Kigoma, Rufaa Mbeya, Mhimbili, Moshi.....n.k na Viwanja vya michezo kila mkoa wa Tanzania, vililetwa hivihivi. Muanzisha thread inaonekana either umri wako ni mdogo na hujui historia ya Tanzania na Dunia kwa ujumla au una lako jambo, au umetumwa au unapima bongo za Watz. Nyerere aliongoza katika vipindi vizuri na vibaya kabisa kwa historia ya Dunia. Wakati mfumo wa Kidunia unabadilika kutoka Vita baridi kuja hali ya sasa yenye Unitary super power nchi ilikuwa chini ya Nyerere. Nyerere ameongoza nchi during world oil crisis. Mwalimu kaongoza Tanzania wakati wa vita na Uganda.Hujui nchi hii imetoka wapi. Ni kweli Nyerere alikwa na mapungufu yake lakini huwezi kufananisha utawala wake na Kiongozi yoyote aliyefuata. Kama unaamini Nyerere aliacha nchi katika hali mbaya, basi kwa taarifa yako kama umri wako mdogo mpaka Mwinyi anaondoka mwaka 1995, ofisi za Serikari zilikuwa hazina hata karatasi, mahakamani kama umemshitaki mtu, tulikuwa tunanunua karatasi wenyewe. Mkapa alichofanya ni kuuza viwanda na mashirika, na alikuwa makini kidogo kukusanya kodi na alifanya vizuri muhula wa kwanza. Muhula wa pili alianza kujilimbikizia mali na fedha nyingi alizokusanya alijigawia vya kutosha. Huyu mkwere ndio hamna kitu kabisa. Alivyoingia madarakani alikuta mabaki ya fedha aliyoacha Mkapa. Akachanganyikiwa akaanza kuzigawa, kwa kubuni utaratibu kama Mabirilioni ya JK, akagawa anavyojisikia, kwa kuwa Mkwere masikini hakuzoea kuona hela nyingi kama ile, wala hajui kama ni fedha za selikari na wala kwa sasa hatujui yeye alikwapua ngapi. Na sasa selikari haina akiba ya kutosha.

Tusubiri mkwere amaliza muda waka ila kwa mwendo anaokwenda wala hata hamfikii hata punje Mwalimu. Mwalimu mwache apumzike kajenga Taifa la Tanganyika, hilo namkubali ila ukichanganya na Zanzibar hapo nakubali kuna kasoro kwenye muungano na ni changamoto ya viongozi wa sasa kuweka mambo sawa.
 
Watu wanafata mkumbo tu hii mifumo yote ya kiutawala tunayopambana nayo ni matunda ya Nyerere.
Ulaya na Marekani mpaka leo huwa wanawashangaa watanzania kumpa sifa Nyerere.
Gazeti la Newsweek la marekani lilitoa makala yake October 1999.
The death of Julius Nyerere. African independece leader andlongtime Dictator of Tanzania, evoked a flood of encomiums worldwide. Thepraise is mis-placed. Nyerere's approach devastated much of postcolonial Africa (Forbes 1999).
How does a leader wreck a country's economy yet Diea national Hero? Julius Nyerere's inefficient leadership dried Tanzania of fund, but his personality was irresistible...ni habari ndefu tembelea newsweek.com

Ni majibu mepesi ambayo yote yaliyoandikwa katika makala hiyo yanaweza kupingwa na kuonyesha udhaifu wake. Ni lazima ujue mwandishi aliyeandika hayo ni mtu wa mrengo au mtazamo gani? Si kila kinachoandikwa na magazeti hayo ni sahihi. Mtu mwenye uelewa mdogo wa mambo atakubaliana na maoni au makala hiyo lakini mwenye uelewa mkubwa atapangua hoja moja hadi nyingine. Hii imenithibitishia kuwa watoa hoja hizi ni wepesi katika nyanja hii ya Sayansi ya Kisiasa na Siasa za kilimwengu. Jielimisheni ndiyo mje mjadiliane katika jukwaa kama hili.
 
Mmeuza vyote alivyoanzisha mwalimu leo mnaona hata hafai, hao ndio watanzania wa sasa wa kizazi cha bongo freva, hamjui hata mlikotoka. Wewe unaamini kiswahili unachozungumza kutoka Mtwara, Pemba, (Kalya) Kigoma, mpaka Bukoba kimekuja hivihivi. Hospital za Bugando,Maweni Kigoma, Rufaa Mbeya, Mhimbili, Moshi.....n.k na Viwanja vya michezo kila mkoa wa Tanzania, vililetwa hivihivi. Muanzisha thread inaonekana either umri wako ni mdogo na hujui historia ya Tanzania na Dunia kwa ujumla au una lako jambo, au umetumwa au unapima bongo za Watz. Nyerere aliongoza katika vipindi vizuri na vibaya kabisa kwa historia ya Dunia. Wakati mfumo wa Kidunia unabadilika kutoka Vita baridi kuja hali ya sasa yenye Unitary super power nchi ilikuwa chini ya Nyerere. Nyerere ameongoza nchi during world oil crisis. Mwalimu kaongoza Tanzania wakati wa vita na Uganda.Hujui nchi hii imetoka wapi. Ni kweli Nyerere alikwa na mapungufu yake lakini huwezi kufananisha utawala wake na Kiongozi yoyote aliyefuata. Kama unaamini Nyerere aliacha nchi katika hali mbaya, basi kwa taarifa yako kama umri wako mdogo mpaka Mwinyi anaondoka mwaka 1995, ofisi za Serikari zilikuwa hazina hata karatasi, mahakamani kama umemshitaki mtu, tulikuwa tunanunua karatasi wenyewe. Mkapa alichofanya ni kuuza viwanda na mashirika, na alikuwa makini kidogo kukusanya kodi na alifanya vizuri muhula wa kwanza. Muhula wa pili alianza kujilimbikizia mali na fedha nyingi alizokusanya alijigawia vya kutosha. Huyu mkwere ndio hamna kitu kabisa. Alivyoingia madarakani alikuta mabaki ya fedha aliyoacha Mkapa. Akachanganyikiwa akaanza kuzigawa, kwa kubuni utaratibu kama Mabirilioni ya JK, akagawa anavyojisikia, kwa kuwa Mkwere masikini hakuzoea kuona hela nyingi kama ile, wala hajui kama ni fedha za selikari na wala kwa sasa hatujui yeye alikwapua ngapi. Na sasa selikari haina akiba ya kutosha.

Tusubiri mkwere amaliza muda waka ila kwa mwendo anaokwenda wala hata hamfikii hata punje Mwalimu. Mwalimu mwache apumzike kajenga Taifa la Tanganyika, hilo namkubali ila ukichanganya na Zanzibar hapo nakubali kuna kasoro kwenye muungano na ni changamoto ya viongozi wa sasa kuweka mambo sawa.

Asante ndugu yangu kwa kuwakumbusha mbumbumbu wa historia ya nchi yetu nini kilikuwa kinaendelea na hali ilivyokuwa. Hii inaonesha tuna jukumu kubwa la kuandika vitabu kuwaelimisha Watanzania wenzetu ili watu wenye nia mbovu waweze kuwekwa hadharani.
 
Nakubaliana na wewe, Nyerere ameongoza wajinga na akaendelea kututia ujinga, kwani alihakikisha wa-Tz hawajui chochote kinachoendelea duniani, hebu angalia nchi gani duniani inapata uhuru baada ya miaka zaidi 30 haina TV yake ya taifa!, hata kinchi kidogo kama Zanzibar kimekuwa na TZ tangu 1972, hii Nyerere aliifanya kwa makusudi kuwanyima watanganyika elimu ili waendelee kumuona mtukufu asiyekosea. Wenye kutafakari tunajua mabaya ya Nyerere.

Nenda kawalaumu baba yako na mama yako kwa kushindwa kutumia opportunity ya Elimu bure na usafiri bure kwa wanafunzi, ambayo mwalimu aliitoa. Your parents were lazy and coward that why huoni matunda ya mwalimu. Kama wazazi wako walisoma enzi za mwalimu nenda wadadisi wanavyopata tabu kukusomesha kwa sasa kwenye huu mfumo wa cost sharing mpaka unaweza kukoment upupu wako humu JF. Mwalimu alitoa elimu bure kwa wote wenye kuweza kufaulu na ndio maana mawaziri wengi wanatoka vijijini kwa sababu walisoma bure ndio maana wako hapo. Kwa kutoa elimu bure tu ilitosha au kama ulitaka Nyerere akae darasani, amsomee na amfanyie mitihani mzazi wako enzi zake basi mmenoa na utaendelea kumlaumu nyerere mpaka kesho. Mchawi wa Maisha yako ni wewe mwenyewe na ndugu zako ambao hamkutumia elimu bure ya mwalimu leo hii mnamlaumu Nyerere kama vile alimtoza ada yoyote mzazi wako na eti hakutaka watu wasome acha kumsingizia mwalimu soma hostoria ya Elimu ya Tanzania, tumetoka wapi tuko wapi na tunaenda wapi.......................
 
Tunamsifia Nyerere pale tunapomlinganisha na wale waliofuata baada yake, vinginevyo kama unatafuta kasoro utaziona nyingi tu kwani na yeye alikuwa binadamu lakini weka kwenye mizani upime yale aliyofanikiwa utakubaliana na wengi kuwa Mwalimu alikuwa kiongozi bora.
Ninalokataa mie ni hizi kampeni za kutaka atangazwe mtakatifu! Kama angekuwa hai hata yeye mwenyewe asingekubali.
 
Kwa kila mwanasiasa wa Tanzania anaetaka kuungwa mkono na wananchi wengi amekuwa akijitahidi kujionesha kuwa ni mfuasi wa Rais wa kwanza wa Tzania Mwl Nyerere. Anasifiwa kwa kila kitu lakini kwangu mimi simkubali kabisa Mwl Nyerere. Siamini kama alikuwa na kipaji cha uongozi. Alikuwa ni dikteta. Alifinya uhuru wa habari, aliwafunga wapinzani wake, alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa Tzania. Si kwamba alikuwa anapendwa bali alikuwa anaongoza wananchi wengi wasiojua dunia inakwendaje"wajinga".

Huyo ndio Nyerere. Kwa miwani yangu namuona kuwa ana mabaya mengi kuliko mazuri kama tunavyolazimishwa kuamini. Kutojilimbikizia mali au kutoa huduma za jamii bure si kigezo cha kutokuwa dikteta maana hata Pinnochet, Hitler na Mussolin walikuwa wanatoa huduma za jamii bora na bure kabisa kwa watu wao.

Kwanza sehemu ya kwanza ya hoja yako haina ukweli; ni wapi Nyerere "anasifiwa kwa kila kitu?"

Pili tuangalia hoja zako ambazo umeziweka kiujumla na bila ya shaka wapo wanaoamini kama unavyoamini: Ili hoja zako ziwe na ukweli ni lazima zipimwe na ukweli wa historia na vile vile kutafuta sehemu nyingine ya kulinganishia. Unasema Nyerere:

Alifinya uhuru wa habari - Kwa vipi? Sheria ya Magazeti ya 1976 (ya wakati wa Nyerere) bado ipo; Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970 bado zipo na zinatumika sasa ni nani aliyefungua uhuru wa vyombo vya habari kuliko aliyehakikisha sheria ipo ya kufungua? Lakini unafikiri ni kweli upo uhuru wa habari kulinganisha na wakati wa Nyerere?

aliwafunga wapinzani wake -
Ni mpinzani gani wa Nyerere aliyefungwa kwa kumpinga Nyerere na ili hoja iwe na nguvu ni vizuri kuonesha ni nani aliyefungwa bila ya kutumia sheria zilizokuwepo?

alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa Tzania.
- Kabla ya Nyerere "kuuleta" umaskini, Tanzania ilikuwa na utajiri gani ambao ulipotea? Unataka tuamini kuwa wakati wa Mkoloni Tanzania ilikuwa ni tajiri na Watanzania walikuwa na unafuu zaidi kuliko wakati wa Nyerere? Hapa inabidi ulete figure na hali ya watu wa wakati huo.

Sasa hiyo sehemu moja; sehemu ya pili unalinganisha utawala wa Nyerere na utawala wa nchi gani nyingine iliyofanana na ya kwetu ili tuweze kupima na kusema kuwa "wao" walipiga hatua kubwa ya maendeleo kwa sababu viongozi wao walifanya kinyume kabisa na alichofanya/kilichofanyika wakati wa Mwalimu.
 
Kwa kila mwanasiasa wa Tanzania anaetaka kuungwa mkono na wananchi wengi amekuwa akijitahidi kujionesha kuwa ni mfuasi wa Rais wa kwanza wa Tzania Mwl Nyerere. Anasifiwa kwa kila kitu lakini kwangu mimi simkubali kabisa Mwl Nyerere. Siamini kama alikuwa na kipaji cha uongozi. Alikuwa ni dikteta. Alifinya uhuru wa habari, aliwafunga wapinzani wake, alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa Tzania. Si kwamba alikuwa anapendwa bali alikuwa anaongoza wananchi wengi wasiojua dunia inakwendaje"wajinga".

Huyo ndio Nyerere. Kwa miwani yangu namuona kuwa ana mabaya mengi kuliko mazuri kama tunavyolazimishwa kuamini. Kutojilimbikizia mali au kutoa huduma za jamii bure si kigezo cha kutokuwa dikteta maana hata Pinnochet, Hitler na Mussolin walikuwa wanatoa huduma za jamii bora na bure kabisa kwa watu wao.

Unayo hoja fulani inajadilika
ila tatizo ni kwamba usipomkubali Mwalimu hawa wengine waliomfuta( Mwinyi Mkapa na sasa Mrisho Kikwete) utakuwa sio tu hautawakubali bali utawachukia.

Unless una ajenda yasiri naomba umalizie na walimfuata ili nikusome vizuri.

Pamoja na mapungufu ya nyerere bado ni kinara na mfano mzuri wa uongozi sababu waliovaa viatu vyake mpaka sasa ni worse.
 
Back
Top Bottom